Monday, December 24, 2012

CHADEMA YARONGA MAKAMU MWENYEKITI TUTUPA KADI YAKE YA UANACHAMA


"KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema chama hicho kinasubiri kupokea taarifa ya mgogoro unaofukuta ndani ya chama hicho mkoani Katavi na kusababisha Makamu Mwenyekiti wake Taifa , Said Arfi, kutupa kadi yake ya uanachama."

KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa amesema chama hicho kinasubiri kupokea taarifa ya mgogoro unaofukuta ndani ya chama hicho mkoani Katavi na kusababisha Makamu Mwenyekiti wake Taifa , Said Arfi, kutupa kadi yake ya uanachama.

Ameeleza kuwa Katiba ya chama hicho inaeleza wazi kwamba unapoibuka mgogoro, unatakiwa kuripotiwa katika ofisi ya Katibu Mkuu Taifa ndani ya siku 14.

Tukio la Arfi kutupa kadi ya Chadema lilikuwa la pili ndani ya wiki moja, kwani juma lililopita uliibuka mgogoro mwingine wilayani Karatu ambako pamoja na mambo mengine uliishia kwa Kamati Kuu kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya.

Arfi ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini, alitishia kujitoa Chadema juzi, katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya chama hicho Mikoa ya Katavi na Rukwa kilichoketi Namanyere, Nkasi na kufikia uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Rukwa, Laurent Mangweshi.

Katika kikao hicho, Arfi anadaiwa kuichukua kadi yake ya Chadema na kumtupia Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Rukwa, John Mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha kuondoka ukumbini, kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi aichukue kadi yake hiyo.

Hata hivyo, Mangweshi jana aliliambia Mwananchi kwamba hajapewa barua hiyo mpaka sasa na kwamba yeye bado ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Rukwa, kauli ambayo ilipingwa na Katibu wa chama hicho mkoani Rukwa na Katavi, Ozem Chapita aliyesema kuwa ipo tayari na wameisafirisha kwa basi jana mchana ili imfikie.

Akizungumzia tukio hilo jana Dk Slaa alisema  taarifa hizo amezisikia ila hawezi kutoa maamuzi kwa kuwa Chadema kinafuata taratibu za vikao pamoja na Katiba yake.

“Utaratibu wa chama ni kwamba malalamiko yeyote ni lazima yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu ndani ya siku 14” alisema Dk Slaa na kuongeza;

“Mimi kama Katibu Mkuu ni lazima nifuate taratibu za chama na sio kufanya vinginevyo.”

Alisema kuwa taarifa hizo amezisikia kupitia vyombo vya habari na kwamba anachokisubiri ni taarifa rasmi ya maandishi ili kama chama kiweze kukaa vikao na kujadili mgogoro huo.

Alipoulizwa kuna taarifa kwamba baadhi ya makada wa chama hicho wanatumiwa kukivuruga, Dk Slaa alisema kuwa inawezekana hilo likawa na ukweli lakini kama kawaida ya chama hicho, hakitoi maamuzi bila ya kukaa vikao.

“Hizo ni taarifa ambazo zipo na zinaandikwa kila siku katika vyombo vya habari, zikija rasmi katika ofisi ya chama zitajadiliwa” alisema Dk Slaa.

Arfi alifikia hatua hiyo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana.


Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilifafanua kuwa Arfi alikerwa na kauli iliyotolewa na Mangweshi kuwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alipokea rushwa kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, Arfi alipandwa na hasira na kuamua kumrushia kadi Mallack kisha kutoka nje ya ukumbi.

“Hatua hiyo ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo na kisha wakamwekea kadi yake ya uanachama katika mfuko wake wa shati,” alisema mmoja wa makada hao.

Arfi mwenyewe hakupatikana juzi kuzungumzia tukio hilo na hata jana alipotafutwa simu zake zote zilikuwa zimezimwa.

Mangweshi aeleza ya moyoni

Akizungumzia kitendo cha kuvuliwa madaraka
Mangweshi alisema mara baada ya kukabidhiwa barua yake atakata rufaa kwa maelezo kuwa haki haikutendeka katika kikao hicho.

Alisema mpaka sasa taarifa za kuwa amevuliwa uongozi anazisikia katika vyombo vya habari, huku akisisitiza kuwa yeye bado ni Mwenyekiti wa Bavicha wa mikoa  ya Rukwa na Katavi.

Alipohojiwa juu ya kuonywa mara kadhaa katika vikao kutokana na utovu wake wa nidhamu alisema, “Katika maisha yangu sijawahi kuonywa na hata Chadema sikuwahi kuonywa tangu nilipojiunga mwaka 2001, hakuna kikao cha baraza la uongozi kilichokaa kunijadili.”

