Saturday, March 19, 2011

KANISA KATORIKI HAIFUSIANI NA CHADEMA

KANISA KATORIKI HAIFUSIANI NA CHADEMA  Send to a friend
Saturday, 19 March 2011 09:37
0diggsdigg
Israel Mgussi, Dodoma
RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Mkuu Yuda Thadeus Ruwa'ichi amewaponda wanasiasa wanaotaka kuwafumba mdomo viongozi wa dini nchini wanaokemea rushwa, ufisadi na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali na vyama vya siasa.Ruwai'chi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki, Mwanza pia amewajia juu wanaolihusisha kanisa hilo na ustawi wa Chadema akisema kuwa huo ni uzushi na kuwanyooshea kidole baadhi ya wanaCCM na baadhi ya waandishi wa habari aliosema hawapendi kuchanganua mambo na kuwa na uhakika nayo.

Askofu Ruwai`chi (pichani) alisema Kanisa Katoliki halikiteulii chama chochote cha siasa mgombea na akakipa angalizo CCM akitaka kijidodose juu ya sababu zilizomfanya Dk Willbrod Slaa kukihama na sasa kuonekana kama ni mtu anayekichanganya akili na kutaka iache alichokiita propaganda zenye malengo ya kuwagawa watu katika misingi ya dini.

“Kama Slaa (Dk Willbroad Slaa) alikuwa mwanaCCM akaikimbia. Sasa jifunzeni na kukumbuka historia, CCM wana mchango gani katika hilo la Dk Slaa kuikimbia, wakijibu swali hilo itakuwa vizuri sana," alisema akisisitiza.Askofu Ruwai'chi alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Parokia ya Kibaigwa, Dodoma muda mfupi baada ya kumpokea Askofu mteule wa Jimbo Katoliki la Dodoma, Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye atasimikwa rasmi leo mjini Dodoma.

Kuhusu Kanisa Katoliki kudaiwa kuwa limekuwa likikiunga mkono Chadema, Askofu Ruwai'chi alisema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu uvumi huo na kwamba kauli hizo zimekuzwa na baadhi ya wanaCCM ambao wamekosa sera na kukurupuka kutoa kauli zisizo za msingi.

“Hizo ni kauli danganya toto, Kanisa halina chama, ila likibidi kuzungumza litazungumza kama lilivyokuwa likifanya kwa maslahi ya watu wote. Viongozi wa dini wasipozungumza watakuwa hawalitendei haki taifa, wanapaswa kusimamia haki pale inapoonekana kupotoshwa, kanisa halina chama," alisema Askofu huyo.Alisema Chadema ni chama chenye mkusanyiko wa watu wa dini na madhehebu yote, hivyo watu watumie akili zao kutafuta ukweli wa uvumi huo aliosema ni wa kupotosha.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki nchini alisema kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa njema. Akaeleza kushangazwa kwake na wachache wanaotaka kupandikiza mbegu ya udini ambayo alisema kimsingi haipo nchini.

Alisema kauli kama hizo alizoziita za kichochezi pia zinajenga swali kuwa, huenda CCM ni chama cha watu fulani, lakini akasema kuwa wao viongozi wa dini na kanisa kwa ujumla kazi yao ni kuhakikisha maslahi ya taifa hayachezewi wala hayaendi kiholela, akisisitiza kuwa ni haki ya kila mtu kuwa na mtazamo tofauti wa kisiasa muhimu asivunje sheria.
Huku akisisitiza kuwa Tanzania haiendeshwi katika misingi ya falsafa za kidini wala madhehebu, Askofu Ruwai'chi alisema kuwa viongozi wa dini zote nchini wanapaswa kuzungumza na kukemea dosari za kiutendaji na kiuwajibikaji zinazofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma na kwamba bila hivyo itakuwa ni kutowatendea haki Watanzania.

Alisema viongozi wa dini wanapaswa kuzungumzia matatizo yaliopo nchini, kuhamasisha haki, ukweli, amani na kushughulikia maendeleo ya watu wote bila kuogopa wanaowabeza na kutaka kuwaziba midomo kwa kisingizio kuwa wanaingilia Serikali.

