Sunday, July 1, 2012

FEDHA ZA MATIBABU ZAPATIKANA,MADAKTARI WAKATAA MSAADA WA SERIKALI

Ulimboka apelekwa nje kutibiwa  Send to a friend
Sunday, 01 July 2012 08:12
0digg
Wananchi wakiwa wamelizunguka gari la wagonjwa lililompeleka Dk Steven Ulimboka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nje kwa matibabu.Picha na Silvan Kiwale

Geofrey Nyang’oro
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.Kusafirishwa kwake kunafuatia hatua ya jopo la madaktari waliokuwa wakimhudumia, kueleza mabadiliko ya hali ya afya yake, yaliyosababisha figo kushindwa kufanya kazi, hali iliyolazimu pamoja na matibabu mengine, kwenda   kusafishwa damu.

Ingawa madaktari hao wamekataa kuweka wazi nchi anayopelekwa, kuna taarifa kwamba huenda amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini.

Katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) jana makundi mbalimbali ya watu yalifurika wakiwamo wanaharakati na ndugu wa Dk Ulimboka,  waliofika kwa lengo la kumsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Watu hao waliofika hospitalini hapo kuanzia asubuhi, waliendelea kubaki  eneo hilo hadi saa 6:45 mchana msafara ulipoanza.

Dk Ulimboka alisafirishwa kwa gari la kubebea wagonjwa la kampuni ya AAR. Alipofika uwanjani, alisafirishwa kwa  ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini, akisindikizwa na watu watatu.

Usiri safari ya Dk Ulimboka

Mapema jana asubuhi, taarifa za kusafirishwa kwake zilizagaa, lakini hapakuwa na mtu wa kuthibitisha safari hiyo na namna atakavyosafiri.

Katika safari hiyo, Dk Ulimboka amesindikizwa na  Dk Pascal Lugajo, kaka yake, Dk Hobakile Ulimboka na mke wake,  Dk Judith Mzovela.

Madaktari watoa tamko

Baada ya Ulimboka kusafirishwa, madaktari walilaani kitendo cha kutekwa na kupigwa mwenzao na kuitaka Serikali itoe tamko juu ya usalama wao.

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwan Chitage aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo na vitisho vya kufukuzwa kazi wanataaluma hao kunakofanywa na Serikali, kumezua  hofu kwa  madaktari wote nchini.

“Tunaamini Serikali inawajibika kwa watu wake, kwa hali ilivyo sasa madaktari wapo kwenye hofu kubwa, tunataka itoe tamko juu ya usalama wa madaktari,” alisema Dk Chitage.

Akizungumzia hali ya Dk Ulimboka, alisema imekuwa ikibadilika mara kwa mara hali ambayo imesababisha kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi .

Chitage alisema kama Serikali ingekuwa na nia ya kuboresha huduma hospitalini hapo ingeweza kununua mashine ya CT Scan ambayo alisema bei yake ni sawa na Toyota ‘Shangingi’ moja.

Kwa upande wao wanaharakati wa haki za binadamu, jana walifika Uwanja wa Ndege wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti wakilaani kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka.

Dk Chitega alisema hadi kufikia jana, walikuwa wamepata fedha zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya matibabu yake. Juzi madaktari hao walisema wanahitaji Dola za Marekani 40,000 (Sh63.2 milioni) ili kumtibu mwenzao nje ya nchi.


Serikali na tiba ya Ulimboka


Wakati mgomo wa madaktari ukiingia siku ya nane leo, Serikali imesema ilikuwa tayari kugharimia matibabu ya Dk Ulimboka.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja jana alisema Serikali ilikuwa tayari kugharimia matibabu ya daktari huyo.

Mwamaja aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa ni haki ya mgonjwa anayepewa rufani ya kutibiwa nje, kugharimiwa na Serikali, lakini
msaada huo wa Serikali ulikataliwa na madaktari hao na kuitaka ikae mbali na matibabu ya kiongozi wao.

“Sisi tulishaanza maandalizi ya kugharimia matibabu yake, lakini madaktari wenyewe walikataa msaada wa Serikali,” alisema Mwamwaja.

Hali yazidi kuwa tete

Kutokana na mgomo huo, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, umewatimua zaidi ya madaktari 80 walioko kwenye mafunzo kwa vitendo.

Hadi kufikia juzi, madaktari 146 walikuwa wamefukuzwa kutokana na mgomo huo katika hospitali za Bugando na Sekou Toure mkoani Mwanza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na ile ya Mkoa wa Dodoma.

Mbeya

Habari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya zinadai kwamba, baada ya uongozi wa hospitali hiyo kulazimika kuomba madaktari wengine kutoka hospitali za jijini Mbeya ili kuongeza nguvu, madaktari hao nao wameonekana kutoridhishwa na ombi hilo.

Habari hizo zinasema kwamba, licha ya madaktari hao kupatikana na kwenda hospitalini hapo, walisikika wakilalamika kwamba wao hawapo tayari kufanya kazi sehemu yenye mgogoro na kwamba wao hawawezi kufanywa kama chambo kwa kuhofia usalama wao.

Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo,  Dk Eliuter Samky alikiri kuzidiwa na kusuasua kwa utoaji huduma kwa wagonjwa ambapo alisema kuwa hadi sasa huduma zinazotolewa ni zile za dharura pekee na zile za kawaida wagonjwa wanaambiwa waende Hospitali ya Mkoa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina, alisema kwa sasa hali inaendelea vizuri kutokana na kujipanga vyema kukabiliana nayo, licha ya kuwa bado kuna tatizo la upungufu wa vitanda hivyo kusababisha wagonjwa kulala chini.

Tanga

Baadhi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya  Bombo, wameitaka Serikali kukaa pamoja na madaktari ili kumaliza tatizo hilo.

Wamesema hali iliyofikia sasa ni mbaya hivyo ni busara pande hizo mbili kukaa meza moja kutatua mgogoro huo bila kujali nani kati yao amesababisha.

Sakina Abdallah ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi ya Gallanis, alisema amesikitishwa na baadhi ya wanasiasa wanaoshabikia kutekwa Dk  Ulimboka.

“Binafsi hali inayoendelea ya mgomo wa madaktari inanihuzunisha sana kwani tunaoumia ni sisi wananchi tunaotibiwa katika hospitali hizi,” alisema Sakina.


Godfrey Jambia ambaye ni majeruhi aliyelazwa katika hospitali hiyo, alisema Serikali inatakiwa kutatua madai ya madaktari hao ili kuwanusuru raia wasio na hatia.

                   
NCCR yaivaa Serikali

Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema Serikali ina maswali ya kujibu kutokana na kushindwa kutatua mgomo wa madaktari nchi nzima.

Chama hicho kimesema Serikali haitakiwi kutumia nguvu ya dola kumaliza mgomo na kuitaka ifute kesi iliyofunguliwa mahakamani ili kukaa meza ya majadiliano na madaktari hao kwa kuwa raia wasio na hatia, wanapoteza maisha kwa kukosa matibabu.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama, James Mbatia, alisema hata kama suala hilo limefika mahakamani, bado linazungumzika kwa kuwa afya za Watanzania zinawahusu wote.

“Hivi Serikali inashindwa kuliondoa jambo hilo mahakamani na kukaa meza moja na madaktari kumaliza tatizo hili..., katika hili lazima tuseme, yaani watu wanakufa tukae kimya, haiwezekani hata kidogo,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Ubabe hauwezi kuingizwa katika uhai wa Watanzania, kama majadiliano ya awali hayakufanikiwa basi wawekwe watu makini watakaosimamia majadiliano haya, hata wabunge wanaweza kusimamia suala hili, mgomo huu hauna itikadi za vyama unawahusu wananchi wote.”


Habari Hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, Claud Mshana, Dar, Burhani Yakub,Tanga na Godfrey Kahango, Mbeya

Sunday, June 10, 2012

NAPE ASHIDWA KUKANUSHA MADAI YA CHADEMA KTK VIWANJA VYA CHADEMA-SQUARE

Saturday, 09 June 2012 08:13
0digg
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
Dotto Kahindi na Leon Bahati
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama chake hakina mpango wa kuutumia mkutano wake wa leo kwenye Viwanja vya Jangwani kujibizana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake, kitajikita zaidi katika kutoa somo kwa wajumbe wapya wa mashina na viongozi wa matawi Mkoa wa Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya Nape inatoa mtazamo tofauti na tetesi kwamba  CCM kitatumia mkutano huo kukijibu chama hicho kikuu cha upinzani ambacho nacho kilifanya mkutano kwenye viwanja hivyo hivi karibuni.
Katika mkutano huo ambao Chadema kilizindua Mpango wake wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) mwishoni mwa mwezi uliopita, kiliorodhesha shutuma nyingi dhidi ya Serikali ya CCM zikiwemo za kusababisha maisha magumu kwa Watanzania.

Nape alisema mkutano huo uliandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es Salaam hata kabla ya huo wa Chadema na lengo lake ni kuwakutanisha viongozi wapya wa chama hicho tawala na viongozi wa juu wa chama na Serikali, wakiwemo mawaziri watakaofafanua shughuli zao za kiutendaji.
“Mkutano huu unalenga kuwafundisha wajumbe wa nyumba kumi na viongozi wa mashina waliochaguliwa hivi karibuni namna ya utendaji wa Serikali, kwa kuwa wao bado ni  wapya kiuongozi na wanahitaji kupewa somo,” alisema Nape.

Alipoulizwa kama mkutano huo ni moja ya hatua za kufuta nyayo za Chadema hasa baada ya kuzindua M4C, Nape alisema: “Mkutano huu tuliuandaa mapema kabla hata ya Chadema hawajafanya mkutano wao. Ila kilichochelewesha ni Mkutano wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM,” alisema Nape na kuongeza:

“Mkutano huu awali, ulikuwa ufanyike ndani ya ukumbi lakini kwa kuwa watu wengi walipenda kushiriki tumeamua kuufanyia Jangwani ambako wanachama na viongozi wa CCM watapata fursa ya kusikia sera za viongozi wa chama na watendaji wa Serikali.”

Aliwataja mawaziri ambao watakuwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ambaye atazungumzia masuala ya usafiri wa reli, bandari na anga na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ambaye atazungumzia masuala ya miundombinu na barabara.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira ambaye atazungumzia hatima ya Watanzania katika masuala ya ajira na vijana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye atazungumzia mipango ya wizara yake.

M4C
Mei 25 mwaka huu, Chadema kilizindua mkakati wake mpya wa ‘Movement For Change-M4C’ ukiwa na lengo la kukiandaa chama hicho kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwataka wanachama na wananchi kwa ujumla kukichangia fedha chama hicho ili kufanikisha kampeni aliyoielezea ni ya kukiondoa CCM madarakani mwaka 2015.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alisema maisha ya Watanzania si mazuri, vyakula vinaongezeka bei kutokana na Serikali ya CCM kutokuwa makini hivyo akawataka wabunge wa chama hicho kuibana kupitia Bunge lijalo la Bajeti.

