Mkulo alisema kuboreshwa kwa maslahi ya watumishi wa umma kutatokana na uwezo wa mapato yake, jambo ambalo litawasaidia kumudu gharama za maisha. “Serikali imeahidi kuboresha maslahi ya watumishi ikiwa ni pamoja na kuongeza mishahara kwa watumishi hao, lengo ni kuhakikisha kuwa wanamudu gharama zilizopo za maisha,"alisema Mkulo. Alisema maeneo ambayo yatatiliwa mkazo ni pamoja na malipo ya mishahara na likizo kwa wakati, na kwamba watahakikisha watumishi hao wanalipwa mafao yao mara baada ya kustaafu, pamoja na pensheni zao za kila mwezi.
Alisema sambamba na hilo,serikali itatoa mafunzo kwa maofisa wa Hazina ndogo na mahakama zote zinazoshughulikia mirathi, na kuweka mikakati ya pamoja kuwaondolea kero wasimamizi na warithi wa mali za marehemu ambao walikuwa watumishi wa serikali enzi za uhai wao.
Mwaka jana, serikali ilitumia zaidi ya Sh2.332 trilioni kwa ajili ya kugharimia malipo ya mishahara,ajira mpya, upandishwaji vyeo na kulipia madai ya malimbikizo na mapunjo ya mishahara kwa watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Katika bajeti hiyo ya mwaka jana, Mkulo alitangaza punguzo la asilimia moja kwa kodi ya mishahara kutoka asilimia 15 hadi 14 ya mishahara hiyo.
Nalo Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi(Tucta), liliwahi kuwasilisha mapendekezo ya mishahara ya watumishi wa umma na sekta binafsi ambapo kiwango cha chini lilitaka kiwe Sh315,000 kwa mwezii, lakini serikali ilishindwa kuongeza kiasi hicho badala yake iliongeza hadi Sh135,000 mwaka jana
No comments:
Post a Comment