Twiga Stars yaichakaza Namibia
Timu ya Soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, imewapa raha Watanzania, baada ya kuibanjua kibabe, Timu ya Wanawake ya Namibia.
Golikipa wa Namibia, alikabiliana na adhabu kali baada ya kutunguliwa mara tano katika ushindi wa jumla wa mabao 5-2 ambao Twiga imeupata leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Twiga inasogea hatua ya pili ya kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake ikiwa na ushindi wa jumla ya mabao 7-2.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Windhoek, Namibia, Twiga iliichakaza timu hiyo mabao 2-0.
Mchezo wa leo, Twiga ilianza kwa kusuasua lakini baadaye ilicharuka na kuipeleka puta Namibia, hivyo kuilazimisha mabao matatu ya haraka dakika za lala salama.
Kwa matokeo hayo, Twiga sasa itapambana kwenye mzunguko unaofuata na mshindi wa mechi ya Misri dhidi ya Ethio
No comments:
Post a Comment