Alifafanua kwamba hata Baraza la Usuluhishi halina mamlaka ya kumvua mtu madaraka na kuongeza kuwa  kikao kilichofanyika  Namanyere kilikuwa ni cha Baraza la Usuruhishi na si cha Baraza la Uongozi ambalo alidai kuwa ndio lenye mamlaka.

Alisema ameshangazwa na kitendo cha viongozi  wa Chadema mkoani Katavi kukimbilia katika vyombo vya habari kutoa tamko la kumfukuza kabla ya kukamilisha taratibu za kichama.

“Mimi ndio nilitakiwa kukimbilia katika vyombo vya habari kudai haki yangu kama wangenikabidhi barua yangu, kinyume chake wao ndio wamekimbilia huko tena bila kufuata taratibu” alisema na kuongeza;

“Kama hawatanitendea haki sitahama Chadema, nitafia hapa hapa kwa sababu chama hiki lengo lake ni kulikomboa taifa kutoka mikononi mwa CCM.”

Katibu wa chama hicho mkoani Rukwa na Katavi, Ozem Chapita alikiri kuchelewa kwa barua ya kumvua madaraka  Mangweshi  na kusema kuwa tatizo ni kwamba  mwenyekiti huyo anaishi mkoani Katavi  huyu yeye ambaye ni mtendaji mkuu wa chama hicho akiwa anaishi mkoani Rukwa.

Alisema barua hiyo ipo tayari na wameisafirisha kwa basi ili iweze kumfika Mangweshi.



Tanga kwazidi kufukuta

Katibu wa Bavicha mkoani Tanga, Deogratius Kisandu ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kubatilisha Uchaguzi Mkuu wa Rais mwaka 2010  kwa kuwa ulikuwa na wagombea wawili kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kitendo hicho kinatakiw akufanywa haraka baada ya Dk Slaa ambaye aligombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya Chadema kukiri  kwama mpaka sasa bado anayo kadi ya CCM.

“Katika hili ni  ni wazi kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ulikuwa batili na kulikuwa na wagombea wawili kutoka chama kimoja” alisema Kisandu.

Kisandu aliyasema hayo jana wakati akijibu tuhuma alizotupiwa na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tanga, Said Mbweto  kwamba amekurupa kutoka tamko la kumtaka Dk Slaa ajiuzulu.

“Mara baada ya Dk Slaa kukiri kuwa na kadi ya CCM , Nec inastahili kubatilisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuitisha upya uchaguzi wa Rais ili wajitokeze wagombea wapya wa nafasi hiyo” alisema Kisandu.

Alisema kwa maana hiyo ni kwamba hata Rais Kikwete kwa sasa hastahili kuwa katika nafasi hiyo kwa sababu kauli ya DK Slaa imebatilisha nafasi yake.

Alisema hakukurupuka kutoa kauli hiyo na kwamba yalikuwa mawazo yake binafsi na kusisitiza kuwa msmimamo wake uko palepale.

Karatu wapitisha bajeti

wilayani Karatu Kamati ya Ushauri ya wilaya ya hiyo (DCC), juzi imepitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya  mwaka 2013/14 ya Halmashauri ya wilaya hiyo, ambapo kiasi cha Sh 20.6 bilioni kinatarajiwa kukusanywa.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Clementi Berege akiwasilisha taarifa ya mapendekezo hayo,katika kikao hicho, kilichoongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Felix Ntebenda, alisema bajeti hiyo ya 20.6 bilioni ni ongezeko la  sh 51.7 milioni ya bajeti iliyopita ya mwaka 2012/13.

Alisema mapato ya ndani ya halmashauri hiyo yanatarajiwa kufikia 1.9 bilioni,Ruzuku ya matumizi ya kawaida 17.3 bilioni na ruzuku ya miradi ya maendeleo 2.1 bilioni.

Hata hivyo, alisema bajeti hiyo, inaweza kubadilika kutokana na maoni na vyombo vingine vya maamuzi, ikiwepo baraza la madiwani na vyombo vingine kabla ya kufikishwa kwenye bajeti kuu.

Akichangia taarifa hiyo, Mkuu wa wilaya hiyo, Ntibenda aliwataka wadau wa maendeleo katika wilaya hiyo, kuendelea kushirikiana na serikali katika kuifanikisha bajeti hiyo.

Hata hivyo, Ntibenda aliwataka watendaji na halmashauri na wanasiasa kushirikiana kwa pamoja kuisaidia wilaya hiyo, kwani wakati wa siasa umekwisha na kazi iliyombele yao wote ni kusaidia maendeleo ya wakazi wa wilaya hiyo.

"sitaki kusikia kuna miradi imekwama kwa ajili ya mambo ya siasa, chaguzi zimekwisha sasa tuchape kazi"alisema Ntibenda.

Awali wajumbe hao pia walipitisha mapendekezo ya kupeleka kwenye kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa Arusha(RCC), kuomba barabara ya kutoka Ayasi-Endabash hadi Manyara kibaoni.

