Tuesday, May 17, 2011

AMAZING,WAS SITA THE FOUNDER OF CCJ?

Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ  Send to a friend
Monday, 16 May 2011 21:39
0diggsdigg
Kada wa Chadema, Fred Mpendazoe akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa National Housing mjini Njombe.Picha na Edwin Mjwahuzi
Waandishi Wetu
KADA wa Chadema, Fred Mpendazoe amewataja mawaziri wawili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, mbunge mmoja wa CCM na makada wengine wawili wa chama hicho tawala kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa katika harakati za kukihama na kujiunga na CCJ.Mpendazoe ambaye alikuwa kada wa kwanza wa CCM kuhamia CCJ wakati huo akiwa Mbunge wa Kishapu, aliwataja waanzilishi hao wa CCJ kuwa ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri mmoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa Mpendazoe, katika kundi hilo pia wamo kada wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM na mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Mbeya. Hatukuandika majina ya baadhi ya viongozi waliotajwa kwa sababu hatukufanikiwa kuwapata kujibu tuhuma hizo.Hata hivyo, Sitta alipipogiwa simu alisema asingeweza kuzungumza lolote kuhusu madai hayo akisema anasubiri kusoma alichosema Mpendazoe.

Mpendazoe aliwataja makada hao jana wakati akihutubia umati uliokusanyika kwenye Viwanja vya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Njombe Mjini katika mkutano wa hadhara wa Chadema."Nilipoondoka CCM mimi nilikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ, lakini wengine walikuwa hawajulikani na leo nitawataja hao wengine kwa kuwa CCM inajidai kujivua gamba ili kuwadanganya wananchi," alisema Mpendazoe.Alisema hao aliowataja ndiyo waliotaka kukihama CCM, lakini walibaki si kwa ajili ya maslahi ya Taifa, bali ni kwa maslahi yao binafsi.

"Sitta na (makada wengine) wameingia katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, lakini ni wasaliti na Serikali ya CCM ya sasa haiwezi kuwasaidia Watanzania," alisema na kuongeza:
"Wamevaa ngozi ya kondoo kwa kupinga ufisadi kwa maslahi yao, lakini leo bado wako pale."
Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema viongozi wa CCM ni wanafiki na ndiyo maana, hawaelewi wanachokifanya zaidi ya kuwadanganya wananchi.

Aliitaka serikali kuacha ubabaishaji na kuchukua hatua zinazoweza kuwaletea wananchi maendeleo na kuliinua Taifa.
Dk Slaa alitumia nafasi hiyo kumshambulia Spika wa Bunge, Anne Makinda. Aliwahoji wakazi wa Njombe waliohudhuria mkutano huo kama uspika wake unawasaidia chochote na wao wakajibu kwa kupiga kilele: "Hakuna chochote."

"Nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, niliwahi kukagua Njombe na miradi yenu nikagundua kuwa hakuna maendeleo yoyote ikiwamo kituo cha basi cha Njombe ambacho hakifai," alisema Dk Slaa.
Alisema kutokana na kuendelea kumpigia kura kwa muda mrefu, wananchi hao wataendelea kunyanyasika na familia ya mbunge wao itaendelea kuneemeka kwa kutumia mgongo wao.

Mukama: Chadema kiache ubabaishaji
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuacha kile alichodai kuwadanganya wananchi kwamba CCM kujivua gamba si kitu akisema hatua hiyo imefikiwa kukiimarisha chama baada ya kutambua kuwa bila hivyo nchi itayumba. Mukama alisema hayo kwa nyakati tofauti juzi na jana katika Kijiji cha Kibara, wilayani Bunda na katika Kijiji cha Kaburabura, wilayani Musoma katika mikutano ya hadhara, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nane mkoani Mara.

Alisema CCM kimetumia dhana hiyo ya kujivua gamba ili kiweze kurudi kwenye misingi imara, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa, hali ambayo itakiweka kwenye mstari unaotakiwa ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo na huduma zote muhimu.
Alisema anawashangaa wapinzani wanaotumia muda mrefu kujadili falsafa ya kujivua gamba na kuhoji uwezo wao katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Alisema amesikitishwa na kauli ya viongozi wa Chadema kwamba kuna uwezekano Rais Kikwete kuondoka madarakani kabla ya 2015 kwa kutolea mfano wa Waziri Mkuu wa Japan aliyeondolewa madarakani.
Alifafanua kuwa viongozi wa Chadema wanatakiwa kufanya uchunguzi kabla ya kutoa matamko kwa maelezo kuwa Waziri Mkuu wa Japan hawezi kufananishwa na Rais Jakaya Kikwete kwa vile aliwekwa madarakani na Bunge wakati Rais alichaguliwa na wananchi.

Alisema kuwa, hata Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wake aliwahi kutamka kuwa, bila CCM ya kweli nchi itayumba na kwamba ndiyo maana chama hicho kimeamua kutumia dhana hiyo ya kujivua gamba ili kiweze kuwa imara na kinachoweza kusimamia maendeleo ya wananchi.

"Tunakiweka katika misingi ya kukiimarisha ili kiwe chombo imara ambacho kweli kinaweza kusimamia maendeleo katika maeneo yetu tunayoishi. Sasa hawa Chadema wameichukua dhana hiyo ya kujivua gamba visivyo kabisa," alisema.

Alisema hiyo inatokana na viongozi wa Chadema kuwa na tabia ya kurukia mambo bila kuyafanyia uchunguzi na kwamba wameichukua dhana hiyo visivyo na kuendelea kuwarubuni wananchi ili wakichukie CCM na serikali yao... "Hawa wanataka kwenda Ikulu kwa maneno ya udanganyifu kabisa na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote."
Pia alisema kuwa CCM haiwezi kufa kama upinzani wanavyoendelea kuwaambia wananchi, kwani ni chama kikubwa, taasisi na si kampuni ya kibiashara.

Aidha, Mukama amekiponda Chadema ambacho kimekuwa kikidai kwamba CCM imekumbatia wafanyabiashara na kueleza kuwa Chadema ndicho kinayofanya hivyo."Sasa watu wanaokumbatia sera ambazo mwalimu alikuwa anazipinga, eti ndio wanakwenda kwenye kaburi pale wanasema tunakuomba leo utusikilize tuweze kutawala nchi hii kidogo," alisema.

Alisema CCM kina matajiri wachache ambao wanataka kukitumia kwa ajili ya kujinufaisha na kuonya kuwa wafanyabiashara ambao maadili yao hayaendani na chama chao wataondolewa na kuwekwa pembeni mara moja.

Amewataka wakuu wa wilaya nchini na viongozi wa CCM, kusimama imara na kuhakikisha fedha za miradi mbalimbali zinazoletwa na Serikali katika halmashauri husika, zinafanya kazi iliyokusudiwa na si kuishia kwenye mikono ya wajanja wachache.
Alisema kuwa ni lazima wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wa chama hicho watekeleze wajibu wao ipasavyo wa kusimamia fedha za Serikali zinazopelekwa kwenye  halmashauri.Habari hii imeandaliwa na Boniface Meena, Njombe; Ahmed Makongo na Christopher Maregesi, Bunda na Beldina Nyakeke, Musoma Vijijini.

Monday, May 16, 2011

JE KUNA UHUSIANO KATI YA UFAULU WA WANAFUNZI NA UPATIKANAJI WA CHAKULA MASHULENI?

Weekend imeenda pouwa sana mtu mzima kwizera! kuhusu mada inayohusanisha chakula na ufaulu wa wanafunzi mashuleni,ni kweli kuna uhusiano mkubwa kati ya ufaulu wa wanafunzi na chakula,vijijini mara nyingi vyakula huwepo kwa wingi wakati wa mavuno lakini msimu wa mavuno ukishapita wanakijiji wengi hukubwa na tatizo la chakula kwa kuwa hawana elimu ya uhifadhi wa chakula,lakini pia mafuno wanakijiji wanayopata hayawawezeshi kufikia msimu mwingine wa mavuno. Hivyo,sehemu nyingi za vijijini wanafunzi wanafunzi hukubwa na njaa,mwanafunzi mwenye njaa hukosa hamasa ya kujifunza kwa bidii kwa kuwa muda mwingi watakuwa wanfikiria namna ya kukabili njaa inayowakumba badala ya kufuatilia yale wanayofundishwa na walimu mashuleni.Ndugu yangu Kwizera mimi mwenyewe ni mhanga wa kutokufaulu vizuri mitihani yangu ya primary school kwa tatizo la njaa,nakumbuka mimi na wenzangu tulikuwa tunakabiri njaa zetu kwa kwenda kuwasidia wafanya biashara kusukuma baiskeli zao zilizobeba mizigo kupanda mlima RUSUNWE wilayani KASULU kuelekea Burundi,na kisha kupatiwa fedha kiduchu ambazo tuliweza kunnua chakula, hali hiyo ilituathiri sana kitaaluma kwa kuwa kazi za kusukuma baiskeli kupanda mlima RUSUNWE tulikuwa tunaifanya wakati wa masomo. Hali hiyo ingeweza kuzuwilika kama tungekuwa tunapewa chakula mashuleni maana tungeelekeza mawazo yetu na fikira zetu katika masomo badala ya kuelekeza mawazo yetu na fikra zetu katika kusukuma baiskeli kupandisha mlima RUSUNWE ili kupata fedha za kununulia chakula.
Hivyo kama kutakuwapo mpango unaotekelezeka wa kuwapatia wanafunzi wa shule zetu za msingi chakula walau cha mchana,licha ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi lakini pia mpango wa chakula mashuleni utaweza kuongeza mahudhurio ya wanafunzi mashuleni,kupunguza utoro reja reja wa wanafunzi mashuleni na kuongeza molari za wanafunzi kujifunza na kufuatilia kile wanachofundishwa madarasani.
Mimi ni LEONARD KILAMHAMA

JE NI KWELI NCHI HAITAWALIKI?