Aliilaumu Serikali kwa kutotumia vizuri kodi za Watanzania kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa kuwalipa watumishi ambao nafasi zao hazina manufaa kwa wananchi.
Dk Slaa alilalamikia kitendo cha kuongeza kodi katika mafuta ya taa ili watu wasichakachue mafuta ya dizeli akisema ni mwiba kwa Watanzania.

R.I.P BOB MAKANI, TUTAUENZI MCHANGO WAKO KATIKA KUPIGANIA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NCHINI TANZANIA


 Send to a friend
Sunday, 10 June 2012 09:38
0digg
Mzee Bob Makani
Na Mwandishi Wetu
MWASISI wa Chadema na Mwanasheria mkongwe nchini Bob Makani, amefariki dunia usiku katika hospitali ya Aga khan, jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Makani alizidiwa ghafla saa 3: 00 usiku wa kuamkia leo na kukimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako alifariki dunia saa 4.15 usiku.

“Amekuwa anaumwa muda mrefu, mara kadhaa akipelekwa hospitali na baada ya muda anaruhusiwa, lakini hii ya sasa alikua nyumbani akazidiwa ghafla wakampeleka hospitali na ilipofika saa 4.15 wakasema amefariki,” alisema Zitto.

Zitto alisema kuwa, suala la wapi utakapozikwa Makani ambaye ni Katibu Mkuu wa Kwanza na Mwenyekiti wa pili wa Chadema, litajulikana baada ya kujadiliana na familia ya marehemu.

“Suala la wapi atazikwa kama ni Shinyanga ama Dar es Salaam, litajulikana baada ya kuzungumza na familia yake, kwa sasa tunashughulika kwanza na kuhifadhi mwili wa mzee wetu,” alisema Zitto.
Zitto alisema msiba wa utakuwa nyumbani kwa marehemu eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kwa siku za hizi karibuni afya yake imekuwa ikizorota na kumfanya kuripotiwa kuanguka mara kwa mara alipokuwa akifanya shughuli zake.

Januari 17 mwaka huu katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema Regia Mtema, Makani alianguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu.

 Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake

Alikuwa Katibu Makuu wa kwanza wa Chadema kati ya mwaka 1993 hadi 1998, alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 na amegombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa mara tatu kati ya mwaka 1995 na 2000 na mwaka 2005.

Kazi ambazo amewahi kuzifanya serikalini; alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 1966 na elimu yake ana shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha Makarere nchini Uganda.

Ni mzaliwa wa Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga akitokea kwenye ukoo wa kichifu wa Makani.

Sunday, April 8, 2012

KANUMBA WATANZANIA WALIKUPENDA SANA, LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI, R.I.P KANUMBA THE GREAT

Kanumba afariki  Send to a friend
Saturday, 07 April 2012 21:45
Marehemu Steven Kanumba
MAELFU ya wapenzi wa sanaa ya filamu nchini, alfajiri ya kuamkia jana waliduwaa mithili ya watu waliopigwa sindano ya ganzi baada ya kuenea kwa taarifa za kifo cha ghafla cha msanii namba moja wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba (28).

Taarifa za kifo cha Kanumba zilisambaa kwa kasi mithili ya moto katika nyika kavu na kuikuta alfajiri ya jana, ikigeuka kibarua kigumu kwa idadi kubwa ya watu, kusaka stesheni mbalimbali za redio, televisheni mitandao ya kompyuta huku wengine wakihangaika kupiga simu huku na kule, kutafuta ukweli wa tukio hilo,lililotikisa si Tanzania tu bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.


Kanumba alifariki usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi, Kanda ya Kinondoni, Charles Kenyela, ziinaeleza kuwa kifo cha msanii huyo kilitokana na ugomvi uliotokea kati yake na mpenzi wake ndani ya nyumba yake.

Taarifa za kifo cha Kanumba zilianza kusambaa kuanzia saa 10.00 alfajiri na kuenea kwa kasi ambapo hadi kufikia saa moja asubuhi, mamia ya watu walikuwa wamejazana nyumbani Kanumba kutaka kuthibitisha habari hizo.

Kadri muda ulivyozidi kusogea ndivyo idadi ya watu ilizidi kuongezeka nyumbani kwa msaani huyo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutoka na filamu zake kuuzwa na kuoneshwa katika vituo mbalimbali vya televisheni, ndani na nje ya nchi.

Miongoni mwa watu waliomiminika kwa haraka nyumbani kwa kanumba jana ni wasanii wa fani mbalimbali nchini,  wanasiasa na viongozi mbalimbali wa Serikali

Chanzo cha kifo chake

Kwa mujibu wa maelezo ya mdogo wake aitwaye Seth ambaye alikuwepo eneo la tukio, alisema kaka yake alishinda nyumbani na baada ya kula chakula cha jioni, alimwambia wajiandae kutoka.

Seth alisema kuwa wakati Kanumba akiwa tayari amejiandaa, walisikia mlio wa gari lifunga breki nje ya nyumba.

Alisema gari hilo lilikuwa limemleta mpenzi wa kaka yake msanii wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ambaye aliingia ndani na kwenda moja kwa moja chumbani kwa Kanumba.

Baada ya kuingia ndani, muda mfupi alisikia sauti zilizoashiria kuwa kulikuwa na ugomvi kati ya wapenzi hao.

“Ghafla ulizuka mzozo ndani na dakika chache baadaye, Lulu alitoka na kuja kuniambia kuwa Kanumba amedondoka baada ya kujigonga ukutani na kwamba yupo taabani hajitambui,” alisema Seth.

Alisema alipoingia chumbani, alimkuta kaka yake akiwa katika hali mbaya hivyo akaamua kumpigia simu daktari wake, ambaye alipofika na kuwashauri wampeleke haraka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.

Seth alisema kabla ya kufika Muhimbili  walipitia Kituo cha Polisi cha Oysterbay kupatiwa Fomu ya matibabu (PF3).

Hata hivyo, baada ya polisi kupata maelezo ya awali ya ugomvi huo, walimshikilia Lulu kituoni hapo na kumwacha Seth akimpeleka Kanumba hospitali.

Alisema walipofikia Hospitali ya Muhimbili, madakati waligundua kuwa tayari Kanumba alishaaga dunia.

Kamanda Kenyela

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema Kanumba alikufa kutokana na ugomvi uliotokea kati yake na rafiki yake wa kike Lulu.

 "Kanumba amefariki usiku wa kuamkia leo (jana) majira ya saa tisa usiku, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ugomvi kati yake na rafiki yake wa kike anayejulikana kwa jina la Elizabeth Michael 'Lulu' mwenye umri wa miaka 18.

Alisema kabla ya ugomvi huo kutokea kati yao wakiwa chumbani, simu ya Lulu iliita na akaamua kutoka nje kupokea kitendo kilichomuudhi Kanumba.

Kamanda Kenyela alisema Kanumba aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti akitaka aelezwe kwanini alitoka nje kupokea simu huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine.

Aliongeza baada ya Lulu kuona Kanumba akimfuata aliamua kukimbia kutoka nje ya geti , lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba  alimkamata na kumrudishwa ndani.

Kamanda Kenyela, alisema Kanumba akiwa amemshikilia waliingia wote chumbani na kufunga mlango.

Hata hivyo, alisema haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa maelezo ya Lulu anadi kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba.

Kamanda huyo alisema Lulu anaeleza kuwa baada ya Kanumba kufunga mlango, alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho kabla ya kuanguka chini.

Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Kanumba alikuwa amekunywa Whisky (pombe kali) aina ya Jacky Daniel, hata hivyo, bado wanachunguza zaidi kujua kama kweli Kanumba alilegea tu na kuanguka, ama alipigwa na kitu kizito kichwani au alisukumwa kwa nguvu na kumfanya aangukie kisogo.

“Uchunguzi ukikamilika tutampeleka mahakamani kwa tuhuma za mauaji,” aliongeza Kamanda Kenyela.

Rais Kikwete atoa pole

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania –TAFF kuomboleza kifo cha Kanumba,

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Kikwete ameelezea kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha msanii huyo ambaye amemtaja kuwa mahiri na mwenye kipaji kikubwa.

“Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya filamu nchini hautasahaulika,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Rais Kikwete alisema Kanumba ametoa mchango mkubwa kupitia sanaa ya filamu na kutokana na uwezo mkubwa wa kisanii, Watanzania wataendelea kumkumbuka kwa mchango wake.

“Nakutumia wewe Rais wa TAFF salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa wasanii wote wa filamu na sanaa nyingine kufuatia msiba huu mkubwa kwa fani yetu ya sanaa.

Mama wa Kanumba azungumza

Mama mzazi wa Kanumba, Flora Mutegoa amesema alizungumza na Kanumba kwenye simu saa chache kabla ya kifo chake, huku akimtaka arudi Dar es Salaam haraka, kutoka Kagera alikokwenda kumsalimia mama yake (bibi wa Kanumba), ili aje amuage kabla hajasafiri kwenda Marekani.

 Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba wakati akijiandaa kusafi kwenda jijini Dar es Salaam, Flora alisema alizungumza na mwanawe  kwa simu usiku huo huo saa chache kabla ya kufikwa na mauti kumkuta.

Mama huyo ni mzaliwa wa Kijiji cha Itoju, Kata ya Izigo, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera lakini kwa sasa anaishi  Dar es Salaam .

 "Mwanangu niliongea naye usiku akiwa mwenye furaha na tulitaniana sana,alisema anatuma nauli nirudi Dar es Salaam tuagane, kwani alikuwa na safari ya kwenda Marekani,"alisema Flora.

 "Sina cha kuongea naomba mniombee katika kipindi hiki kigumu jana nimeongea naye kwenye simu leo naambiwa mwanangu amekufa,"alisema huku akibubujikwa machozi.
Aliongeza kuwa Kanumba aliwahi kumdokeza kuhusu ndoto zake za baadaye kuwa alikuwa na matarajio ya kufika mbali zaidi katika sanaa ya uigizaji.

Maneno ya mwisho ya Kanumba

Siku za hivi karibuni Kanumba alikuwa akichapisha habari mbalimbali katika mitandao ya kijamii zilizokuwa zikisisitiza  upendo.

Katika mtandao wake wa Twiter na Blog yake  juzi saa sita mchana alichapisha habari akiwasi watu kufanya mambo mema kwa watu wengine ili wapate baraka.

"Tunavyofanya kwa ajili yetu huwa yanakufa nasi, lakini tunayoyafaya kwa ajili ya wengine hubaki duniani," sehemu ya maneno yake ya mwisho aliyoyaweka katika Balog yake juzi kabla ya kifo chake .