Mkuu wa wilaya hiyo, alisema barabara hiyo ni muhimu sana kwa maendeleo ya wilaya hiyo lakini halmashauri imeshindwa kuitengeneza kutokana na gharama kubwa kuhitajika ikiwepo ujenzi wa daraja.

Akizungumza katika kikao hicho, mbunge wa jimbo la Karatu, Mchungaji Israel Natse, aliwataka watendaji wa halmashauri ya Karatu kuacha kuwa vikwazo vya maendeleo.

Natse alisema hivi sasa wilaya hiyo, inakabiliwa na migogoro kadhaa  na kukwama kwa miradi ya maendeleo kutokana na baadhi ya watendaji wa halmashauri, wakiwepo watendaji wa vijiji kuwavuruga wananchi.

Kikao hicho, lichofanyika ukumbi ya maendeleo Karatu,pia kilishirikisha wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya siasa, wakuu wa idara wa halmashauri ya karatu na viongozi katika ngazi mbali mbali za wilaya hiyo.

Imeandaliwa Fidelis Butahe, Dar na Juddy Ngonyani, Katavi, Burhani Yakub, Tanga na Mussa Juma, Arusha

Wednesday, December 19, 2012

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA SANA ZABAINIKA KUVUNJA UNYUMBA KWA KUADIMIKA KWA WATOTO NA HUDUMA ISIYORIDHISHA KITANDANI


“Kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” alisema Dk Massawe"

TAFITI za kisayansi zimebaini kuwa nguo za ndani hasa zinazobana kwa wanaume na zile za aina ya nailoni (nylon) zinaathiri uwezo wa mbegu za kiume, hivyo kushindwa kutunga mimba.

Utafiti huo uliofanyika katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zilizotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba.

Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama Dar es Salaam.

Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga ujauzito katika nyumba ya uzazi ya mwanamke.
Akizungumzia utafiti huo jana, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi katika Hosipitali ya Taifa Muhimbili, Dk Cyril Massawe, alisema una ukweli kutokana na mbegu za kiume kuwa nje ya mwili wa mwanamume tofauti na mwanamke ambaye kizazi chake kipo ndani.

“Kwa kawaida mwanamume anayeishi maeneo ya joto anapaswa kuwa makini sana, ili kuhifadhi vizuri manii yake anatakiwa kutumia mavazi yenye kupitisha hewa,” alisema Dk Massawe.

Ufaransa na Uingereza
Utafiti uliofanywa Ufaransa umebaini kuwa, upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi ulianza kutokea tangu mwanzoni mwa 1990.

Awali, ilikuwa ikiaminika kuwa kupungua kwa uwezo wa mbegu za kiume kulitokana na sababu kama vile mtindo wa maisha, ulaji na matumizi ya dawa kupindukia na matumizi ya vyakula vyenye kemikali nyingi, lakini safari hii utafiti umebaini kuwa matumizi ya nguo za ndani yamekuwa yakiwaathiri wanaume wengi.

Mtafiti wa Uingereza, Profesa Richard Sharpe anasema tatizo hilo linaweza kuepukwa ikiwa mhusika atajitahidi kuvaa nguo zinazokubalika na mahala alipo. Hata hivyo, anapendekeza uchunguzi zaidi ufanywe ili kulinda kizazi cha sasa na kijacho.

Mtafiti huyo kutoka Chuo Kikuu cha Edinburgh anasema: “Uingereza suala hili halijawahi kuonekana wala kutiliwa mkazo na kuwa kipaumbele katika afya, labda kwa sababu ya wasiwasi kwamba sehemu za mwanamume zinatakiwa kubanwa. Hivi sasa hakuna shaka kwamba suala hilo ambalo liliongelewa hapo awali lina ukweli ndani yake, hivyo ni wakati kwa watu wote kuchukua hatua.”

“Kutokuchukua hatua kutasababisha familia nyingi kukosa watoto na hivyo idadi ya watu itapungua, lakini katika hali ya kawaida, ni vyema watu wakaelimishwa namna ya uvaaji. Sehemu za joto mtu anatakiwa kuvaa pamba na si nailoni ili kulinda mbegu zake.”

Profesa Sharpe anasema bado wanasayansi wana kazi kubwa kwani mpaka sasa karibu kila eneo ambalo wanasayanasi wamelichunguza limebainisha kuchangia tatizo hilo, lakini mpaka sasa wanafikiri kuwa vyakula vyenye mafuta na vile vyenye kemikali nyingi vina mchango mkubwa zaidi katika tatizo hilo.

Watafiti ambao walitumia takwimu kutoka katika vituo vya afya 126, waligundua kuwa tangu mwaka 1989 mpaka 2005, kulikuwa upungufu wa uwezo wa manii kwa mwanamume kufanya kazi kwa asilimia 32.2, kiwango ambacho ni karibu asilimia mbili kwa mwaka.