Dk. Slaa:
[Image] KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Willbrod Slaa, sasa ametamka rasmi kwamba nchi haitatawalika, kwani chama chake hakiko tayari kuona Watanzania wakiendelea kuwa katika hali ngumu ya maisha, huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikitekeleza mkakati wa siri wa kuwajaza matumaini hewa badala ya kutatua matatizo yao.
Dk. Slaa ameeleza kuunasa waraka wa siri wa CCM ambao ndani yake chama hicho kimekiri waziwazi kupoteza ladha kwa umma, huku mkakati pekee wa kujinusuru ukielezwa kuwa ni kubadili sura za viongozi wa chama hicho ili kuwajengea matumaini mapya Watanzania.
Kwa mujibu wa Dk.Slaa, waraka huo wenye mhuri mkubwa wa neno “siri” uliandaliwa na baadhi ya wataalam wa CCM waliofanya tathmini ya hali ya chama chao kisiasa na kuuwasilisha kwa viongozi wa juu wa chama hicho ambao tayari wameanza kuufanyia utekelezaji wa “kujivua gamba” kwa lengo la kuwapa matumaini hewa wananchi.
Dk. Slaa alifichua siri za waraka huo wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja wa shule ya sekondari Msakila mjini Sumbawanga ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya chama hicho mkoani Rukwa, baada ya kuutikisa mkoa wa Mbeya kwa maandamano na mikutano ya hadhara kwa siku tatu mfululizo.
Alisema katika waraka huo CCM imekiri kuwa haikubaliki kwa Watanzania na kwamba iliporomoka sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, lakini badala ya kurejesha tunu za taifa kama uadilifu, upendo, amani, umoja na uwajibikaji wa kuleta maendeleo yatakayoirejeshea imani toka kwa wananchi, chama hicho kimeamua kubadili tu sura za viongozi wake wa kitaifa.
“CHADEMA tunafanya mambo kwa utafiti. CCM wana waraka wa siri uliowafanya wajivue gamba lakini wanaume tayari tumeshaunasa, tena una mhuri mkubwa wa neno siri lakini tayari tunao. Katika waraka wao CCM wamekiri wenyewe kwamba hawakubaliki tena kwa Watanzania walio wengi, wamekiri wenyewe kwamba wamepoteza ladha kwa wananchi. Wamekiri wenyewe katika waraka huo, kwamba hawakubaliki kwa sababu wameacha siasa ya ujamaa na kujitegemea.
“Na ni kweli wameacha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Mabilioni ya Kikwete sio ujamaa na kujitegemea. Mabilioni ya mtoto wake, anayeitwa Ridhawani nayo ni ushahidi tosha kuwa wameacha ujamaa na kujitegemea kama walivyokiri wenyewe kwenye waraka wao.
“Tatizo lao ni kwamba badala ya kuacha ufisadi na kurejesha tunu za taifa kama uadilifu, upendo, amani, umoja na uwajibikaji…badala ya kupunguza kodi kwenye mafuta, sukari, saruji, na bidhaa nyingine, ili wajijengee uhalali kwa umma, wao katika waraka wao wameamua wabadili sura za viongozi kwa kujivua gamba. Hawataji popote kwenye waraka wao jinsi watakavyoboresha maisha yenu,” alisema Dk.Slaa na kuongeza.
“CHADEMA hatuko tayari kuona Watanzania wakiteseka huku CCM yenye serikali badala ya kuchukua hatua za dharura kuwanusuru, inapanga kuendelea kuwadanganya kwa kubadili viongozi kwa kujivua gamba. Arusha nilitoa hotuba moja wakasema Dk. Slaa mchochezi…sasa leo nawatuma usalama wa taifa nendeni mkawaambie CCM kwamba nchi haitatawalika. Wasipochukua hatua CHADEMA itachukua hatua…kama Watanzania hawajui wanakula nini, wanavaa nini, watoto wao wanasoma vipi, wanatibiwa vipi, basi nchi hii haitatawalika.”
Alisisitiza kuwa nchi haitatawalika kwani kila kukicha ufisadi unakithiri badala ya kupungua huku akibainisha kuwa hata ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ya hivi karibuni imeonyesha katika wizara moja pekee, wizara ya fedha na uchumi, jumla ya sh bilioni 365 ziliibiwa wakati zingeweza kutumika kunusuru maisha ya Watanzania.
Mwenyekiti wa chama hicho akihutubia wakazi hao wa Sumbawanga, alisema kupitia maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na chama hicho nchi nzima, CHADEMA imedhamiria kuamsha nguvu ya umma katika kuishinikiza serikali kupunguza kodi kwenye bidhaa na huduma muhimu ili bei zishuke na maisha ya wananchi yawe nafuu.
Alisema kupanda kwa gharama za maisha kumesababishwa na ufisadi na sera mbovu za serikali ya CCM, ambayo inawatoza kodi kubwa wananchi maskini kupitia bidhaa na huduma mbalimbali huku serikali hiyo hiyo ikiwasemehe kodi wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.
Katika hotuba yake hiyo iliyoonekana dhahiri kuwateka wakazi wa Sumbawanga, Mbowe alisema CHADEMA haipingi watu kulipa kodi, lakini haiko tayari kuona Watanzania maskini wakilipishwa kodi kubwa, huku serikali ikishindwa kuwapa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akifafanua zaidi historia ya kodi na athari zake kwa wananchi, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alisema baada ya serikali ya Rais Benjamin Mkapa kuondoa kodi ya maendeleo, ilileta kodi nyingine ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo wananchi wote sasa wanatozwa kila wanaponunua bidhaa dukani na kulipia huduma mbalimbali kama usafiri.
“Nyerere alikuwa akikusanya kodi bilioni saba kwa mwezi, mzee Mwinyi aliondoka akiwa anakusanya kodi ya bilioni 27, akaja Mkapa yeye hadi anaondoka alikuwa anakusanya bilioni 300 na ushei. Baada ya hapo akaja Kikwete, yeye anakusanya bilioni 420 kwa mwezi. Anakusanya fedha nyingi kwa sababu kuna kodi ya VAT iliyoongezwa katika bei za bidhaa na huduma mnazolipia. Mnalipa kodi bila kujua, mnalipa kodi kwenye mafuta, kwenye soda, usafiri, sukari, sanda, pipi...kila kitu kodi kodi kodi,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Kwa sababu ya kodi ya VAT, leo katika nchi hii kila mwananchi analipa kodi, mtoto, mjane, kijana, mwanafunzi wote wanalipa kodi …hadi maiti nazo zinalipiwa kodi mnaponunua sanda kwa ajili ya kuzikia. ...lakini kodi hizo zinaishia kustawisha maisha ya vigogo wa serikali, wananchi wa Sumbawanga na Watanzania wengine wanazidi kuwa maskini, mmefikia mahali hamuwezi hata kununua kilo moja ya sukari kwa ajili ya chai au kilo ya mafuta mnaanza kupimiwa kwenye vifuko vya shilingi mia moja...hali ya hatari hii, taifa lina msiba wa umaskini, wananchi wanalia kila mahali sasa, kila kona ya nchi,” alisema.
Akitoa mfano wa jinsi kodi inavyofanya bei za vitu kuwa juu, Mbowe alisema katika kila Sh elfu moja anayotumia Mtanzania kununua bidhaa sokoni au dukani au kulipia huduma, serikali humkata kodi ya wastani wa sh 500 hadi 600, kodi ambayo kama ikiondolewa gharama za maisha zitakuwa nafuu.
“Soda moja inapotoka kiwandani inapaswa kuuzwa kwa Sh 150 lakini kwa sababu ya kodi iliyowekwa na CCM kuanzia viwandani soda moja mnauziwa kwa sh 500 hadi 600. Kila mnaponunua mfuko mmoja wa cement mnakatwa kodi ya Sh 7,500 ambayo kama ikiondolewa au kupunguzwa bei ya saruji itakuwa nafuu na wengi mtaweza kujenga.
“Kila chupa moja ya bia unayonunua unakatwa kodi ya sh 800. Ndiyo maana Kikwete kwa mwezi anakusanya bilioni 420 kutoka kwenu, lakini maendeleo hakuna. CHADEMA tutakomaa na suala la gharama za maisha ndani na nje ya bunge mpaka Watanzania maisha yao yawe nafuu,” alisema Mbowe na kushangiliwa.
Katika mkutano huo pia Mbowe aliwahamasisha wakazi wa Sumbawanga kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata Katiba mpya na kushinikiza katiba hiyo itokane na wananchi na sio itokane kwa utashi na maamuzi ya Rais Kikwete kama ilivyopendekezwa katika Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi hao alisema kwa nafasi yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, ameagizwa na chama chake kuwasilisha bajeti mbadala katika bunge lijalo la bajeti ambayo pamoja na mambo mengine itashinikiza serikali kupunguza kodi kwenye mafuta ya petroli na dizeli kwa asilimia 50 ili yauzwe kwa angalau Shs 1665 kwa lita kutoka kwenye bei ya zaidi ya sh 2000 ya sasa.
“Gharama za maisha ziko juu kwa sababu ya mfumuko wa bei za mafuta ambao unasababisha na kodi. Bei ya mafuta ikishuka hadi 1,665 gharama za usafiri na bei za sukari na vyakula nazo zitakuwa angalau. Tutawataka waondoe kodi kwenye mafuta halafu wapunguze misahamaha ya kodi wanayoitoa kwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa … serikali inasemehe bilioni 635 za kodi zinazopaswa kulipwa na matajiri, sasa hizo zikafidie kwenye mafuta baada ya kupunguza kodi. Wakikataa watakiona cha moto, tutafanya maandamano ndani na nje ya bunge mpaka kieleweke,” alisema Zitto.

Friday, May 13, 2011

VIONGOZI WETU SI VYEMA KUINGILIA MAJUKUMU YA MAAFISA HABARI,HESHIMUNI WEREDI WA WANAHABARI

Ndimbo ajiuzuru Simba  Send to a friend
Thursday, 12 May 2011 21:05
Clara Alphonce
ALIYEKUWA Afisa Habari wa Simba, Clifford Ndimbo jana alitangaza kujiuzuru wadhifa wake kwa madai kuwa hashirikishwi kwa chochote na viongozi wake waliopo madarakani.

