Wednesday, March 16, 2011

MOJA YA MAHAFALI YA F6 NILIYOHUDHURIA

WASICHANA WALOICHANA PAPER WAPATA NAFASI SHULE ZA A-LEVEL

WASICHANA WALOICHANA PAPER WAPATA NAFASI SHULE ZA A-LEVEL  Send to a friend
Thursday, 17 March 2011 07:52
0diggsdigg
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa
Fredy Azzah
WASICHANA wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 na kufaulu kwa kupata daraja la I mpaka la III (Division One mpaka Three), wamepata nafasi za kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya Serikali, huku wavulana waliopata nafasi hiyo wakiwa ni asilimia 97. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema wanafunzi wote hao wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa Aprili tatu mwaka huu kuanza masomo.
Kwa mujibu wa Dk Kawambwa, wanafunzi waliokuwa
na sifa za kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi ni 36,990 wakiwamo wasichana 11,210 na wavulana 25,780.
“Wanafunzi 36,366 ambao ni asilimia 98.31 ya waliokuwa na sifa stahili wamepangwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi, kati yao wasichana ni 11,210 sawa na asilimia 100 ya wenye sifa na wavulana ni 25,156 ambao ni asilimia 97.58 ya wanafunzi wenye sifa,” alisema Dk Kawambwa.
Wanafunzi wa kike waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi ni asilimia 30.83 ya wanafunzi wote 36,366 waliopangwa.
Mwaka 2010 wanafunzi wa kike 12,638 walichaguliwa kuendelea na masomo, ikiwa ni asilimia 42.33 ya wanafunzi wote.
Kutokana na hali hiyo, idadi ya wanafunzi wa kike waliochaguliwa kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka huu, ni pungufu ya wanafunzi 1,428 ukilinganisha na ile ya mwaka jana.
Kwa ujumla, wanafunzi waliopangiwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi mwaka jana, walikuwa 33,662. Wasichana walikuwa 12,638 na wavulana 21,024.
Hata hivyo, Dk Kawambwa alisema mwaka 2010 wanafunzi waliochaguliwa walikuwa asilimia 83.52 ya wenye sifa, hivyo mwaka huu kuna ongezeko la asilimia 12.63, kwa awamu ya kwanza.Alisema wavulana 624 sawa na asilimia 2.42, hawakuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kutokana na sababu mbalimbali.
Alizitaja sababu hizo kuwa ni kutokuwa na uwiano wa alama za masomo (credits), alama kutotimia na baadhi kuwa na umri wa zaidi ya miaka 25.
Alisema wanafunzi 29 walikuwa na umri uliozidi miaka 25 ambao kisheria hauwaruhusu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa shule za Serikali.
Wanafunzi wengi wa kike wamepangwa kusoma masomo ya Historia, Jiografia na Kiingereza (HGL), kati ya wote waliochaguliwa wanafunzi 1,610 sawa na asilimia 14.4 walichagua masomo hayo.
Alisema wanafunzi 1,593, watasoma CBG; 1,574 watasoma HKL, 1,472 watasoma PCB, 1,108 watasoma HGK na wanafunzi 1,035 watasoma HGE.
Kwa upande wa wavulana, wanafunzi wengi wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi. 4,307 sawa na asilimia 17.1 watasoma PCM; 4,177 sawa na asilimia 16.6 wakichaguliwa kusoma PCB, 3,079 HGL, 2,722 HGK, 2,504 HKL na wanafunzi 2,249 wakichaguliwa kusoma CBG.
Wanafunzi 916, wasichana wakiwa 55 na wavulana 861 wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya vyeti katika vyuo vya ufundi vya Mbeya (MIST), Dar es Salaam (DIT), Arusha (ATC) na Chuo Maji Dar es Salaam.
Kutokana na hali hiyo, wanafunzi wa kike waliochaguliwa kusoma masomo ya sayansi na vyuo vya ufundi mwaka huu ni  4,357 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 195, ikilinganishwa na wanafunzi 4,162 waliochaguliwa kusoma masomo hayo mwaka jana.
Kwa upande wa wavulana, idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kusoma masomo hayo mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 25.9, kutoka wanafunzi 12,664 waliopangiwa kusoma masomo ya sayansi ikilinganishwa na mwaka jana ambapo wanafunzi 10,057 ndio waliochaguliwa kusoma masomo hayo.
Pia idadi ya wanafunzi hao waliopangiwa kusoma sayansi ni asilimia 50.3 ya wanafunzi wote wa kiume waliochaguliwa kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi.
Katika hatua nyingine, Waziri Kawambwa alisema wanafunzi 624 wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya ufundi, bado wana nafasi za kuendelea na masomo hayo kwa kujiunga na shule za sekta binafsi.
Dk Kawambwa pia alieleza kuwa wanafunzi ambao bado Baraza la Taifa Mitihani (Necta), halijatangaza matokeo yao, pindi yatakapotoka na kama watakuwa na sifa zinazotakiwa, watachaguliwa kujiunga na shule au vyuo vya ufundi.
Dk Kawambwa aliwataka wakuu wa shule zisizokuwa za Serikali kuwasilisha majina ya wanafunzi wa kidato cha tano waliojiunga na shule zao ili kuiwezesha  wizara yake kuwa na kumbukumbu sahihi.
Waziri huyo alitoa angalizo kuwa mtindo wa wazazi kuomba uhamisho wa watoto wao kabla ya kuripoti katika shule walizopangwa, safari hii hautakubaliwa kwa kuwa wizara hiyo imewapanga wanafunzi katika shule walizoomba.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Thursday, 17 March 2011 08:05
 

