Data And Research Enterprises[DARE] Tanzania is the fast growing company in the field of social,economic and health Research. DARE Tanzania focus poverty reduction through research and it deals with consultancy,advocacy and training on project/seminars/proposal/journals/data collection/data management/data analysis
Tuesday, November 22, 2011
HOTUBA YA RAISI KIKWETE KWA WAZEE WA CCM-DAR ES SALAAM
HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,
KWA WANANCHI KUHUSU HALI YA UCHUMI NCHINI NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA, TAREHE 17 NOVEMBA, 2011
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa,
Mstahiki Meya,
Viongozi wa Serikali,
Wazee wangu,
Ndugu Wananchi,
Nakushukuru Mkuu wa Mkoa na viongozi wenzako wa Jiji la Dar es Salaam kwa kuniandalia fursa hii ya kukutana na Wazee wa Dar es Salaam. Nawashukuru sana wazee wangu kwa kuitikia wito wangu huu wa kukutana nanyi. Nimefarijika sana kwa mahudhurio yenu makubwa pamoja na taarifa kuwa ya muda mfupi.
Nimewaiteni wazee wangu nizungumze nanyi na kupitia kwenu nizungumze na wananchi wote wa Tanzania. Mwisho wa mwezi uliopita sikuweza kufanya hivyo kupitia utaratibu wetu wa kawaida kwa sababu nilikuwa kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola nchini Australia. Mwisho wa Mwezi huu nitakuwa Bujumbura kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, hivyo sitaweza kuongea na wananchi wakati huo. Lakini, yapo masuala kadhaa ambayo ni muhimu watu kupata ufafanuzi kutoka kwangu. Kwa ajili hiyo nimeona nitumie fursa hii kuzungumza nanyi siku ya leo. Leo nataka kuzungumzia hali ya uchumi na mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Hali ya Uchumi
Ndugu Wananchi;
Katika kuelezea hali uchumi nchini, naomba nianze kwa kuelezea hali ya uchumi duniani kwani yanayotokea nchini yana uhusiano mkubwa na yanayotokea duniani. Hali ya uchumi duniani siyo shwari. Ukweli ni kwamba hali katika uchumi wa mataifa ya Marekani, Ulaya Magharibi na Japan haijatengemaa kufuatia machafuko ya masoko ya fedha na mdororo wa uchumi wa miaka miwili iliyopita. Hivi sasa uchumi wa mataifa tajiri ya Ulaya , wanachama wa Umoja wa Ulaya na hasa wanachama wa Umoja wa Sarafu ya Euro unapita katika kipindi kigumu na mashaka. Thamani ya sarafu hiyo inashuka na hata kuaminika kwake ni kwa mashaka. Mfumuko wa bei umepanda, ukosefu wa ajira umeongezeka na ipo hofu kubwa ya uchumi wa nchi hizo kudorora tena. Lakini nchi hizi ndiyo masoko makubwa ya bidhaa zetu, watalii na bidhaa za viwandani. Hivyo, athari zao zinatugusa na sisi. Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kunaongeza bei ya bidhaa tunazonunua kutoka kwao. Aidha, kutetereka kwa uchumi wao nako kumepunguza masoko ya bidhaa zetu.
Lakini kulegalega kwa sarafu ya Euro kumesaidia kuimarika kwa sarafu ya dola ambayo kabla ya hapo ilikuwa imepungua nguvu. Kwa sababu hiyo thamani ya sarafu ya dola imepanda duniani ikilinganishwa karibu na sarafu nyingine zote pamoja na yetu. Wakati huo huo bei ya mafuta imeendelea kupanda duniani kutoka dola 76.1 kwa pipa Septemba,, 2010 hadi dola 100.5 Septemba, 2011. Jumla ya yote haya ni kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka asilimia 4.2 Oktoba, 2010 hadi asilimia 17.9 Oktoba, 2011.
Ndugu Wananchi;
Serikali na vyombo husika vimekuwa vinachukua hatua mbalimbali kukabiliana na matatizo ya kushuka kwa thamani ya shilingi, bei ya mafuta, bei ya sukari na matatizo ya umeme. Kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi Benki Kuu imeendelea kuchukua hatua zilizopo ndani ya mamlaka yake hususan kubana ulanguzi wa fedha za kigeni, kudhibiti matumizi ya fedha kigeni kufanyia malipo hapa nchini na kuongeza fedha za kigeni katika masoko ya fedha. Kwa kweli uwezo wao una ukomo. Jawabu la uhakika lipo kwenye uchumi wa mataifa makubwa kuchukua hatua thabiti kuimarisha uchumi wao ili thamani ya dola irejee mahali pake stahiki na bidhaa zetu zipate masoko ya uhakika na bei nzuri ili mapato yetu ya fedha za kigeni yaongezeke.
Kwa upande wa mfumuko wa bei, ni vyema tukatambua kuwa Asilimia 75 ya ongezeko hili imetokana na kupanda kwa bei ya chakula na mafuta. Asilimia 25 iliyobaki imechangiwa na sera za fedha. Kwa upande wa mafuta, tunaamini utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja utasaidia kudhibiti bei za ndani za bidhaa hiyo. Aidha, itsaidia kupunguza makali ya athari ya bei za dunia zinazopanda. Kwa upande wa bei za vyakula, tatizo kubwa ni uhaba wa chakula katika nchi jirani unaosababisha wote kututegema sisi na hivyo kupandisha bei nchini. Tunaendelea kudhibiti magendo ya chakula na wakati huo kutengeneza taratibu rasmi za kuziuzia chakula nchi jirani.
Kwa upande wa sukari tumeamua kuruhusu tani 120,000 ziagizwe ili kupunguza uhaba wa bidhaa hiyo na kushusha bei yake.
Hatuko Peke Yetu
Ndugu Wananchi;
Ni vizuri tukafahamu kuwa, matatizo ya mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha yetu siyo yetu peke yetu. Nchi zote za Afrika Mashariki zinakabiliana na matatizo haya. Kwa mfano, mfumuko wa bei kwetu ni asilimia 17.9, Kenya wako asilimia 18.9 na Uganda asilimia 30.5. Wakati mwaka wa jana sote tulikuwa kwa watani karibu asilimia 5. Kwa upande wa kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola sote tumeathirika. Shilingi ya Tanzania imeshuka kwa asilimia 9.4, Kenya kwa asilimia 6.8 na Uganda kwa asilimia 17.4. Randi ya Afrika Kusini kwa asilimia 18.7, Rupia ya India kwa asilimia 9.8, Pauni ya Uingereza kwa asilimia 6.6. na Euro kwa asilimia 9.7.
Ndugu Wananchi;
Katika kukabiliana na tatizo la umeme, Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa dharura wa kuongeza uzalishaji wa umeme. Serikali imewawezesha TANESCO kukodi mitambo ya kuzalisha umeme kutoka kwenye makampuni ya Symbion (112 MW) na Aggreko (100 MW) na kununua mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL (100 MW).
Napenda niwahakikishie wananchi kuwa, ifikapo Desemba, 2011 hali ya upatikanaji wa umeme itakuwa nzuri na mgao utapungua sana baada ya kufunga mitambo mingine mipya ya kuzalisha umeme ya TANESCO (160 MW) na Symbion (60 MW). Mikakati tuliyonayo ya muda mrefu ni kuongeza mitambo zaidi na kuongeza upatikanaji wa gesi ya kuendeshea mitambo kwa kujenga bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Mchakato wa Katiba
Ndugu Wananchi;
Kama mtakavyokumbuka tarehe 31 Desemba 2010 katika hotuba yangu ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011 nilizungumzia maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa ni Tanzania Bara tarehe 9 Desemba, 2011. Miongoni mwa mambo ambayo niliyataja kuwa tutayafanya katika kusherehekea siku hiyo adhimu ilikuwa ni kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya nchi yetu kwa nia ya kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba mpya.
Nilifafanua siku ile kwamba tunataka kufanya hivyo si kwa sababu Katiba yetu ya sasa ni mbaya, la hasha! Nilieleza kwamba Katiba yetu ya sasa ni nzuri na imelilea vyema taifa letu. Tuna nchi yenye amani, utulivu na umoja pamoja na watu wake kuwa wa rangi, makabila, dini na itikadi mbalimbali za kisiasa. Tunayo nchi ambayo imepiga hatua kubwa sana ya maendeleo ukilinganisha na ilivyokuwa miaka 50 iliyopita. Pamoja na hayo tunataka kuihuisha Katiba yetu ili tuwe na Katiba inayoendana na Tanzania ya miaka 50 baada ya Uhuru wa Tanzania Bara, Tanzania ya miaka 47 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Tanzania ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa ajili hiyo nilielezea dhamira yangu ya kuunda Tume Maalum ya Katiba yaani Constitutional Review Commission itakayojumuisha Watanzania wa makundi mbalimbali katika jamii yetu na kutoka pande zetu mbili za Muungano. Aidha, nilifafanua kuwa jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibu mchakato wa kupata maoni ya Watanzania kuhusu nini wanachokitaka kiwemo katika Katiba yao.