Ndimbo alijiriwa kuwa msemaji wa Simba ikiwa ni kigezo kimoja wapo cha kanuni za TFF na FIFA cha kuzitaka klabu zote za Ligi Kuu kuwa na vitengo vya Afisa Habari.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabri Ndimbo alisema ameamua kujiuzuru mwenyewe na wala hajashawishiwa na mtu yoyote ila ameamua hivyo kwa sababu viongozi wa Simba wamekuwa hawamthamini kwa kazi yake ya Afisa Habari wa klabu.

Alisema uongozi wa Simba hivi sasa chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage umekuwa ukimbagua kwa kutokumshirikisha kwa kitu chochote ikiwemo safari za timu na kufanya mikutano bila kumshirikisha na mambo mengine mengi tofauti na mkataba wake unavyoeleza.

Alisema ameamua kukatisha mkataba wake wa miaka miwili alioingia na klabu hiyo toka wakina Rage waingie madarakani  japo kipindi cha miezi tisa amekuwa akifanya kazi kwa hali ngumu, lakini alipokuwa akiwahoji viongozi wake walikuwa wakimuahidi watamtekelezea.

Alisema barua hiyo aliyoiwakilisha jana kwa uongozi Simba itakuwa ni barua ya pili baada ya ile ya awali aliyoandika Aprili 5, 2011 kutokubaliwa baada ya kikao na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji na Katibu Mkuu wa klabu na kushauriana mambo kadhaa ambayo yalimrudisha kuendelea na kazi.

Alisema ameamua kujiuzuru baada ya kuona kuwa hakuna utekelezaji wowote wa yale waliyokubaliana katika kikao chao walichokaa Jumatatu Machi 28, 2011 na kamati ya utendaji na kamati ya fedha makao makuu ya klabu Simba kuanzia saa 7 mchana.

Alisema hata hivyo anashukuru kwa ushirikiano aliopewa na wanachama wa Simba, wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Simba kwa kipindi chote kwani amepata uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania na klabu mbali mbali kupitia Simba ambalo kwa upande wake anaamini ni somo kubwa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #6 Kifaru 2011-05-13 15:04
Niliota hili lingetokea na limetokea.
Quote
 
 
0 #5 LUGEYE 2011-05-13 13:02
Mh Rage kweli umezidi maana kila kwenye taarifa za habari za michezo we ndo msemaji hv uoni aibu sasa nini kazi afisa wa habari?mlimwajiri kwa kaz ipi?Samata kauzwa we ndo umetoa habari sijui nan mwingine kauzwa we ndo msemaji!hv hujui mipaka ya kaz yako mh?hv hamuwaoni wenzenu wa ulaya jaman?Abromovich wa chelsea mmiliki wa timu tangu mwaka uanze umemuona au kumsikia mara ngapi kwenye tv au press conference?yeye ni mtu wa kutoa order tu wako watendaji aliowaajiri sio kila kitu yeye hata kama ni boss,usilete siasa na mpira plz!jifunze kwa Berluscon wa Italia.
Quote
 
 
+1 #4 HAMAD SIMBA DAMU 2011-05-13 09:58
RAGE NI MWANASIASA, SAYANSI YAKE NDIYO HIYO YA KUMUONA KILA SIKU NA WAANDISHI WA HABARI WAKATI MSEMAJI WA KLABU YUPO NA ANALIPWA MSHAHARA HII NI AJABU,,,!!RAGE USITUHARIBIE KLABU YETU KAMA ULIVOVURUGA FAT, ENDELEA NA UBUNGE NA DHAMANA TULIYOKUPA SIYO YA KUMILIKI KILA KITU MWISHOWE TUTAAMBIWA HATA MINUTES ZA KIKAO UNATAKA UWE UNACHUKUA WEWE...SOKA LA SASA NI LA KISOMI HUENDESHWA KISOMI KWA KILA MMOJA KUSIMAMIA IDARA YAKE...
Quote
 
 
0 #3 Mosses 2011-05-13 08:25
Kaka Ndimbo ndio soka la bongo viongozi wetu wako kimaslahi zaidi.Nafikiri kungekuwa na chuo cha kuwapa mafunzo viongozi wote wanaotaka kuongoza vilabu,ama wangepata basi nafasi ya kwenda hata kwa chini hizi za bara la ulaya nakujifunza ni kwa namna gani watu wanafanya kazi kama team work
Quote
 
 
0 #2 Gulio 2011-05-13 08:22
Kwa kweli hiyo ni dalili mbaya wanasimba - tuliambiwa mambo yataendeshwa kisayansi - sayansi iko wapi hapa? - kwa nini mtumie waandishi wa habari badala ya kuyamaliza ndani kwa ndani? Acheni mambo ya siasa ndani ya klabu tutaambulia aibu badala ya mafanikio
Quote
 
 
0 #1 A 2011-05-13 05:50
Mbona hivo tena Simba au ndio mnataka kuwa maadui kicheko? Huu sio hata kidogo wakati wa malumbano bali ni wakati wakujipanga upya na kuirejesha Simba katika ahadi yake. Kwanini hamzitatui tafauti zenu kwa njia ya busara na ukimya na hivo nndivo wanavofanya waungwana. Simba inasifika kwa ustaarabu. Madhali kazi ipo na kila mmoja anataka kuona maendeleo, lazima kuwepo tafauti za maoni kwa lengo la kufikia mafanikio wala sio mtafaruki. Jamani jeepusheni na mambo ambayo yatayotupeleka kubaya. Chondeni hatutaki kusikia mijadala ya kubomowa tunataka mijadala ya kujenga. Tunapingia magazetini tunataka kufurahi na wala hatutaki kulia. Simba ina viongozi wenye ujuzi na waliosoma na msiwache mambo kufika hadi hiyo.
Quote
 
This little and beautiful girl was found 
uswahili,mburahati-dar es salaam

sometimes our reasoning and thinking
may be restricted by the environment
people we are enbraced as our friends

The failure of  previous set goal provides
an opportunities to plan for new goals

Net-working has power in recent world
only if u do it with a plan

Clean enviroment should be enhanced
for our health and proper thinking
because dirty environment results into
 unproper thinking

PENYE UKWELI,UONGO HUJITENGA! CCM KAMA HAINA JIPYA HIVI?

Marando, Nape ni jino kwa jino  Send to a friend
Thursday, 12 May 2011 22:06
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye
Ramadhan Semtawa na Elias Msuya
CCM na Chadema, vimeendeleza siasa za jino kwa jino kufuatia viongozi wake kuzidi kurushiana makombora yaliyobeba tuhuma ndani yake.Jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alimtaka Dk Willibrod Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema aliombe radhi Bunge, huku Chadema nayo ikimtaja Nape kwamba ni mtuhumiwa wa ufisadi wa EPA uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo Sh133 bilioni zilikwapuliwa. 

Tuhuma hizo kutoka kila upande, ambazo sawa na siasa za jino kwa jino, zimekuja baada ya Nape kutaja alichokiita unafiki wa Dk Slaa kwa kushinikiza kulipwa mshahara wa Sh7.5 milioni na Chadema, wakati alikataa mshahara wa Sh7 milioni alipokuwa mbunge akidai ni mkubwa na uliwanyonya Watanzania.Vyama hivyo jana kwa nyakati tofauti, kila kimoja kiliongeza mashambulizi dhidi ya kingine, ambapo Nape alikwenda mbali zaidi akimtaka Dk Slaa aliombe radhi Bunge na wabunge kwa alichoeleza kuwa Dk Slaa alipokuwa Mbunge wa Karatu, alichochea chuki kwa wananchi dhidi ya taasisi hiyo.

"Najua Chadema watakuwa wanajibu, lakini nasema msimamo wangu uko mbele zaidi kwamba Dk Slaa aliombe radhi Bunge na wabunge, kwani alichochea chuki kwa wananchi dhidi ya Bunge, halafu yeye anakuja kuchukua mshahara zaidi ya ule aliojidai kuukataa. Huu ni unafiki," alisisitiza Nape.Nape alisema Dk Slaa ni Padre hivyo pia alipaswa kuungama kwa Mungu kwa kutokuwa mkweli ndani ya dhamira yake."Bahati nzuri Dk Slaa ni Padre, namshauri pia amuombe radhi Mungu, kwani amekuwa akipita mitaani kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kumbe naye hana maadili yoyote," aliongeza Nape.

Alifafanua kwamba mshahara anaolipwa Dk Slaa ni kodi ya wananchi inayotokana na ruzuku, hivyo ni matumizi mabaya kumpa mshahara mkubwa kama huo wakati aliukataa akiwa mbunge.Kama alivyofanya katika mkutano wa kwanza aliofanya Kata ya Ulugu jimboni Iramba, Nape alisema ataendeleza mashambulizi dhidi ya Dk Slaa katika mikutano yake yote itakayofanyika mkoani Singida ili kuweka wazi maovu ya kiongozi huyo kwa kile alichokiita uchonganishi.

"Hapa naelekea Iramba Mashariki, lakini ninachosema ni kwamba, nitaendelea kuwaeleza Watanzania unafiki wa Dk Slaa. Hatutaki viongozi wanaoeneza chuki wakati wao wenyewe hawana maadili yoyote,"aliongeza.
Alisema ndani ya Chadema wapo baadhi ya watu wanalipwa kiasi cha fedha ambacho ni kidogo na wanaishi kwa shida kubwa hivyo, kama Dk Slaa ni mwadilifu awaangalie hao.

MJumbe wa kamati kuu ya Chadema Mabere Marando akionyesha ripoti ya fedha ya chama hicho kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
Chadema waja juu
Lakini mkutano na waandishi wa habari jana, licha ya kufafanua kuhusu mshahara wa Katibu Mkuu wake, Dk Slaa na ununuzi wa magari, Chadema jana  ilimuita Nape kuwa ni 'Vuvuzela' na kwamba hana sifa ya kuinyooshea kidole Chadema. “Tuna ushahidi wa kutosha kuwa mmoja wa watu walionufaika na fedha za EPA kupitia kwa Jeetu Patel ambaye ameeleza vizuri jambo hili katika maelezo yake mbele ya kamati ya Rais,” alisema Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mabere Marando alidai kuwa Nape aliwahi kuomba kugombea ubunge kupitia Chadema baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo kupitia CCM, lakini wakamtosa kwa kuwa hakuwa na sifa.