Comments 

 
0 #1 ANOLD MADANDI 2011-03-17 08:42
ushauri toeni nafasi kwa wavulana na wasichana wafanye mitihani tena ili waweze kuongezwa ktk vyuo vya ufundi vilivyoko hapa inchini kwani wanahitajika sana nchini iwe na wataalam wengi ahsante
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!

ELIMU KUHUSU KATIBA KWA WATANZANIA



Katiba iweke misingi ya usawa na fikra za utaifa  Send to a friend
Wednesday, 16 March 2011 00:00
0diggsdigg
Na Charles Kayoka
HIVI karibuni, hasa wakati na baada ya uchaguzi, gumzo juu ya udini katika siasa limeibuka na limekuwa moja ya mada katika mikutano ya CHADEMA. Niliona bango moja katika maandamano likisomeka, “Udini ni ghilba za Wanasiasa.” Nami nakubaliana na maelezo hayo ya kuwa wanasiasa wanapoona wanashindwa kupata uhalali wa kutawala wanakimbilia makundi yao ya kiimani kuomba msaada kwa kisingizio kuwa watu wa imani ingine- imani pinzani, hawamtaki kwa sababu ya kuwa wa imani tofauti.

Hili huweza kupata mashiko kama watu wa dini husika hawana uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu. Ndio maana udini unaweza kuwa ni ghilba tu ya wanasiasa kuomba msaada wa kundi.

Lakini kwa Tanzania udini katika siasa hauwezi kuelezeka kwa kauli rahisi namna hii! Udini ni matokeo ya matumizi ya makusudi ya nguvu za kundi ili kujijengea uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani na pia kutumika kama ajenti wa kuwasaida watu wa kundi lako kwa sababu wamekutuma ufanya hivyo, au unahisa una wajibu wa kufanya hivyo.

Kumekuwa na madai ya namna hiyo dhidi ya uongozi tangu wakati wa Nyerere. Na hakuna Rais Tanzania aliyekwepa tuhuma za kuwa anatumiwa na dini yake. Lakini wakati huu pia tuhuma hizi aidha zinasema uongozi uliopo unatumiwa kidini au unawatuhumu wapinzani kuwa wawakilishi wa dini.

Hizi ni dalili kuwa Tanzania kama nchi imekosa itikadi unganishi ambayo ingewatambulisha viongozi kwa itikadi hiyo na tungetambuana hivyo kama raia na uongozi ungepimwa kwa utekelezaji wa itikadi husika.

Nchi inapoendeshwa kwa msingi wa fedha na mashindano katika kupata fedha na mali, ni wazi umoja utajengwa kwa msingi wa fedha na mali. Lakini kwa sababu binadamu lazima tuishi katika makundi, dini na kabila huweza kuwa moja ya makimbilio ya kujengeana umoja na kujitambua.

Lakini ufisadi unapozidi na kuwa kupata ajira, kwa mfano,kunategemea unajuana na nani, ukoo, kabila au dini, ni lazima watu watadhani kuwa ili ufanikiwe ni lazima uwe na uhusiano wa kiitikadi na anayekusadia kufanikiwa.

Udini unaweza kutokana na kukosa fikra yakinifu ya vyanzo, na katika kutatua matatizo, hasa ya umasikini. Watu wanaweza kudhani wamekuwa masikini kwa sababu tu watu wa dini fulani wanatawala badala ya kuuchungunza mfumo mzima wa uchumi unavyowafanya watu wote masikini na wachache matajiri.

Kwa kawaida huwa ni rahisi hao matajiri wachache kuwaghilibu mlio wengi kwa lugha za kuwafanya msione ukweli wa jinsi wanavyowanyonya. Na mkadhani hata ni matajiri kwa kudra ya Mwenyezi Mungu.