Mbali na ujumbe alioandika siku moja kabla ya kufikwa na mauti, Kanumba amekuwa akichapisha katika mitandoa yake ya kijamii maneno ya busara na kukemea chuki miongoni mwa jamii tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Maneno ya mwisho kwa wasanii wenzake

Kanumba mbali ya kutoa maneno ya busara kwa jamii, pia alikuwa akitumia mitandao yake kutoa maneno ya kuwapa moyo wasanii wenzake.

Kwa mfano Januari 24 mwaka huu baada ya kutwaa Tuzo ya ZIFF, aliandika kwenye mtandao maneno aliyoyaelekeza kwa wasanii wenzake akisema,:

 "Maneno yangu ya mwisho, hata tukiwa na uwezo wa kuhamisha milima kama hatupendani katika tasnia ni kazi bure,kile kilicho moyoni ndio kioneshe usoni na si vinginevyo".

"Kama wanichukia moyoni basi onyesha usoni na kama wanipenda moyoni basi onyesha usoni na si vinginevyo,Isiwe moyoni wanichukia halafu usoni wanichekea,Hii sanaa ni karama tuliyobarikiwa na Mungu tuitumie vyema kwa ajili ya utukufu wake maana ipo siku atatuuliza na kutudai,kama katupa bure basi anao uwezo wa kutuny'ang'anya pia','soma Wakorintho uone jinsi Mungu alivyogawa karama hizi na ni kwanini katugawia." sehemu ya maneno yake kwa wasanii wenzake nchini.

Mamia wafurika nyumbani kwake

Mamia ya watu jana walifurika nyumbani kwa msanii huyo kiasi cha barabara ya Sinza Uzuri inayopita karibu na nyumba hiyo kufungwa.

Watu kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam baadhi yao wakiwa wanabubujikwa, machozi walifika kushuhudia kwa macho yao kile wanachokisikia kwenye vyombo vya habari. Kulikuwa na msongamano mkubwa pia wa magari katika eneo hilo.

Historia yake

Kanumba alizaliwa Januari 8, 1984  mkoani Shinyanga,  ni mtoto wa tatu katika familia yao akiwa na dada zake wawili.

Alisoma Shule ya Msingi Kaboya, mjini Bukoba na baadaye akahamia Shinyanga ambako alimalizia elimu yake ya msingi katika Shule ya Bugoi.

Alijiunga kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari, Christian Seminari iliyopo Kongowe na baadaye akaendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee.

Dada wa marehemu

Dada wa marehemu, Abela Kajumolo alisema kuwa mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican.

Alisema familia imepanga mazishi ya Kanumba yatafanyika Jumanne wiki ijayo na kwamba bado hawajaamua kama atazikwa Dar es Salaam au Bukoba," alisema.

Tayari kamati ya mazishi imeundwa na ikiwajumuisha Gabriel Mtitu,  Stephen Jacob (JB) William Mtitu na Issa Mussa (Cloud) ambao wote ni wasanii wa filamu nchini.

Kamati ya usafiri itakuwa na Meneja wa  Clouds Media Group,  Ruge Mutahaba na Vincent Kigosi (Ray).

Enzi za Uhai wake

Marehemu alianza uigizaji miaka ya 2000 akiwa na Kundi la Kaole na baadaye kuingia katika fani ya filamu wakati huo akifanya kazi zake chini ya Kampuni ya Game First Quality.

Hata hivyo, alifanya kazi na kampuni hiyo hadi alipofanikiwa kumiliki kampuni yake binafsi ya Kanumba The Great Film.

Marehemu Kanumba pia ameshirikiana na wasanii wakubwa barani Afrika katika uingizaji akiwamo Ramsey Nouah wa Nigeria ambaye amecheza naye filamu ya Devil’s Kingdom na ambayo imezinduliwa mapema mwezi huu nchini Ghana.

Pia hadi mauti yanamkuta, Kanumba alikuwa akiendelea kutengeneza filamu ya Ndoa yangu ambayo alikuwa akiiandaa na mwigizaji mahiri wa kike, Jackline Wolper.

Kuingia kwenye siasa

Marehemu Kanumba pia katika siku za hivi karibuni aliwahi kukaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, akini hakuweka bayana kupitia chama gani wala jimbo.

Kanumba amekuwa  msanii wa kwanza nchini kuitangaza Tanzania ndani na nje ya bara la Afrika kupitia filamu.

Wasanii wenzake wanasemaje?

Suzan Lewis maarufu kama 'Natasha'  ambaye ni msanii mkongwe anasema kifo cha Kanumba kimemwachia kumbukumbu ambayo haiwezi kusahaulika.

“Nitamkumbuka Kanumba daima katika maisha yangu, alikuwa ni mtu wa watu alikuwa ni msanii pekee aliyepiga hatua na kuishi maisha ya wasanii wa kimataifa.

Yvonne Cherryl (Monalisa): “Kifo cha Kanumba kimefifisha ndoto zangu za kuigiza pamoja na wasanii maarufu kutoka Hollywood, tulikuwa na maandalizi hayo na Kanumba ndio alikuwa kila kitu katika suala hilo sikutegemea kama hili lingetokea.”

Wema Sepetu: "Siamini, na sitaki kuamini kabisa, nipo ndotoni sijui niseme nini,"alisema Wema huku akiangua kilio kilichomfanya ashindwe kuendelea kuongea.

Hatman Mbilinyi: " Alikuwa ni mcheshi sana, alipenda watu waliofanya naye kazi, nimepokea kwa ugumu, siamni kwa sababu ni saa chache tu tulikuwa pamoja, hakuumwa ni bora angeumwa tukajua aliumwa."

Jerison Tegete ambaye ni Mchezaji wa Yanga alisema alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kupata habari za msiba, na kwamba ameguswa sana na kifo cha Kanumba.

"Inasikitisha sana kwani tumepoteza kijana mdogo na ambaye alikua na nafasi kubwa katika kuielimisha jamii kupitia filamu zake.
Single Mtambalike maarufu Richie alisema ana mwachia Mungu kuhusu kifo cha Kanumba. "Sijui nizungumze vipi kuhusu marehemu kwanza siamini kama kweli Kanumba hatutakua naye katika tasnia hii na si filamu tu hata katika kazi nyingine ambazo tumekua naye karibu yote namwachia Mungu.”

Jacob Steven  amarufu JB alisema ni vigumu kuamini kuwa kanumba kafa kwa vile saa chcahe walikuwa pamoja.

“Ni pigo lisiloelezeka kwa sasa na ni vigumu kuamini kilichotokea kwani saa chache kabla ya kifo chake tuliwasiliana na alioongea kwa furaha bila kutambua nini kitatokea mbele yake katika muda mchache ujao.”

Tangana Iringa wamlilia
Naye Burhani Yakub kutoka Tanga anaripoti kuwa waandaaji wa filamu wa Mkoa wa Tanga wameleza kuguswa kwao na taarifa za kifo cha Kanumba na kuwataka wasanii wa tasnia hiyo kuwa watulivu katika kipindi hiki cha majonzi.
Wakizungumza na Mwananchi Jumapili mara baada ya kusikika taarifa za kifo cha Kanumba jana asubuhi, walisema kifo cha Kanumba ni pigo kubwa kwa tasnia hiyo nchini.
Mtunzi Mkongwe  wa riwaya na mwandishi wa hadithi za Filam wa Jijini Tanga, Faki A. Faki  alisema taarifa za kifo cha Kanumba zimeshtua kwa kuwa ni msanii aliyeikuza sanaa ya filamu nchini.

Tumaini Msowoya anaripoti kutoka Iringa kuw Tumaini Msowoya, Iringa
Wakazi wa Mkoa wa Iringa wakiwamo wasanii wa filamu wamesema kuwa wamepokea kwa masikitiko msiba wa msanii nyota wa filamu Tanzania, Steven Kanumba na kwamba taifa limepata pigo kwa kumpoteza mtu muhimu aliyeweza kutangaza filamu za Kitanzania ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya maduka, kati kati ya mji wa Iringa wameamua kuomboleza kifo cha msanii huyo kwa kutoa nje televisheni zao ili kusaidia watu kuona filamu ambazo zimeigizwa na msanii huyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao walisema msiba huo umewashtua na kwamba msanii huyo alikuwa na mchango mkubwa kwenye sanaa sanaa kupitia filamu zake.
Katibu wa kundi la sanaa la Mundu, mkoani Iringa, Athanas Kipera alisema hata kundi lake limepata mchango mkubwa kutoka kwa marehemu Kanumba.

Basata wahuzunika
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amesema kuwa baraza lake limepokea kwa masikitiko makubwa  kifo cha Kanumba.
"BASATA inaungana na familia za wafiwa na wasanii wote nchini kwa maombolezo  ya msiba huu mkubwa na wa kihistoria, kufiwa na msanii huyu mahili kwenye tasnia ya filamu ni pengo kubwa kwa familia, Sekta ya sanaa na Taifa kwa ujumla kutokana na ukweli kuwa, aliweza kuutangaza utamaduni na sanaa yetu nje ya mipaka,"alisema Gonche Materego ambaye ni katibu mkuu wa Basata.

Alisema Kanumba atakumbukwa kwa moyo wake wa kujituma na kuthamini kazi ya Sanaa toka akiwa Kundi la Maigizo la Kaole ambapo moyo wake huo ulimfanya awe miongoni mwa wasanii walioleta mageuzi kwenye tasnia ya filamu kwa kuifanya kuanza kupendwa na wadau wengi zaidi.

Imeandaliwa na Julieth Kulangwa, Jesca Nangawe, Vicky Kimaro na Phinias Bashaya, Bukoba

Thursday, March 22, 2012

MAWAZIRI MUACHE SIASA KATIKA MATATIZO MAZITO YANAYOHITAJI UTEKELEZAJI, NI NANI ASIJEJUA MATATIZO YA AJIRA TANZANIA?

 Send to a friend

Waziri wa Kazi na Ajira,Kabaka gaudencia

YASEMA AJIRA KWA VIJANA SIYO BOMU, WAZIRI KABAKA AMWAGA TAKWIMU, AELEZA MAANA YA AJIRA

Geofrey Nyangoro

SERIKALI imetoa takwimu za ajira kwa vijana nchini  ikiwa ni majibu kwa kauli za mara kwa mara za Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye amekuwa akisema tatizo hilo ni kubwa akililinganisha na bomu linalosubiri kulipuka.

Lowassa amenukuliwa katika matukio manne tofauti kuanzia mwishoni mwa mwaka jana na mwaka huu, akionya tatizo hilo la ajira kwa vijana kwamba linahitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka.