Watafiti walisema: “Kwa ufahamu wetu, ni utafiti wa kwanza kufanyika na umehusisha mbegu za kiume hai na uwezo wa manii katika nchi nzima kwa kipindi kirefu.”
“Huu ni utafiti mkubwa na unatoa onyo kali kiafya kwa jamii. Lakini huwezi kumlazimisha mtu kuhusu matumizi ya nguo za ndani,” wanasema.

LULU BADO MAJI YA SHINGO, ANAENDELEA KUSOTA JERA NA UJAUZITO WAKE

"Hata hivyo, jana upande wa mashtaka ulieleza mahakamani kuwa kwa sasa imebadilisha mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha CP"

MSANII Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, ameepuka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa tuhuma za kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kumbadilishia mashtaka, ambapo sasa anatuhumiwa kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, Lulu ameepuka adhabu hiyo kwani hata kama atapatikana na hatia, adhabu yake ni kifungo cha maisha au kuachiwa huru.
Hii inatokana na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu ya kosa la kuua bila kukusudia, ambapo anayepatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru.
Hata hivyo, baadhi ya wanasheria waliliambia gazeti hili kwamba uzoefu wa adhabu nyingi za kuua pasipo kukusudia zilizowahi kutolewa nchini, ni kati ya miaka 15 na wengine waliachiwa huru.
Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Aprili 11, mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za kumuua Kanumba Aprili 7, 2012.
Alikuwa akidaiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), shtaka ambalo mshtakiwa anayepatikana na hatia adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.
Hata hivyo, jana upande wa mashtaka ulieleza mahakamani kuwa kwa sasa imebadilisha mashtaka kutoka kuua kwa kukusudia na kuwa kuua bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha CP.
Mshtakiwa huyo alitarajiwa kusomewa mashtaka hayo mapya jana pamoja na maelezo yote ya kesi, ambapo angesomewa ushahidi wa mashahidi wote pamoja na vielelezo muhimu katika kesi hiyo.
Hata hivyo, hatua hiyo ilikwama kutokana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka anayeiendesha kesi hiyo kutokuwapo mahakamani na badala yake aliwakilishwa na Wakili wa Serikali, Ofmedy Mtenga.
“Upelelezi wa shauri lako umeshakamilika na tungeweza kukusomea comital (maelezo ya kesi) leo, lakini kwa kuwa waendesha mashtaka hawapo basi tunaliahirisha mpaka tarehe nyingine.”, alisema Hakimu Mkazi Agustina Mmbando, anayesikiliza kesi hiyo katika hatua hiyo ya awali.
Taarifa hizo za kukamilika kwa ushahidi wa kesi hiyo zilipokewa kwa furaha na shangwe na msanii huyo, kiasi kwamba alishindwa kujizuia kuonyesha furaha yake.
Wakili wake Peter Kibatala aliiomba mahakama itoe ahirisho fupi hadi Ijumaa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa mashtaka haya mapya pamoja na maelezo ya awali.
Hakimu Mmbando alikubaliana na ombi hilo la Wakili Kibatala na akaahirisha kesi hiyo hadi Ijumaa.

CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI CHAMEGUKA MKOANI MANYARA

 
"Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Godbess Lema akipeana mkono na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi (Bara) Lawrence Surumbu Tara na Diwani wa kata ya Bashnet Wilayani Babati Mkoani Manyara  ambaye jana  alitangaza kujivua udiwani na vyeo vyote alivyokuwa navyo NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema mjini Babati jana" 