Tume itasikiliza maoni hayo na baadaye kutengeneza rasimu ya Katiba mpya ambayo baada ya kukubaliwa na Bunge itafikishwa kwa wananchi kutoa ridhaa yao kwa kupiga kura. Nilisisitiza kuwa mchakato huo utawahusisha Watanzania wote wa ngazi zote na popote walipo mijini na vijijini. Hapatakuwa na aina yoyote ya kuwabagua watu kwa itikadi zao za siasa, shughuli wazifanyazo, dini zao, rangi zao au jinsia zao.
Ndugu Wananchi;
Nilifarijika sana na kauli za pongezi kwangu na kwa Serikali kwa uamuzi wa kuanzisha mchakato wa kupata Katiba mpya. Miongoni mwa waliotoa pongezi alikuwa Ndugu Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye wakati akichangia hotuba yangu ya kufungua Bunge Jipya, tarehe 11 Februari, 2011; nanukuu Hansad ya Bunge aliposema “Mheshimiwa Spika, ninapenda kwenye hili, nimpongeze Rais kwa kuwa msikivu, na Rais anapofanya jema tutampongeza, Serikali yake inapofanya jema tutaipongeza na Chama chochote kitakapofanya jambo jema kwa Taifa letu, tutakipongeza. Napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa sababu moja ya msingi sana, kuridhia mabadiliko au kuitafuta upya Katiba ya nchi yetu.” mwisho wa kunukuu. Lakini siku chache baadaye Chama chake kikaja na msimamo tofauti, wakawa wanalalamikia kunyang’anywa hoja yao na kukataa Rais asiunde Tume ya Katiba na wala asihusike kabisa na mchakato huu. Tangu wakati huo wameendesha kampeni kubwa ya kutaka Rais asihusishwe kwenye mchakato wa kubadili Katiba
Kwa kweli watu wengi wanaoitakia mema nchi yetu walishangazwa na madai hayo na vitendo vya ndugu zetu hao. Hii si mara ya kwanza kwa nchi yetu kufanya zoezi la marekebisho ya Katiba au hata kuandika upya Katiba tangu Uhuru na Muungano. Mara zote hizo iliundwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi ambayo iliundwa na Rais. Ndivyo ilivyokuwa wakati wa Rais wa Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Pili, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais wa tatu Mzee Benjamin Mkapa. Mwalimu Julius Nyerere alifanya hivyo mara tatu. Mara ya kwanza mwaka 1963 wakati wa kubadilisha mfumo wa vyama vingi kwenda Chama kimoja, Rais aliunda Tume ya Mheshimiwa Rashid Kawawa, Amon Nsekela. Mara ya pili wakati wa kutengeneza Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 aliunda Tume ya Mzee Sheikh Thabit Kombo.
Mwaka 1984 Mabadiliko ya Katiba ya 1977 yaliyoweka ukomo wa Urais na kuingiza katika Katiba Haki za Binadamu, yaliyotokana na mchakato uliokuwa ni wa Kichama, ambapo CCM ilikusanya maoni kupitia mtandao wa kichama kuanzia Matawi hadi kufikia Makao Makuu. Wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi wa Awamu ya Pili, kulikuwa na Tume ya Jaji Mkuu Francis Nyalali iliyotuletea mabadiliko ya nane ya Katiba yaliyoruhusu vyama vingi vya siasa. Wakati wa Rais wa Awamu ya Tatu, mzee Benjamin Mkapa kuliundwa Tume ya Jaji Kisanga iliyoleta mabadiliko ya 13 na 14 ya Katiba ya nchi.
Hivyo la ajabu lipi kwa Rais wa sasa kuunda Tume ya Katiba? Amepungukiwa nini Kikatiba na Kisheria ambacho Marais wenzake walikuwa nacho katika madaraka yao? Hakipo hata kimoja! Madaraka waliyokuwa nayo Marais waliomtangulia ndiyo aliyonayo Rais wa sasa. Hajapungukiwa chochote kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Kwa kweli hakuna hoja yoyote ya msingi ya kumuengua Rais katika mchakato wa kutengeneza Katiba ya nchi. Haipo hoja ya Kikatiba wala ya Kisheria. Hivi Rais asipounda Tume, nani aiunde Tume hiyo? Na huyo atakayeunda atapatikanaje?
Juzi Bungeni msemaji wa kambi ya upinzani, katika mjadala wa Muswada wa Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni alisema Rais ni dikteta. Ama kweli “akutukanae hakuchagulii tusi” kama ulivyo msemo wa Kiswahili. Hivi mimi kweli ni dikteta? Kwa jambo lipi? Hivi ndugu zangu Rais dikteta anatoa uhuru mkubwa kama uliopo sasa wa vyombo vya habari na wa watu kutoa maoni yao? Kama mimi ningekuwa dikteta kweli nina hakika hata yeye asingethubutu kusema hivyo na kama angethubutu basi mpaka sasa asingekuwa anatembea kwa uhuru. Mimi ninachofahamu ni kuwa nasemwa kwa kuwapa watu, vyama vya siasa na vyombo vya habari uhuru mkubwa mno ambao watu wanaona unatumika vibaya kusema maneno yasiyokuwa na staha au hata matusi, fitina na kupandikiza chuki katika jamii. Labda, nijaribu kuwa dikteta kidogo watu waone tofauti yake. Naamini kungekuwa na malalamiko makubwa zaidi ya haya.
Ndugu Wananchi;
Mimi na wenzangu Serikalini tumefanya yote ambayo Katiba ya nchi na Sheria vinaruhusu. Ndivyo Marais walionitangulia na Serikali zao walivyofanya tena sisi tumefanya zaidi ya wao. Wote waliunda Tume za kukusanya maoni ya Katiba na wakati wa Mwalimu Julius Nyerere liliundwa Bunge Maalum la Katiba lililojumuisha Wabunge na wananchi wengine kama tulivyoamua kufanya sisi. Ilifanyika hivyo wakati wa kutengeneza Katiba ya Tanganyika kuwa Jamhuri na Katiba ya Kudumu ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977. Sisi tulichofanya cha ziada ni kulihusisha Bunge kutunga Sheria ya Kuunda Tume ya kusimamia mchakato wa Katiba mpya na vile vile kuwapa wananchi wote ridhaa ya kuamua kwa kuipigia kura Katiba inayopendekezwa. Ni kutokana na nyongeza hii ndipo tukaona busara ya kuwepo kwa Sheria maalum ya kuongoza mchakato wa kupata Katiba mpya. Tumepanua demokrasia na kuwahusisha wananchi wenyewe siyo tu katika kutoa maoni bali pia kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu Katiba ya nchi yao, badala ya kuwaachia Wabunge na viongozi wengine Serikalini peke yao. Kwa kweli tunastahili pongezi badala ya shutuma na lawama zisizokuwa na msingi.
Pia inasikitisha kuona au kuwasikia watu wanaojua wakijifanya ukweli huu hawaoni au hawajui. Baya zaidi ni pale wanapojihusisha na kupotosha ukweli na kuipaka sura isiyokuwa ya kweli kuhusu kinachofanywa na Serikali. Mimi hujiuliza kwa nini wanafanya hivi. Kwa nini wanafanya hiyana ya upotoshaji wote huu? Kwa kweli sipati majibu ya uhakika. Labda ndiyo ile dhamira ya kutaka nchi isitawalike. Au ndiyo pengine ni ile nia ya kutaka kwenda Ikulu kwa njia ya mkato. Ati kwa kutumia nguvu ya umma. Basi hata hiyo nguvu unaitumia bila ya kuwa na hoja za kweli?
Ndugu Wananchi;
Nayasema haya kwa sababu kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wa jambo hili tangu baada ya hotuba yangu ya tarehe 31 Desemba, 2010 mpaka wakati wa kuwasilishwa kwa Muswada wa Sheria wa Kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba uliomalizika leo Bungeni. Upotoshaji wa kwanza ulikuwa ni ule wa kujenga dhana kana kwamba Serikali imewasilisha Muswada wenyewe wa Katiba mpya. Wapo watu wamefanywa waamini hivyo wakati si kweli hata kidogo. Huu ni Muswada ambao ukipitishwa, itaundwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu nini wanachokitaka kijumuishwe katika Katiba yao mpya. Kwa maneno mengine, maoni yenu mtakayoyatoa wananchi kwa Tume ndiyo yatakayotumika kutengeneza Katiba mpya.
Ndugu Wananchi;
Katika Muswada huu kuna mambo tuliyotaja kuwa ni ya msingi ambayo yamewekewa wigo wa kuhakikisha yanalindwa. Mambo hayo ni yale ambayo yanalitambulisha taifa letu na tunu zake kuu. Mambo yenyewe ni haya yafuatayo: Kuwepo kwa nchi yetu na mipaka yake; kuwepo kwa Serikali, Bunge na Mahakama; kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; kuwepo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; umoja wetu, mshikamano wetu na usalama wetu; Mfumo wa uchaguzi kwa kura unaotoa fursa kwa wote; Hifadhi ya haki za Binadamu; Haki za watu; Usawa mbele ya sheria na haki; Uhuru wa kuabudu na kuvumiliana kwa imani zetu.