Jana, Waziri wa Kazi na Ajira alisema tatizo hilo haliwezi kufafanishwa na bomu na kusema wanaosambaza uvumi huo hawaitendei haki Serikali, kwani tatizo hilo limepungua kutoka asilimia 12.9 mwaka 2000/1 hadi asilimia 11.7, mwaka 2006.


Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake Dar es Salaam jana, Kabaka alitoa ufafanuzi wa hali ya ajira nchini na hatua ambazo Serikali inachukua kushughulikia tatizo hilo.

“Hali halisi ya ukuaji wa uchumi nchini ni nzuri lakini, haiwezi kuonekana kama wananchi wake ni maskini na hawana ajira. Hata hivyo, Serikali imekua ikichukua hatua mbalimbali kushughulikia suala hilo ikiwamo la kuhimiza uwekezaji nchini,” alisema Kabaka na kuongeza:


“Kitendo cha wanasiasa kuendelea kusema tatizo la ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka, siyo kweli na kudai Serikali hayaijafanya kitu wanakuwa hawaitendei haki.”

Alisema utafiti uliofanywa na wizara yake kwa kushirikiana na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS), unaonyesha kuwa tatizo hilo limepungua kwa asilimia 1.2.


Mikakati

Waziri Kabaka alisema utafiti uliofanywa na NBS mwaka 2006 ikishirikiana na wizara hiyo unabainisha kuwa nguvu kazi ya Tanzania ni 20.6milioni kati ya watu 37.5 milioni, kwa wakati huo.


Alisema kutokana na utafiti huo, watu 18.3milioni sawa na asilimia 88.3 ya watu hao 20.6milioni walikuwa na ajira huku waliokuwa kwenye ajira ya sekta rasmi wakiwa ni 17milioni sawa na asilimia 92.7.


Kabaka alisema katika utafiti huo, watu 1.3milioni walikuwa kwenye ajira isiyo rasmi huku utafiti ukibaini kuwa kila mwaka watu 800,000 hadi milioni moja wanaingia kwenye soko la ajira.


“Utafiti unaonyesha hali ya ukosefu wa ajira nchini umeshuka kidogo kutoka asilimia 12.9 mwaka 2000/1 na kufikia asilimia 11.7 mwaka 2006, hata hivyo kiwango hicho ni cha juu kwa nchi kama Tanzania ambayo haina huduma za kinga kwa watu wasio na ajira,” alisema Kabaka.


Waziri Kabaka alisema pamoja na kushuka kwa kiwango cha ajira, bado kiwango cha ukosefu wa ajira ni kikubwa huku kikitofatutiana baina ya kundi moja na jingine akisema Tanzania siyo kisiwa hivyo, tatizo linaloikumba dunia la ukosefu wa ajira pia linaikumba nchi hiyo.


Alitaja mikakati ya Serikali kuwa ni pamoja na utekelezaji wa mipango mbalimbali yenye lengo la kukuza ajira ambayo ni pamoja na mpango wa mafunzo yenye kuwezesha vijana kujiajiri, mfuko wa maendeleo ya vijana, mpango wa kukuza ajira kwa vijana na mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi na kukuza ajira.


Kabaka alitaja mipango mingine kuwa ni ule wa uwekezaji katika elimu na mafunzo, kujengea uwezo mamlaka za Serikali za mitaa (LGAs) na ajira za moja kwa moja zinazotolewa na Serikali kupitia sekta mbalimbali.


“Serikali imetoa ajira kwa walimu 15,000 wa shule za sekondari na msingi na pia kwa kipindi cha miaka mitano 2007 hadi 2011, ajira 414,679 zimepatikana kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC),” alisema Kabaka.


Waziri Kabaka alibainisha mpango kabambe uliowekwa na Serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira, ambao alisema hadi kufikia mwaka 2015, itakuwa imepunguza tatizo la ajira kutoka asimilia 11.6 ya mwaka 2006 hadi kufikia asilimia tano.


Alisema katika kutekeleza hilo, Serikali imeanza kuchukua hatua na kwamba imeanda programu ya kwanza itakayolenga kutambua vijana wote wenye taaluma  aina ya ujuzi walionao katika kila wilaya hapa nchini.


“Programu hii ambayo utekelezaji wake unatarajia kuanza mwaka wa fedha wa 2012/13, imejikita katika kuwatambua vijana na shughuli zao ili kuwajengea uwezo katika kukuza tabia ya kijasiriamali, kuwawezesha kupata ujuzi wa kujiajiri na kukuza soko la bidhaa za ndani kwa kuweka mazingira kutumia bidhaa za Tanzania,” alisema Kabaka.


Alisema pia mpango huo umejikita kuwezesha kijana mmojamoja au kikundi kujiajiri, vijana wasomi na wenye ujuzi wanaohitimu katika vyuo vya elimu ya juu kujiajiri na kutengeneza mazingira ya kuajiri wengine na pia kuwezesha sekta binafsi na taasisi za umma kuwekeza katika sekta zenye kipaumbele katika kutoa ajira.


Waziri Kabaka alisema Serikali imejipanga kutekeleza mpango wa kukuza ajira katika maeneo ya mikoa na wilaya ili kuwezesha kupunguza tatizo la ajira na kuwafanya vijana wasikimbilie mijini.


Maana ya ajira

Akinuuku tafsiri inayotumika duniani na kutambuliwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO), Waziri Kabaka alisema maana ya ajira ni shughuli yoyote halali anayoifanya mtu mwenye umri wa kufanya kazi kwa kujipatia kipato na kwa kawaida shughuli hiyo ni ya hiari inayotambuliwa kisheria na hufanywa kwa saa 40 hadi 45 kwa wiki.


Alisema ukosefu wa ajira ni hali ambayo hutokea wakati watu walioko kwenye umri wa kufanya kazi na ambao wangependa kufanya kazi wanatafuta bila ya kuipata.


“Tafisiri hii ya kimataifa haiwajumuishi wale wasiotafuta kazi, wasiopenda kufanya kazi hata kama hawana kazi,” alisema Kabaka na kuongeza:

“Lakini tafisiri inayotumika zaidi Tanzania inatambua wote wasio na kazi na ambao wako tayari kufanya kazi  bila kujali wanatafuta kazi au la na inawahusisha hata  wasio na uhakika wa kufanya kazi hata ya siku moja.”

Alitaja aina tatu za ajira ambazo ni kazi ya staha, kazi chini ya kiwango na ajira maskini.


Alisema ajira za staha ni zile ambazo zina tija kiusalama, heshima haki za wafanyakazi na kipato cha kutosha, wakati ya ile ya chini ya kiwango ni ile ambayo haitoshelezi kutumia uwezo, muda na taaluma yote ambayo ambayo mhusika anayo. Ajira maskini ni ile ambayo kipato kinachopatikana ni cha chini ya kiwango kisichomwezesha mtu kuishi.


Akirejea utafiti wa ILO wa mwaka 2010/11, Waziri Kabaka alisema ripoti hiyo inaonyesha hali ya umaskini na ukosefu wa ajira duniani ni kubwa. Watu 205 milioni dunia kote mwaka 2010 hawakuwa na ajira.

Alisema idadi hiyo ilikuwa sawa na ongezeko la nguvu kazi isiyo na ajira duniani ya watu 27.7 milioni kulinganisha na ile ya mwaka 2007.


Alisema sababu za ongezeko la ukosefu wa ajira kwa mujibu wa ripoti hiyo, ni kutokana na utandawazi, maendeleo ya mawasiliano, mabadiliko ya teknolojia ambayo hayahitaji nguvu kazi nyingi katika utendaji kazi na kudidimia kwa nguvu za kiuchumi hasa katika nchi zinazoendelea.


Lowassa na ajira

Novemba 15, mwaka jana akiwa katika harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Makasa, Parokia ya Nyakato, Mwanza, Lowassa alionya kuhusu tatizo hilo na kulitaka lisaidie kujenga vyuo vya ufundi.


Alitoa takwimu akisema utafiti wa mwaka 2006, ambao hata hivyo, hakusema ulifanywa na taasisi gani, ulionyesha tatizo hilo kwa sasa limekuwa na kufikia asilimia 15 huku likigusa zaidi vijana wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 24 ambao ndiyo nguvukazi ya taifa... “Ninapozungumza hili siyo nia yangu kumlenga mtu. Mimi ni Yohana Mbatizaji, hii ni sauti inayolia nyikani.”


Novemba 29, mwaka huo wa jana akiwa harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKT), Usharika wa Amani Sabasaba, Singida, Lowassa alirudia tena suala hilo la tatizo ajira.


Mapema mwaka jana, Lowassa pia alifanya mkutano na waandishi wa habari Mjini Arusha na kuzungumzia tatizo hilo la ajira ambalo alilifananisha na bomu.


Jumatatu iliyopita, Lowassa alirejea kauli hiyo alipokuwa katika sherehe za uzinduzi wa Jimbo jipya la Kanisa Katoliki Ifakara akisema: “Nawaomba maaskofu katika miradi yenu mlipe kipaumbele suala la tatizo la ajira kwa vijana.... hili kama tulivyosema ni bomu linalosubiri kulipuka...”

Monday, March 19, 2012

Wananchi tunaitaka chadema

Default

Kuna upotoshaji mkubwa sana unafanyika hivi sasa ambao unafanyika katika namna ya hatari sana, naiweza kuifafanisha namna hiyo sawa sawa na mtu anaesema moto ni joto au upofu ni usingizi. Wanasiasa waliomadarakani wanajaribu kuyawekea mahitaji ya wananchi dhana ya kisiasa.

Wakati wananchi wanasema tunataka Mfumo bora wa elimu watawala wanasema CHADEMA haiwezi kuuleta, sababu DR SLAA Aliiba pesa kanisani.


Wananchi wanasema tunataka mfumuko wa bei udhibitiwe, watawala wanasema CHADEMA haiwezi kudhiti mfumuko wa bei sababu MBOWE ni DJ


Wananchi wanasema tunataka huduma bora za afya, watawala wanasema, DR Slaa anampenda sana Josephine.


Wananchi walia wanakufa njaa, watawala wanasema, CHADEMA ni chama cha Kichaga.


Wananchi wanapiga kelele wanalalamika mariasiri za Taifa letu zinanufaisha wachache na nyingi zinaibiwa na wageni, watawala wetu wanasema Ushindi ni Lazima.


Naomba tukumbushane historia mbichi kabisa, waliomfurumusha Hussein Mubarak kutoka Madarakani sio wanasiasa, Kijana aliyejichoma moto tunisia na kuacha laana nyuma yake hakuwa analalamikia wizi wa kura, waliomkamata Gadafi kwenye mtaro wa daraja walikuwa hawajebaba bendera ya chama chochote kile cha siasa, Hata sasa huko Siria wananchi hawapiganii kuundwa katika mpya wala kuwa na tume huru ya Uchaguzi.