Lakini kutokukubali kufanya mkutano wa katiba ambako ndiko kutakapo patikana majadiliano ya namna siasa itakavyoendeshwa kunaweza kuwa moja ya chachu ya udini.

Katiba ni chombo muhimu sana katika kujenga itikadi ya umoja wa kitaifa. Wanaohofu isitengenezwe kwa mkutano wa pamoja wanaogopa kuwa ile misingi wanayoitumia sasa ya udini na ukabila itaondolewa na watawajibika kwa misingi ya usawa na fikra za utaifa. Wananchi tusidanganyike.

mohamedmusta@gmail.com This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it , 0766959349

EDWARD LOWASA IS ONE OF THE FORMER PRIME MINISTER IN TANZANIA

Lowassa apata kikombe Loliondo  Send to a friend
Tuesday, 15 March 2011 23:47
0diggsdigg
Waandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.
Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.
Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”
Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini ambao wameshafika kwa mchungaji huyo kupata tiba hiyo wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya.


Katika jitihada za kudhibiti usalama na kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma kwa mchungaji huyo bila matatizo, Serikali imeimarisha ulinzi kwa kuweka askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), katika kijiji hicho na kusimamia magari. Pia imepeleka wauguzi kusaidia wagonjwa mahututi kabla ya kumfikia mchungaji na imetoa pia jenereta kwa ajili ya kufua umemeKaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Raymond Mushi alisema jana kuwa, sasa walau hali ni nzuri kwani msongamano umepungua.

"Ni kweli sasa hali inaridhisha na jana watu wamekwenda kupata tiba na kurejea makwao mapema hili ndilo serikali inalolitaka. Tunaomba watu wanaopeleka wagonjwa wawe wanauliza kwanza hali ya msongamano," alisema Mushi.Mushi alisema inawezekana watu wanaokwenda katika kijiji hicho kusubiriana katika Mji wa Mto wa Mbu ambako kuna huduma nyingi muhimu kuliko wote kwenda huko kwa wakati mmoja.

Alitoa wito kwa watu wenye wagonjwa mahututi kuacha kuwapeleka moja kwa moja kwa mchungaji huyo kabla ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya zao.Katika hatua nyingine, wagonjwa kadhaa waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wameanza kutoroka wodini na kwenda Loliondo kupata matibabu ya magonjwa sugu yanayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwaisapile, Mwananchi imeelezwa.
Habari zilizopatikana hospitalini hapo jana zimeeleza kuwa wagonjwa hao walianza kuondoka Muhimbili juma lililopita baada ya Serikali kubariki matibabu hayo. Ofisa mmoja mwandamizi wa hospitali hiyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, amesema kuwa wakati baadhi ya wagonjwa hao wakiwa wanatoroka wodini, wengine wamekuwa jasiri kwa kuwaaga madaktari wao.
“Wagonjwa wameanza kuondoka na wengine bila hata ya kuaga, hivyo hatujui hatima yao kama watafika salama huko Loliondo,” alisema.Ofisa huyo alisema juma lililopita, mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa chumba namba 15 katika Wodi ya Kibasila, aliondoka baada ya kusikia taarifa kuhusu huduma hiyo.
“Kuna mgonjwa mmoja aliyekuwa amelazwa Kibasila Wodi namba 15 aliondoka aliposikia kuwa Babu ameanza tena kutoa matibabu hayo ambayo awali yalisitishwa,” alisema.Hata hivyo, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaisha alisema hana taarifa za kutoroka wodini kwa wagonjwa hao na kwenda kufuata tiba huko Loliondo... “Sina taarifa zozote za kuondoka kwa wagonjwa hapa hospitalini.”

Matibabu Loliondo yapandisha nauli Ubungo
NAULI za kwenda Arusha kutoka Ubungo, Dar es Salaam zimepanda kwa kasi katika siku za hivi karibuni kutokana na wingi wa wasafiri wanaoelekea Loliondo kupata tiba hiyo ya magonjwa sugu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka kituoni hapo zimeeleza kuwa, nauli hizo zimepanda kutoka Sh18,000 hadi Sh30,000 tangu juma lililopita.
Mmoja wa mawakala wa mabasi ya abiria katika kituo hicho ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema ongezeko hilo la nauli limetokana na baadhi ya mawakala kukodi mabasi na kuwasafirisha abiria.“Nikupe siri moja tu ambayo inatufanya tupandishe nauli. Lengo letu ni kupata faida, ujue sisi tunakodi basi zima kisha tunakatisha tiketi kwa bei yetu ili na sisi tupate faida,” alisema.

Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri kuelekea Arusha, Charles Manyama alisema mabasi yaendayo huko yamegawanyika katika madaraja matatu yale ya bei ya juu, bei ya kati na bei ya chini lakini kwa sasa bei imekuwa ni moja kwa mabasi yote.
Kwa mujibu wa abiria huyo, zamani nauli za Arusha zilikuwa Sh25,000 kwa basi la daraja la juu, Sh18,000 kwa mabasi ya daraja la kati na Sh15,000 kwa daraja la chini, lakini sasa mabasi yote yanatoza kati ya Sh25,000 hadi Sh30,000.“Mawakala hawa wanadhani kila mtu anayepanda magari haya anakwenda Loliondo lakini siyo kweli, wengine tuna safari nyingine kabisa," alisema Manyama na kuongeza:

"Unakuta bei zinashangaza na kupanda sana. Hata hivyo, inashangaza kuona wanadamu tunakosa utu. Watu wanakwenda kupata matibabu wanapandishiwa nauli, walipaswa kuwaonea huruma wagonjwa hawa,” alisema Manyama.Jitihada za kumtafuta Meneja wa kituo cha mabasi Ubungo ziligonga mwamba baada ya taarifa kutoka ofisi kwake kueleza kuwa alikuwa nje kikazi.

Polisi Arusha wadhibiti usafiri wa Loliondo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limeitaka Halmashauri ya Jiji la Arusha kuweka vituo vinavyotambulika kwa ajili ya wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu kwa Mchungaji Mwasapile ili kuepuka utapeli.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu kutaka kwenda Loliondo, kumezuka vituo vingi ambavyo vinaweza kuwa chanzo cha utapeli kwa watu wanaotoka mikoani."Nafahamu hili ni jambo ambalo manispaa wanahusika nalo, wahakikishe kuwa hakuna vituo visivyo rasmi ili wananchi wasije kudanganywa na watu wabaya," alisema.

Katika kituo kilichoibuka ghafla baada tiba ya magonjwa sugu kuanza kutolewa cha Chini ya Mti, kulizuka vurugu za madereva na madalali waliokuwa wakibishania kiwango cha nauli, hatua iliyosababisha polisi wenye silaha kupelekwa katika eneo hilo.
Hatua ya polisi kuonekana katika kituo hicho, ilisababisha wasiwasi kwa wananchi kuwa huenda Serikali imesimamisha utaratibu wa wananchi kwenda Loliondo, jambo ambalo kaimu kamanda huyo alilikanusha.

"Tunachokifanya ni kuweka utaratibu mzuri, polisi wanasimamia sheria. Magari mengine yanazidisha idadi ya watu na kutoza pesa nyingi zaidi. Sumatra wakisema nauli sahihi ni kiwango fulani na madereva wakizidisha basi tunawakamata," alisema.
Wananchi waliozungumza na gazeti hili bila kutaja majina yao walisema kuwa wanashangazwa na bei ya nauli kuwa juu hata baada ya Serikali na KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati kuboresha mazingira ya kuwahi kupata tiba na kuondoka kijijini Samunge.

"Mwanzoni walikuwa wanasema magari yanakaa sana huko, kwa hiyo wanafidia hizo siku za kungoja wagonjwa lakini sasa hivi ukienda leo unarudi kesho na nauli bado iko juu," alisema mmoja wa wananchi hao.Nauli ya kutoka Mjini Arusha hadi Samunge, Loliondo ni Sh100,000 kwenda na kurudi kwa magari aina ya Land Cruser ,huku nauli ya mabasi ikiwa pungufu zaidi.
Habari hii imeandaliwa na Nevile Meena, Ibrahim Yamola, Dotto Kahindi Dar na Mussa Juma, Filbert Rweyemamu, Arusha

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

KUMEKUCHA LOLIONDO NCHINI TANZANIA

Tusherehekee dawa ya Loliondo kwa hadhari kubwa  Send to a friend
Tuesday, 15 March 2011 21:19
0diggsdigg
Mchungaji Ambilikile Mwasapile
KAMA kuna tukio ambalo liliwahi kugusa hisia na maisha ya  wananchi wengi katika historia ya nchi yetu, basi tukio hilo ni kupatikana kwa dawa inayosemekana inatibu magonjwa sugu na yaliyoshindikana, yakiwamo Kisukari, Kansa na Ukimwi. Hakika, tunashindwa kupata maneno stahiki ya kuelezea jinsi Watanzania walivyopokea habari za kupatikana kwa tiba hiyo iliyoelezwa kupatikana katika Kijiji cha Samunge, wilayani Loliondo, mkoani Arusha.