Kumekuwepo na upotoshaji ati huko ni kuwaziba watu midomo. Siyo hivyo hata kidogo. Mambo hayo yanajadiliwa, lakini siyo kwa nia ya kuyaondoa bali kuboresha. Kwa mfano, kuhusu Muungano, tunachosema ni kwamba hatujadili kuwepo au kutokuwepo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bali namna bora ya kuendesha shughuli za Muungano wetu. Lakini, tulichokifanya siyo kitu kigeni, hata Rais wa kwanza alifanya hivyo mwaka 1963 alipounda Tume ya Mfumo wa Chama Kimoja cha Siasa iliyoongozwa na Mheshimiwa Rashid Kawawa. Alitoa mwongozo na aliyataja mambo ya kulinda. Sisi tulichokifanya ni kuyataja kwenye sheria badala ya kuwa Mwongozo wa Rais.
Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu;
Kwani Katiba ya Nchi ni kitu gani. Katiba hutaja nchi na mipaka yake. Kwetu sisi nchi yenyewe ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na kuungana kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika. Pili, Katiba inaelezea jinsi nchi hiyo itakavyoendeshwa kwa maana ya mihimili mikuu mitatu ya dola ya Utawala/Serikali, Bunge na Mahakama. Katiba inafafanua jinsi Serikali inavyopatikana, muundo wake na inavyofanya kazi.
Aidha, inaeleza jinsi Bunge linavyopatikana, jinsi linavyofanya kazi ya kutunga sheria na mahusiano yake na mihimili mingine. Vile vile, Katiba inaeleza jinsi Mahakama inavyofanya kazi ya kutoa haki, muundo wake na jinsi Majaji na Mahakimu wanavyofanya kazi. Kwa kweli mchakato wote huu unahusu hayo. Tunatakiwa kutoa maoni juu ya namna gani bora zaidi na ikiwezekana namna mpya ya kuendesha shughuli za Muungano wetu na jinsi mihimili yetu inavyopatikana na kufanya shughuli zake.
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine lililopotoshwa ni dhana ya muswada kusomwa mara ya kwanza. Kwa mujibu wa utaratibu wa kutunga sheria, Miswada, husomwa mara tatu Bungeni. Muswada kusomwa mara ya kwanza ni pale unapogawiwa kwa Wabunge baada ya kuchapishwa katika gazeti la Serikali siku 21 kabla ya kuwasilishwa Bungeni. Baada ya kuchapishwa, hugawiwa kwa Wabunge. Muswada husomwa mara ya kwanza Bungeni ili kutoa fursa kwa Mheshimiwa Spika kuwasilisha Muswada huo kwenye Kamati iuchunguze na kuutolea maoni. Mheshimiwa Spika anaweza pia kuielekeza Kamati kutafuta maoni ya wananchi.
Baada ya Kamati kukamilisha kazi yake, Muswada husomwa mara ya pilli ambapo Muwasilishaji atatoa hoja kwamba Bunge liujadili Muswada pamoja na kutoa maelezo ya Muswada. Mjadala huanza kwa Kamati ya Bunge kutoa maoni yake ikifuatiwa na maoni ya Kambi ya Upinzani. Wakati Kamati ya Bunge inapojadili Muswada, Waziri mhusika huwepo na mara nyingi maoni ya Kamati ya Wabunge na wadau hujumuishwa wakati Waziri anapowasilisha hoja Bungeni ya Muswada unaposomwa mara ya pili. Baada ya mjadala, Bunge hukaa kama Kamati ya Bunge zima ambapo hupitia Muswada kifungu kwa kifungu.
Katika hatua hii Wabunge huweza kupendekeza mabadiliko mahsusi kwenye kila kifungu. Aidha, Waziri nae anaweza kutetea marekebisho ya Muswada. Baadaye Bunge hurejea, taarifa ya Kamati ya Bunge zima hutolewa kwamba Muswada umepitiwa kifungu kwa kifungu na kukubaliwa. Kisha Muswada husomwa mara ya tatu kuashiria kwamba Muswada umepitishwa. Mara nyingi Muswada hutokana na majadiliano katika hatua hizi zote, mabadiliko hufanywa na wakati mwingine mabadiliko huwa makubwa kiasi kwamba kufanya Muswada uliochapishwa na kusomwa mara ya kwanza na ule uliokubaliwa mwishoni uwe tofauti kabisa.
Ndugu Wananchi;
Muswada huu ulisomwa mara ya kwanza mwezi Aprili na kupelekwa kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala mwezi Aprili, 2011. Tangu wakati huo Kamati imekuwa ikiufanyia uchunguzi Muswada huo na kukusanya maoni ya wadau. Walisikiliza wadau Dodoma, Dar es Salaam na Zanzibar pamoja na kufuatilia maoni ya makongamano, magazetini na kwenye mitandao. Kisha Kamati ikayajadili na kutoa mapendekezo yake ambayo Serikali iliyasikiliza na kuyajumuisha wakati uliposomwa mara ya pili. Muswada huu haukuwahi kuondolewa Bungeni. Kwa sababu hiyo, hakuna sababu ya kurudia kusomwa mara ya kwanza kwa mujibu wa taratibu za kuendesha Bunge.
Tukumbuke kwamba baadhi yao waliahidi kwamba wangetoa Katiba Mpya katika siku mia moja tu. Serikali imechukua miezi kumi na mmoja na wanalaumu kwamba eti inawahisha mchakato!! Hiyo Katiba ya siku mia moja sijui wangeipataje bila kuwashirikisha wananchi?
Ndugu Wananchi;
Ni kutokana na hoja hizo Spika akaamua Muswada uendelee kujadiliwa na Bunge na leo Bunge limeupitisha Muswada huo. Baadae Muswada utaletwa kwangu kwa ajili ya kutiwa saini uwe Sheria. Baada ya hapo itabakia kazi yangu na Rais wa Zanzibar kuunda hiyo Tume ili mapema mwakani kazi ya kukusanya maoni ya wananchi ianze. Lengo letu ni kuwa ifikapo mwaka 2014 zoezi zima liwe limekamilika ili mwaka 2015 tufanye uchaguzi tukiwa na Katiba mpya. Itapendeza tukisherehekea miaka 50 ya Muungano na Katiba mpya. Ni matumaini yangu kwamba wananchi wote watashiriki kwa ukamilifu kutoa maoni yao kwa Tume hiyo.
Ndugu Wananchi;
Nimechukua muda wenu mwingi kuyafafanua masuala haya kwa umuhimu wake. Nia ni kutaka watu waelewe maoni ya upande wa Serikali. Matatizo ya kiuchumi yanayotukabili tunaendelea kuyashughulikia. Yale yaliyo kwenye uwezo wetu tutayamaliza na yale yaliyo nje ya uwezo wetu tutaendelea kuchukua hatua za kupunguza makali. Aidha, tutaendelea kutoa wito kwa mataifa husika kuchukua hatua thabiti kutatua matatizo yao kwani tunaoumia ni wengi.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa mchakato wa kupata Katiba mpya nawasihi Watanzania tujiandae kwa maoni ya kutoa kwenye Tume ya Katiba mara itakapoanza kazi. Kwa wale ambao hawatapata walichokitaka nawaomba warudi kundini, sote tuungane kwa hatua inayofuata. Najua wanayo maoni mengi mazuri wayatayarishe na kuyawasilisha kwa Tume itakayoundwa. Njia ya maandamano na vurugu si ya busara kufuata. Haijengi bali inabomoa, haina faida bali hasara nyingi, haina faraja bali machungu kwa pande zote. Busara ituongoze sote kuchagua njia inayojenga, yenye faida, furaha na faraja kwa wote. Tutofautiane bila kupigana. Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu.
Mwisho
Ndugu Wananchi,
Naomba nimalizie kwa kuwashukuru wananchi kwa kuwa na subira kwa kipindi chote hiki toka tutangaze nia yetu ya kuanza mchakato wa kupata Katiba mpya. Kwa mara nyingine tena nawaomba mjiandae kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata Katiba mpya mara utakapoanza ili tuendelee kuijenga na kuiendeleza nchi yetu na vile vile tuendelee kuithamini na kuitunza amani ya nchi yetu.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni sana kwa kunisikiliza!
Monday, October 10, 2011
RAISI MSAAFU WA CAPE VERDE ATWAA MABILIONI YA MO IBRAHIMU KWA UONGOZI ULIOTUKUKA
The former president of Cape Verde, Pedro Pires, has been awarded an African leadership prize of U.S. $5 million for transforming his country "into a model of democracy, stability and increased prosperity."
Pires is the recipient of the 2011 Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership, established by the Sudanese business pioneer, Mo Ibrahim. The award is paid over 10 years, and is accompanied by an additional annual payment of U.S. $200,000 for life.
Salim Ahmed Salim, former secretary-general of the Organization of African Unity and chairman of the prize committee, said Cape Verde had won international recognition for its record on human rights and good governance. It was also the second African country to improve its position and rise above the United Nations category of the world's least developed countries.
Gabonews
Cape Verde President Pedro Pires, left, with Gabon President Ali Bongo. (file photo)
Salim said Pires enhanced his credentials when he stepped down at the end of his second term. "Dismissing outright suggestions that the constitution could be altered to allow him to stand again, he said: 'This is a simple matter of faithfulness to the documents that guide a state of law.' Throughout his long career President Pires has been dedicated to the service of his people, including those in the diaspora, while retaining his humility and personal integrity."
The prize is open to democratically-elected former heads of government who have observed term limits and left office within the last three years.
The prize has been awarded only twice: to Joaquim Chissano of Mozambique in 2007 and Festus Mogae of Botswana in 2008. In 2009 and 2010 the prize committee said it could not find a worthy recipient among Africa's recently-retired leaders.