“Nilikuwapo kwenye kikao cha kumjadili Nape, tukaona kuwa hana sifa kumzidi John Mnyika ambaye sasa ni mbunge” alisema Marando. Lakini akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Nape aliwataka Chadema kutoa ushahidi unaoonyesha kuwa alihusika na ufisadi wa EPA.

“Atoe ushahidi hadharani, unajua hawa watu ni waongo, hata Watanzania watawashangaa,” alisema Nape.
Kuhusu suala la kuhamia katika chama hicho, Nape alisema: “Tena uandike kabisa, mimi ndiyo ninao ushahidi wa wao kunitaka nikagombee kupitia chama chao nikakataa, kwa sababu siwezi kuhamia kwenye chama cha Wachagga, kile ni chama cha ukoo,” alisema Nape.

Mishahara ya Makatibu Wakuu
Akifafanua mshahara wa Dk Slaa, Komu alisema kuwa Katibu wake hawajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi cha Sh 7.5 milioni kama inavyodaiwa bali analipwa Sh 1,725,000 milioni wakati mbunge analipwa Sh 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.
Alifafanua kuwa Dk Slaa pia hulipwa Sh900,000 za mafuta kwa ajili ya kwenda na kurudi ofisini. Vingine ni malipo ya nyumba, mawasiliano na uwajibikaji na hivyo kuufanya mshahara wake kufikia Sh7,174,000 kwa mwezi.

“Sekretarieti ya Kamati Kuu ilipeleka pendekezo hilo katika vikao vyake vya Kamati Kuu na Baraza Kuu na pendekezo hilo likapitishwa kwa njia ya uwazi na likaingizwa katika mpango kazi wa chama,”  alisema Komu.
Naye Mabere Marando alikituhumu CCM kuwa kinamlipa Katibu Mkuu wao Sh 11 milioni akisema:  “CCM wanapigia kelele mshahara wa Dk Slaa, mbona Mukama (Wilson) analipwa Sh11 milioni?. Mbona Rais Jakaya Kikwete analipwa posho nyingi tu? Ofisi yake iko Dodoma, lakini akienda huko analipwa posho, akirudi Dar es Salaam analipwa,” alisema Marando.

 Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai ya Marando, Mukama alikataa kutaja mshahara wake akisema kuwa ni siri yake.
 “Mimi leo ndiyo natimiza mwezi mmoja tangu niingine ofisini, hata mshahara wenyewe sijauona. Mshahara ni siri yangu mwenyewe, nimeingia hapa baada ya kustaafu kwa hiyo ndiyo hivyo, naomba msiniingize kwenye hizo ‘debate’ (malumbano)” alisema Mukama.

Lakini akijibu hoja hiyo, Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara kulingana na daraja la viongozi na hurekebishwa kama watendaji wengine serikalini.
“Katibu Mkuu wetu analipwa Sh1.5 milioni na hukatwa kodi. Vilevile hulipwa posho isiyokatwa kodi ya Sh300,000. Hayo mengine ya usafiri ni mambo ya kawaida tu. Usafiri anao na hulipiwa umeme wa LUKU na nyumba. Siyo suala la kificho hilo,” alisema Nape.

Mafuso ya Chadema
Wakijibu hoja ya Nape kuwa Chadema kimenunua magari chakavu, walikanusha wakisema kuwa magari hayo licha ya kutokuwa chakavu, siyo magari ya kawaida bali ni mitambo maalumu ya uenezi.

“Katika magari hayo kuna vipaza sauti (Public addressing system 3 sets) zenye thamani ya dola za Marekani 148,000 (Sh 222 milioni), jenereta tatu kila moja Sh15.5 milioni sawa na Sh47,000,000,” alifafanua Komu.

Naye Marando alisema kuwa chama ndiyo kilimwomba Mwenyekiti Freeman Mbowe awauzie magari hayo ndipo akakubali. “Mimi mwenyewe nilihusika kumwomba Mbowe atupe magari yale, akakubali. Baada ya hapo Kamati Kuu iliunda kamati ya watu wanne chini ya makamu mwenyekiti Zanzibar Mohamed Issa kumwomba mwenyekiti akiachie chama magari hayo.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema kuwa CCM inatumia ujinga wa Watanzania kama mtaji wake na kuwataka Watanzania kutoyumbishwa na propaganda za CCM.

Thursday, May 12, 2011

SI HAKI KUFUNGA SHULE KWA UTOFAUTI WA ITIKADI ZA VYAMA

Wabunge Chadema wageuka mbogo  Send to a friend
Wednesday, 11 May 2011 21:27
0diggsdigg
Boniface Meena, Kwela
WABUNGE wawili wa Chadema jana walikuwa mbogo baada ya kufanya ziara katika Kijiji cha Lusaka, Jimbo la Kwela, mkoani Rukwa na kubaini  Shule ya Sekondari Lusaka imefungwa bila maelezo.Mbali na hilo wabunge hao waliwaeleza wananchi kwamba wamebaini mbolea ya ruzuku inayotolewa na serikali ni ufisadi mtupu kwa sababu wananchi wanatozwa fedha nyingi kununua mbolea ya ruzuku.

Wananchi wa Kijiji cha Lusaka walilalamika mbele ya wabunge hao kwamba Serikali imekuwa ikiwanyanyasa na kibaya zaidi imefunga Shule ya Sekondari ya Kijiji hicho baada ya wananchi wa eneo hilo kumchagua Diwani wa Chadema.

Mbali na hilo wananchi hao walilalamika mbele ya wabunge hao kwamba shule hiyo iko moja tu katika eneo hilo na ilifungwa ghafla miezi mitatu iliyopita na viongozi wa Seriklali wa Manispaa ya Sumbawanga Vijijini bila kutoa maelezo yoyote.

Baada ya kusikia malalamiko ya  wananchi wa eneo hilo, Mbunge wa Viti Maalumu kutoka mkoani Arusha, Joyce Mukya na Raya Ibrahimu kutoka Zanzibar walikwenda katika shule hiyo na kuwaona madiwani wakiendelea na kikao na kushindwa kupata maelezo kutoka kwa madiwani na mbunge wa jimbo hilo.

Mukya aliwaambia wananchi hao kwamba atapambana na viongozi wa halimashauri hiyo ili ajue ni kwa nini shule hiyo imefungwa bila maelezo na kusababisha wanafunzi kutokwenda shuleni.

"Yani ni aibu, nitakufa nao kwa kuwa wamefunga shule halafu wanafanyia vikao vya madiwani kwenye majengo ya shule bila kujali haki za wanafunzi kusoma, hawa watu sijui ni wa aina gani,"alisema Mukya.

Alisema hilo ni moja ya maswali atakayowasilisha bungeni kwenye maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu ili aelezwe ni kwa nini shule hiyo imefungwa."Kata ina vijiji vitano, tunataka tujue ni kwa nini shule imefungwa, tutaliwasilisha bungeni kutaka kujua hilo. Inashangaza sana kwa nini mbunge wenu ananyamaza kuhusu shule kufungwa na anafanya mikutano huko ndani bila hata kujali,"alisema.

Raya Ibrahimu alionekana kuchukizwa na kitendo hicho na kuishambulia serikali kwa kushindwa kuwajali wananchi wake hasa wanachanga fedha zao kujenga shule, lakini zimekuwa zikifungwa bila wananchi kuelezwa sababu za kufanya hivyo.

"Unajua hawa watu wanatia aibu, mimi sijui ni wa aina gani watu wazima wanafunga shule bila kufikiria madhara gani wanafunzi wanapata, halafu wakikimbilia mijini wanalalamika," alisema.

Alisema kitendo kilichofanywa na Serikali kinatia aibu kwa kuwa kinasababisha vijana kukimbilia mijini kwa ajili ya kuuza pipi na biskuti.

Raya alisema suala la huduma za jamii limekuwa ni vituko kijijini ambako kuna barabara mbovu na aliwashauri wananchi kuipunzisha CCM ili wajifunze kuwajali wananchi wao.

Kuhusu mbolea alisema ni bora serikali ikaondoa ruzuku kwenye mbolea ili ishuke bei na wananchi wanunue kwa bei ya chini."Serikali iondoe vocha za ruzuku kwa kuwa zinafaidisha watu wachache na kuwaumiza wananchi wengi ambao ni masikini,"alisema Mukya.

Alisema nchi inanuka rushwa kwa sababu wananchi wamekwua wakilalamika kutopata mbolea kwa kuwa kila mtu ni mla rushwa."Viongozi wa CCM wanachukua zile vocha wanajigawia. mwananchi maskini akitaka vocha mpaka utoe rushwa, mbolea ni kwa ajili yenu ninyi watu maskini ili mjikomboe kwa vijana kufanya shughuli za kilimo, lakini inashindikana kutokana na ufisadi unaofanyika kwenye vocha hizo,"alisema Mukya.

LOLIONDO IKIWEKEWA MIKAKATI MIZURI INAWEZA KULIINGIZIA TAIFA PESA NYINGI ZA KIGENI,WAZIRI WA UTALII UNAMPANGO GANI?

Marais, mfalme watarajiwa kutua Samunge kwa Babu  Send to a friend
Wednesday, 11 May 2011 21:50
0diggsdigg
Abiria waliofika kwa mchungaji Ambilikile Mwasapila katika kijiji ch Samunge kunywa dawa jana, wakiteremka kutoka katika helikopta inayomilikiwa na kampuni ya Akagera aviation ya Rwanda. Picha na Mussa Juma
Mussa Juma, Samunge
MARAIS kadhaa wa nchi za Afrika akiwamo mfalme, wanatarajiwa kwenda Samunge, Loliondo kupata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapila.

