Waziri Magufuli hajajiuzulu
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 18th March 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 426; Jumla ya maoni: 0
Baadhi ya magazeti ya kila siku nchini (si HABARILEO), leo yaliandika taarifa kuhusu kujiuzulu kwa Magufuli.
Magazeti hayo yalidai kuwa Magufuli kajiuzulu kwa kuwa hakufurahia katika kile kinachodaiwa kuwa ni kuingiliwa kiutendaji na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Serikali iimekanusha taarifa hizo na kusisitiza kuwa, Magufuli anaendelea na kazi , hajajiuluzu, hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na pia hana sababu za kujiuzulu.
Taarifa hiyo ya serikali imo katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Herbert Marango.
“Tunataka kuchukua nafasi hii kuwaarifu na kuwahakikishia kwamba, taarifa hizi si za kweli. Mheshimiwa Waziri anaendelea na kazi zake vizuri, amekuwepo ofisini jana na leo na anaendelea na programu zake za kazi kama kawaida.
“Tunaomba kuwahakikishia wananchi kwamba, Mheshimiwia Waziri Magufuli hajajiuzulu, hajawahi kuwa na wazo la kujiuzulu na hana sababu za kujiuzulu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo iliyokuwa imepewa baraka zote na Waziri Magufuli.
Amesisitiza kuwa, kutokana na ufafanuzi huo, Waziri Magufuli ambaye ni mmoja wa mawaziri wachapakazi hodari katika serikali ya Rais Kikwete, anaendelea na jukumu alilopewa na Rais la kuiongoza Wizara ya Ujenzi.
Tangu kuchapishwa kwa habari hizo jana, chumba cha habari cha gazeti hili kilipokea simu nyingi zikiuliza ukweli wa kujiuzulu kwa Waziri Magufuli kama ilivyokuwa imeandikwa, ingawa `kiujanjaujanja’.
Uvumi juu ya kujiuzulu kwa Magufuli ulianzia kwenye mitandao na ujumbe mfupi wa simu ikidaiwa kuwa, waziri huyo alifikia uamuzi huo baada ya kushindwa kuvumilia kitendo cha Waziri Mkuu kumtaka apunguze kasi ya bomoabomoa ya nyumba na mabanda yaliyojengwa katika hifadhi za barabara kote nchini.
Pinda, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kagera hivi karibuni, alisema ameonesha kasi kubwa katika kushughulikia suala hilo.
No comments:
Post a Comment