Saturday, September 10, 2011
FAINALI ZA MASHINDANO YA MISS TANZANIA NI LEO JUMAPILI TAREHE 11, 2011
KITENDAWILI cha nani ataibuka kuwa Vodacom Miss Tanzania 2011 kitateguliwa leo usiku ambapo warembo 30 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania wakichuana kuwania taji hilo.
Ni ukweli usiofichika kuwa mashindano ya mwaka huu ambayo ni ya 18 tokea kuanzishwa kwake mwaka 1994 ni ya kihistoria kutokana na sababu mbali mbali. Mbili kubwa ni mashindano ambayo yatakuwa moja ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru na pili ni mshindi wa mwaka huu atazawadiwa zawadi nono tokea kunzishwa kwa mashindano hayo.
Mwaka huu mrembo atapewa zawadi ya Jeep Patriot model ya mwaka huu yenye thamani ya shs. Milioni 72 huku akipewa fedha taslimu sh. Milioni 8. Hii ni zawadi ya kihistoria kwani imevunja rekodi ya mwaka 2003 ya Sylvia Bahame ambaye alizawadiwa gari aina ya Nissan Hardbody yenye thamani ya shs milioni 55 na fedha taslimu shs. 7 million.
Ikumbukwe mwaka jana ambapo mrembo anayemaliza muda wake, Geneieve Mpangala alipewa gari maarufu kwa jina la Mkoko na fedha taslim shs milioni 10 na kufanya jumla ya zawadi zote kufikia milioni 20.
Hii ni hatua kubwa kwani tofauti ya shs milioni 60 si haba na zawadi ya kwanza imewafanya warembo wengi kupagawa kwani hawakuamini macho yao kile walichokuwa wanakiona.
Zawadi nyingine za washindi ni sh. Milioni 6.2 kwa mshindi wa pili, sh. 4 millioni kwa mshindi wa tatu na sh. Milioni 3 kwa mshindi wane. Mshindi wa tano atapewa sh. Milioni 2.4.
Warembo watakaoshika nafasi ya sita mpaka 15 watapewa sh. Milioni 1.2 na waliobaki (16-30) watapewa kifuta jasho cha sh. 700,000.
ìTunatarajia kuwa mashindano magumu sana, hii inatokana na zawadi ya mshindi wa kwanza ambayo warembo wengi wameelekeza nguvu zao huko kwa sababu ya ukubwa wake na vile vile kiu ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia (Miss world) mjini London,î alisema meneja masoko wa kampuni ya kuuza magari ya CFAO zamani DT Dobie, Alfred Minja.
Minja alisema kuwa wametambua na kuamua kurudisha hadhi ya mashindano hayo ili kuleta mvuto wake wa awali kwani mwaka 2005, Nancy Sumari alizawadiwa nyumba iliyojengwa kule Tabata.
Tofauti na miaka ya nyuma, mashindano ya mwaka huu ni yana ugumu wa aina yake kutokana na ukweli kuwa imekuwa vigumu kujua nani ataibuka mshindi tofauti na mwaka jana, juzi na miaka ya nyuma.
Genevieve Mpangala ambaye atalivua taji lake alionekana wazi wazi kuwa hana mpinzani na hata wakati wa Miriam Gerald na Nasreem Karim. Ukali wa warembo hao ulikuwa wa aina yake na kupewa nafasi hata kabla ya kupanda jukwaani.
Ni vigumu kutabiri nani mshindi, nimefuatilia maonyesho mbali mbali ya televisheni wakiwa kwenye nyumba na mengine, ushindani ni mkubwa sana, lakini mshindi ni mmoja tu,alisema Rodrick Mwambene ambaye kupitia duka la Mama Tike aliwahi kudhamini mashindano mbali mbali ya vituo.
WALIOINGIA TOP 15:
Mwajabu Juma (Temeke, Miss Top Model), Rose Hurbert (Kaskazini, Vipaji), Alexia Williams (Ilala, Miss Personality), Tracy Mabula (Kanda ya Ziwa, Miss Photogenic), Loveness Flavian (Kanda ya Mashariki, Mrembo bora wa michezo).
WANAOWANIA TOP 15:
Weirungu David, Neema Mtitu (Chuo Kikuu Huria), Cynthia Kinasha (Temeke), Zerulia Manoko, Christina Mwenegoha (Kanda ya Kati), Jeniffer Kakolaki, Salha Israel (Ilala), Dalila Ghribu, Maua Kimambo (Kanda ya Kati), Blessing Ngowi, Glory Lory (Elimu ya Juu), Stacey Alfred, Zubeda Seif (Kanda Kaskazini), Stella Mbuge, Husna Maulid, Hamisa Hussein (Kinondoni), Princess Chiaro Masonobo (Udsm), Atu Daniel, Leila Juma, Christine William (Nyanda za Juu Kusini) , Mariaclara Mathayo, Asha Saleh (Mashariki), Irene Karugaba, Glory Samwel (Kanda ya Ziwa).
Warembo wanaoiwakilisha Dar es Salaam:
Weirungu David, Neema Mtitu (Open University), Mwajabu, Cynthia Kinasha, Husna Twalib (Temeke), Alexia Williams, Jeniffer Kakolaki, Salha Israel (Ilala), Blessing Ngowi (Institute of Social work), Glory Lory (IFM), Stella Mbuge, Husna Maulid, Hamisa Hussein (Kinondoni), Princess Chiaro Masonobo (Udsm).
KIINGILIO: SHS. 100,000
BURUDANI
Diamond, kidumu, Juliana, Akili the Brains, Bob Junior maarufu kama Rais w Sharobaro,
MAJAJI WA MWAKA HUU:
Prashant Patel, Crescentius Magori, Victoria Lukindo, Cynthia Masaki, John Njoroge, Benard Mlunya , Javier Diz Rio, Martin Ngadada, Pratma Shah.
WAREMBO WA MIAKA YA NYUMA:
1994 -Aina Maeda,
1995- Emily Adolf
1996- Shose Sinare
1997 - Saida Kessy
1998- Basila Mwanakuzi
1999- Hoyce Temu
2000 - Jacqueline Ntuyabaliwe
2001- Happiness Magese
2002- Angela Damas
2003- Sylvia Bahame
2004- Faraja Kotta
2005 - Nancy Sumari alishinda taji la Miss World Africa
2006- Wema Sepetu
2007- Richa Adhia
2008- Nasreen Karim
2009- Miriam Gerald
2010 - Genevieve Emmanuel
TALAKA SI SURUHISHO LA MATATIZO YA UHUSIANO, SURUHISHO NI KUONGEA NA MWENZA WAKO
Watu bwana, wakikwaruzana ‘Nenda kwenu mbwa wee’…wengine ‘Nipe talaka hunifai!”
“MBWA wewe, najuta sijui kwanini nilikuoa, yaani kati ya wanawake, wewe si lolote, pumbavu kabisa….” Ni kati ya kauli ambazo wanawake wamekuwa wakikumbana nazo kwenye ndoa.
Kama wewe mwanamke uko kwenye ndoa ambayo haina majuto na kero, ni suala la kumshukuru Mungu. Ukweli ni kwamba kuna wanawake wengi wanateswa na wanaume.
Usione wanaume mitaani, usifikiri mwanaume ambaye unakwenda naye gesti na kuachana, ndivyo anavyokuwa kwenye ndoa, wengi ni kero. Si wengi ambao wanawaheshimu wake zao.
Baadhi ya wanaume ni wasomi, ni watu maarufu, lakini kwenye nyumba zao ni takataka. Hawana heshima kwa familia, ndio unaweza kuona kwa mfano baba mtu mzima, anakataa kutoa huduma kwa watoto, eti kisa kagombana na mkewe. Akili iko wapi ndugu yangu kama sio upumbavu?
Kuna wanaume, eti mkewe haruhisiwi kupanda kwenye gari, anapandisha machangudoa…huu ni upumbavu. Dalili kwamba huna akili ni kuendekeza vitu ambavyo haina maana katika maisha. Kuna wanaume wengi hawana akili. Wanachojua wao ni kutembea kwenye nyumba nzuri za starehe na makahaba.
“Mke wangu amekuwa kero, dawa yake naona ni ndogo tu kumchukua nyumba ndogo” ndivyo wengi wanavyojidanganya. Wanafikiri kwamba nyumba ndogo ni mali, lakini nyumba ndogo hawa ni wafanyabiashara, wanachokifanya ni kwamba anakusikiliza eeeh mke wangu hana maana, hanipi raha, eeeh ooh na ujinga mwingine mwingi unamwambia.
Yeye yuko kibiashara zaidi, kwamba anaangalia matatizo uliyonayo kisha anajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha unapata raha, hasa kwa sababu anaamini yuko kibiashara kwa maana kuwa utampa fedha na mambo mengine kama haya.
Nyumba ndogo ni wezi, ni majambazi, na ni wafanyabiashara, baadhi yao huwa wanakuwa bize kujifunza namna ya kuwanasa wanaume. Kuna wengine wanasoma vitabu mbalimbali vya mahaba, ili kumnasa mwanaume asikumbuke kwao.
Kwa wanaume wasio na akili, wanafikiri wanayofanyiwa ni kwa upendo, kumbe hakuna lolote la maana. Bali kinachofanywa na nyumba ndogo ni kusaka njia za kuishi kupitia migongo ya hao wanaume.