Kutokana na ujio huo, ulinzi umeimarishwa kuanzia jana. Ofisa mmoja wa polisi wa Wilaya ya Ngorongoro, alithibitisha ujio wa wakuu hao bila ya kutaka kutoa maelezo zaidi. Hakutaja siku wala muda ambao watawasili hapa.
Jana kulikuwa na idadi kubwa zaidi ya polisi kijijini hapa. Ofisa mwingine wa polisi ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe alisema, wamepokea taarifa za ujio wa marais hao na walitegemea kwamba wangewasili Samunge kuanzia jana.

 "Ni kweli, kuna wageni watakuja. Nadhani ni wakubwa bado taarifa kamili hazijatufikia watatua lini," alisema.
Helikopta kutoka Rwanda inayomilikiwa na Kampuni ya Akagera Aviation, imeanzisha safari za kwenda Samunge kila siku ikitokea Uwanja wa Ndege wa Arusha.

Helikopta hiyo ni kubwa kuliko nyingine ambazo zimekuwa zikitua Samunge kuleta wagonjwa kupata tiba ya kikombe kwa Babu.Ujio wa helikopta hiyo, sasa unalifanya anga la Samunge kutawaliwa na helikopta nne, zinazofanya safari takriban mara tatu kwa siku kwenda na kutoka Samunge.

Gharama za nauli kwa abiria mmoja kutoka Arusha hadi Samunge kwa helikopta hiyo ya Rwanda ni Dola za Marekani 1,000 hivyo kufanya usafiri huo kuwa wa watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
 Baada ya kuongezeka wimbi la viongozi kutoka nchi jirani ya Kenya wanaofika Samunge na habari zao kuandikwa, sasa vigogo wengi wa huko wamebuni njia nyingine ya kufika kijijini hapo bila kujulikana.

Vigogo hao sasa wanafika Samunge kupitia mpaka wa Narock ambako huenda moja kwa moja hadi Loliondo na kukodi magari ya wenyeji ili kuwapaleka Samunge.  Kwa takriban wiki mbili sasa, viongozi kadhaa wa Serikali ya Kenya, wakiwamo maofisa wa Ikulu ya Kenya, mawaziri na wabunge wamekuwa wakitua Samunge.

Babu: Wagonjwa waruhusiwe
Mchungaji Mwasapila ameomba vituo vinavyoratibu magari yanayokwenda Samunge, kuruhusu magari zaidi kupeleka wagonjwa ili wapate huduma kutokana na kupungua kwa foleni.Msaidizi wa Mchungaji Mwasapila, Frederick Nisajile alisema jana kwamba kutokana na huduma kuboreshwa, idadi ya magari yanayopaswa kuingia Samunge kwa siku yanapaswa kuongezeka.

"Tunaomba wawe na mawasiliano na sisi ya mara kwa mara kwani sasa kama unavyoona hakuna foleni, lakini kuna magari yamezuiwa maeneo ya vituo yasije huku," alisema Nisajile.

Jana, zaidi ya magari 500 yakiwamo mabasi makubwa kutoka Mikoa ya Kigoma, Dodoma, Mwanza na Arusha yalifika Samunge na abiria kupata kikombe na kuondoka.Hadi majira ya tisa jioni jana, foleni ya magari ilielekea kumalizika kabisa.

Bei ya kikombe iko palepale
Mchungaji Mwasapila jana alitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya kikombe akieleza kuwa hajawahi kupandisha gharama zake tangu mwanzo. Alisema Watanzania wanalipa Sh500 na wageni kutoka nje ya nchi, wanalipa Dola moja au Sh1,500.

JE KAULI NAPE WA CCM INAATHARI KWA CHADEMA?

Chadema, CCM sasa ni kulipuana  Send to a friend
Wednesday, 11 May 2011 21:53
0diggsdigg
Gasper Andrew, Singida na Boniface Meena, Nkasi
VITA ya maneno baina ya vyama vikubwa vya siasa nchini CCM na Chadema, imezidi kushika kasi kwa vyama hivyo kurushiana tuhuma katika mikutano ya hadhara inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.CCM kinawaita Chadema wanafiki na Chadema kinaendelea kudai kuwa chama hicho tawala ndicho kinachoisababishia nchi umasikini.

Jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alidai kuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ni mnafiki kwa kula matapishi yake anapodai kuwa chama tawala kinafuja mali ya umma huku naye (Dk Slaa) akiwa katika mwelekeo huohuo.

Alidai kuwa Dk Slaa ameingia mikataba ya kukishinikiza chama chake kimlipe Sh7.5 milioni kila mwezi wakati alipokuwa mbunge alikuwa akiilalamikia serikali kwamba inawabebesha wananchi mzigo mkubwa kwa kuwalipa wabunge kila mmoja Sh milioni sita. Nape alisema hayo jana alipokuwa akizungumza kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katikia Kituo Kikuu cha mabasi cha zamani mjini Singida.

Alisema anazo nyaraka halali za chama hicho zinazoonyesha kwamba baada ya Dk Slaa kuukosa urais, sasa amekigeukia chama chake na kuanza kukishinikiza kimlipe mshahara mkubwa kuliko aliokuwa akiupata alipokuwa mbunge.Nape alisema madai kwamba Dk Slaa haombi alipwe si ya kweli akidai kwamba ndiye anayeshiniza kulipwa kiasi hicho kwa vile ameachishwa ubunge na ameukosa urais.

"Anashangaza sana bungeni alikuwa akipanua mdomo hadi mwisho kupotosha jamii kuwa wabunge pamoja na posho, mishahara na marupurupu mengine, wanalipwa shilingi milioni sita kiasi ambacho alidai kuwa kinawaumiza wananchi. Kwa hiyo ndiyo tuseme Sh7.5 milioni ni kiwango ambacho hakitawaumiza wanachama wa Chadema na walipa kodi wengine," alihoji Nape huku akishangiliwa na wananchi waliohudhuria.

 Katibu huyo alisema kwa kitendo chake hicho cha kushinikiza alipwe kila mwezi mamilioni hayo, anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadanganya alipokuwa bungeni kuwa Sh milioni sita ni mshahara mkubwa mno.
 Aidha, alisema kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliwahi kutoa msaada wa Fuso (malori aina ya Mitsubishi Fuso) tatu ili zikisaidie chama hicho katika shughuli mbalimbali za ustawi wake lakini sasa anakidai Sh500 milioni za ununuzi.

Madai ya Nape kuhusu mshahara wa Dk Slaa yaliwahi kutolewa maelezo na Chadema ambacho kilisema kilifikia uamuzi wa kumlipa, Dk Slaa mshahara na maslahi yanayolingana na anayopata mbunge kwa sababu ndicho kilichomshawishi aache kugombea ubunge katika Jimbo la Karatu mkoani Arusha, ambako alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda na kumtaka agombee nafasi ya urais ambayo mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alishinda.

Kilisema uamuzi huo ulifuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na vikao vikuu vya chama hicho, kama vile Kamati Kuu, kuidhinisha malipo hayo.Kuhusu malori Chaadema kilisema kiliamua kufanya mkakakti wa kununua magari matatu ambayo Mbowe aliyanunua na kuyatoa kwa muda ili yakisaidie kwenye kampeni.

Mbowe: CCM wanajipa mamlaka ya uungu mtu
Wakati Nape akisema hayo Mbowe amesema viongozi wa Serikali ya CCM wamelewa madaraka na kujivika mamlaka ya uungu watu na kusahau kuwatumikia Watanzania: "viongozi wa nchi hii, wanajipa mamlaka ya umungu-mtu na wananchi wanawaogopa."
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa mji mdogo wa Namanyere, Wilaya ya Nkasi, Rukwa, ikiwa ni sehemu ya operesheni ya Chadema ya kuishinikiza serikali kusikiliza kilio cha wananchi.

Alitoa mfano akisema, iwapo wananchi wa Wilaya ya Nkasi watajengewa barabara, wajue kuwa hiyo ni haki yao na pia wana haki ya kuiuliza serikali sababu za kuchelewa kujengewa kwa miaka 50 ya uhuru.
Alisema katika mkoa kama wa Kilimanjaro, wamekuwa wakijengewa barabara za lami kwa kadri inavyohitajika, tofauti na Mikoa kama ya Rukwa, Iringa, Mbeya na Ruvuma ambayo imeachwa nyuma kimaendeleo, licha ya kuzalisha chakula kinachohifadhiwa katika Hifadhi ya Chakula ya Taifa.

Kutokana na hali hiyo, alisema iwapo wananchi wa Mkoa wa Rukwa hawatapiga kelele kudai maendeleo, kamwe hawezi kushuka Malaika Gabriel kuwapigia kelele."Kwa hiyo ndugu zangu, si kila kitu ni cha kupongeza, muwatume wabunge wenu wakapige kelele," alisema Mbowe.Alisema tangu Chadema ianze kupiga kelele Rukwa, imefanikiwa kutoa Mbunge mmoja tu, Said Arfi na barabara zikianza kutengenezwa.

Mbowe alisema serikali imeshindwa kusimamia reli ya kati kiasi ambacho wananchi wanaotaka kusafiri kulazimika kutumia gharama kubwa kupata usafiri wa ndege.Alisema kuwa baadhi ya wabunge kutumia muda mwingi bungeni kuishukuru serikali katika mambo ambayo ni wajibu wake kuwatekelezea wananchi.Alisema wabunge hao wamekuwa wakifanya hivyo, huku wakijua wazi kuwa ni kinyume na jukumu la mbunge, ambalo ni kuisimamia serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.
"Kitendo cha kuishukuru serikali, ndicho kinatuchelewesha kupata maendeleo. Wananchi wanaiomba serikali, wabunge wanaishukuru..." alisema.Alisema vitendo hivyo vimechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya viongozi wa serikali nchini kujiona kuwa ni miungu kwa sababu wanatukuzwa.