Wito wangu kwa viongozi wa CCM ni huu ufuatao.

Kwanza, kuna ushahidi wa kutosha kwamba hivi sasa duniani, mabadiriko yanatokea kwa kasi ambayo haijawahi kutokea huko nyuma katika kila nyanja ya maisha.

Pili na mwisho, Muda si mrefu watanzania watagundua kwamba wanachokihitaji sio katiba mpya na wala sio tume huru ya uchaguzi wala sio maridhiano ya kitaifa ya namna yoyote ile wala sio ushindi wa wagombea wao.


Narudia tena, Punde kidogo, upepo wa mabadiriko utabidiri mkondo wake, watu watakapoamua kuweka magwanda na kuachana na ustaarabu wa kuonyeshana alama ya V sijui mtawaambia nini

Friday, March 16, 2012

LIHANA KUBALI YAISHE, CRISS BROWN TAYARI YUKO ENGAGED

Pop star Rihanna called her recent musical collaboration with ex-boyfriend Chris Brown "innocent," after critics and fans split on the duo working together three years after Brown assaulted the pop star. "We did two records, one for my fans and one for his fans, and that way our fans can come together. There shouldn't be a divide, you know, it's music and it's innocent," Rihanna told Ryan Seacrest on his syndicated morning radio show on Thursday.
Rihanna provided vocals on a remix of Brown's new dance song "Turn Up The Music" while Brown lent his voice to Rihanna's sexually-charged "Birthday Cake." Both tracks were released last month after the Grammy awards on February 12.
"I reached out to him about doing "Birthday Cake" because that's the only person that really it made sense to do the record, just as a musician, despite everything else, that was going to be the person," Rihanna told Seacrest.
"I thought about rappers and I've done that so many times, and the hottest R&B artist out right now is Chris Brown, so I wanted him on the track," she added.
Brown nearly derailed his career three years ago on the night before the Grammys, after he was arrested for beating up his then-girlfriend, Rihanna. Since that time he has tried to rehabilitate himself in the eyes of fans with mixed results.
The musical reunion of Rihanna and Brown had social networks abuzz as fans split on the pair working together with some making cynical comments, others calling it a publicity stunt and many embracing the new songs.
Brown has yet to comment openly on the collaboration.

Wednesday, February 1, 2012

SERIKARI YA TANZANI IWEKEZA KWA SOKA LA WANAWAKE, ILI KUEPUKA AIBU KWA SOKA LA WANAUME

Twiga Stars yaichakaza Namibia
Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, imewapa raha Watanzania, baada ya kuibanjua kibabe, Timu ya Wanawake ya Namibia.

Golikipa wa Namibia, alikabiliana na adhabu kali baada ya kutunguliwa mara tano katika ushindi wa jumla wa mabao 5-2 ambao Twiga imeupata leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Twiga inasogea hatua ya pili ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake ikiwa na ushindi wa jumla ya mabao 7-2.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Windhoek, Namibia, Twiga iliichakaza timu hiyo mabao 2-0.
Mchezo wa leo, Twiga ilianza kwa kusuasua lakini baadaye ilicharuka na kuipeleka puta Namibia, hivyo kuilazimisha mabao matatu ya haraka dakika za lala salama.
Kwa matokeo hayo, Twiga sasa itapambana kwenye mzunguko unaofuata na mshindi wa mechi ya Misri dhidi ya Ethio

SODOMA, SODOMA, SODOMA HIYOOOOOO INAKARIBIA

Mume wangu ananidandia ukuta, nimezoea, napenda, kuna athari kiafya?’
Mungu ni mkubwa sana. Tunakutana tena leo katika kona yetu. Karibu msomaji lakini nina kitu tofauti. Nimeamua nimsaidie dada yetu ambaye ana tatizo la kuzoea mchezo wa kwenda kinyume. Kudandia ukuta.

Ni msomaji wangu, hivyo naomba nisitaje jina lake. SMS yake inasomeka: “Nimeolewa lakini sijazaa. Mume wangu ananipenda na mimi kumridhisha nimekuwa nikimpa kila anachotaka.
“Moja ya vitu ambavyo aliniomba ni kuruka ukuta. Mwanzoni sikumuelewa lakini baadaye nilimkubalia. Tulipoanza nilisikia maumivu lakini sasa nimezoea, ninapenda. Wakati mwingine tukiwa faragha, sitaki amalizie kwa kawaida, akipita na ukutani angalau ndiyo natosheka.
“Kusema kweli nimezoea na sipendi kuacha, je, kuna athari kiafya baadaye?”
JIBU
Kutokana na unyeti wa swali la dada yangu, naomba jibu langu liwe refu ili mwisho aweze kuelewa. Hii ni mada nzima ambayo naamini itampa jibu linalotakiwa;
Binadamu ni watundu! Walipoona njia ya kawaida imezoeleka wakaamua kujaribu na nyingine ambayo hairuhusiwi. Lengo lao ni kupata utamu zaidi. Sodoma na Gomora iliangamizwa lakini haijasaidia, mapenzi ya kinyume na maumbile yameshika kasi ulimwengu wa sasa.
Utafiti uliofanywa na wanafunzi wa Chuo cha Marekani mwaka juzi, ulibaini kuwa mtu mmoja kati ya wanne anajihusisha na vitendo vya kudandia ukuta na tathimini ya jumla inaonesha kati ya 30% na 40% ya wakazi wote wa nchi hiyo wanashiriki ngono ya kinyume na maumbile.
Hiyo ni Marekani! Tanzania hali si shwari. Hakuna takwimu iliyotolewa na watafiti lakini muamko wa watu kuchangamkia mchezo wa kudandia ukuta ni mkubwa. Kinachowafanya wengi wageuke waumini wa ‘ibada’ hiyo haramu ni simulizi za utamu unaopatikana.
Kama Mwandishi wa Habari na Mshauri wa Saikolojia katika Masuala ya Kijinsia, najua ni kiasi gani hali ni mbaya. Ukiachana na msomaji huyo, pia nina malalamiko ya wanawake ambao wanadai kugeuzwa watumwa wa ngono ya mlango wa nyumba na waume zao au wapenzi wao.
Upo msemo kuwa wanaume wengi wanaathirika mno kisaikolojia kwa maneno ya vijiweni kuhusu mapenzi ya mlango wa nyuma. Kwamba stori za watu wakisifia uhondo ambao wanadai kuupata hujenga kitu tofauti kwa wale ambao hawajajaribu.
Watu hao ambao walikuwa hawajawahi kujaribu kabla, wakitoka kwenye vijiwe vyao, hubeba maneno hayo kwa umakini mkubwa, huku wakisumbuliwa na hisia za kutaka kujaribu. Matokeo yake, usiku ukiingia hutaka kulazimisha kwa wake zao.
Moja ya kesi ambazo nimewahi kukabiliana nazo ni kutoka kwa mwanamke mtu mzima ambaye ni mke mdogo wa mganga mmoja wa tiba za asili mwenye jina kubwa nchini (simtaji jina tafadhali). Mwanamke huyo nilikutana naye ofisini kwetu.
Mwanamke huyo alisema kuwa wakati anaanza mapenzi na mganga huyo ilikuwa kabla ya ndoa lakini baadaye mume alimbadilikia na kumtaka amruhusu awe anampitia kwa mlango wa nyuma. Eti, akamuahidi kwamba akimruhusu hilo, atampangia nyumba halafu atafunga naye ndoa.
Kwa kunasa maneno kutoka kwenye kinywa chake, mwanamke huyo baadaye alikubali baada ya kushawishiwa sana na kupewa ahadi nyingi. Alikuwa Mkristo, akabadili dini akawa Muislam, akapangiwa nyumba na akaolewa. Mapenzi yakawa matomoto.
Mambo yaliendelea mpaka akaathirika. Akawa hawezi hata kukaza misuli kuidhibiti haja! Wakati anakuja kunisimulia hayo, alikuwa yupo kwenye kipindi kigumu katika ndoa, yeye na mume wake walikuwa hawaelewani kabisa.
Huyo ni mmoja, mwingine ni mfanyakazi mmoja wa kampuni inayojihusisha na usambazaji wa vipodozi. Huyu ni mdada tu, alipokuja kuzungumza nami, kwa haraka nilimpa hongera za ndani ya moyo wangu kwa mafanikio niliyodhani anayo.
Alikuja na gari lake la kifahari, nikaamini ana mafanikio ya kimaisha na anafurahia mzunguko wake, kumbe sivyo! Alifunua kinywa chake kunisimulia alivyonavyo nilichoka! Dada huyo naye ni mmoja wa watumwa wa ngono ya kupitia mlango wa nyuma.
Alinieleza kuwa yeye kazi yake haiwezi kumfanya aishi maisha ya kifahari, akae kwenye nyumba nzuri na kumiliki gari la bei mbaya, ila katika mizunguko yake ya kimaisha, alipata kigogo mmoja ambaye alimua kumgharamia vitu hivyo.
Walianza kama wapenzi na akawa anamhudumia vizuri. Hakuwa na shida ya matumizi ya kawaida, kigogo huyo anayefanya kazi kwenye moja ya makampuni ya simu za mkononi alikuwa anakata. Baada ya miezi michache alimbadilikia.
Kigogo huyo akaanza kuomba njia haramu na kuahidi kumbadilishia maisha. Kwa kuanzia alimpangia nyumba ya kifahari mikocheni halafu akamtaka atekeleze ombi lake ili ampe gari. “Alianza kuniomba kama utani,” alisema dada huyo kisha akaongeza:
“Siku moja alikuja pale aliponipangia akiwa na gari mpya ambalo ndilo ninalotumia, akaendelea kunibembeleza halafu akaweka ufunguo wa gari mezani, kwamba nikikubali matakwa yake, litakuwa langu. Nilijifikiria sana lakini baadaye nilifumba macho nikakubali.
“Siku hiyo niliumia mpaka nikashindwa kukaa vizuri, nililia akanibembeleza, wiki nzima sikutoka ndani. Nilipoona anataka tena nikamkatalia lakini akasema ataninyang’anya gari, ikabidi nikubali. Gari amenipa lakini kadi anayo, kila nikikataa ananitishia kuninyang’anya, naendelea kuwa mtumwa mpaka najihisi kulegea.”
Yupo mwingine ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Sheria, huyu aliingia kwenye matatizo makubwa na mfadhili wake, aliyekuwa anafanikisha ada yake ya chuo baada ya kukataa matakwa ya kigogo huyo ya kushiriki mapenzi ya mlango wa nyuma.
“Aliniambia eti njia ya kawaida wamepita wengi, kwa hiyo akataka nimruhusu afungue njia yake mwenyewe, yaani kinyume na maumbile, akaniahidi kuninunulia gari lakini nilipokataa, akagoma kuniunganisha na wafadhili ambao wangenilipa ada ya chuo,” alisema dada huyo.
Kauli hizo zinatoa picha kwamba wanaume wengi wanawageuza wanawake watumwa wa mchezo huo wa kudandia ukuta kwa jeuri ya pesa. Eti, wananogeshwa na stori kwamba ndiyo mlango mdogo na unaobana kuliko ule wa kawaida. Hawazingatii athari ambazo mwanamke anazipata.