“Kuzungumza siyo kuingilia, viongozi wa dini wana wajibu wa kutoa kauli na kuwashuhudia watu mambo mbalimbali yanayotokea katika nchi, wasipoongea watakuwa hawalitendei haki Taifa,” alisema Askofu Mkuu Ruwai'chi.
Askofu Ruwaichi alisema kuwa viongozi wa dini mbali na kutunza dini, lakini wana wajibu mkubwa wa kusimamia mustakabali wa taifa kwa kuhakikisha wanakemea na kusemea mienendo ya kiovu ambayo kwa namna moja au nyingine, inaweza kuvuruga amani na umoja wa kitaifa.

Askofu mteule Nyaisonga atasimikwa leo katika Kanisa Kuu la Paulo wa Msalaba Mjini Dodoma na Rais Jakaya Kikwete pamoja na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na viongozi wengine wa dini na madhehebu mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria.
Juzi, mamia waumini wa Kanisa katoliki walijitokeza na kuandamana kwa ajili ya mapokezi ya askofu huyo mteule aliyewasili majira ya saa 7:00 mchana Kibaigwa, Dodoma akitokea Mbeya ambako alikuwa akitumika katika shughuli za kitume akiwa Padri Daraja la Pili.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
Last Updated on Saturday, 19 March 2011 09:46
 

Comments 

 
0 #7 elibariki yerald 2011-03-19 11:01
umenena baba askofu..nawapenda viongozi wa dini kama ninyi mnaochana ukweli bila kumung'unya,,na akija leo mhuyo jamaa.mumwambie kwa msisitizo zaidiiiiiiiiiii iii
Quote
 
 
+1 #6 yamasoft 2011-03-19 11:01
Naam, askofu umesema kweli, nafikiri umefika wakati wananchi kutanzua kwa akili zetu bila kuyumbishwa na wanaopandikiza mbegu ya udini katika mambo mbalimbali. Kwa mtazamo wangu CCM wanapaswa kutambua ndani ya vyama vya siasa kikiwamo chenyewe kuna watu wana imani zao tofauti lakini hoja ni kutenganisha shughuli za dini na siasa! Shughuli za siasa zikifanya na mtu mwenye imani furani ni wajibu wao kutambua anasimama pale kama mwanasiasa na si mwana dini furani! Tukumbuke ikiwa tutasahau hili na nje ya hapo hata CCM nayo itakuwa na udini! Watanzania wenzangu akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu! Haipaswi kuliruhusu swala la udini liwe chanzo cha watu wachache kuficha uozo wao wakitutaadhalis ha tukisema tutakuwa na udini! Maendeleo ni matam kwa watu wa dini zote, hivyo pale yanapoitaji kuyapigania ni wajibu wetu sote tukemee hata kama wanaofanya uozo ni wafuasi wa dini zetu!
Quote
 
 
+1 #5 J.G.Z 2011-03-19 10:55
tutafika tu tunapotaka kwenda, lakini sharti la kwanza lazima tumalize hizi changamoto zilizopo mbele yetu.
Quote
 
 
0 #4 Katiba TANGANYIKA 2011-03-19 10:45
Angalau tutapumua sasa!

Tulichoka na mambo ya loliondo. Haya ndio mambo yenyewe, tuendelee na ujenzi wa taifa tuwabane MAFISADI
Quote
 
 
+3 #3 itondo 2011-03-19 10:26
Yangu ni machache tu: Kwa hii hoja ya udini iliyopandikizwa na CCM dhidi ya CHADEMA wakitegemea support ya wananchi kiukweli itawamaliza wao CCM; ni suala la muda tu. CCM hawakujua unaposema CHADEMA (au chama kingine chochote) kina udini, unamaanisha wewe (CCM) pia una-suuport ya hao wa dini nyingine. Hii inaonesha jinsi viongozi wa CCM wanavyokurupuka na kutoa kauli bila kupima athari za kauli hizo. Wao ni ku-focus short term political success. Hii ni hatari.
Quote
 