Waliopewa siku 90 CCM wataaibika karibuni
Katika hatua nyingine, Nape alisema kuwa viongozi walioombwa na chama wajipime wenyewe na kuchukua uamuzi wa kuachia nyadhifa zao mapema kutokana na kutuhumiwa na wananchi juu ya tabia zao za kifisadi, kwamba sasa siku zao za kuja kuaibishwa, zinahesabika.

"Watu sasa wameanza kusema kuwa Nape hana nguvu tena za kupambana na ufisadi nchini, nawaambia kuwa si kweli. Sijalala wala sijaishiwa nguvu za kutokomeza ufisadi. Hawa wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanakipa chama machungu na kuanza kukikosesha imani kwa wananchi, wanapaswa kujiondoa wenyewe na wasisubiri kuja kuapishwa kwa kufukuzwa kwa nguvu," alisema.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chilingati aliwataka viongozi na wanachama wa chama hicho ngazi ya wilaya na mikoa kusaidia kukirudisha kwenye misingi yake ya awali ili wananchi waendelee kukiamini.
Chiligati ambaye pia ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, alitoa wito huo juzi alipozungumza na wananchi wa Kata ya Ikungi, Singida.
Alisema vikao vya Halmashauri Kuu vilivyofanyika hivi karibuni mjini Dodoma, vilibaini kuwa CCM imefika mahali pabaya kwa kuanza kuacha misingi yake na kusababisha baadhi ya wanachama wake na wananchi kwa ujumla, kuanza kukosa imani nacho.

Tuesday, May 10, 2011

MAPUMZIKO NI MUHIMU KWA WANAFUNZI

Je, wanafunzi huhitaji kupumzika?  Send to a friend
Monday, 09 May 2011 21:30
0diggsdigg
Na Minael Msuya
NIMEWAHI kusikia baadhi ya wanafunzi wakilumbana kuhusu suala la mapumziko pindi wanapomaliza masomo na kurudi majumbani mwao.Malumbano yao yalinifanya nitafakari kwa kina kuhusu elimu husika na mapumziko hayo ndipo nilipojaribu kuwauliza wadau wa elimu.

Wadau hao walinifafanulia kuwa hakuna kazi isiyokuwa na mapimziko, hivyo masomo yanahitaji mapumziko ili mwanafunzi aweze kurejesha akili mpya na kufanya kazi kwa umakini zaidi.

Wanafunzi hao waliokuwa wakilumbana kuhusu mapumziko, baadhi walisema baada ya kutoka shuleni mwanafunzi anapaswa kupata muda mfupi wa kupumzika ili aweze kupata nguvu na akili yake iweze kutulia.

Walisisitiza kuwa mtu anaposoma wakati wote anachoka akili na mwili wake unashindwa kumudu kufanya hata kazi za kawaida mbali na masomo hivyo kila kitu kina faida zake katika kuimarisha mwili na akili ya mtu.
Lakini, wengine walisema baada ya kutoka shule mwanafunzi anapaswa kufanya kazi za nyumbani ili asipoteze muda wake wa kujisomea suala ambalo kimsingi halikuwa na nguvu kwa kuwa tayari wadau wa mambo hayo walisema kila kazi inahitaji mapumziko.

Katika  udadisi  wangu niligundua kuwa wapo wanafunzi wanaojitengea muda mzuri wa kusoma na kufanya kazi pindi wanapotoka shuleni lakini wanasahau kuwa wanapaswa kupata muda wa kupumzisha akili zao japo kwa robo saa.
Hata hivyo fikra zangu zilifika mbali na kujikuta nikiwamulika wazazi kuhusu kuwapangia watoto wao muda wa kazi na kusoma, hapo nilitambua kuwa wazazi wanaweza kuwa chanzo cha kuwafanyisha watoto kazi pindi wanapotoka shuleni kuliko kuwapa muda wa kupumzika na kujisomea.

Katika hili wadau wa elimu wanasema mwanafunzi anapojisomea bila mpangilio wowote ukiwemo muda wa kupumzika anaweza asifikie malengo yake kwa kuwa atakuwa anajichosha kwa kudhani kuwa atafanikiwa kumbe anapotea.

Ni vyema kila mwanafunzi akatambua wajibu wake kimasomo, kupumzika na kusaidia kazi za nyumbani ili aweze kuimarisha afya na kutengeneza msingi mzuri utakaomfanya afaulu vizuri kwa kuzingatia mambo hayo matatu.

Wazazi nao wanatakiwa kuwapangia watoto wao muda wa kupumzika, kujisomea  na kufanya kazi za nyumbani na si kuwapangia watoto kazi  wanapotoka shuleni bila kuwapa muda wa kupumzika.

Wapo baadhi ya wazazi wanawapangia watoto wao kazi nyingi pale wanapotoka shuleni bila kufahamu kuwa watoto wamechoka kwa kiwango gani walipokuwa shuleni.

Kufanya hivyo kutamsaidia mwanafunzi yeyote yule kuweza kumudu masomo yake vizuri kwa kuwa atakuwa na uwezo wa kusoma na kufanya kazi kwa wakati na hata kuweza kupumzisha akili yake pale inapokuwa imechoka.
 

MAISHA NI MAGUMU MNO,

JK: Pato litaongezeka muhula huu  Send to a friend
Monday, 09 May 2011 21:44
0diggsdigg
Habel Chidawali,Dodoma
Rais Jakaya Kikwete, amesema kasi ya kukua kwa pato la Mtanzania ni ndogo na kwamba  juhudi za makusudi lazima zifanyike ili kuongeza pato hilo.Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma, alipokuwa akifungua semina elekezi kwa viongozi na watendaji wakuu kwa serikali.

Hata hivyo alitamba kuwa pato la Mtanzania litaongezeka katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa na kwamba hiyo inatokana na baadhi ya nchi wahisani, kuahidi kuongeza misaada kwa Tanzania.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, umasikini umepungua kwa asilimia mbili tu, lakini alisisitiza kuwa hiyo itabadilika kwa kiwango kikubwa katika muhula wa pili na mwisho wa uongozi wake.

Alisema mkakati uliopo  sasa serikalini ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025, Tanzania inakuwa nchi yenye uchumi wa kati na pato la Mtanzania wa kawaida linatarajia kufikia kati ya Dola 2,500 na 3,000 za Marekani, ikilinganishwa na Dola 600 za sasa.

Kuhusu kipindi cha miaka mitatu alisema kama mipango ya wahisani na Benki ya Dunia, itakuwa mizuri na kukubali kuisaidia Tanzania Dola 2.8 milioni za Marekani, taifa litakuwa katika nafasi mzuri ya kutengeneza ajira na kupambana na umaskini.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo wa nchi alisema hali ya nchi ni salama na itaendelea kuwa salama kama Watanzania, watashikamana na kuwa wamoja.Semina hiyo ilihudhuriwa na Waziri mkuu, Jaji mkuu, Mwanasheria mkuu mawaziri, manaibu mawaziri,makatibu na manaibu makatibu wakuu na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya.Mada zinazotarajia kutolewa katika semina hiyo itakayodumu kwa ipindi cha siku nne ni pamoja na masuala ya uongozi itakayowasilishwa na Msekwa.

Mada nyingi ni ushirikiano wa viongozi wa serikali na vyama vya siasa itakayowasilishwa Msuya, Masuala ya Uchumi (Mwakilishi wa Benki ya Dunia),Ulinzi (Wakuu wa vyombo vya Ulinzi)  na masuala ya Muungano ambayo yatazungumzwa na viongozi wahusika.

Katika semina hiyo serikali inapanga mipango ya muda mfupi na muda wa kati itakayoitekeleza katika kipindi cha miaka mitano.

Semina hiyo imefadhiliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki ya NMB.

KIKWETE MAWAZIRI WAKO UMEWAPA MAJUKUMU MENGI MNO,MAWAZIRI WKO NDIO WABUNGE,WAKUU WA MIKOA,WAJUMBE WA NEC! JE NI MUDA UPI WATAFUATILIA KERO ZA WANANCHI?

Kikwete alia na mawaziri mizigo  Send to a friend
Monday, 09 May 2011 21:54
0diggsdigg
Rais Jakaya Kikwete
Habel Chidawali, Dodoma
RAIS Jakaya Kikwete amewataka mawaziri na makatibu wakuu kujiamini katika utendaji wao wa kazi badala ya kutegemea maelekezo ya mamlaka zilizo juu yao.Alisema hayo jana alipokuwa akifungua semina elekezi kwa viongozi na watendaji wakuu wa Serikali iliyofanyika katika Ukumbi wa St Gasper nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma.“Hadi leo sijui kwa nini hasa watu (mawaziri) wanashindwa kuzungumza mambo yaliyofanywa na Serikali na kuwapa uwanja mpana wenzetu wa upande wa pili (wapinzani) ambao wanajua kweli kuvitumia vyombo vya habari. Sisi tunaendelea kulalamika kila siku kwamba hatuandikwi, nani atakuandika wakati hutoi taarifa,” alisema Kikwete.


“Kuna wakati waziri mmoja aliwahi kunipigia simu na kusema 'Mheshimiwa Rais habari hii tuikanushe?' Nilichokifanya nilimwambia pima wewe baada ya hapo nikakata simu,” alisema
Rais Kikwete alisema kitendo cha mawaziri kukataa kutoa habari na kuwafanya maofisa habari wa wizara kuwa kama waandishi wa habari ni hatari kwa serikali.


Katika hotuba yake, Rais Kikwete aliwataka watendaji hao kufanya kazi kwa kufuata misingi ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu ili kukwepa hasara inayoweza kutokana na uamuzi usiofuata kanuni na kuiaibisha Serikali.
"Ni muhimu kwenu kama viongozi mkajielimisha juu ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi katika sehemu zenu za kazi. Uhalali wa maamuzi mtakaoyafanya hupimwa na sheria," alisema Kikwete na kuongeza:
"Ukifanya uamuzi unaokinzana na sheria utahojiwa wewe binafsi lakini pia utaibebesha Serikali mzigo wa hasara na fedheha itakayotokana na uamuzi huo. Uamuzi usiofuata sheria unaweza kuwa na madhara kwa wananchi.
"Heshimuni Katiba na fuateni sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yenu. Katika semina hii masuala hayo yatafafanuliwa na kuzungumzwa. Kadhalika, uhusiano wa Serikali na mihimili mingine ya dola yaani, Bunge na Mahakama utafafanuliwa."