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Lawrence Tara, amejivua uanachama wa chama hicho na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Tara ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Bashnet, wilayani Babati,  Mkoa wa Manyara tangu mwaka 2000, alitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jana, baada ya kupokewa Chadema na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Godbless Lema.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na kiongozi mwingine wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini, Ally Bananga.
Tara alitoa sababu mbili zilizomfanya aihame NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chadema; upendeleo na dhuluma kwa watumishi wa chama hicho.
Alidai kwamba baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi wanaonyesha upendeleo wa wazi kwa kigezo cha urafiki kama kifanyavyo chama tawala, CCM.
Alisema yeye ni mmoja wa waathirika wa mfumo huo mbovu ndani ya NCCR- Mageuzi, baada ya chama hicho kumtelekeza katika kudai haki yake ya ubunge aliyodai kwamba iliporwa na CCM.
“Tunahitaji chama cha siasa kilicho makini na ambacho Watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja bila kutengana na kwa maoni yangu NCCR-Mageuzi siyo chama cha aina hiyo,” alisema Tara.
Akifafanua madai ya kudhulumiwa na CCM, Tara alidai kwamba alishinda ubunge wa Jimbo la Babati Vijijini, lakini akadhulumiwa.
Alisema katika mazingira hayo amebakiwa na chaguo mojawapo kati ya kubaki ndani ya chama kisichokerwa na hali hiyo na ambacho baadhi ya viongozi wake wanaendeleza upendeleo wa urafiki na undugu.
“Nikaona bora kujitenga na kuachana na chama chenye viongozi wa aina hiyo na kutafuta chama imara ambacho hakina simile na mambo kama hayo. Pia chenye kupigania haki, ukweli na ambacho kimepania utawala bora na ustawi wa Watanzania,” alisema.
“Ninaamini Chadema ni chama makini kilichopania kutokomeza dhuluma, uovu na ufisadi wa kidola na kuleta ustawi wa Tanzania,” alisema na kuwaomba wakazi wa Bashnet, Manyara na
Watanzania kumuunga mkono.
Akizungumza katika mkutano huo, Lema alimpongeza Tara na kusema chama hicho sasa kimeongezewa nguvu.
“Huyu ni sawa na Leonel Messi (mchezaji soka mahiri wa klabu ya Barcelona na Argentina). Sasa huwezi kumleta achezee AFC ya Arusha na Babati Stars halafu mpate mafanikio kutokana na mfumo uliopo, huyu anatakiwa awe Manchester United au timu nyingine kubwa,” alisema Lema.
Alisema viongozi wa chama chake badala ya kumpa ushirikiano ili aweze kushinda ubunge, Mwenyekiti wake alikubali kupewa ubunge wa kuteuliwa na Rais na hivyo Tara kuachwa mwenyewe.
“Uso umeumbwa na haya kuna vitu ukishakula huwezi kupinga. Hivyo jambo bora ni kuondoka huko na kwa hili nampongeza Tara kwa kuacha vyeo vyote ikiwemo posho za vikao vya udiwani na posho ya kila mwezi,” alisema Lema.
Alisema Tara anatarajiwa kupewa kadi ya chama hicho na Mwenyekiti wa Chadema,  Freeman Mbowe au Katibu Mkuu wake, Dk Wilbroad Slaa kwa kuwa yeye hawezi kufanya hivyo kutokana na nafasi kubwa aliyokuwa nayo mwanachama huyo mpya.

KAMATI KUU YA CHADEMA IMEADHIMIA MAKUBWA, YASOME HAPA

 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
“Kama CCM wakitumia polisi sisi tutapambana kwa njia nyingine ambayo sio vurugu wala kugombana na vyombo vya dola” alisema Mbowe".
0
Share
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema mwaka 2013 utakuwa mwaka wa chama hicho kutumia nguvu ya umma, itakayolenga kuishinikiza Serikali kuyafanyia kazi mambo ya msingi ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele tangu mwaka 2010.
Amesema kutokana na hali hiyo kuanzia Januari mwakani hakuna kulala wala mtu kupumua, kwamba chama hicho kitafanya harakati za kisiasa za aina yake ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho Operesheni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).
Akisoma maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutaka kwa siku mbili Dar es Salaam jana, Mbowe alisema tangu 2010 wamekuwa wakiitaka Serikali kutekeleza masuala mbambali lakini imekuwa haifanyi hivyo.



“Kama CCM wakitumia polisi sisi tutapambana kwa njia nyingine ambayo sio vurugu wala kugombana na vyombo vya dola” alisema Mbowe.

Alifafanua, “Septemba 9, mwaka huu tulifanya kikao cha Kamati Kuu baada ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Channel Ten, Daudi Mwangosi na kumwandikia barua Rais Jakaya Kikwete tukimtaka aunde tume huru ya kimahakama ya uchunguzi wa jambo hili, ila mpaka leo kimya.”

Mbowe ambaye alikuwa ameambatana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema, “Pia nimewahi kukutana na Rais Kikwete na kumsisitiza suala hili, lakini mpaka leo hii umepita zaidi ya mwezi mmoja hakuna jibu lolote.”
Alisema kwa muda wa miezi mitatu chama hicho kilisitisha mikutano yake ya M4C iliyokuwa ikifanyika mikoa mbalimbali nchini, ili kusubiri hatua zitakazochukuliwa na Rais Kikwete baada ya kumwandikia barua hiyo, ambayo pamoja na mambo mengine ilitaka kuchukuliwa hatua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, maofisa wa juu wa Jeshi la polisi pamoja na Makamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro na Iringa.

Alisema katika kikao hicho mambo yaliyojadiliwa na ambayo watakayowasilisha bungeni ni pamoja na kutofanyika kwa chaguzi za marudio katika kata 13 nchini, licha ya kuwa umeshapita zaidi ya mwaka mmoja.

“Katika hili inaonekana wazi kuwa CCM ina hofu ya kushindwa, zipo kata 13 nchini ambazo zipo wazi kwa zaidi ya mwaka sasa na uchaguzi haujafanyika, hii ni kinyume na sheria za uchaguzi zinazoeleza kuwa uchaguzi unatakiwa kufanyika ndani ya siku 90 baada jimbo au kata kutokuwa na mwakilishi” alisema Mbowe.

