Mawaziri wengine wapata kikombe | Send to a friend |
Sunday, 27 March 2011 05:59 |
0diggsdigg Neville Meena na Mussa Juma, LoliondoNI kama mbio za kupokezana vijiti kwa mawaziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ambao wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge, Loliondo kwa ajili ya kunywa dawa ya kutibu magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile. Jana ilikuwa ni zamu ya mawaziri wawili ambao ni Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Hovisya, ambao walifika Samunge na kila mmoja kupata kikombe cha babu. Mawaziri hao walifika Loliondo asubuhi kwa ndege ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kisha kwenda Samunge na jioni waliondoka kwenda mkoani Manyara. Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Loliondo mara baada ya kurejea kutoka Samunge, Maige alisema: "Nimekunywa dawa mimi binafsi, si kwa niaba ya Serikali wala kitu kingine chochote…". Maige ambaye pamoja na Hovisa walionekana kuwa na haraka kutokana na kubanwa na sheria za uwanja wa ndege kutotumika zaidi ya saa 12.00 jioni, pia alizungumzia mazingira ya utoaji wa dawa hiyo akisema lazima zichukuliwe hatua za haraka kubadili mfumo wa sasa wa utoaji. Alisema hivi sasa taratibu za utoaji wa dawa hiyo si nzuri kwani zinawalazimisha baadhi ya wagonjwa kukaa kwenye foleni kwa siku saba wakisubiri zamu zao hali ambayo alisema ingeweza kuepukwa. Kauli ya Maige imekuja wakati ambao Serikali inasubiriwa kutoa tamko rasmi kuhusu kuendelea ama kusitishwa kwa tiba hiyo baada ya kujadili hali ilivyo katika vikao vilivyokuwa vikiongozwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi. |
No comments:
Post a Comment