Wednesday, December 14, 2011

WABUNGE MMECHAGULIWA KUWAWAKILISHA WANANCHI NA KUTATUA KERO ZAO, JE UGUMU WA MAISHA NI KWENU TU?

Nyongeza ya posho za wabunge yaibua mjadala mzito  Send to a friend
Wednesday, 14 December 2011 10:45
0digg
Na Joyce Mmasi
NYONGEZA ya posho za wabunge imekuwa gumzo na kuzua mijadala isiyo na kikomo katika jamii ya Tanzania.
Tofauti na mijadala ya awali ya kupinga ama kuiunga mkono, sasa kinachojadiliwa ni kauli tata za viongozi waandamizi wa bunge juu ya jambo hilo.
Kauli tata ni zile za Spika wa Bunge, Anne Makinda na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah ambazo zimeonekana kutofautiana kana kwamba zimetolewa na watu wasiofanya kazi katika taasisi moja.
Utata huu unatokana na ukweli kuwa viongozi hao wanatoa majibu yanayotofautiana kuhusiana na suala moja.
Viongozi hao ambao wanafanya kazi katika ofisi moja wamezua maswali kufuatia kutoa matamko tofauti kuhusiana na suala moja ambapo wakati mmoja anapinga habari ya kuwapo kwa nyongeza hiyo ya posho kwa wabunge mwingine anaibuka na kueleza kuwa nyongeza inayozungumzwa ipo na imefanywa kwa makubaliano baina ya ofisi, serikali na wabunge wenyewe.
Mparaganyiko huo wa mawazo unatokana na taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu kuongezeka kwa posho za wabunge kutoka Sh70,000 hadi 200,000 kutwa hivyo kufanya bajeti ya posho hizo kwa mwaka kufikia Sh28 bilioni.

Kutokana na ongezeko hilo, kila mbunge atakuwa akilipwa Sh 80,000 kama posho ya kujikimu (per diem) anapokuwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao,  Sh200,000 na mafuta ya gari Sh50,000 kila siku, sawa na Sh330,000 kwa siku huku mshahara jumla kabla ya makato ukielezwa kuwa ni sh 2.3 milioni.

Kauli tata za viongozi
Kwa mujibu wa Dk Kashillilah, mapendekezo ya kutaka posho za wabunge zipande, yaliibuka katika mkutano wa wabunge mjini Dodoma Novemba 8 mwaka huu, lakini hadi wakati anatoa tamko anasema yalikuwa hayajaanza kutekelezwa.
Siku kadhaa baadaye, Spika wa Bunge, Anne Makinda akaibika na kauli inayoonekana kupingana na ile ya katibu wake na akakiri kuwa ni kweli posho za wabunge zilikuwa zimeongezeka kutoka Sh 70,000 hadi Sh 200,000 kwa kikao na zilikuwa zimeanza kutumika.
Mbunge huyu alikuwa anapata Sh 70000 kwa hiyo tumemwongezea Sh130,000 na hupati 'unless' (isipokuwa) umefanya kazi ya Bunge na umesaini asubuhi na jioni hujafanya hivyo hupati hizo hela, anasema Makinda katika kauli inayokinzana na ile ya Dk Kashillilah ambaye wanafanya kazi katika ofisi moja.
Utata huu wa kauli toka kwa watendaji wakuu wa taasisi hii nyeti ya Bunge ndio ulioongeza kasi ya mjadala wa nyongeza za posho za wabunge. Waliopata fursa ya kuchangia wanahoji sababu ya kukinzana kwa majibu katika suala nyeti kama hilo.
Wengine wanaenda mbali zaidi kwa kusema utata huo unaonyesha ni jinsi gani suala hilo lilivyo tata na ambalo huenda likawa halikuwa na ‘baraka’ hata na baadhi ya watendaji hao na kwamba utekelezaji wake huenda umepelekwa haraka haraka bila kupata baraka za wahusika.
Utata huo unazungumziwaje?
Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR- Mageuzi), anasema suala la kupishana kauli kwa viongozi wawili wa taasisi moja, ni udhaifu mkubwa kwa taasisi hiyo. 
Suala la posho linatakiwa litazamwe upya katika mihimili yote ya dola, panapokuwa hakuna kanuni ya kuweka uwiano miongoni mwa mihimili hii, kunasababisha manung’uniko na malalamiko kwa wananchi, inatakiwa itazamwe upya,  hili suala la posho lipatiwe ufumbuzi kabisa,” anasema Kafulila. 
Kwa upande wake, Profesa Ruth Meena ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii na msomi aliyebobea anasema ni jambo la kusikitisha kuwa viongozi wa bunge wanapishana kauli juu ya suala hilo la posho.
Inasikitisha sana hawa wawakilishi wetu kujiongezea posho wakisema kuwa gharama za maisha zimepanda, kwenye hali kama hii ya sasa hakuna njia yeyote utakayo weza kutumia kuhalalisha ongezeka kama hili,  anasema.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia anasema mfumo mzima wa utoaji wa posho nchini ni wa kifisadi.
Mbatia anasema ipo haja ya kuutizama upya mfumo huo ambao umeacha pengo kubwa kati ya mwenye nacho na asiyekua nacho.
Jambo hili halitendi haki kwa watanzania, linaweka tofauti kubwa kati ya wenye nacho na wasiokuwa nacho hii si sawa, mfumo mzima wa utoaji posho unatakiwa kutizamwa upya, anasema.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mkoani Kagera, Dk Methodius Kilani anasema ongezeko hilo la posho limekuja ghafla na kwamba kiwango hicho ni kikubwa na hakiendani na hali halisi ya uchumi wa nchi.
Watanzania wengi wanalalamika maisha magumu sasa Wabunge wanapoongezewa posho kwa kiwango kinachofikia Sh 200,000 watambue kwamba kuna wananchi wanaohitaji msaada, hizo nyongeza za posho zingeweza kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine ambapo ongezeko la posho hizo zingeweza kuwasaidia anasema Askofu Kilaini.
Kwa upande wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Alhad Mussa Salum  anasema kwamba haoni tatizo posho za wabunge kuongezeka na kwamba  kutokana na majukumu yao mazito ya kuwahudumia wananchi.
Ni jambo jema lakini wabunge watambue kwamba wananchi waliowachagua wana matatizo mengi ya kiuchumi sasa wanaposikia wabunge wameongezewa posho lazima nao watahoji lakini kinachotakiwa ni kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kutatua matatizo ya wananchi wao”anasema Sheikh Alhad.
Lakini, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema)  anasema ongezeko hilo ni batili kwa sababu halina baraka za Rais Jakaya Kikwete.
Spika wa Bunge anajua kwamba posho zote hulipwa baada ya rais kuidhinisha. Anasema ongezeko la posho halikuidhinishwa kwakuwa uthibitisho wa kuidhinisha ni Masharti Mapya ya kazi kwa wabunge ambayo hayajatolewa na Ofisi ya Rais.
Anasema kitendo cha kuanza kulipa posho mpya bila masharti mapya ya kazi za wabunge ni kukiuka sheria ya utawala wa Bunge kifungu cha 19 na kwamba kutokana na hali hiyo, Tume ya Bunge inapaswa kuwajibika kwa kutumia vibaya mamlaka yake.
Anapendekeza posho mpya zifutwe na zilizolipwa zirejeshwe mara moja kwani zimelipwa kinyume na sheria. “Spika anapaswa kuheshimu sheria ambazo Bunge limepitisha na kwenda kinyume na sheria kwa makusudi ni kosa la kuvuliwa uspika, anaeleza.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo,  John Mnyika (Chadema) anasema ongezeko hilo linatakiwa kusitishwa kwa kuwa mchakato wake umefanyika kinyume na taratibu.
Anasema kauli ya Spika Makinda kwamba nyongeza hiyo inatokana na kupanda kwa gharama za maisha mkoani Dodoma haina ukweli, wala mantiki na ina mwelekeo wa upendeleo

SERIKALI IKITAMBUA MCHANGO WA WALIMU,ITAWAJALI HATA KWA MASLAHI

CWT: Hakuna mwalimu aliyelipwa mpaka sasa  Send to a friend
Tuesday, 13 December 2011 19:45
0digg
Rais wa CWT, Gratian Mukoba
Pamela Chilongola
CHAMA Cha Walimu Tanzania (CWT), kimesema hakuna mwalimu yoyote aliyelipwa malimbikizo ya stahili mbalimbali na mishahara kama ilivyotangazwa  na baadhi ya vyombo vya habari.

Juzi Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philip Mulugo alipozungumza na gazeti moja la kila siku siyo Mwananchi, alisema Novemba, mwaka huu, serikali ilikuwa imelipa Sh29 bilioni, kati ya Sh49.6 bilioni zinazodaiwa na walimu. Lakini jana Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema: “Hadi leo (jana) hakuna mwalimu yeyote ambaye alikuwa amelipwa malimbikizo ya stahili zao au mishahara yao.”

Alisema tangu Juni mwaka huu, CWT na Serikali wamekuwa na vikao kadhaa kuhusu madai hayo.

“Sisi tunadai mishahara yetu  tuliyodhulumiwa, tunakandamizwa sisi walimu tunashangaa badala ya kutulipa hela tunazodai, tunashangaa kusikia wabunge wameongezewa posho na vitu vingine ambavyo vimefikia Sh330,000 milioni.“Msimamo wetu wa kugoma Januari mwakani uko palepale, hivyo hakuna mtu ambaye atatulaumu,  imeshapita miezi mine, serikali haijafanya kitu chochote kuhusu sisi walimu,”alisema Mukoba.

Alisema madai hayo yanawahusu walimu zaidi ya 3,000 ambao hawajalipwa kuanzia mwaka 2008.Mukoba alisema kero nyingine ambayo itawafanya wagome ni walimu walioshushwa vyeo mwaka 2007 na kutopandishwa mpaka sasa.“Na hii imetokana na waraka kandamizi uliotolewa na serikali mwaka 2007 ambao uliwashusha vyeo baada ya kujiendeleza kielimu.