Mwanaume mwenye akili timamu ataangalia namna ya kuondoa kasoro zilizoko kwenye nyumba yake. Ndugu zangu tunapokuwa na shamba kama kwa mfano umepanda mahindi na kumeota magugu, kinachofanyika sio kwamba huwa tunang’oa mahindi na kwenda kuyapanda kwenye shamba jingine, bali tunasaka dawa ya kuua magugu ili mahindi yaweze kuota vizuri.
Kuna wanawake pia wana kauli za ujeuri, eeeh kuna wengine kama ulimgusa jana, ukimwambia na leo tena nataka ‘tupigane’ anaanza kulalamika “aaah bwana eeeh nataka kupumzika, aaah jana umetaka na leo unataka kwani mimi ng’ombe, hata ng’ombe huwa wanapumzika’.
Kauli chafu hazitakiwi katika suala zima la ndoa. Kama kweli unaumwa au una jambo linakusumbua, ni suala la msingi kuzungumza taratibu. Acha kuwa mwenye kauli chafu kwa mkeo, acha kuwa na kauli chafu kwa mumeo.
Kuna watu wengeine, wakikwaruzana kidogo ‘Nenda kwenu mbwa wee’…wengine utawasikia wanasema ‘Nipe talaka hunifai!” Ndoa nzuri huwa inajengwa kwa maneno na fikra za kila mtu kuamini kuwa hata kama kunatokea migogoro, cha msingi ni kuangalia chanzo cha mgogoro na kuumaliza. Utaachana na wangapi?
Kuringa kwenye ndoa kwa sababu eti una mwanamke mwingine nje ya ndoa ni upumbavu…kuringa labda una mwanaume mwingine nje ya ndoa ni ujinga.Mtu mwenye akili sahihi na iliyo timamu, baada ya ndoa anachokiangalia ni namna ya kuboresha maisha yake.
Kuna wanaume wanawapiga sana wake zao, wanasema maneno mabaya. Lakini mwanaume kama kichwa cha familia, anapaswa kuwa na akili nzuri, anapaswa kuwa mfano wa kuigwa, kwa kuwa na kauli nzuri, sio ndio jamani?
Sasa kwabahati mbaya kuna watu ni vichwa, lakini matendo yao ni sawa na unyayo sijui maana hata nikisema ni sawa na kiuno bado hawafai. Je wewe mwanaume unaishije na mkeo au watoto kwenye familia yako? Eti kuna wanaume wanaamini nyumba ndogo ni kila kitu katika maisha…eti akigombana na mkewe ndio atakwenda kupata faraja!!!
Ndugu yangu mbona unakuwa huna akili kiasi hiki. Unapotoka nje, kwanza ni kwamba uniaibisha mwenyewe, yule ambaye uko naye kwa asilimia kubwa hata kama anakuchekea, kwanza anajua yuko kibiashara, lakini katika nafsi yake anaamini wewe ni mwanaume usiyefaa, kama uliyeweza kumdharau mkeo na watoto, utashindwa nini kumdharau yeye ambaye hauna naye mikataba yoyote?
Kama ni suala ni migogoro ndio inakumbikiza nyumbani, kwani unafikiri ni mtu gani ambaye unaweza kuishi naye bila kukwaruzana? Wewe umeishi kwenye tumbo la mama yako kwa miezi sijui tisa au chini ya hapo, na bado kuna wakati mnakwaruzana, iwe mtu tu mmekutana mitaani?
Migogoro ni jambo la kawaida katika uhusiano wa kimapenzi au ndoa. Cha msingi ni kufungua milango ya kujadiliana. Tatizo kubwa kuna watu wana kiburi kichafu kabisa, kwamba hawezi kusema nimekosa nisamehe….hata kama kweli amekosa. Ndoa haiwezi kwenda kokote kama watu wake hawako tayari kusameheana au kuomba msamaha

MELI YAZAMA ZANZIBAR, WATU ZAIDI YA 190 WAFA
WATU 160 wamefariki dunia na wengine 521 kujeruhiwa baada ya meli ya abiria LCT Spice Islanders, iliyokuwa ikisafiri kutoka Unguja kwenda Pemba, kupinduka na kuzama baharini.
Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa meli hiyo iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 600, ilizama usiku wa kuamkia jana kwenye Bahari ya Hindi kati ya Nungwi na Pemba, kilomita 20 kutoka Bandari ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa habari hizo, meli hiyo iliyotokea Unguja kwenye Bandari ya Malindi, ilipata hitilafu ikiwa njiani, kisha ikapinduka na kuanza kuzama taratibu. Ilikuwa na makoti ya uokoaji 200 tu.
Mwandishi Mkongwe nchini, Salim Salim, aliambia gazeti hili kwamba juhudi za kuoka zilianza kufanyika mapema kwa ushirikiana wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), KMKM, Jeshi la Polisi na wananchi kutoka eneo la Nungwi.
Salim alisema saa tata baada ya ajali hiyo kutokea jeshi la polisi lilifika katika eneo la polisi pamoja na wananchi walitoka sehemu mbalimbali. Polisi walitumia helikopta mbili na wananchi asilimia kubwa akiwa wavuvi walitumia mashua.
Pia boti za uokoaji za Azam na Express Zakhir zilifika katika eneo la tukio mapema na kuifanya kazi kubwa ya uokoaji.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP, Said Mwema alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo jana na kwamba chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
Alisema mpaka kufikia jana mchana watu waliokolewa katika ajali hiyo wakiwa hai walikuwa 525 na waliofariki 62.
Mwema alisema imeunda kamati maalum ya kufuatilia tukio hilo ambayo pia itahusisha Usalama wa Taifa.
“Hivi sasa Jeshi la Polisi, JWTZ, Usalama wa Taifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na KMKM ndio wanashughulikia suala zima la upelelezi ili kujua chanzo cha ajali hiyo,” alisema Mwema
Aliongeza: “ Eneo la Usimamizi wa mawasiliano na uratibu itakuwa chini ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, pia kuna kikosi kazi cha uokoaji na kikosi cha kukusanya taarifa na upelelezi wa tukio hilo,”.
Alipoulizwa idadi kamili ya watu waliofariki katika ajali hiyo pamoja na uwezo wa meli hiyo kubeba abiria na mizigo Mwema alisema: “Hivi sasa ndio tunaendelea na uchunguzi ili kubaini idadi kamili ya waliofariki, ila kwa sasa kinachofanyika ni uokoaji”.
Rais Shein
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, alifika kwenye eneo la tukio na kushiriki kikamilifu kutoa huduma ya kwanza kwa walinusurika katika ajali hiyo.
Akizungumza katika kijiji cha Nungwe, Dk Shein aliwataka Wazanzibari kuwa wavumilivu katika kipindi hiki wakitiana moyo kwa yote yaliyotokea.
"Huu ni mtihani wa Mwenyezi Mungu. Wazanzibari tuwe wavumilivu, Serikali itakayogharimia shughuli zote za mazishi," alisema Dk Shein.
Dk Shein alisema maiti waliotambuliwa watachukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi ila wale ambao ndugu hawataonekana watazikwa na Serikali kwa utaratibu maalumu.
Shuhuda
Mwandishi Mkongwe wa habari Zanzibar, Salim Salim, amelieleza gazeti hili kuwa meli hiyo ilizama katikati ya Kisiwa cha Pemba na Unguja eneo ambalo ndilo lenye mkondo mkuu bahari kuliko mikondo yote ya bahari barani Afrika.
Mikondo mingine mikuu ya bahari inayoufuatia mkondo wa Bahari wa Nungwi ni Pemba Channel ulioko nchini Msumbiji na Affond ulioko Somalia
Alisema ajali hiyo ilisababisha maduka yote kisiwani Pemba kufungwa kutokana na wakazi wengi wa pemba kwenda kutambua miili ya marehemu, iliyofanyika katika Viwanja vya Maisara vilivyoko kiwani humo.
"Wananchi walianza kutambua miili ya marehemu saa 8:30 mchana wakiwamo viongozi wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walioongozwa na Rais Shein na Makamu wake wa Kwanza, Maalim Seif Sharif Hamad.
"Maduka yote yamefungwa na misikitini kunafanyika sala maalumu. Pia vituo vyote vya radio na televisheni visiwani hapa, vimeacha kupiga muziki na pia kutakuwa na maombolezo maalumu ya ajali," alisema Salim.
Salim alisema katika viwanja hivyo vya Maisara walikusanyika madaktari kutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar ambao kwa pamoja wanatoa huduma ya kwanza katika mahema maalum kwa majeruhi.
"Sanda zinashonwa hapohapo uwanjani na Serikali imesema itagharimia shughuli zote za mazishi," alisema Salim.
Salim alisema maiti zote zilizokuwa zikitolewa, zilikuwa zimepewa namba na mpaka anaondoka uwanjani hapo jana mchana, maiti 160 zilikuwa zimeopolewa.
"Kazi ya uokoaji inaendelea ila mpaka mimi naondoka eneo la tukio, kulikuwa na maiti 160. Niseme tu kwamba, Serikali safari hii imeonyesha kuwajali wananchi wake, kwa kuharakisha kuanza uokoaji," alisema.