 
+3 #2 mtanzania hai 2011-03-19 09:59
Hapo ni ukweli Padri anachosema; CCM waache kumtafuta mchawi kwa kuingiza udini kama kimbilio la kukiandama CHADEMA; sera zao za kubebana, undugu, ufamilia, ufisadi, kujuana, urafiki etc katika kuendesha serikali ndio unaowafanya washindwe kufurukuta kwa CHADEMA. Watanzania wa sasa sio wale wa mwaka 1977 wana upeo tofauti sana, wanataka kuona na sio kusimuliwa; MKAPA alionyesha na kuboresha nchi mbona haya mambo hayakuwepo yamekuwa tata hivyo? Maisha yamezidi kuwa ghali na hakuna chochote huku mfumuko wa bei na ufisadi vikizidi kushika chati; Tunaelekea wapi Watanzania? Tuchape kazi na serikali iwajibishwe!
Quote
 
 
+5 #1 mabuwe 2011-03-19 09:58
Mhashamu Askofu Yuda , hapo umenena, rudia tena kuwapasha hayohayo kwenye sherehe maana huko cream yote ya viongozi wenye propaganda chafu itakuwepo.
Quote
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!

BURIANI DR. REMMY

BURIANI DR. REMMY



Image
Remmy Ongala

Habari Zaidi:

  • Simba ichangamkie mabilioni ya CAF

  • Dede kuhama Mlimani kwenda Msondo ni manufaa kwa bendi hizo

  • Chipukizi wanane Vijana Stars wanaweza kucheza nje

  • (NYUZ BIN NYUZ):Dk. Remmy aliwahi kuihama Super Matimila

  • Ngulungu:Coastal Tuliwaduwaza Simba mwaka 1990

  • Rose Muhando,Mukabwa kuwashika Dar es Salaam

  • Usiri unavyotawala uchimbaji wa tanzanite

  • Mabadiliko ya tabianchi yaanza kuathiri Tanga

  • KISWAHILI SANIFU:Neno ‘hadi’ linatumiwa tofauti na maudhui yake

  • CCM na Chadema Shinyanga ni ‘watani wa jadi’

  • Mvua zakwamisha Kilimo Shinyanga

  • Ulinzi kwa albino sasa umeijengea sifa serikali

  • Shinyanga wadhibiti mauaji ya vikongwe

  • Utafiti wainua kilimo cha ndizi Kagera

  • Mabaki ya katani yazalisha umeme Hale

  • Mbinu mpya za ufugaji kuku wa kienyeji

  • Wilaya ya Mpwapwa yajikongoja kielimu

  • RASHID WARIOBA:Kutoka kuuza maji hadi kumiliki mgodi

  • Sekretarieti ya Ajira na changamoto ya walio pembezoni

  • Mzizi wa fitina kukatwa biashara za vileo Zanzibar


  • Habari zinazosomwa zaidi:

  • Balaa lingine kwa Chenge

  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi

  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa

  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa

  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya

  • Vatican yamvua jimbo Askofu

  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%

  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa

  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu

  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

  • RAHA ya kona hii kwanza ni kuwatakia kheri wasomaji, nami mwandishi kuwajulisha hali
    yangu, kwa hakika mimi ni mzima na naendelea vizuri kuwapasha mengi yanayohusu muziki wetu wa zamani.

    Leo nianze na kushukuru wa wasomaji wengi kunitumia ujumbe ukiwa na hili au lile, ilimradi wenye dira ya kuberesha safu yetu hii. Kwa walioshiriki kunitumia ujumbe na hata kunipigia simu nawashukuru kwa dhati kabisa kutoka moyoni.

    Lakini kati yetu leo nimalize kiu ya msomaji wetu Ibrahim Vuai, aliyejitambulisha kwamba anaishi Vuoni kisiwani Zanzibar. Yeye alituma ujumbe akilaani tabia ya wanamuziki kuhamahapa kutoka bendi moja kwenda nyingine, akisema kwamba hiyo ni moja ya vigezo vilivyodumaza muziki wa Tanzania.