Rais Kikwete pia aliwataka watendaji hao kuepuka kauli na vitendo vinavyoweza kuwafarakanisha na kuleta mgawanyiko katika Serikali ili kulinda dhana ya uwajibikaji wa pamoja.
"Viongozi na watendaji wakuu wa wizara hamna budi kujenga uhusiano mzuri na uwajibikaji wa pamoja. Haifurahishi kuona waziri na katibu mkuu au waziri na naibu waziri; naibu waziri na katibu mkuu au katibu mkuu na naibu katibu mkuu hawaelewani."


"Wanasemana na hata wanapingana hadharani, yaani mbele ya wafanyakazi. Baya zaidi ni pale wanapopingana katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi au utendaji wa wizara au serikali kwa jumla. Hayo si maadili mema katika taasisi yoyote.


"Kama unaona vigumu kuuafiki ni bora kutoka. Hairuhusiwi kupinga taasisi ambayo wewe umo ndani kama mmoja wa viongozi wake. Ni vyema hili likaeleweka. Msitupe tabu ya kuulizana maswali na kuwasemea."
Rais Kikwete pia aliwataka watendaji hao kuwa mstari wa mbele kuzungumzia mafanikio ya Serikali ili kuziba midomo ya wapinzani wanaopita kila kona nchini na kuwaeleza wananchi kuwa haijafanya chochote.


"Sijui kwa nini hatuwi wepesi kuyasemea mafanikio mengi tuliyoyapata tukaacha wasiotutakia heri wanaosema hatukufanya kitu wasikike mpaka waonekane wanasema kweli," alisema.


Alisema hajui na hana majibu mazuri ya kwa nini Serikali imekuwa ikishindwa kuzungumza mambo mazuri yaliyofanywa katika kipindi cha miaka mitano na hata wakati mwingine kushindwa kuzungumza jambo hadi wampigie simu, kitu ambacho ni aibu.


Alisema kuna udhaifu katika kujipanga kwa wasemaji kutokana na kuchelewa kutoa taarifa au kukanusha habari ambazo zimekuwa zikitolewa na upinzani, jambo linalowafanya wananchi waamini kuwa ni kweli, kwani uongo ukizungumzwa mara nyingi hugeuka na kuwa ukweli.


“Unajua mimi sijui hadi leo ni kwa nini hasa watu wanashindwa kuzungumza mambo yaliyofanywa na serikali na kuwapa uwanja mpana wenzetu wa upande wa pili ambao wanajua kweli kuvitumia vyombo vya habari huku sisi tunaendelea kulalamika kila siku kwamba hatuandikwi, nani atakuandika wakati hutoi taarifa,” aliuliza Kikwete.


Alikanusha madai kuwa baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari za upinzani na kuacha habari nzuri za serikali na badala yake akasema woga na urasimu uliowajaa wasemaji katika serikali, ndilo tatizo hasa kwa kuwa hawajui kuwa vyombo vya habari vinatafuta habari na kama wao hawatoi habari ni lazima waandike zile zinazotolewa na upande wa pili.


Katika hatua nyingine, Kikwete alisema kuwa anategemea kuona Serikali yake ikifanya kazi kwa umoja na ushirikiano mkubwa katika kipindi hiki cha miaka mitano na kwamba kushirikishana na kupeana habari iwe ndiyo dira ya maendeleo yao.


Sikuteua mawaziri wa kusoma mafaili ofisini
Aliwataka viongozi hao kuacha umangimeza, badala yake watoke ofisini kujionea matatizo ya wananchi.
"Mawaziri na makatibu wakuu lazima mtoke. Hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujua mambo yahusuyo wizara zenu na ndiyo njia bora ya kuongoza: kuona wenyewe na kutenda," alisema Rais Kikwete na kuongeza: "Hii itawafanya mjiamini kuelekeza na pia mnaposimama mbele za watu na kusema. Msiwe mamangimeza. Tokeni, tembeeni kuona shughuli zenu. Tembeleeni wananchi muwafahamu, wawafahamu, mjue shida zao muwatatulie."


Alikemea tabia ya viongozi hao kushinda kwenye mitandao kila siku na kusoma ujumbe badala ya kwenda kuwatumikia wananchi vijijini.Alisema tabia hiyo haipaswi kuvumiliwa hata kidogo na akaonya viongozi wa namna hiyo wataishia kuwa wababaishaji na hatakwenda nao katika kipindi chake cha uongozi.


“Mimi sikuteua mawaziri wa kusoma mafaili ofisini, bali niliteua watu wanaoweza kukimbizana kwa kasi zaidi, ari zaidi pamoja na nguvu zaidi, kwani nataka kuwasikia mkichakarika huko kwenye miradi mlikopeleka fedha, siyo kupokea taarifa ofisini bila ya kujua fedha za walipa kodi zinatumikaje huko.”


Dawa ya mawaziri hawa ipo jikoni
Rais Kikwete pia aliwatahadharisha mawaziri ambao wamekuwa wakipinga kauli na miswada ya mawaziri wenzao, huku wengine wakiwa wanatoa siri za Serikali.Alisema kuwa watu wa namna hiyo dawa yao iko jikoni kwa kuwa kitendo wanachokifanya si kizuri ndani ya Serikali.


Alisema anayo mamlaka ya kuchagua na ya kumwondoa waziri wakati wowote akiamua, hasa kama haoni umuhimu wa kuendelea na mtu wa aina hiyo.


“Katika hili nawaambia mapema kabisa kuwa waziri anayeishi kwa kupinga miswaada ya Serikali ajue kuwa anaipinga Serikali na hivyo sitakuwa tayari kufanya kazi na mtu wa aina hiyo. Sehemu kubwa ya kazi zenu mawaziri nataka ziwe za Serikali na zile za jimbo mtajua namna mtakavyojipanga bila ya kuharibu kazi za Serikali,” alisema.


Pato la Mtanzania litakua miaka mitatu ijayo
Rais Kikwete alisema kasi ya kukua kwa pato la Mtanzania ni ndogo na kwamba kunahitajika juhudi za makusudi katika kuongeza pato hilo. Hata hivyo, alitamba kuwa pato la Mtanzania litaongezeka katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa kutokana na baadhi ya nchi wahisani kuahidi kuongeza misaada kwa Tanzania.


Alisema katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, umaskini umepungua kwa asilimia mbili tu hivyo, akaahidi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya awamu ya pili ya uongozi wake, umaskini utapungua kwa kiasi kikubwa.


Alisema mkakati uliopo hivi sasa serikalini ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025, Tanzania inakuwa nchi yenye uchumi wa kati pato la Mtanzania wa kawaida likitarajiwa kufikia Dola za Marekani 2,500 hadi 3,000. Sasa ni Dola 600. Kuhusu kipindi cha miaka mitatu, alisema kuwa, ipo mipango mizuri kutoka kwa wahisani, ikiwamo Benki ya Dunia ambayo imekubali kuisaidia Tanzania kiasi cha Dola 2.8 milioni ambazo zinaweza kusaidia katika kutengeneza ajira na kupambana na umaskini.


Semina hiyo ilihudhuriwa na watendaji wote wa Serikali wakiwamo Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, mawaziri na manaibu waziri, makatibu na naibu makatibu wakuu, Mwanasheria Mkuu na naibu wake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na viongozi wastaafu, akiwamo Spika wa zamani na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya.

Wednesday, May 4, 2011

HATIMAYE AROBAINI YA OSAMA BIN LADEN YATIMIA


World 'safer' without Bin Laden, says barack obama

Map showing location of compound where Bin Laden was killed
Bin Laden killed: How it happened
More details are emerging of how al-Qaeda leader Osama Bin Laden was found and killed at a fortified compound on the outskirts of Abbottabad in north-west Pakistan.
The compound is a few hundred metres from the Pakistan Military Academy, an elite military training centre, which is being described as Pakistan's equivalent to Britain's Sandhurst or the West Point academny in the US.
There were conflicting reports about the compound's distance from the academy, with Pakistan's military saying they are as much as 4km (2.4 miles) apart.
In any case the compound lies well within Abbottabad's military cantonment, and it is likely the area would have had a constant and significant military presence and checkpoints.
Pakistan's army chief is a regular visitor to the academy, where he attends graduation parades.
The operation against Osama Bin Laden began at about 2230 (1730 GMT) and lasted about 45 minutes, military sources told BBC Urdu. Two or three helicopters were seen flying low over the area. Witnesses say they caused panic among local residents.
One report of the operation emerged in real-time: Sohaib Athar, an IT consultant living in Abbottabad, posted on Twitter at about 0100 (2100 GMT) that a helicopter was hoveringabove the city.
He continued tweeting as the operation unfolded before eventually realising: "Uh oh, now I'm the guy who liveblogged the Osama raid without knowing it.
Barbed wire and cameras The target of the operation was the compound, which had at its centre a large three-storey building.