“Serikali ilikubali kuufuta waraka huo baada ya kuridhika kwamba ulikuwa unawakandamiza walimu, lakini hadi sasa unaendelea kutumika, haujafutwa,” alisema Mukoba.   
Alisema kuna walimu ambao wanapata mishahara inayolingana na kwamba haijarekebishwa. “Utakuta mwalimu anaanza kazi anakuwa sawa na yule mwalimu aliyeanza muda mrefu.“Utakuta mwalimu amepanda daraja, lakini mshahara wake haujarekebishwa huku akiendela kupokea mshahara wa zamani,”alisema Mukoba

NDANI YA CUF KWAFUKUTA, USHIKIANO WAO NA CCM BUNGENI NDIO CHANZO

Vita ya Seif, Hamad Rashid yavuta kasi  Send to a friend
Tuesday, 13 December 2011 20:39
0digg
Maalim Seif Shariff Hamad
KAMATI YA MAADILI YAINGILIA KATI, KUWASHUGHULIKIA WANAOKIUKA TARATIBU
Geofrey Nyang’oro
CHAMA Cha Wananchi (CUF), kimetoa tamko kuhusu vurugu zilizofanywa na wafuasi wake katika mikutano ya mbunge Wawi, Hamad Rashid Mohamed, huku kikipanga kumuita mbunge huyo mbele ya Kamati ya Maadili ili ajibu tuhuma za kukiuka taratibu za chama.Desemba 11 na 12 mwaka huu, wanachama wa CUF wamekuwa wakipambana kwa kutumia silaha za jadi yakiwamo mapanga katika mikutano iliyoitishwa na Hamad Rashid kwenye matawi ya chama hicho, Kata ya Manzese, huku tukio la juzi katika tawi la Chechinya, likisababisha umwagaji damu.

Jana akizungumzia vurugu hizo makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam,  Naibu katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro alisema kitendo kilichofanywa na mbunge huyo ni kinyume na taratibu za chama.

Mtatiro alisema  Hamad Rashid  ameungana na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho kuendesha mikutano hiyo kinyume na taratibu.

“Ifahamike kuwa haya yanayoendelea si sahihi. Chama chetu kina namna ya kipekee ya kutafuta uongozi. Hii ya Hamad Rashid  ni zaidi ya kutafuta ukatibu mkuu, ni njia ya kuua chama. Hatuwezi kutafuta ukatibu mkuu kwa njia ya umafia,”alisema Mtatiro.

Mtatiro alisema kutokana na vitendo hivyo, CUF inatarajia kumchukulia hatua mbunge huyo kwa mujibu wa taratibu zake. Katika hatua za awali, mbunge huyo pamoja na wenzake wanaomuunga mkono wataitwa kwenye Kamati ya Maadili na Nidhamu  wakati wowote kuanzaia sasa kwa ajili ya kuhojiwa.

Alisema baada ya mbunge huyo na washirika wake  kuhojiwa, taarifa zitapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya chama ambayo itaamua hatua za chukua  dhidi yao.
“Siwezi kusema ni hatua gani zitachukuliwa, sababu katika hili mimi sijui na wala Seif Shariff Hamad hajui, ila chama ndio kitakachotoa maamuzi kwa mujibu wa katiba,”alisema Mtatiro.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za CUF, mikutano inayofanywa na Hamad siyo halali . Akasisitiza, “huwezi kufanya mikutano bila  kuwajulisha makao makuu ya chama, ofisi za mikoa na wilaya unakokwenda kufanya mkutano ua ziara”.

“Mimi Mtatiro pamoja na nafasi yangu siwezi kuondoka hapa na kwenda Wawi Pemba kufanya mikutano bila ya makao makuu ya CUF kujua na pia ofisi za mikoa na wilaya katika eneo husika. Ni lazima kutoa taarifa,”alisisitiza Mtatiro huku akitolea mfano ziara inayofanywa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif

“Ni kweli anataka ukatibu, kumekuwa na vitisho, lengo nini ni kuua chama! Lakini, Hamadi fedha anapata wapi? Uchaguzi tunafanya 2014, kwanini iwe sasa?,”alihoji Mtatiro.

Hamad Rashid akana
Gazeti hili lilipomtafuta Hamad Rashid kuzungumzia hatua hiyo ya chama chake, alisema "Mtatiro aeleze kwa nini alituma vijana kwenda kuvuruga mkutano wangu juzi badala ya kuleta bla bla."

Alisema awali mkutano wake ulitawaliwa na amani na alipokewa na viongozi wa chama katika tawi hilo na kupelekwa sehemu ya mkutano bila tatizo.

“Aulizwa kama ni haki kwa walinzi kuvamia mkutano wa wananchi, wakiwa na mapanga na sime kwa ajili ya kufanya vurugu ,“alisema.

Mbunge huyo alisisitiza kwamba  hajafanya kosa kwa kuamua kufanya ziara na mikutano ya hadhara bila kutoa taarifa kwa uongozi wa chama na kuongeza,   "Kama viongozi hao wa makao makuu wanaona taratibu zimevunjwa, walistahili kuniandikia barua ya kuniita na kunihoji. Sio kutuma vijana wa Blue guard  kwenda kuzuia mkutano."
Vurugu za juzi
Mtatiro alimtuhumu Mbunge huyo kuwa aliandaa vurugu kwa kukodi vijana zaidi ya 100, kutoka katika eneo la Nakos ambao ni wafuasi na wapenzi wa CCM.

Alisema vijana hao walipewa kazi ya kushambulia hata kwa kuua endapo wangewaona walinzi wa chama hicho maarufu blue guard.
Kuhusu walinzi kufika katika eneo hilo, Mtatiro alisema walikuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku ya kufuatilia na kujua kila kinachoendelea katika chama hicho na pia moja ya kazi yao ni kuhoji jambo lolote linalofanywa kinyume na taratibu za chama.

“Hawa walinzi wa CUF walifika katika eneo hilo baada ya kusikia kuna mkutano unaofanyika kinyume na utaratibu wa chama. Hawa kazi yao ni kuhoji wahusika na kukusanya taarifa za kwanini watu wamekiuka taratibu kisha  kuziwasilisha kwenye ofisi za chama kwa ajili ya hatua zaidi,”alisema Mtatiro.

Alisema walipofika na kuanza kazi, ghafla walivamiwa na kundi la vijana zaidi ya 100 wakiwa na silaha za mapanga na marungu na kuanza kuwashambulia na kusababisha walinzi wanne na baadhi ya wanachama kujeruhiwa.
Ushuda wa majeruhi
Katika hatua nyingine, walinzi wawili walionusurika kifo katika mapambano hayo ya juzi;  Abdallah Kassim na Hamis Idd wakiwa na majeraha ya mapanga mmoja kichwani na mwingine  shingoni, walifika kwenye mkutano huo wa Mtatiro na waandishi wa habari na kueleza kilichotokea juzi.

Akizungumzia tukio hilo, Kassim ambaye alikuwa ameshikilia RB yenye namba MAG/RB/22150/2011 aliyoifungua katika kituo cha polisi Magomeni,  alisema ni Mungu tu ndiye aliyemuokoa.

“Sisi tulisikia kuna mkutano unafanyika kinyume na utaratibu wa chama eneo la Chechnya , tulikuwa walinzi 8, tulichukua gari na kwenda eneo la tukio. Tulipofika wenzetu waliingia ndani kwa lengo la kutaka kujua kinachoendelea ndipo tulipovamiwa,”alisema Kassim.

Alifafanua kwamba, kundi la vijana wakiwa na mapanga, Sime na marungu walianza kwa kutaka kutoa upepo gari walilokwenda nalo.

Kassim aliyekatwa panga shingoni, alisema wakati akifanyiwa unyama huo nyuma yake kulikuwa na kijana aliyetaka kumkata na panga kichwani lakiin mlinzi mwenzake akadaka mkono wa kijana huyo na kumuokoa.
“Panga hilo lingenikata sijui kama ningekuwa hai mimi, yaani ni Mungu tu alininusuru na kifo, ” alisimulia  Kassim kuhu akiwa na jereha  shingoni na kueleza kuwa anakabilia pia na maamivu mbavuni.
Naye Hamiss Idd aliliambia Mwananchi kuwa, tukio hilo na la hatari ambalo kamwe hakulitegemea na tayari ameshonwa nyuzi nne.

Alisema vijana hao waliowakata mapanga pia waliwapora  vitu vyote, walivyokuwa navyo pamoja na simu nane na kwamba yeye binafsi aliporwa  fedha tasilimi Sh 35,000.

Tuesday, November 22, 2011

Katiba: Chadema yataka kukutana na Kikwete


 Send to a friend
Monday, 21 November 2011 18:42
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe ,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maamuzi ya kamati Kuu ya chama hicho juu ya Muswada wa Katiba mpya jijini Dar es Salaam jana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Willibrod Slaa.Picha na Fidelis Felix
Geofrey Nyang’oro na Keneth Goliama
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda kamati ndogo ya watu sita kwa ajili ya kwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete kuwasilisha madai yake juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, uliopitishwa bungeni juma lililopita.

Kamati hiyo imeundwa katika mkutano wa dharura wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, uliofanyika Dar es Salaam juzi ili kukutana na Rais Kikwete kumjulisha kile walichoeleza kuwa upungufu wa muswada huo na kisha kumtaka atafakari kama ausaini kuwa sheria au la.

Akisoma tamko hilo kwa vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe alisema kamati hiyo ya watu sita, inafanya taratibu za kumuona Rais Kikwete wakati wowote kuanzia sasa.

Mbowe alisema kamati hiyo itaongozwa na yeye, Katibu Mkuu Dk Willbrod Slaa, Makamu Mwenyekiti (Bara) Said Arfi na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed. Wengine ni Mshauri wa Masuala ya Siasa wa chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Abdallah Safari na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye pia atakuwa katibu wa kamati hiyo wakati wa mkutano huo.
“Hivi sasa taratibu za kumuona Rais zinaendelea, tutamuona wakati wowote kuanzia sasa na kumweleza mapendekezo yetu juu ya upungufu uliomo kwenye muswada wa sheria hiyo na kama atatusikiliza tutashirikiana naye akikataa tutawaeleza wananchi hatua za kuchukua,” alisema Mbowe.

Alisema ushiriki wa Chadema katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya utategemea mazungumzo hayo akisema hiyo ndiyo fursa pekee inayoweza kutumika licha ya muswada huo kupitishwa ‘kibabe’.

“Bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja ya nia na mchakato na misingi ya Katiba Mpya, Kamati Kuu imesikitishwa na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete badala ya kuzitumia fursa hizo amejiingiza kwenye upotoshaji uliofanywa na wabunge wa chama chake juu ya misingi na maudhui ya sheria hiyo,” alisema Mbowe na kuongeza,

“Kamati Kuu inaamini badala ya kuwaunganisha Watanzania na kujenga muafaka wa kitaifa unaohitajika katika kuandika Katiba Mpya, hotuba ya Rais Kikwete kwa wazee wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam imezidi kuwagawa wa Tanzania kwa misingi ya ushabiki wa vyama vya siasa kitendo hiki ni hatari kwa Taifa.”