    Kwa kweli akawataja wengi tangu miaka ile ya 1960 mpaka akaja hivi karibuni akalikumbushia tukio la bendi mbili za African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Extra Bongo Next Level kuchukuliana wanamuziki.

    Huko sikutaka kuingia sana, ila kubwa jingine ni pale alipowataka wanamuziki waige mfano wa
    aliyekuwa kiongozi wa bendi ya Super Matimila Dk Remmy Ongala ambaye alimtaja kuwa ni mwanamuzikji aliyetulia, kwani alipotoka Makassy na kujiunga Orchestra Matimila basi hakutoka hadi umauti ulivyompata mwishoni mwa mwaka jana.

    Hapa kidogo ndipo kwenye masahihisho yaliyonifanya niandike makala hii, kwa vile zipo kumbukumbu za kimuziki zinazoonesha kwamba licha ya uvumilivu wa muda mrefu Dk Remmy akiwa na bendi ya Super Matimila lakini aliwahi kuhama.

    Ikumbukwe mwaka 1985 mwimbaji huyo alitangazwa kuikimbia bendi ya Matimila, na alipohojiwa na vyombovya habari alikiri kuiacha bendi hiyo na kurejea bendi ya Orchestra
    Makassy.

    Ndicho kipindi hicho alichotunga wimbo Narudi Nyumbani, lakini ndani yake kulikuwa na maneno siyo yale yaliyorekodiwa baadaye Wimbo huo ulikuwa ukisema "Narudi kwa mjomba" ikiwa na maana anarejea kwenye bendi ya mjomba wake Mzee Makassy ambaye ilielezwa miaka hiyo kuwa wana undugu fulani.

    Hata katika msiba wa mwanamuziki huyo mtu aliyeitwa Kiteguru Makassy ndiye huo aliyekuwa mmiliki wa bendi ya Makassy na ndiye aliyekuwa msmemaji wa familia. Kilitokea nini wakati huo?

    Labda watu wengi na hasa wale wasiojua historia hii watakuwa wakijiuliza kilichojitokeza kwenye bendi ya Matimila ambayo yeye alikwa akiiongoza tangu alipoachiwa kijiti na aliyekuwa mpiga solo hatari wa bendi hiyo Mosese Fanfan ambaye naye alitokea Orchestra Makassy.

    Baada ya kuwa kiongozi wa muda refu na pia kuweza kutunga nyimbo nyingi ndani ya kundi hilo ilitokea wakati umuliki wa bendi hiyo ulihitaji kuiweka bendi kwenye utawala kwa idara maalum.

    Kama vile idara ya fedha na masuala mengine yawe nje ya kiongozi mkuu Dk Remmy ili kumpa nafasi yeye afanye vizuri kazi yake ya muziki.

    Labda tukio hilo na mengine ambayo hayakufahamika kirahisi yalimfanya mwimbaji huyo kutangaza kuikimbia bendi hiyo na kweli alipokewa kwa shangwe kwenye bendi yake ya zamani aliyopata kutamba nayo na nyimbo kama Siku ya Kufa, Harusi ya Mwanza, Namolema, Athumani Valuvalu, Sisca na Mosese.

    Hatimaye mzee mwenyewe Makassy akasimma jukwaani na kuimba pamoja na Dk Remmy na pia walifanikiwa kurekodi wimbo mmoja uitwao Shida za Dunia.

    Baadhi ya mashairi ya wimbo wa Dk Remmy alioimba na Mzee Makassy baada ya kurejea bendi ni haya:- Kweli nasikitika mtoto anapozaliwa anakuta shida nyingi za duniani, njaa kali, magonjwa mengi,shurua kuhara homa kali"

    Hata hivyo katika bendi ya Matimila ilikohesabiwa na wapenzi wa muziki kwamba kutakuwa na pengo, nako kulichangamka kiasi chake. wanza kitu kilichowashangaza wapenzi wengi ni kuwepo kwa sauti ya Dk Remmy licha ya yeye mwenyewe kutokuwepo kwenye bendi hiyo.