Abbottabad

  • Abbottabad - known as "city of pines"- is a small town nestled in the beautiful lush, green hills of north-west Pakistan.
  • It is an agricultural community, but with a population of about 120,000, it provides a centre for many of the neighbouring villages
  • It is a military garrison town and has one of Pakistan's most prestigious training academies
  • It takes its name from British Major James Abbott who founded it in 1853 after he annexed the Punjab area
When the helicopters landed outside, men emerged from the aircraft. The raid was conducted by a special team of US Navy Seals.
People living in the area, known as Thanda Choha, told BBC Urdu that they were commanded in Pashto to switch off their lights and not to leave their homes.
Shortly afterwards residents said they heard shots being fired and the sound of heavy firearms.
At some point in the operation one of the helicopters crashed, either from technical failure or having been hit by gunfire from the ground.
The compound was about 3,000 sq yds in size but people from the area told the BBC that it was surrounded by 14ft-high walls, so not much could be seen of what was happening inside.
The walls were topped by barbed wire and contained cameras.
There were two security gates at the house and no phone or internet lines running into the compound.
'Waziristan Mansion'
After the operation witnesses said all they could see was fire snaking up from inside the house.
Osama Bin Laden did resist the assault and was killed in battle, US officials told White House reporters.
Footage from inside Bin Laden's compound
The officials described the operation as a "surgical raid" and said three adult males, including Bin Laden's adult son, were killed. But, they added, a woman who was being used as a shield was also killed.
According to local residents speaking to BBC Urdu the forces conducting the operation later emerged from the compound, possibly with somebody who had been inside.
They said that women and children were also living in the compound.
One local resident told the BBC Urdu that the house had been built by a Pashtun man about 10 or 12 years ago. The resident said that none of the locals were aware of who was really living there. However, the New York Times said US officials believed that the house was specially built in 2005.
According to one local journalist, the house was known in the area as Waziristani Haveli - or Waziristan Mansion.
The journalist said it was owned by people from Waziristan, the mountainous and inhospitable semi-autonomous tribal area close to the Afghan border, which until now most observers believed to be Bin Laden's hiding place.
This house was in a residential district of Abbottabad's suburbs called Bilal Town and known to be home to a number of retired military officers from the area.
Intelligence officials in the US are quoted by AP as saying that the house was custom-built to harbour a major "terrorist" figure.
'Trusted' courier
Compound in Abbottabad Police walk past the compound where the battle took place
As details of the raid emerged it became clear that the operation had been long in the planning. US officials said they received intelligence that Osama Bin Laden might be in that compound as long ago as last summer.
CIA experts analysed whether the "high value target" living at the compound could be anyone else but they decided in the end that it was almost certainly Bin Laden.
US intelligence agents focussed in particular on one of Bin Laden's couriers - a man identified as a protege of captured al-Qaeda commander Khalid Sheikh Mohammed.
He appeared to be one of the few couriers completely trusted by Osama Bin Laden, who helped keep the al-Qaeda figurehead in touch with the rest of the world.
For years US intelligence had been unable to name the courier. But four years ago they worked out who he was and two years later they discovered where he operated.
It was only in August 2010 that they located him in Abbottabad, Pakistan.
US officials described as "extraordinary" the security measures in the Abbottabad compound - among them high walls and barricades, very few windows, and a 7ft high privacy wall on the second floor.
After the US attack Pakistani troops arrived at the scene and began securing the area.

More on This Story


Saturday, April 30, 2011

ADHABU DHIDI YA VIGOGO AMBAO HAWAKUSAIDIA CAMPAIGN ZA CHAMA ZAANZA,


Tido Mhando afungua ukurasa wa adhabu hizo:
Ninampango wa kurudi kijijini kwangu Tanzania,na kushirikiana na wanakijiji wenzangu katika shughuri za maendeleo” hiyo ilikuwa ni kauri yake Tido baada ya kuulizwa na mtangazaji wa shirika la utangazaji la uingereza(BBC) anatarajia kufanya nini baada ya kustaafu kazi yake ya utangazaji (BBC). Binafsi namuona Tido kama muungwana aliyekuwa tayari kushirikiana na watanzania wenzake katika kuleta maendeleo na ndio maana pamoja na pesa nyingi alizopata mara baada ya kustaafu BBC lakini alikubari kutoa mchango wake wa uzoefu katika nchi yake, nasema Tido ni muungwana na mzalendo kwa kuwa hakutaka kubaki ughaibuni ambapo angepata kazi za mkataba na kupata mapesa mengi lakini akakubali kurudi Tanzania.
Mchango wa Tido unaonekana katika kulibadirisha television ya taifa(TVT) na kuwa Shirika la utangazaji la tanzania(TBC) ambayo imejiongezea watazamaji wengi si Tanzania tu bali hata nje ya nchi, TBC imeweza  kuondoa mtazamo wa watanzania wengi ambo awali walikiona chombo hicho kama cha chama kinachoongoza dola, TBC chini ya uongozi wake Tido hakika imekuwa kama chombo cha umma na si chombo cha ccm,hii imechangiwa na msimamo thabiti wa mkurugenzi wake ndugu Tido ambaye aliruhusu habari kurushwa pasipo upendeleo wa chama chochote cha siasa, dini, kabila na mahali.
Enzi za TVT mchakato majimboni uliosusiwa na wanaccm na ambao umekigharimu sana chama hicho na kupoteza viti vingi vya ubunge, usingeweza kuoneshwa  kama ulivyooneshwa na TBC, huo ni mfano tosha kwamba ndugu Tido alikuwa jasiri ambaye hakumugwaya hata bosi wake aliyempa ukurugenzi.
Leo kumekuwa ni mijadara mbalimbali mara baada kuona kichwa cha habari katika gazeti moja la kila siku likinadi kuwa Tido mhando ametimuliwa, mtangazaji wa leo wa  jambo Tanzania Raheli MHANDO wa  TBC hakuweza kusoma habari hiyo pamoja na mesaji nying tulizo mtumia kumtaka atufafanulie kuhusu habari hiyo! Wengi tunajiuliza je, mchango wa Tido katika TBC ulikuwa unapingwa hata na wafanyakazi wenzake wa TBC? Je mwajiri wa Tido ameona Tido hajafanya lolote katika kukiendeleza chombo hicho cha umma? Je Tido amekamatwa mchawi kwa CCM kupoteza viti vya ubunge na udiwani? Je Tido ni kigogo wa kwanza aliyefungua ukurasa wa adhabu dhidi ya waliochangia ccm kupoteza viti vya ubunge kwa kuruhusu mchakato majimboni? Maswali hayo tumekosa majibu yake kabisa kwa kuwa Tido kwetu sisi watazamaji wa TBC na wapenda habari zisizoegemea upande wowote, amekuwa ni shujaa wa kipekee ambaye hana hudi kupongezwa kwa kukuza democrasia hapa Tanzania na nchi za jilani kupitia TBC!
Hivi mcango wa Tido hauonekani mpaka kufikia hatua ya kufukuzwa kama mbwa ambaye hana uwezo wa kubweka au ubwa mla kuku wa kufugwa? Ugumu ulikuwa wapi kumuongezea muda wa miaka miwili ndugu Tido mhando ili kukamilisha mipango yake aliyokuwa nayo katika kukiendeleza chombo hicho cha umma wakati huu ambapo chombo hicho kinafanya mabadiriko ya kitechnolojia? Ndugu yangu Tido, je ulikuwa huelewani hata na wafanyakazi waliokuwa chini yako, mbona wanakwepa kuhabarisha umma habari zozote zinazokuhusu ili kuweka udharimu huo uliofanyiwa hadharani?udharimu huo uliofanyiwa ndugu yangu Tido, naufanisha na ule aliofanyiwa mhadhili wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof. Baregu ambaye naye alifukuzwa kama mbwa baada ya mkataba wake kuisha,  walau yeye alipedwa na jumuia nzima ya chuo kikuu ambao walifikia hata hatua ya kugoma ili kushinikiza Proffesa huyo masuala ya siasa arudishwe chuoni hapo.
Tukifuata ule usemi unaosema ukiona mwenzako anyoa wewe tia zako maji, basi vigogo wote ambao hawakuchangia katika kufanikisha kampeni za chama dola wajiandae kwa adhabu za kufukuzwa kama mbwa pasipo kujali mchango wenu katika taifa letu! Vigogo wa TANESCO ambao umeme ulikatika wakati wenye dola wakifanya kampeni, wakuu wa wilaya na mikoa ampapo wenye dola walizomewa na kusodolewa wakati wakifanya kampeni, na viongozi wa chama ambao hawakufanya maandalizi mazuri kuwapokea wenye dola wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kukodi piki piki na tex, nyote mjiandae kwa kuwa kigogo mwenzenu Tido wa TBC tayari amefungua ukurasa wa adhabu zichukuliwazo.
naitwa Leonard, nipo Rukwa.    

MUUNGANO NIUTAKAO MIMI MWANANCHI WA KAWAIDA

Kumekuwa na hoja nyingi kuhusu muungano viswa vya Zanzibar na Tanganyika,ambavyo vyot kwa pamoja viliiunda Tanzania,waasisi wa muungano huo marehemu mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shehe Abeid Karume walilenga kukuza na kudumisha undungu baina ya watanganyika na wazanzibara. Muungano ambao juzi umetimiza miaka 47 umepoteza malengo ya awali ya kujenga na kudumisha undugu,nionavyo mimi ubinafsi wa viongozi wa kisiasa walioshika dola baada ya waasisi Nyerere na karume ndio chanzo cha chokochoko za muungano.Nionavyo mimi waasisi wa muungano walifikia hatua ya kwanza ambayo ilizaa serikari ndogo ya Zanzibar na Serikari ya muungano wa Tanzania, hivyo ingekuwa jukumu la viongozi wa sasa kuendelea kujenga na kudumisha undugu kwa kendeleza hatua ya pili kwa kufanya serikari mbili kuwa serikari moja ya Tanzania yenye raisi mmoja tu badala ya serikari tatu au mbili ambazo zimekuwa zikipigiwa upato. Sioni kwanini viongozi wa kisiasa wanaendeleza kuweka vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine ndio vyanzo vya chokochoko za muungano wetu? kulikuwa na na haja ipi kwa zanzibar sehemu ya Tanzania kuwa na Bendera yake,wimbo wake wa taifa,majeshi yake na serikari yake? viongozi wa kisiasa tuache ubinafsi, sisi wananchi wa kawaida tungependa kuona muungano wa zanzibar na Tanganyika unazaa serikari moja chini ya raisi mmoja ili kuwa na nguvu za kuharakisha maendeleo ya Tanzania kwa ujumla wake! Kuna ugumu upi zanzibar ambayo wakazi wake ni takribani millioni moja sawa na idadi ya watu katika mikoa mingine tanzania,kuongozwa na wakuu wa mikoa kama ilivyo kwa mikoa mingine?hakika kero za muungano zitakoma pale ambapo tanzania itakuwa na serikari moja tu.