Alisema Katiba si mali ya viongozi wala wanasiasa, bali ni ya wananchi inayohitaji mchango mpana wa maoni yao juu ya kuunda sheria itakayokusanya maoni na hata kuundikwa kwake.

Alisema Chadema kitaendelea kuwaelimisha wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na umuhimu wa kuwa na sheria bora itakayoratibu uundwaji wa tume ya kukusanya maoni.
Chama hicho kimewaagiza wabunge na viongozi wake kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya sheria hiyo na madhara yake.

Yalia na Polisi

Kamati Kuu ya Chadema pia imelaani kitendo cha Serikali kukizuia chama hicho kufanya mikutano na maandamano nchi nzima kwa kile ilichodai ni kukinyima haki ya kikatiba ya kufanya shughuli zake.

“Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya Chadema na maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga mchakato uliopitishwa kuwa  sheria siyo tu kwenda kinyume na haki za msingi za kikatiba, bali pia unahatarisha amani na utulivu wa nchi,” alisema Mbowe.

Aliitaka Serikali kutoa tamko la kufuta amri hiyo huku akisisitiza kuwa Chadema kitaendelea kutumia njia zote za amani zilizopo ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyoainishwa katika Katiba ya sasa.

Kwa nini waligoma?
Awali, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alitaja sababu saba zilizowafanywa wasusie mjadala huo ikiwamo kukiukwa kwa Kanuni za Kudumu za Bunge wakati wa uwasilishwaji muswada huo.

Alisema Kamati ya Bunge iliingiliwa kazi zake kwa kuzuiliwa kukusanya maoni katika kanda 10 kama ilivyokuwa imepanga na badala yake maoni yakakusanywa kinyume na utaratibu na kuingizwa kwenye muswada huo.
Aliishutumu Serikali akidai kuwa iliingilia mchakato huo kwa kumtumia Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Akizungumzia hatua ya wabunge hao kususa, Dk Slaa alisema kamati ilipongeza hatua hiyo akisema ulikuwa uamuzi wa kijasiri uliowafanywa wasiwe sehemu ya kupitishwa sheria mbovu.

“Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa Chadema kwa kususia vikao vya kupitisha sheria hiyo kwani ushiriki wao ungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii, sheria ambayo haikuzingatia nia ya haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya,” alisema.

Wabunge wa Chadema na wenzao wa NCCR-Mageuzi, walisusia kikao cha Bunge kilichojadili na kupitisha Muswada wa Sheria mpya ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.

HALI SI SHWARI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

CCM kwachafuka Send to a friend
Monday, 21 November 2011 18:54
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa, wakifurahia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
UVCCM WAPANGA KUASI, NI HOFU YA KUFUTWA KWA UMOJA WAO
Neville Meena, Dodoma
HALI imezidi kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kundi kubwa la Umoja wa Vijana wa Chama hicho (UVCCM), linadaiwa kupanga mkakati wa kuasi, endapo mkakati unaodaiwa kuandaliwa wa kuuvunjwa umoja huo utafanikiwa.Hatua ya viongozi wa UVCCM kutoka karibu mikoa yote nchini kukusanyika mjini Dodoma kufanya kile walichokiita kuwa ni “kupigania umoja wao na chama chao,” imezidi kuchafua hali ya hewa.

Taharuki ndani ya chama hicho tawala imekuja kipindi ambacho vikao vikuu vya chama hicho ambavyo ni Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), vinakutana chini ya mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kamati Kuu ilianza jana saa 8:00 mchana pasipo Rais Kikwete kutoa maelezo yoyote ya ufunguzi. Kilitanguliwa na kikao cha Kamati ya Maadili kilichoanza juzi na kumalizika jana asubuhi, pia kikiongozwa na Kikwete.

Juzi usiku, wenyeviti wa UVCCM kutoka mikoa 18 nchini walikutana katika ukumbi wa baa moja maarufu iliyopo eneo la Area D mjini hapa kupanga mikakati jinsi ya kuuokoa umoja wao usivunjwe na hatua za kuchukua iwapo azma hiyo itatekelezwa.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya washiriki wa kikao hicho zinasema, moja ya maazimio ni kwamba ikiwa UVCCM utavunjwa, basi watahamia vyama vya upinzani, huku wakikitaja Chadema kuwa ni mahali panapowafaa kwa ajili ya kuendeleza harakati za ukombozi wa nchi.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM na wale wa Baraza Kuu, kiliweka msimamo wa kutetea kuendelea kuwepo kwake kwa gharama yoyote, hata ikiwa ni kuwafungia ndani wajumbe NEC ya CCM iwapo wataridhia kufanya hivyo.

Kauli za viongozi
Hata hivyo, mmoja wa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM ambaye hakupenda kuandikwa jina gazetini alisema hakuna mpango wa kufuta UVCCM na kuziita taarifa hizo kuwa ni za kupika.

Kauli yake iliungwa mkono na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye alisema: “Hakuna kitu kama hicho, mimi ni mshiriki wa vikao vyote vya Sekretarieti hakuna ajenda hiyo kwenye vikao vyetu hivi.”

“Ndiyo maana kwenye mkutano na waandishi wa habari nimesema kwamba watu waache kupandikiza vitu ambavyo kimsingi havipo, vikao hivi ni vya kawaida na ajenda zimewekwa wazi, sasa kama kuna watu wanaleta hizi hoja, basi wana malengo yao tu.”

Mapema Nape akizumgunza na waandishi wa habari alisema kumekuwapo na taarifa nyingi zinazowafanya Watanzania kutaharuki kana kwamba kuna vita inayotarajiwa kutokea mjini hapa.

“Naomba wanahabari wenzangu, nisaidieni maana haya yote yanatokana na taarifa zinazoandikwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari, lakini ajenda zetu kama nilivyosema jana (juzi) zinafahamika, kubwa ni kupitia utekelezaji wa mabadiliko ndani ya chama chetu,” alisema Nape.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema hana taarifa zozote kuhusu kuwepo kwa mpango wa kufutwa kwa umoja huo ambao yeye ni mtendaji wake mkuu na kwamba hata katika kikao cha sekretarieti ambacho yeye ni mjumbe hakukuwa na ajenda ya aina hiyo.

Hata hivyo, Shigela hakuwa tayari kuweka bayana iwapo alifahamu mkusanyiko wa viongozi wa UVCCM kutoka mikoani waliopo Dodoma, zaidi ya kusisitiza kwamba kipindi hiki ni cha kutulia kwa wana CCM kutokana na kuwepo kwa taarifa nyingine ambazo wakati mwingine vyanzo vyake si bayana.

Chimbuko la hisia
Chimbuko la hisia za kufutwa kwa UVCCM ni taarifa zisizo rasmi kutoka ndani ya vikao vya Kamati ya Maadili ambayo katika siku yake ya kwanza iliwahoji baadhi ya viongozi wake akiwamo Kaimu Mwenyekiti, Benno Malisa.

Wengi walihojiwa kuhusu utendaji wa kamati ya kutathmini upya uendeshaji wa UVCCM, ambayo tayari imefanya kazi yake katika mikoa 19 ya Tanzania Bara. Kamati hiyo inayoongozwa na Mjumbe wa Baraza Kuu ya UVCCM, Hussein Bashe, inatuhumiwa kuendesha mikutano iliyotumika kuwakashifu viongozi wa juu wa CCM wakiwamo Mwenyekiti Kikwete na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

“Kuna taarifa za uhakika kwamba ajenda hii haikupitia kwenye sekretarieti, inatoka kwenye kamati ya maadili kwa tuhuma kwamba eti sehemu kubwa ya UVCCM tuko nyuma ya kundi moja ndani ya chama,” alisema mmoja wa wenyeviti wa umoja huo na kuongeza:

“Sasa mpango wao ni kufuta viongozi wote wa kuchaguliwa na baada ya hapo waandae uchaguzi mwingine ili kuwaweka viongozi wanaowataka, sasa hili sisi tunasema hapana kama ni tatizo litatuliwe lakini wasituulie umoja.”

Mmoja wa maofisa wa CCM makao makuu alisema jana kuwa taarifa kwamba UVCCM inafutwa zimezagaa katika ofisi hizo lakini bado zilikuwa hazijathibitishwa kutokana uamuzi wa vikao vya Kamati ya Maadili kufanywa kwa siri kubwa.

Mkakati wa Kupinga
Taarifa za mpango huo ndizo zilizowatia wazimu UVCCM kiasi cha kuitana Dodoma kwa lengo la kukabiliana na NEC ikiwa ‘itathubutu’ kuubariki.

Habari kutoka ndani ya kikao cha juzi usiku zinasema wenyeviti hao walikubaliana kwa kauli moja kuwaita wenyeviti wa wilaya wa umoja huo wa vijana ili kuongeza nguvu za kuwakabili wakuu wa CCM.

Mmoja wa wenyeviti kutoka mikoa ya Kanda ya Mashariki alisema juzi usiku kwamba: “Katika hili tumejipanga, tunao vijana zaidi ya 300 wapo kambini, tutawaleta hapa, tutaungana nao kupinga uamuzi huu.”

Harakati za UVCCM zinakwenda sambamba na kupinga utekelezaji wa mpango wa kujivua gamba ambao wanasema unatekelezwa kwa upendeleo ukiwalenga baadhi tu ya watu.

Mmoja wa viongozi hao alinukuliwa na chanzo chetu akisema wanaopaswa kufukuzwa au kuchukuliwa kwa hatua na CCM ni makada ambako Rais Kikwete alipata kura chache wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Kwa mantiki hiyo, vijana hao walisema mpango wa kujivua gamba hauna tija kwa sasa kwani unakigawa chama na kwamba CCM kina matatizo makubwa zaidi kinayopaswa kushughulikia badala na siyo kuchochea chuki miongoni mwa wanachama wake.

Maazimio ya NEC
NEC inakutana miezi minne tangu kilipokutana mara ya mwisho na kutoa maazimio ambayo yalisababisha mmoja wa makada wake, Rostam Aziz kujiuzulu ubunge katika Jimbo la Igunga pamoja na ujumbe wa NEC.

Rostam katika kujiuzulu huko aliitupia lawama sekretarieti ya chama hicho kwa kile alichokiita kuwa ni kuendesha siasa chafu dhidi yake na kuwataja kwa majina Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, John Chiligati na Nape kuwa wahusika.

Kujiuzulu kwa Rostam ni miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi katika mjadala wa CC na NEC.

Katika mazingira hayo, kuna kila uwezekano wa kutathmini jinsi falsafa ya kujivua gamba ilivyotekelezwa. Kuna madai kwamba Sekretarieti inayoongozwa na Mukama nayo imegawanyika katika suala la utekelezaji wa uamuzi wa NEC, hali inayoongeza sintofahamu ndani ya chama hicho.