    Sauti hiyo ilikuwa na mwimbaji anayeitwa Bink Wabinsalunjivu, ambaye pia uvaaji wake wa kofia alishabihiana na Dk Remmy licha ya kumudu sauti yake. Vilevile alikuwepo mwimbaji
    mwingine Nkhulu Wabangoie aliyejiunga na bendi hiyo akitokea Orchestra Marquiz Du Zaire.

    Kipindi hicho Binki aliibuka na kibao kiitwacho Roda Binti Rashid, na Talakaka Changamka, ambapo Wabangoie alikuja na wimbo wa Sifa za Mage.

    Kwa kuwepo na 'vichwa' hivyo na vilevile kuimarika kwa ukumbi wa Wami Bar iliwawezesha wapenzi wa Matimila kuendelea kuingia kwenye kumbi wanazofanya maonesho kwa vile kulikuwa na mabadiliko fulani ya muziki.

    Kwani licha ya waimbaji hao kubuni mbinu mpya lakini pia aliyekuwa mpiga solo wa bendi
    hiyo Batii Osenga Lipopolipo aliweza kuchangamsha mkono na hivyo kujikuta wakipiga mtindo
    mpya wa Talakaka Changamka.

    Hata hivyo Dk Remmy alikuwa yari amejawa na mapenzi ya bendi ya Orchestra Matimila kwani hata kabla ya miezi mitatu akatangaza kurejea Matimila na safari hii akiubadilisha wimbo uliokuwa ukiimbwa Narudi kwa Mjomba sasa ukawa Narudi Nyumbani Matimila.

    Aliporejea mwimbaji Binki aliacha bendi hiyo na kwenda kuanzisha bendi ya Salna Brothers
    akiwa na mwimbaji mwingine Kapelembe Kokoo ambao waliisuka bendi hiyo hadi kunyakuwa ubingwa wa pili wimbo wa taifa kufuatia kibao chao kiitwacho Ufitina, wakati washindi wa kwanza walikuwa ni Mk Group kufuatia wimbo wao Utakuja Kuanguka Kwenye Matope.

    Dk Remmy naye aliifanyia ukarabati mkubwa bendi ya Matimila kwa kuwakaribisha wanamuziki wengine kama vile wapiga solo wengine Christopher Kasongo aliyepiga wimbo wa Mariam Wangu na Cobra Wabilumbu.

    Hapo ndipo alipoibuka na vibao kama Mariam wangu, Mwanza Mji Mzuri na nyimbo nyingine kadhaa, Kwa hiyo zipo kumbukumbu kuwa Dk Remmy alitoka Matimila wakati fulani na kurejea Makassy lakini baadaye akarejea kwenye bendi hiyo hadi alipofariki.

    WAZARI MAGUFURI BADO TUNAKUHITAJI, DONT EVER THINK OF KUJIUZULU

    Waziri Magufuli hajajiuzulu
    Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 18th March 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 426; Jumla ya maoni: 0



    Habari Zaidi:

  • Anaswa akiuza kichwa cha mkewe, matiti

  • Kikwete acharuka, amtaka Ngeleja awe makini

  • Waziri Magufuli hajajiuzulu

  • Wanaochakachua mafuta kufungiwa maisha

  • Wabunifu majengo hawataki kuingiliwa

  • Sekondari 'ya kitapeli' yafungwa

  • Waliouawa baada ya kuua polisi wafikia sita

  • Kikwete amteua Kamishina Magereza

  • Moto watekekeza nyumba, duka la vipuri Dar

  • Tanzania ina uhaba wa Wafamasia 14,000

  • Askofu awafunda vijana

  • Maliasili Mpanda waelemewa

  • Waliokuwa wamekosa madarasa kuanza masomo

  • Nahodha awaponda wanasiasa

  • Babu wa Loliondo ageuzwa mradi

  • Watuhumiwa walioua Polisi 2 wauawa

  • Wanafunzi wanaofeli wamkera Kikwete

  • Mkulo ataja vipaumbele 12 vya bajeti ijayo

  • Chadema, vyombo vya habari walaumiwa

  • 'Wananchi waruhusiwe kuwawajibisha wabunge'


  • Habari zinazosomwa zaidi:

  • Balaa lingine kwa Chenge

  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi

  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa

  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa

  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya

  • Vatican yamvua jimbo Askofu

  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%

  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa

  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu

  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

  • SERIKALI imetamka kwamba, habari za kujiuzulu kwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli hazina ukweli wowote, na ni uzushi wa baadhi ya vyombo vya habari.