Alisema jambo jingine lililojadiliwa ni kuboreshwa kwa daftari la kudumu la wapiga kura ili kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura awe na haki ya kufanya hivyo.

“Jambo jingine ni Katiba, kamati kuu imetoa mapendekezo yake kwamba wakati mchakato wa kupata Katiba Mpya ukiendelea, tunataka ufanywe utaratibu wa kubadili sheria mbalimbali ikiwemo ya uchaguzi ya mwaka 1985,” alisema Mbowe.

Alifafanua zaidi, “Sheria hii ikibadilishwa italifanya taifa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi isiyofungamana na upande wowote pamoja na kuboresha daftari la kudumu la wapigakura.”

 source facebook

Haya ndiyo tuliyoadhimia kama kamati kuu ya chama, kikao kilichodumu kwa siku mbili mfululizo hapa jijini Dar es salaam,

1.KIKAO cha kamati kuu kilikuwa cha
kawaida ,hakuna jambo la dharula

2.Mchakato wa katiba mpya usiathiri
mabadiliko ya sheria nyingine kama
mabadiliko ya sheria ya uchaguzi

3.Mwaka 2013,ni mwaka wa nguvu ya
umma,hakuna kubembelazana na
serikali rais kikwete hajajibu madai ya
yetu kwa hiyo tutamshinikiza.

4.sehemu ambazo CCM wanaogopa kuitisha
uchaguzi,tutawalazimishwa kuitisha
uchaguzi kata za arusha
mjini,sengerema,nk.ziko 15

5.Uongozi wa KARATU wa CHADEMA
Tumeusimamishwa kwa muda mpaka chama
kitakapokamilisha uchunguzi wake
huko wanasheria Marando na Prof Safari
watachunguza kashfa za mtu mmojammoja
huko karatu, kumekuwa na kashfa kwenye
miradi ya maji na ardhi.

6.Hatua za kisheria kufuatia matukio ya
uchaguzi wa ilemela mwanza,baada ya
madiwani 2 kufukuzwa uanachama
zitaendelee kuchukuliwa,pia hatua za kisiasa
zianzishwe kudai uwajibikaji wa
halmashauri ya jiji la mwanza ili haki
itendeke.

7.kamati kuu imetambua kutapatapa kwa
CCM juu ya sera zake za katiba mpya,elimu
bure na bei ndogo za vifaa vya ujenzi CCM
haiaminiki,kwa hiyo CHADEMA tutaendelee
kuunganisha umma ili CCM iondolewe 2014
na 2015

8 M4C itaendelee kwa kasi mapema mwaka
2013,sekretariati itatangaza ratiba januari.

9.juu ya hoja binafsi za wabunge wetu zito na mdee(kuhusu uporaji wa
ardhi na mabilioni ya Uswis),pamoja na
hoja ya Tundu Lisu juu ya uteuzi holela wa
rais wa majaji,kamati kuu imependekeza
maazimio ya bunge yafuatwe na baadaye
kidogo kama hairidhiki kamati kuu
itaelekeza nini kifanyike kwa hatua za ziada

10.Kamati kuu imesikitika kuwa rais
amepuuza barua ya yetu juu ya
kuunda tume ya kimahakama kuhusu
mauwaji mbalimbali nchini.hivyo M4C
itatumika mwaka 2013 kumshinikiza rais
kujibu barua hiyo na kutekeleza yale barua
inaelekeza yafanyike
Kamati kuu imesisitiza kuwa mwaka 2013
ni mwaka wa nguvu ya umma,na hakuna
tena kubembelezana na serikali.

Sisi kama chama tunatambua mchango wenu sana, kwa pamoja tutapata mabadiliko tuyatakayo

Kiongozi wenu
Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)

Monday, December 17, 2012

UKAHABA UDOM NI AIBU KWA TAIFA LA TANZANIA

by Alex Nicholaus Thomas Mushi .


Kwa dhati ya moyo wangu nimesikitishwa sana na taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari kuhusu kujiuza kwa dada zetu wa UDOM. Wasomi ambao wana Dodoma na watanzania kwa ujumla walitegemea kujifunza kutoka kwao. Taarifa hizi zimenichochea kukaa chini na kuandika waraka huu huku nikizingatia ukweli kwamba UDOM ndipo nilikosomea masomo yangu ya shahada ya kwanza; mbali na matatizo yote yaliyonikumba katika safari hiyo ya kukamilisha shahada hiyo lakini nalazimika kusema kitu kwa faida yetu wote.

