Tido Mhando afungua ukurasa wa adhabu hizo:
“Ninampango wa kurudi kijijini kwangu Tanzania,na kushirikiana na wanakijiji wenzangu katika shughuri za maendeleo” hiyo ilikuwa ni kauri yake Tido baada ya kuulizwa na mtangazaji wa shirika la utangazaji la uingereza(BBC) anatarajia kufanya nini baada ya kustaafu kazi yake ya utangazaji (BBC). Binafsi namuona Tido kama muungwana aliyekuwa tayari kushirikiana na watanzania wenzake katika kuleta maendeleo na ndio maana pamoja na pesa nyingi alizopata mara baada ya kustaafu BBC lakini alikubari kutoa mchango wake wa uzoefu katika nchi yake, nasema Tido ni muungwana na mzalendo kwa kuwa hakutaka kubaki ughaibuni ambapo angepata kazi za mkataba na kupata mapesa mengi lakini akakubali kurudi Tanzania.
Mchango wa Tido unaonekana katika kulibadirisha television ya taifa(TVT) na kuwa Shirika la utangazaji la tanzania(TBC) ambayo imejiongezea watazamaji wengi si Tanzania tu bali hata nje ya nchi, TBC imeweza kuondoa mtazamo wa watanzania wengi ambo awali walikiona chombo hicho kama cha chama kinachoongoza dola, TBC chini ya uongozi wake Tido hakika imekuwa kama chombo cha umma na si chombo cha ccm,hii imechangiwa na msimamo thabiti wa mkurugenzi wake ndugu Tido ambaye aliruhusu habari kurushwa pasipo upendeleo wa chama chochote cha siasa, dini, kabila na mahali.
Enzi za TVT mchakato majimboni uliosusiwa na wanaccm na ambao umekigharimu sana chama hicho na kupoteza viti vingi vya ubunge, usingeweza kuoneshwa kama ulivyooneshwa na TBC, huo ni mfano tosha kwamba ndugu Tido alikuwa jasiri ambaye hakumugwaya hata bosi wake aliyempa ukurugenzi.
Leo kumekuwa ni mijadara mbalimbali mara baada kuona kichwa cha habari katika gazeti moja la kila siku likinadi kuwa Tido mhando ametimuliwa, mtangazaji wa leo wa jambo Tanzania Raheli MHANDO wa TBC hakuweza kusoma habari hiyo pamoja na mesaji nying tulizo mtumia kumtaka atufafanulie kuhusu habari hiyo! Wengi tunajiuliza je, mchango wa Tido katika TBC ulikuwa unapingwa hata na wafanyakazi wenzake wa TBC? Je mwajiri wa Tido ameona Tido hajafanya lolote katika kukiendeleza chombo hicho cha umma? Je Tido amekamatwa mchawi kwa CCM kupoteza viti vya ubunge na udiwani? Je Tido ni kigogo wa kwanza aliyefungua ukurasa wa adhabu dhidi ya waliochangia ccm kupoteza viti vya ubunge kwa kuruhusu mchakato majimboni? Maswali hayo tumekosa majibu yake kabisa kwa kuwa Tido kwetu sisi watazamaji wa TBC na wapenda habari zisizoegemea upande wowote, amekuwa ni shujaa wa kipekee ambaye hana hudi kupongezwa kwa kukuza democrasia hapa Tanzania na nchi za jilani kupitia TBC!
Hivi mcango wa Tido hauonekani mpaka kufikia hatua ya kufukuzwa kama mbwa ambaye hana uwezo wa kubweka au ubwa mla kuku wa kufugwa? Ugumu ulikuwa wapi kumuongezea muda wa miaka miwili ndugu Tido mhando ili kukamilisha mipango yake aliyokuwa nayo katika kukiendeleza chombo hicho cha umma wakati huu ambapo chombo hicho kinafanya mabadiriko ya kitechnolojia? Ndugu yangu Tido, je ulikuwa huelewani hata na wafanyakazi waliokuwa chini yako, mbona wanakwepa kuhabarisha umma habari zozote zinazokuhusu ili kuweka udharimu huo uliofanyiwa hadharani?udharimu huo uliofanyiwa ndugu yangu Tido, naufanisha na ule aliofanyiwa mhadhili wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof. Baregu ambaye naye alifukuzwa kama mbwa baada ya mkataba wake kuisha, walau yeye alipedwa na jumuia nzima ya chuo kikuu ambao walifikia hata hatua ya kugoma ili kushinikiza Proffesa huyo masuala ya siasa arudishwe chuoni hapo.
Tukifuata ule usemi unaosema ukiona mwenzako anyoa wewe tia zako maji, basi vigogo wote ambao hawakuchangia katika kufanikisha kampeni za chama dola wajiandae kwa adhabu za kufukuzwa kama mbwa pasipo kujali mchango wenu katika taifa letu! Vigogo wa TANESCO ambao umeme ulikatika wakati wenye dola wakifanya kampeni, wakuu wa wilaya na mikoa ampapo wenye dola walizomewa na kusodolewa wakati wakifanya kampeni, na viongozi wa chama ambao hawakufanya maandalizi mazuri kuwapokea wenye dola wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kukodi piki piki na tex, nyote mjiandae kwa kuwa kigogo mwenzenu Tido wa TBC tayari amefungua ukurasa wa adhabu zichukuliwazo.
naitwa Leonard, nipo Rukwa.