Ndimbo ajiuzuru Simba | Send to a friend |
Thursday, 12 May 2011 21:05 |
Clara Alphonce ALIYEKUWA Afisa Habari wa Simba, Clifford Ndimbo jana alitangaza kujiuzuru wadhifa wake kwa madai kuwa hashirikishwi kwa chochote na viongozi wake waliopo madarakani. Ndimbo alijiriwa kuwa msemaji wa Simba ikiwa ni kigezo kimoja wapo cha kanuni za TFF na FIFA cha kuzitaka klabu zote za Ligi Kuu kuwa na vitengo vya Afisa Habari. Akizungumza kwenye mkutano na wanahabri Ndimbo alisema ameamua kujiuzuru mwenyewe na wala hajashawishiwa na mtu yoyote ila ameamua hivyo kwa sababu viongozi wa Simba wamekuwa hawamthamini kwa kazi yake ya Afisa Habari wa klabu. Alisema uongozi wa Simba hivi sasa chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage umekuwa ukimbagua kwa kutokumshirikisha kwa kitu chochote ikiwemo safari za timu na kufanya mikutano bila kumshirikisha na mambo mengine mengi tofauti na mkataba wake unavyoeleza. Alisema ameamua kukatisha mkataba wake wa miaka miwili alioingia na klabu hiyo toka wakina Rage waingie madarakani japo kipindi cha miezi tisa amekuwa akifanya kazi kwa hali ngumu, lakini alipokuwa akiwahoji viongozi wake walikuwa wakimuahidi watamtekelezea. Alisema barua hiyo aliyoiwakilisha jana kwa uongozi Simba itakuwa ni barua ya pili baada ya ile ya awali aliyoandika Aprili 5, 2011 kutokubaliwa baada ya kikao na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji na Katibu Mkuu wa klabu na kushauriana mambo kadhaa ambayo yalimrudisha kuendelea na kazi. Alisema ameamua kujiuzuru baada ya kuona kuwa hakuna utekelezaji wowote wa yale waliyokubaliana katika kikao chao walichokaa Jumatatu Machi 28, 2011 na kamati ya utendaji na kamati ya fedha makao makuu ya klabu Simba kuanzia saa 7 mchana. Alisema hata hivyo anashukuru kwa ushirikiano aliopewa na wanachama wa Simba, wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Simba kwa kipindi chote kwani amepata uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania na klabu mbali mbali kupitia Simba ambalo kwa upande wake anaamini ni somo kubwa. |
Comments
0 #6 Kifaru 2011-05-13 15:04
Niliota hili lingetokea na limetokea.
Quote 0 #5 LUGEYE 2011-05-13 13:02
Mh Rage kweli umezidi maana kila kwenye taarifa za habari za michezo we ndo msemaji hv uoni aibu sasa nini kazi afisa wa habari?mlimwajiri kwa kaz ipi?Samata kauzwa we ndo umetoa habari sijui nan mwingine kauzwa we ndo msemaji!hv hujui mipaka ya kaz yako mh?hv hamuwaoni wenzenu wa ulaya jaman?Abromovich wa chelsea mmiliki wa timu tangu mwaka uanze umemuona au kumsikia mara ngapi kwenye tv au press conference?yeye ni mtu wa kutoa order tu wako watendaji aliowaajiri sio kila kitu yeye hata kama ni boss,usilete siasa na mpira plz!jifunze kwa Berluscon wa Italia.
Quote +1 #4 HAMAD SIMBA DAMU 2011-05-13 09:58
RAGE NI MWANASIASA, SAYANSI YAKE NDIYO HIYO YA KUMUONA KILA SIKU NA WAANDISHI WA HABARI WAKATI MSEMAJI WA KLABU YUPO NA ANALIPWA MSHAHARA HII NI AJABU,,,!!RAGE USITUHARIBIE KLABU YETU KAMA ULIVOVURUGA FAT, ENDELEA NA UBUNGE NA DHAMANA TULIYOKUPA SIYO YA KUMILIKI KILA KITU MWISHOWE TUTAAMBIWA HATA MINUTES ZA KIKAO UNATAKA UWE UNACHUKUA WEWE...SOKA LA SASA NI LA KISOMI HUENDESHWA KISOMI KWA KILA MMOJA KUSIMAMIA IDARA YAKE...
Quote 0 #3 Mosses 2011-05-13 08:25
Kaka Ndimbo ndio soka la bongo viongozi wetu wako kimaslahi zaidi.Nafikiri kungekuwa na chuo cha kuwapa mafunzo viongozi wote wanaotaka kuongoza vilabu,ama wangepata basi nafasi ya kwenda hata kwa chini hizi za bara la ulaya nakujifunza ni kwa namna gani watu wanafanya kazi kama team work
Quote 0 #2 Gulio 2011-05-13 08:22
Kwa kweli hiyo ni dalili mbaya wanasimba - tuliambiwa mambo yataendeshwa kisayansi - sayansi iko wapi hapa? - kwa nini mtumie waandishi wa habari badala ya kuyamaliza ndani kwa ndani? Acheni mambo ya siasa ndani ya klabu tutaambulia aibu badala ya mafanikio
Quote 0 #1 A 2011-05-13 05:50
Mbona hivo tena Simba au ndio mnataka kuwa maadui kicheko? Huu sio hata kidogo wakati wa malumbano bali ni wakati wakujipanga upya na kuirejesha Simba katika ahadi yake. Kwanini hamzitatui tafauti zenu kwa njia ya busara na ukimya na hivo nndivo wanavofanya waungwana. Simba inasifika kwa ustaarabu. Madhali kazi ipo na kila mmoja anataka kuona maendeleo, lazima kuwepo tafauti za maoni kwa lengo la kufikia mafanikio wala sio mtafaruki. Jamani jeepusheni na mambo ambayo yatayotupeleka kubaya. Chondeni hatutaki kusikia mijadala ya kubomowa tunataka mijadala ya kujenga. Tunapingia magazetini tunataka kufurahi na wala hatutaki kulia. Simba ina viongozi wenye ujuzi na waliosoma na msiwache mambo kufika hadi hiyo.
Quote