Dk Shein ashiriki kutoa
huduma ya kwanza
Katika hatua nyingine, jana Rais Shein alikuwa miongoni mwa madaktari waliokuwa wakitoa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa ajali hiyo ya meli.
Dk Shein ambaye siku nzima alikuwa katika eneo la tukio, akishirikiana na madaktari kuwapokea wagonjwa katika mahema maalumu na kuwapa huduma ya kwanza.
Watu wengi walionusurika katika hali hiyo walionekana kupata mshituko mkubwa, ingawa hawakuwa na majeraha makubwa.
Kazi hiyo ya uokoaji ilikuwa ikiongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na KMKM.
Wakati Dk Shein akiwa anashiriki kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alionekana muda wote akiwa sambamba na vikosi vya uokoaji akisimamia kwa karibu zoezi hilo.
"Maalim Seif alionekana akisimamia upatikanaji wa vifaa na vitu vingine muhimu vya uokoaji," kilisema chanzo cha habari kutoka Pemba
Kichanga aokoka kifo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi minne hadi mitano, aliokolewa katika ajali hiyo.
Televisheni ya Channel Ten, ilieleza kuwa mtoto huyo alikutwa akielea juu ya maji licha ya kutovalishwa kifaa chochote maalumu vya kuogolea. Kwa mujibu wa Kituo hicho cha Televisheni, mtoto huyo anaendelea vizuri.
Sumatra wazungumza
Akizungumza na Mwananchi Jumapili Meneja Mawasiliano kwa Umma wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), David Mziray.
Alisema taarifa walizonazo zinaeleza kuwa meli hiyo iliondoka Unguja kwenda Pemba saa 4:20 usiku jana.
“Mpaka sasa meli ya Mv Jitihada imeelekea eneo la tukio kwa ajili ya kuokoa watu, meli ilikuwa na abiria 500 na wafanyakazi 12,” alisema Mziray.
Aliongeza: “Meli hii imesajiliwa Zanzibar na taarifa za kuzama kwake zilifika saa 9:10 usiku wa kuamkia leo(jana),”.
Kikosi cha wanamaji Dar
Awali gazeti hili lilifika katika ofisi za kikosi cha wanamaji jijini Dar es Salaam na kuelezwa kuwa meli hiyo iliondoka jana (juzi) jioni ikiwa na abiria 229.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea ilipozamia meli hiyo Kamanda wa Kikosi hicho, Mboje Kanga, alisema meli hiyo ilizama ikiwa na zaidi ya watu 500.
“Mpaka sasa sijui kinachoendelea ndio niko njiani naelekea eneo la tukio, nipigie baadaye nitakuwa nimetapa kila kitu,” alisema Kanga.
Wafanyakazi Bandarini
Baadhi ya wafanyakazi wa bandarini pamoja na wabeba mizigo walilieleza gazeti hili kuwa huenda meli hiyo ilizama kutokana kubeba mizigo mingi.
Wafanyakazi hao ambao walikuwepo katika bandari hiyo wakati ikiondoka katika bandari ya Zanzibar wanasema kuwa jinsi ambavyo ilipakia abiria na mizigo huenda itakuwa ndiyo sababu ya kuzama kwake.
Mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema wakati meli hiyo ikiondoka Unguja alikuwepo na kwamba ilikuwa imeelemewa upande mmoja.
“Meli iliruhusiwa kuondoka bandarini Unguja kwa nguvu kwa kuwa watu waliokuwa wakitaka kupanda licha ya kuwa kuambiwa imejaa na walikuwa wengi. Meli ilipakiwa idadi kubwa ya nondo, madirisha, magunia ya unga wa ngano na mahindi,” alisema.
Mfanyakazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Shadrack alisema meli nyingi zinazotoka Unguja kwenda Pemba huwa zinajaza mizigo na watu wengi na kusisitiza kuwa, eneo la Nungwi ni baya hasa kama meli ina mzigo mkubwa kwa kuwa eneo hilo lina mkondo mkubwa wa maji.
“Nakwambia wazi meli hii ilikuwa na watu zaidi ya 600 maana wanasema waliookolewa tu ni 500…,” alisema Shadrack.
Hekaheka Bandarini Dar
Mwananchi Jumapili lilifika asubuhi bandarini jijini Dar es Salaam na kuta idadi kubwa ya watu wakitafuta usafiri wa meli kuelekea Zanzibar kwenda kutambua ndugu zao waliokuwa katika meli hiyo.
Ally Hamisi alilieleza gazeti hili kwamba, katika meli hiyo kulikuwa na ndugu zake saba ambao hajui kama wako hai ama wamekufa.
“Walikuwa wametoka katika harusi…, kwa kweli nimechanganyikiwa kabisa, pia alikuwemo jirani yangu ambaye nilikabidhiwa ili nimpeleke Zanzibar na mpaka sasa hajaonekana,” alisema Hamis.
Alisema meli hiyo ilipofika Unguja walipanda ndugu zake wengine watatu.
“Ni jambo la kusikitisha sana, usiku nilipigiwa simu na mmoja wa ndugu zangu akanieleza kuwa tumuombee kwa kuwa meli ilikuwa ikizama, baadaye simu yake haikupatikana tena na sijui kama yupo salama au la,”.
Naye Khamisi Abdallah alisema kwa masikitiko kuwa katika meli hiyo alikuwa na ndugu 10.
“Nimekata tiketi ili niende kushuhudia mwenyewe…, mpaka sasa siamini na sijui nani kapona nani kafariki, inaniuma sana,” alisema Abdallah kwa masikitiko.
Mwantumu Suleiman ambaye ni mkazi wa Zanzibar, alisema alikuja jijini Dar es Salaam na mume wake na mdogo ambao waliondoka na meli hiyo.
“Wao walikwenda ila mimi nilibaki hapa Dar es Salaam nilikuwa naumwa tumbo, niliposikia habari hizi nimechanganyikiwa kweli, bado sijapona, lakini acha niende nikashuhudiwa kilichotokea,” alisema Mwantumu kwa masikitiko.
Hii ni mara ya pili meli kuzama katika bahari ya Malindi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Mei 29, 2009, meli ya mizigo inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul, MV Fatih, ilipinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi, Zanzibar na kuua watu watatu na kujeruhi wengine 27.
Meli hiyo ilipinduka na kuzama ghafla ikiwa tayari imeshafunga gati katika Bandari ya Malindi majira ya saa 4.00 usiku na abiria waliokuwemo walikuwa wanataka kushuka.
Akisimulia mkasa wa ajali hiyo kepteni aliyekuwa akiendesha meli hiyo, Ussi Ali Ussi, alisema wakati akiingia bandarini ghafla aliona meli hiyo ikijaa maji na kulala upande wa kushoto.
Habari hii imeandaliwa na Talib Hamad, Fidelis Butahe, Claud Mshana, Elias Msuya na Geofrey Nyang’oro, Igunga
Wednesday, August 17, 2011
JOSE CHAMELEONE ABADILI DINI
Msanii wa mziki kutokea pande za uganda ameamua rasimi kubadili dhehebu lake la dini, msanii huyo ambaye alikuwa muumini wa roman catholic ameingia rasimi dini la kiislamu
Friday, June 10, 2011
CHADEMA WAIKOSOA BAJETI YA TANZANIA 2011-2012
Thursday, 09 June 2011 23:
Neville Meena, Dodoma
KAMBI ya Upinzani Bungeni imedai kwamba kuna upotoshaji mkubwa katika Bajeti ya S 200erikali iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, huku ikidai kwamba bajeti hiyo ni ya kulipa posho na madeni.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kambi hiyo mjini Dodoma na kusainiwa na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe inabainisha kuwa upembuzi uliofanywa umebaini kuwapo kwa upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwalengo la kuwajengea matumaini wananchi.
"Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (asilimia 27), asilimia 14 kulipa madeni na asilimia 13 kulipa posho mbalimbali," ilisema taarifa hiyo.
Miongoni mwa maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na upotoshaji ni kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umeme, ongezeko la jumla la Bajeti ya Serikali ikilinganishwa na ile ya mwaka 2010/11, posho mbalimbali, faini kwa madereva wazembe na ulipaji wa madeni ya Serikali.
Hakuna mradi mpya wa umeme
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tamko la Serikali kwamba imetenga kiasi cha Sh537 bilioni kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme, si kweli kwani kwa jumla Wizara ya Nishati na Madini, imetengewa Sh402.071 bilioni na kwamba hakuna mradi mpya wa umeme hata mmoja utakaoanzishwa.
"Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi ya kawaida Sh76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa Sh325,448,137,000. Sh325 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160 MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza,"inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alisema katika taarifa hiyo kuwa, kutokana na hali hiyo hakuna mradi mpya wa umeme unaoonekana katika bajeti hiyo na kwamba kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa na si hatua za kweli kumaliza matatizo ya umeme nchini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hakuna ongezeko lolote halisia la fedha katika bajeti ya mwaka huu, kwani kati ya Sh13.525 trilioni zilizotengwa, Sh1.901 trilioni, sawa na asilimia 14.06 ya bajeti yote ni kwa ajili ya kulipa madeni ya Taifa.
"Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha Serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki Sh11.624 trilioni ambazoni ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka unaomalizika wa 2010/2011," alisema Zitto katika taarifa yake hiyo na kuongeza: "Kwa kuzingatia kwamba thamani ya shilingi imekuwa ikishuka, bajeti iliyotangazwa ni ya kulipa madeni".