    Baadhi ya magazeti ya kila siku nchini (si HABARILEO), leo yaliandika taarifa kuhusu kujiuzulu kwa Magufuli.

    Magazeti hayo yalidai kuwa Magufuli kajiuzulu kwa kuwa hakufurahia katika kile kinachodaiwa kuwa ni kuingiliwa kiutendaji na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

    Serikali iimekanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa, Magufuli anaendelea na kazi , hajajiuluzu, hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na pia hana sababu za kujiuzulu.

    Taarifa hiyo ya serikali imo katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Marango.

    “Tunataka kuchukua nafasi hii kuwaarifu na kuwahakikishia kwamba, taarifa hizi si za kweli. Mheshimiwa Waziri anaendelea na kazi zake vizuri, amekuwepo ofisini jana na leo na anaendelea na programu zake za kazi kama kawaida.

    “Tunaomba kuwahakikishia wananchi kwamba, Mheshimiwia Waziri Magufuli hajajiuzulu, hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu za kujiuzulu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyokuwa imepewa baraka zote na Waziri Magufuli.

    Amesisitiza kuwa, kutokana na ufafanuzi huo, Waziri Magufuli ambaye ni mmoja wa mawaziri wachapakazi hodari katika serikali ya Rais Kikwete, anaendelea na jukumu alilopewa na Rais la kuiongoza Wizara ya Ujenzi.

    Tangu kuchapishwa kwa habari hizo jana, chumba cha habari cha gazeti hili kilipokea simu nyingi zikiuliza ukweli wa kujiuzulu kwa Waziri Magufuli kama ilivyokuwa imeandikwa, ingawa `kiujanjaujanja’.

    Uvumi juu ya kujiuzulu kwa Magufuli ulianzia kwenye mitandao na ujumbe mfupi wa simu ikidaiwa kuwa, waziri huyo alifikia uamuzi huo baada ya kushindwa kuvumilia kitendo cha Waziri Mkuu kumtaka apunguze kasi ya bomoabomoa ya nyumba na mabanda yaliyojengwa katika hifadhi za barabara kote nchini.

    Pinda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera hivi karibuni, alisema ameonesha kasi kubwa katika kushughulikia suala hilo.

    UGUMU WA MAISHA USITUFANYE TUTUMIE NJIA AMBAZO NI KINYUME NA SHERIA,MILA NA TAMADUNI

    ANASWA NA MZIGO WA KICHWA NA MATITI YA MKWEWE
     
    Imeandikwa na Raymond Mihayo, Kahama; Tarehe: 18th March 2011 @ 23:58 Imesomwa na watu: 423; Jumla ya maoni: 0



    Habari Zaidi:

  • Anaswa akiuza kichwa cha mkewe, matiti

  • Kikwete acharuka, amtaka Ngeleja awe makini

  • Waziri Magufuli hajajiuzulu

  • Wanaochakachua mafuta kufungiwa maisha

  • Wabunifu majengo hawataki kuingiliwa

  • Sekondari 'ya kitapeli' yafungwa

  • Waliouawa baada ya kuua polisi wafikia sita

  • Kikwete amteua Kamishina Magereza

  • Moto watekekeza nyumba, duka la vipuri Dar

  • Tanzania ina uhaba wa Wafamasia 14,000

  • Askofu awafunda vijana

  • Maliasili Mpanda waelemewa

  • Waliokuwa wamekosa madarasa kuanza masomo

  • Nahodha awaponda wanasiasa

  • Babu wa Loliondo ageuzwa mradi

  • Watuhumiwa walioua Polisi 2 wauawa

  • Wanafunzi wanaofeli wamkera Kikwete

  • Mkulo ataja vipaumbele 12 vya bajeti ijayo

  • Chadema, vyombo vya habari walaumiwa

  • 'Wananchi waruhusiwe kuwawajibisha wabunge'