Ni tukio lililoitikisa na linaloendelea kuitikisa nchi yetu wakati maelfu kwa maelfu ya wananchi, wazee kwa vijana, wanaume kwa wanawake wa itikadi na imani zote wakielekea kijijini Samunge kumuona Mchungaji Ambilikile Mwasapile ili awapatie tiba ya magonjwa hayo sugu. Ndio maana tunasema kuwa hilo ni tukio kubwa na la kihistoria, na ukubwa wa tukio hilo hasa unatokana na ukweli kwamba ni tukio la kiimani. Kwamba Mchungaji huyo alioteshwa katika ndoto mwaka 1991 kuwa kuna dawa itakayoshushwa kwake ili aitumie kutibu  magonjwa ambayo yameshindikana kutibiwa na binadamu. Mashuhuda wengi wanasema walitibiwa na dawa ya mchungaji huyo tangu alipoanza kutoa huduma hiyo mwaka 2009. Baadhi wamejitokeza hivi karibuni na kusema kuwa wamepona maradhi hayo sugu.

Na kama hiyo haitoshi, watu waliopata dawa ya Mchungaji Mwasapile tangu habari za tiba yake zilipochapishwa na gazeti hili kwa mara ya kwanza wiki iliyopita, wamesema dawa hiyo imewatibu na sasa wanaona wako fiti. Baadhi ya madaktari wamethibitisha kuwa wateja wao ambao awali walikuwa wanasumbuliwa na magonjwa hayo wamethibitika kupona baada ya kutumia dawa hiyo inayojulikana kwa jina la Mugariga.
 
Hicho hasa ndicho kielelezo cha sababu ya maelfu kwa maelfu ya wananchi kumiminika Loliondo wakitokea kila pembe ya nchi yetu wakifuata dawa hiyo inayosemekana ni ya ajabu. Pia hicho ndicho kielelezo cha akili, mawazo, macho na masikio ya Watanzania wote kuelekezwa katika Kijiji cha Samunge na kutekwa na nguvu anayosemekana kuwa nayo Mchungaji Mwasapile.
 
Na hasa hiyo ndio sababu ya Serikali kujikuta njia panda pasipo kujua la kufanya. Katika kuonyesha hali ya kuchanganyikiwa, Serikali kwanza ilitangaza kupiga marufuku shughuli za Mchungaji  Mwasapile na baada ya wananchi kupaza sauti wakitaka huduma hiyo iendelee, Serikali ilisalimu amri mara moja hasa baada ya kutambua kuwa sauti za wananchi zilikuwa za kiimani zaidi.
 
Ni kwa sababu hiyo tunaipongeza Serikali kwa kutambua kuwa badala ya kuweka vizuizi ili maelfu kwa maelfu ya watu wasifuate tiba hiyo kijijini Samunge, ilikuwa busara kuwawezesha watu wapate tiba hiyo. Serikali ilifanya vyema kugundua kuwa maelfu ya watu waliokuwa wanafuata tiba hiyo wasingeogopa vizuizi au vitisho vyake, kwani baadhi yao walikuwa wamekata tamaa kutokana na maradhi sugu yaliyokuwa yanawasumbua, hivyo walikuwa tayari kwa lolote, hata kufa.
 
Vilevile, Serikali iligundua kuwa isingekuwa na askari wa kutosha kusimamia amri zake kwa sababu askari wengi walikuwa njiani kuelekea kijijini Samunge na wengine tayari walikuwa wamewasili huko kupata dawa hiyo. Pia, baadhi ya  mawaziri, wabunge na watendaji wakuu serikalini walikuwa miongoni mwa wananchi waliokuwa wanafuata dawa hiyo.Ndio sababu tangazo la Serikali kuruhusu shughuli hizo za tiba kuendelea ziliwapa watu wengi faraja na matumaini makubwa.
 
Sisi tunawahadhalisha wananchi na Serikali kuwa, pamoja na tiba hiyo kuwa suala la kiimani, tusifanye makosa kuanza kufanya sherehe. Tunawashauri wananchi wote kwanza waipe dawa hiyo muda wa kutosha ili itoe matokeo na baadaye wataalamu wa afya wayathibitishe pasipo shaka.
 
Kwa upande mwingine, tunawashauri wale wanaohisi wameponywa au hawajaponywa na dawa hiyo wajitokeze kutoa ushuhuda ili mamlaka husika ziweze kufanya tathmini na kuwapa wananchi maelekezo stahiki. Ni imani yetu kuwa watakaoponyeshwa na dawa hiyo hawatafanya vitendo hasi, bali watamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwaletea nuru mpya