Bajeti ya posho sasa Sh987 bilioni
Kuhusu hatua za kupunguza posho, kiongozi huyo alisema hakuna ukweli wa kauli hiyo kwani Serikali imetenga kiasi cha Sh987 bilioni kwa ajili ya kulipa posho mbalimbali, fedha ambazo ni sawa na asilimia 13 ya bajeti nzima.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa kutokuwapo kwa nia ya dhati ya kupunguza posho, inaonekana katika hatua za kufanya marekebisho katika sheria ya kodi sura ya 332 ili kusamehe kodi ya mapato katika posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi katika taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye Bajeti ya Serikali.
"Hii inaonyesha kuwa kauli ya kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi, lakini haina udhati,"alisema.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa bajeti imeongeza mzigo mkubwa kwa wananchi kutokana na hatua yake ya kuongeza kiwango cha faini kwa madereva wazembe kutoka Sh20,000 hadi Sh300,000, na kwamba kiasi cha Sh50,000 kilichotangazwa na Waziri Mkulo juzi kinatofautia na maelezo kwenye vitabu vya bajeti.
Alisema hatua hiyo itawaathiri wananchi hasa vijana walioajiriwa ama kujiajiri katika huduma za usafiri na usafirishaji na kwamba kipengele hicho pia kinalenga kuuhadaa umma.
Serikali juzi ilitangaza hatua kadhaa za kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima katika mwaka wa fedha wa 2011/2012, lakini fedha za matumizi mengineyo, maarufu kama Other Charges (OC), zimeongezwa kwa asilimia 8.62 ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayofikia ukomo tarehe 30 mwezi huu.
Fedha za OC katika bajeti mwaka ujao wa fedha ni Sh3.089 trilioni ikilinganishwa na kiasi cha Sh2.823 kilichotengwa katika mwaka wa fedha wa 2010/2011, likiwa ni ongezeko la Sh266.599 bilioni.
Fungu la fedha za OC ndilo hutumika kugharimia posho mbalimbali kwa watumishi wa umma na uendeshaji wa semina, warsha na makongamano pamoja na kugharimia safari za viongozi ndani na nje ya nchi.
Kafulila adai bajeti haijazingatia vigezo vya uchumi
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila aliliambia Mwananchi katika viwanja vya Bunge kuwa, hali hiyo inadhihirisha kwamba bajeti iliyowasilishwa na Mkulo ililenga zaidi kutafuta kuungwa mkono kuliko kuzingatia vigezo vya kiuchumi.
"Kama mwaka wa fedha unaoishia mwishoni mwa mwezi huu fedha za OC ni kidogo kuliko zile ambazo zimetengwa mwaka ujao wa fedha, basi ni dhahiri kwamba hatuwezi kusema posho zitapunguzwa, hapa nadhani kuna tatizo,"alisema Kafulila.
Alisema fungu la fedha za OC lazima lipitiwe upya kwani fedha zilizotengwa ni zaidi ya kiasi cha fedha ambazo Serikali imeomba kutoka kwa nchi wahisani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Iwapo fedha za OC ni Sh3 trilioni na fedha za miradi ya maendeleo tunazoomba kutoka kwa wafadhili ni kiasi hicho hicho, utaona kwamba ni jambo la kushangaza, hapa kuna mambo mengi ya kuweka sawa,"alisema Kafulila, huku akibainisha kuwa bajeti hiyo ya Serikali si mbaya sana kwani imekumbuka umuhimu wa miundombinu ya usafirishaji.
Akiwasilisha bungeni juzi Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12, Waziri Mkulo alibainisha hatua kadhaa za Serikali kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima akiahidi kupunguza posho zisizo na tija, safari za ndani na nje za viongozi na ukubwa wa misafara ya viongozi hao ili fedha husika ziweze kutumika kugharimia shughuli nyingine za maendeleo.
"...........Serikali itasitisha ununuzi wa samani za ofisi, hususan zile zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija, kupunguza matumizi ya mafuta kwa magari ya Serikali, kupunguza safari za ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa misafara na kuendelea kupunguza semina na warsha, isipokuwa pale inapobidi na kwa kibali cha Ofisi ya Waziri Mkuu..," alisema Mkulo.
Sh3 trilioni kutoka nchi wahisani
Kadhalika majedwali ya ufupisho wa hesabu za bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12 yanabainisha kuwa fedha za maendeleo zinazotarajiwa kutoka kwa nchi wahisani ni kiasi cha Sh3.054 trilioni. Kiasi hicho kinazidiwa kwa asilimia 18.9 sawa na Sh5.853 bilioni kikilinganishwa na fedha za OC ambazo ni Sh3.089 trilioni.
Katika bajeti hiyo, fedha zote zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni Sh4.925 trilioni, ambapo fedha za ndani ni Sh1.871 trilioni.
Mchanganuo mzima wa bajeti hiyo unaonyesha kuwa fedha za miradi ya maendeleo zilizotengwa ni sawa na asilimia 31 ya bajeti nzima, wakati fedha za matumizi mengineyo (OC) ni sawa na asilimia 32, mishahara asilimia 23, malipo ya madeni asilimia 8, madeni mengine asilimia 3 na riba ya madeni ya ndani na nje asilimia 3.

KIZURI CHAPASWA KULIWA NA WOTE WANAOKIHITAJI
The Mandela Rhodes Scholarships BUILDING EXCEPTIONAL LEADERSHIP IN AFRICA | | |
Home
The Mandela Rhodes Scholarships
- About the Scholarships
- The vision
- Eligibility
- Characteristics Sought in a Mandela Rhodes Scholar
- Selection criteria
- The award
- Applications
- Terms & Conditions
- FAQs about the Mandela Rhodes Scholarships
The Mandela Rhodes Scholars
- Overview
- Meet the Mandela Rhodes Scholars
- The Mandela Rhodes experience
- Mandela Rhodes Scholars: where are they now?
- Alumni - the Community of Mandela Rhodes Scholars
The Mandela Rhodes Foundation
- The Mandela Rhodes Foundation
- Milestones of The Mandela Rhodes Foundation
- Organisational structures
- Trustees
- Staff
- Yearbooks
- Financial Results
Donors
Related Links
- The Rhodes Trust
- Nelson Mandela Foundation
- The Nelson Mandela Children's Fund
- Friends of The Mandela Rhodes Foundation (USA)
- Community of Mandela Rhodes Scholars
Contact Us
The Mandela Rhodes Scholarships aim to help in building leadership excellence in Africa.
A Mandela Rhodes Scholarship is more than a bursary, though the costs of Scholars are generously covered during their period of study.
The Mandela Rhodes Foundation offers young Africans who exhibit academic prowess as well as broader leadership potential an educational opportunity unique on the continent. While pursuing their chosen post-graduate degree, each Scholar benefits from access to leadership development programmes, rooted in the principles underpinning the Foundation.
In addition to the opportunity to interact with a diverse group of fellow-Scholars that spans the continent and academic disciplines, they become part of a wide-ranging network of young Africans of excellence who are expected to play leadership roles in their fields and societies in the years following their time ‘in residence’. More...
Since the selection of the first cohort of eight Scholars in 2005, a total of 123 Mandela Rhodes Scholarships has been awarded. More...
The intention to establish The Mandela Rhodes Foundation was announced in February 2002 when The Rhodes Trust, as part of its centenary celebrations, entered into a partnership with Mr Mandela and pledged a founding benefaction over 10 years.
The Mandela Rhodes Foundation is a unique partnership seeking to close a circle of history for the benefit of current and future generations of Africans. It brings together the 20th century legacy of leadership and reconciliation embodied by Nelson Rolihlahla Mandela, and Cecil John Rhodes's 19th century legacy as it relates specifically to education and entrepreneurship
The overarching mission of The Mandela Rhodes Foundation is to help build exceptional leadership capacity in Africa, by providing excellent educational and leadership development opportunities to individual Africans with leadership potential; as well as by creating over time a network of well-rounded leaders of talent, effectiveness and integrity across African society. More...
©2010 Mandela Rhodes Foundation, all rights reserved
I would like to take this opportunity of thanking all of you around the world who are assisting in the great project of building The Mandela Rhodes Foundation.
The central purpose of The Mandela Rhodes Foundation is to build exceptional leadership capacity in Africa.
The bringing together of these two names represents a symbolic moment in the closing of the historic circle; drawing together the legacies of reconciliation and leadership and those of entrepreneurship and education.
Already the Mandela Rhodes Scholarships are changing the lives of young Africans, who will play vital roles in the future of the continent.
The achievements of The Mandela Rhodes Foundation so far have been remarkable, but it is its future potential that is most exciting.
I urge you to help in every way you can, knowing that you have my personal appreciation.