  • Habari zinazosomwa zaidi:

  • Balaa lingine kwa Chenge

  • Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi

  • Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa

  • ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa

  • Kikwete achekecha wakuu wa wilaya

  • Vatican yamvua jimbo Askofu

  • Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%

  • Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa

  • Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu

  • JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

  • POLISI wamemkamata mkazi wa Kijiji cha Mwamala wilayani Nzega katika mkoa wa Tabora, Tano Katinda, akiwa katika harakati za kuuza kichwa cha mtu anayesadikiwa kuwa ni mkewe na viungo vingine vya mwili wa mwanamke.

    Katinda alikamatwa Ijumaa asubuhi wakati alipokwenda kuuza 'bidhaa' hizo kwa Polisi waliokuwa lindoni benki.

    Mtuhumiwa huyo pia amekutwa na sehemu nyingine za viungo vya mwili yakiwemo matiti na sehemu za siri za kike.

    Alikuwa akizunguka na viungo hivyo vikiwa katika mfuko wa plastiki maarufu kama Rambo kwa lengo la kusaka wateja katika mitaa ya mjini wa Kahama mkoani Shinyanga.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani, amethibitisha kukamatwa kwa mwananchi huyo, na kwamba, mtuhumiwa alikamatwa jana saa 3 asubuhi baada ya kufika katika benki ya CRDB, tawi la Kahama.

    Alisema , baada ya kuzunguka kutafuta soko la viungo hivyo vya binadamu hadi katika Stendi Kuu ya mjini Kahama, akidai anauza nyama ya nguruwe maarufu kama Kitimoto, baadhi ya watu walimwelekeza akawauzie watu waliopo eneo na benki.

    Katinda alisonga mbele hadi tawi la NMB akawakuta askari aliowatangazia kuwa anauza kitimoto, walimjibu kuwa wao ni Waislamu, labda akajaribu kwa askari waliokuwa lindo katika benki ya CRDB iliyopo jirani na NMB.

    Anasema, mtuhumiwa alitii ushauri huo na kusonga mbele hadi CRDB alikoinadi nyama aliyokuwa anaiuza.

    Lakini mmoja wa askari hao baada ya kuchungulia alibaini kuna kichwa cha binadamu na viungo vingine, walimweka chini ya ulinzi na kumfikisha katika kituo cha polisi cha wilaya, mjini Kahama.

    “Awali kijana huyo alionekana kwenye eneo la stendi mabasi maeneo ya CCM Kahama akiuza viungo, hivyo ndipo alipoelekezwa kwenda kuuza kwa askari waliokuwa katika malindo ya benki za CRDB na NMB huku watu hao wasijue kijana huyo ni nini amebeka katika furushi lake,” alisema Kamanda Athumani.

    Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, kijana huyo baada ya kukamatwa alikiri kuwa viungo hivyo vilikuwa vya mke wake aliyetajwa kwa jina la Kabula Luziga (18), mkazi wa Itobo, Nzega.

    Alisema, kijana huyo baada ya kuulizwa alisema alimuua mkewe usiku kwa kutumia panga baada ya kumvizia akiwa amelala.

    Mtuhumiwa huyo aliwaeleza Polisi kuwa, kiwiliwili cha mwili wa marehemu Luziga alikiacha katika chumba chake nyumbani kwa babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mwanandilila huko katika Kijiji cha Mwamala, Nzega.

    Hata hivyo, kamanda huyo alisema baada ya kumhoji kijana huyo alidai kuwa alisikia matangazo kwenye kituo kimoja cha Redio cha mjini Kahama kuwa, viungo hivyo ni mali na tayari kuna wateja wanaovihitajika, ndipo alipoamua kumuua mkewe
    ingawa wakati akiuza alidai ni nyama ya kitimoto.

    Kamanda Athumani amesema, jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na kuchunguza akili ya kijana huyo.

    Kikosi cha askari polisi mjini hapa kiliondoka jana mchana kwenda kijijini Mwamala kuona kama kweli kuna kiwiliwili cha marehemu Luziga.