Kuna upotoshaji mkubwa sana unafanyika hivi sasa ambao unafanyika katika namna ya hatari sana, naiweza kuifafanisha namna hiyo sawa sawa na mtu anaesema moto ni joto au upofu ni usingizi. Wanasiasa waliomadarakani wanajaribu kuyawekea mahitaji ya wananchi dhana ya kisiasa.
Wakati wananchi wanasema tunataka Mfumo bora wa elimu watawala wanasema CHADEMA haiwezi kuuleta, sababu DR SLAA Aliiba pesa kanisani.
Wananchi wanasema tunataka mfumuko wa bei udhibitiwe, watawala wanasema CHADEMA haiwezi kudhiti mfumuko wa bei sababu MBOWE ni DJ
Wananchi wanasema tunataka huduma bora za afya, watawala wanasema, DR Slaa anampenda sana Josephine.
Wananchi walia wanakufa njaa, watawala wanasema, CHADEMA ni chama cha Kichaga.
Wananchi wanapiga kelele wanalalamika mariasiri za Taifa letu zinanufaisha wachache na nyingi zinaibiwa na wageni, watawala wetu wanasema Ushindi ni Lazima.
Naomba tukumbushane historia mbichi kabisa, waliomfurumusha Hussein Mubarak kutoka Madarakani sio wanasiasa, Kijana aliyejichoma moto tunisia na kuacha laana nyuma yake hakuwa analalamikia wizi wa kura, waliomkamata Gadafi kwenye mtaro wa daraja walikuwa hawajebaba bendera ya chama chochote kile cha siasa, Hata sasa huko Siria wananchi hawapiganii kuundwa katika mpya wala kuwa na tume huru ya Uchaguzi.
Wito wangu kwa viongozi wa CCM ni huu ufuatao.
Kwanza, kuna ushahidi wa kutosha kwamba hivi sasa duniani, mabadiriko yanatokea kwa kasi ambayo haijawahi kutokea huko nyuma katika kila nyanja ya maisha.
Pili na mwisho, Muda si mrefu watanzania watagundua kwamba wanachokihitaji sio katiba mpya na wala sio tume huru ya uchaguzi wala sio maridhiano ya kitaifa ya namna yoyote ile wala sio ushindi wa wagombea wao.
Narudia tena, Punde kidogo, upepo wa mabadiriko utabidiri mkondo wake, watu watakapoamua kuweka magwanda na kuachana na ustaarabu wa kuonyeshana alama ya V sijui mtawaambia nini