Nelson Rolihlahla Mandela
Johannesburg, South Africa
Johannesburg, South Africa
TUNAHITAJI WABUNGE WALO NA UCHUNGU NA NCHI YAO KAMA ZITO KABWE, HAKIKA ZITO NI MWAKILISHI WA WATU MASKINI
| Zitto ajitoa kupokea posho za Bunge | Send to a friend |
| Thursday, 09 June 2011 23:25 |
| MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi.Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.Katika barua hiyo, ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, Zitto alisema anaamini kuwa watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida. Zitto alisema kuwa posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao. "Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Act of 2008) na kwa mujibu wa Masharti ya Kazi za Mbunge niliyokabidhiwa, ninastahili kupata posho za vikao, (sitting allowances) kila ninapohudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake,"alisema Zitto na kuongeza: "Ni imani yangu kuwa posho ya kikao haistahili kulipwa kwa mbunge na mtumishi mwingine yeyote wa Serikali kwani kuhudhuria kikao ni sehemu ya kazi yangu,". Kupitia barua hiyo, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha, alieleza kwamba amekuwa akipendekeza posho za vikao hivyo ifutwe, jambo ambalo pia limo katika mapendekezo ya chama chake (Chadema) katika Bajeti ya 2011/2012. "Nimekuwa nikipendekeza kuwa posho hii ifutwe. Chama changu cha Chadema pia kimependekeza jambo hili katika mapendekezo yake ya Bajeti 2011/2012," alisema Zitto na kuendelea: "Mpaka hapo mfumo wa kulipana posho za vikao utakapofutwa, ninaelekeza kwamba stahili zangu zote za posho zielekezwe katika Taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).., utaratibu huu uanze kuanzia tarehe 8/6/2011." Katibu wa Bunge agoma kuizungumzia Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa jana kama amepokea barua hiyo ya Zitto, alisema kuwa, yeye kama mtendaji wa mhimili huo wa Dola, anapokea barua nyingi, hivyo si rahisi kukumbuka kama barua hiyo imefika ofisini kwake. Lakini akasema, hata kama barua hiyo itakuwa imemfikia ofisini, kanuni na taratibu haziruhusu Bunge kutangaza habari za mtu binafsi.Alisema ofisi yake hairuhusiwi kuandika masuala binafsi ya wabunge yanayofikishwa ofisini na kwamba hilo linawezekana ikiwa mhusika (Zitto), ameruhusu lifanyike kwa maandishi. "...Haturuhusiwi kuandika habari za mtu. Nikiwa Katibu wa Bunge, napokea barua nyingi 'personal' (binafsi), lakini kama yeye mwenyewe amewaambieni kuwa kaleta barua hiyo, basi mwambieni pia atuandikie barua kuturuhusu na sisi ili tulitangaze hilo," alisema Dk Kashililah. Bajeti ya posho kulipa walimu laki moja Uamuzi huo wa Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, umekuja huku taarifa za utafiti wa taasisi ya Policy Forum inayojihusisha na tafiti mbalimbali za sera zikionyesha kuwa, katika mwaka 2008/2009, Serikali katika bajeti yake ilitenga Sh506 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho. Kwa mujibu wa utafiti huo, ambao taarifa yake ilitolewa mwaka uliopita, fedha hizo ni sawa na mishahara ya mwaka mzima kwa walimu 109,000 ambao ni robo tatu ya walimu wote nchini. Kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2009/10 kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi wa umma kilikuwa sawa na asilimia 59 ya malipo ya wafanyakazi wa ngazi ya chini . |
Comments
123456
Thursday, June 9, 2011
WHAT IS SO SPECIAL WITH TODAY'S MARRIAGES?
Photo: Thinkstock
The Pew Research Center recently found that 40 percent of Americans think marriage is becoming obsolete. Another recent Pew study found that Millennials (people age 18 to 29) say they think being a good parent is way more than having a good marriage.
Once considered an imperative of sorts, traditional marriage is getting a second look—and research suggests that it may be coming up short. Instead of considering themselves to be happily married, some people are discovering that they're only "semi-happy," and their quest for fulfillment can lead them to extramarital affairs and divorce.
A semi-happy marriage is one of low conflict, low passion, and low satisfaction. "One minute, you love the stability and contentment. The next minute, you think it’s not the right marriage, and there are flaws in the marriage that are serious, even though there are also great things about the marriage," says historian Pamela Haag, author of "Marriage Confidential: The Post-Romantic Age of Workhorse Wives, Royal Children, Undersexed Spouses, and Rebel Couples Who Are Rewriting the Rules." In other words, "one minute you can't imagine staying, the next you can't imagine leaving," Haag says. "It’s these kinds of marriages that are 'low-conflict' but not all that satisfying that contribute the lion’s share to divorce court each year."
Her own 13-year-long marriage almost fit the bill. "Often, in my own case, I really can't tell if my marriage is woeful or sublime," she writes in her book. "Maybe I'm just so profoundly content that it feels like unhappiness, because nirvana is dull in this way, it lacks frisson." (She adds that she thinks her husband is "an amazing sport, and brave, to let me write about this topic of mixed feelings at all, even though a good number of husbands and wives have mixed feelings.")
Boredom can also cause major marital problems. A national survey of 3,341 people by advice website Good in Bed and Kristen Mark of The Kinsey Institute for Research in Sex, Gender, and Reproduction found that 25 percent of people are are bored in their current monogamous relationship, and another 25 percent admit to being "on the brink" of boredom.
“Boredom is basically like an attack on a relationship’s immunity system," says Ian Kerner, PhD, founder of Good in Bed and author of "Love in the time of Colic: A New Parents' Guide to Getting It On Again." "It’s not a coincidence that a fifth of respondents admitted to being unfaithful to their partner as a result of being bored."
While most of the women Haag interviewed said they felt lonely in their semi-happy marriages, men told her that they felt "trapped" or "penned in." It didn't seem to matter if they married "too young" or waited until they were older; what mattered was what people expected from their marriages. And for many, the traditional blueprint that their parents followed is simply no longer a good fit.
"It’s sometimes said that marriage is on the decline because our expectations are too high," says Haag. "I think it’s that our expectations for marriage may be too low—such that single people feel, perhaps rightly, that there isn’t much that marriage would add to their lives."
"My generation—people in their 30s, and 40s, and early 50s—are perhaps caught betwixt and between the old romantic ideals and the new post-romantic expectations," she adds.
Haag emphasizes the fact that she's a historian and not a marriage therapist, and says that she does not "endorse a particular marital style." In her book, she explores several suggestions for "forging a third way between melancholy persistence and divorce," ranging from slightly outside-the-box (rewriting your vows to more accurately reflect your life as it is now, for instance, or sleeping in separate bedrooms) to the extreme (redefining marriage as a temporary parenting agreement or giving the green-light to discreet extramarital affairs, among other things.)
Even so, people can still end up feeling only semi-happy. "There's a part of your soul that isn't nourished in marriage, and it's too big a part to live without," Haag writes. "You've tried, but you fear that you're in the wrong marriage, however wonderful your spouse may be."
JAMANI HIVI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYA KAZI NI DHAMIRA YA KWELI?
Wednesday, 08 June 2011
Mtumishi wa lililokuwa Shirika la Reli la Afrika Mashariki, Kituo cha Kigoma, Said Luziga (88) akifuatilia kupitia radio hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/12, Dar es Salaam jana. Picha na Said PowaPatricia Kimelemeta SERIKALI imeahidi kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa sekta binafsi na watumishi wa umma ili waweze kuondokana na hali ngumu ya maisha. Hayo yalisemwa na Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo wakati wa akiwasilisha bajeti ya mwaka 2011/12 kwenye kikao cha Bunge kilichofanyika mjini Dodoma jana.
Mkulo alisema kuboreshwa kwa maslahi ya watumishi wa umma kutatokana na uwezo wa mapato yake, jambo ambalo litawasaidia kumudu gharama za maisha. “Serikali imeahidi kuboresha maslahi ya watumishi ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara kwa watumishi hao, lengo ni kuhakikisha kuwa wanamudu gharama zilizopo za maisha,"alisema Mkulo. Alisema maeneo ambayo yatatiliwa mkazo ni pamoja na malipo ya mishahara na likizo kwa wakati, na kwamba watahakikisha watumishi hao wanalipwa mafao yao mara baada ya kustaafu, pamoja na pensheni zao za kila mwezi.
Alisema sambamba na hilo,serikali itatoa mafunzo kwa maofisa wa Hazina ndogo na mahakama zote zinazoshughulikia mirathi, na kuweka mikakati ya pamoja kuwaondolea kero wasimamizi na warithi wa mali za marehemu ambao walikuwa watumishi wa serikali enzi za uhai wao.
Mwaka jana, serikali ilitumia zaidi ya Sh2.332 trilioni kwa ajili ya kugharimia malipo ya mishahara,ajira mpya, upandishwaji vyeo na kulipia madai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara kwa watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Katika bajeti hiyo ya mwaka jana, Mkulo alitangaza punguzo la asilimia moja kwa kodi ya mishahara kutoka asilimia 15 hadi 14 ya mishahara hiyo.
Nalo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi(Tucta), liliwahi kuwasilisha mapendekezo ya mishahara ya watumishi wa umma na sekta binafsi ambapo kiwango cha chini lilitaka kiwe Sh315,000 kwa mwezii, lakini serikali ilishindwa kuongeza kiasi hicho badala yake iliongeza hadi Sh135,000 mwaka jana

Subscribe to:
Posts (Atom)
we mzee naona bado akili yako ijakomaa hata kama umezeeka basi umezeeka vibaya kama wazee wenzio wa CCM kama huna cha kusema bora kukaa kimya m-s.n.g.e
Ciao.
Ras Vin. Medical Instute Heidelberg.