Ikumbukwa moja ya mategemeo ya jamii ya wana Dodoma kutoka kwenye chuo cha UDOM kilipo anzishwa mwaka 2007 ilikuwa ni kujionea jamii staarabu iliyoelimika na yenye kila sifa ya kuigwa, na pia jamii ya Dodoma ilitegemea watoto wao wangejionea namna wasomi hawa wanavyoishi kwa kusadifu kwa vitendo elimu, maadili na mila za nchi yao. Zaidi waliamini mambo hayo yangekuwa chachu ya kuwachochea vijana wao kuzingatia masomo ili na wao siku moja wafikie elimu hiyo ya Chuo lakini hali imekuwa tofauti kabisa. Leo jamii hii ya wana Dodoma wanashuhudia wasomi wanaoshinda mitaani wakiranda randa na nguo za kuogelea na za kulalia kana kwamba walikotoka hakuna wazazi, wanashuhudia wasomi wanaojiuza kama njugu.

Kiukweli siwezi hata siku moja kuruhusu kulea au kuipamba tabia hizo hata kama kuna sababu za msingi ambazo zinaweza zikawa zimesababisha tatizo hili kutokea. Kinachofanywa na dada zetu hawa ni kitendo ambacho kila mungwana anapaswa kukikemea kwa nguvu, na zaidi ya yote ni wajibu wetu wote kama vijana kurudia maadili yetu kama watanzania na kulaani kwa nguvu haya. Kama tutaruhusu tabia hii ikaota mizizi tutaandaa wasomi wasio waadilifu na wasio jiamini, tutandaa wasomi wenye shahada za kwenye chupi (nisamehewe kwa hiyo lugha lakini nimekosa neon linalokidhi ninachomaanisha),tutandaa wasomi walioathirika hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa, tutaandaa taifa la wavivu na wasifikiri kwa ufanisi.

Tukumbuke kuruhusu tabia hii kubobea ni kuruhusu kuporomoka kwa elimu ambayo ni msingi wa taifa lolote duniani. Na sidhani kama ni busara kuangalia umauti wa taifa letu kwa kuruhusu tabia hii kuota mizizi, kwani dhambi hiyo haitaishia chuoni tu, itaingia makazini na hapatakuwa na kazi zaidi ya uzinzi tu, baada ya hapo dhambi hii itasambaaa hadi kwa watoto na wajukuu wetu na hatimaye itakuwa ndio mfumo wetu wa maisha. Lakini mbali na yote niliyoeleza hapo juu ninayo yangu kwa serikali yangu, vijana hawa wa UDOM ni watoto wenu na wengine wameingia pale wakiwa hawana hata elimu ya kimaisha au ya kujitegemea, wengine wanakutana na kila aina ya tabia pale.

Mimi nilisha kuwa kiongozi wa mikopo UDOM-HSS kwa karibu miaka yote ya masomo yangu ya shahada ya kwanza, naelewa kiasi sababu na wakati dada zetu hawa wanapojiuza. Kipindi ambacho dada zetu hawa hujiuza huwa ni pale Bodi ya mikopo inapochelewesha mikopo ya wanafunzi, hali huwa mbaya kiasi dada zetu hawa ufika mahali wanalazimika kujidhalilisha ilimradi wapate chochote cha kujikimu. Na ukizingatia majumbani kwao hawa msaada wowote wanaoupata.

Mfano mzuri wa ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa kozi ya Uhusiano wa Kimataifa (BA IR) hawajapewa mikopo yao mpaka leo, na wanatakiwa kula, kunywa, kuwasiliana na kununua vitini vya masomo ili hali familia walizotoka ni masikini wa kutupwa. Haya yote ni mazingira hatarishi kwa dada zetu hawa. Serikali kama mzazi nakuomba mliangalie kwa umakini sana suala hili ili tuwaepushie wale wanajihusisha na tabia hii ya kuuza miili yao kutokana na kuishiwa au kukosa fedha za kujikimu Muda mwingine unaweza kusema serikali inafanya makusudi kuwacheleweshea mikopo yao wa sababu wanaonufaika sana na tabia hiyo ya dada zetu kujiuza ni wabunge wanapokuja kwenye vikao vyao vya bunge.

Kujiuza kwa dada zetu hawa ni dhahiri ni matokeo ya mambo kadhaa ambayo serikali haina budi kuyafuatilia kwa kina na hatimaye kutatua kwa ustawi wa tafa letu la Tanzania. Hatupaswi kufurahia tabia hii hata kidogo kwan kufanya hivyo kunaweza liathiri taifa letu kwa ujumla wake siku za usoni.

……………“ukiona panafuka moshi ujue kuna moto”…………

MTOTO KUMKOSOA BABA HARDHARANI INA MAANA GANI?WATENDAJI WA SERIKALI WAMEWEKWA NA CCM, HIVYO KUSHIDWA KWAO NDIO KUSHIDWA KWA CCM





Viongozi wa CCM mkoa Njombe wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo wa kwanza kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika wa bunge Anne Makinda wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike




Deo Filikunjombe miongoni mwa wananchi









Msafara wa pikipiki kwenye mapokezi ya Mangula Njombe

Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog







Habari na Francis Godwin


MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara Philip Mangula.


Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.


" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .


Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.


Kwa Upande wake Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.


" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.


Aidha amehimiza nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.


Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo...

Tuesday, December 11, 2012

KUMEKUCHA CCM NA CHADEMA VITANI TENA


“Lengo la kutoa mafunzo kwa wenyeviti na makatibu wa ni kuwajengea uwezo wa uwajibikaji, kudai haki zao ili kuleta hamasa kwa Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa mabadiliko,” anasema Kigaila"

KUMALIZIKA kwa chaguzi za ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM kumeamsha joto la kisiasa nchini.
CCM na Chadema ndio hasa vyama vinavyoonekana kutolala. Kila kimoja kimeanzisha mbinu mpya ya kujijenga na kujiongezea wafuasi wanaokiunga mkono.
Nia ya vyama hivi ni moja, kujiongezea mtaji wa kukivusha katika uchaguzi mkuu wa 2015 na kushika dola.
Wakati CCM ‘mpya’ ikitajwa kuanza harakati za kupita mikoani na kutangaza mikakati ya kurejesha imani yake kwa wananchi, Chadema imeingia kambini kwa mbinu mpya za mashambulizi, hasa ngazi ya vijijini ili kuikaba koo CCM.
Safu mpya ya CCM
Katika kile walichokiita kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho, viongozi wa Sekretarieti wamefanya ziara ya kutathmini utekelezwaji wa ahadi zake kama zilivyoelekezwa katika ilani yake ya uchaguzi.
Wakiongozwa na Katibu wake, Abdulrahman Kinana, Makamu mwenyekiti, Philip Mangula wameanza mkakati huo kwa nia ya kuwaeleza wananchi kile kilichofanywa na Serikali yao inayoongoza.
Katika hatua ya kwanza ziara ilianzia Mtwara, ikihusisha mikoa minne, mingine ikiwa ni  Rukwa, Geita, kumalizia Arusha.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, anasema lengo la ziara hiyo katika maeneo hayo yenye fursa nyingi za maendeleo ni kuhakikisha wananchi wanapata majibu ya jinsi utekelezwaji wa ahadi za chama hicho tawala ulivyofanyika.
Anasema ziara hiyo inawahusisha mawaziri wa Serikali ambao wanatoa ufafanuzi wa masuala kadhaa, yakiwemo utekelezaji wa ahadi zikiwemo zilizotolewa mwaka 2010 wakati wa kampeni.
Harakati hizo za CCM zinakuja muda mfupi baada ya kupata viongozi wapya, ambao kwa nyakati tofauti, wameahidi kupambana na rushwa iliyokithiri nchini na ndani ya chama hicho.
Wakiwa mkoani Mtwara, kete ya viongozi hao ilichezwa kwenye matatizo ya wakulima wa korosho, zao ambalo ndilo tegemeo kwa wananchi wa mkoa huo. Pia waligusia bandari na miundombinu mingine ambapo waliahidi kuyafanyia kazi maeneo yote yaliyoonekana kusababisha kero kwa wananchi hao.
Mtindo huo wa CCM kutembea na mawaziri wa Serikali unaelezwa kuwa na manufaa kwani hutakiwa kutolea ufafanuzi utekelezaji uliofanywa na chama hicho, na pale ambapo kuna tatizo, hukumbushwa ili kuhakikisha kasoro hizo zinaondolewa haraka.
Katika baadhi ya maeneo katika mkoa huo viongozi hao wapya wamembana na changamoto ikiwemo kuzomewa kwa mawaziri, ambapo Kinana na Nape waliweza kutuliza hali hiyo kwa kukubali kasoro zilizoainishwa na wananchi na kuahidi kuzirekebisha.
Mawaziri waliokumbana na zomea zomea mni Hawa Ghasia (Serikali za Mitaa na tawala za Mikoa), Naibu wake, Aggrey Mwanri na Waziri Kilimo na Uahirika, Christopher Chiza.
Wananchi walieza kukerwa na hatua ya Serikali kuipeleka gesi inayochimbwa Dar es Salaam huku wananchi wa Mtwara wakikosa kunufaika na rasilimali hiyo.

MATAJIRI WA TANZANIA WANAOTAMBULIKA AFRIKA NZIMA



"Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni)".

WAFANYABIASHARA watano, Said Bakhressa Gulam Dewji, Rostam Aziz, Reginald Mengi na Ali Mufuruki, wametajwa na Jarida la Ventures Africa linalozungumzia masuala mbalimbali ya uchumi wa Afrika kuwa ndiyo matajiri zaidi nchini.

Anayeongoza katika orodha hiyo ni Bakhressa anayemiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 milioni sawa na Sh992 bilioni (Dola moja Sh1,600) akifuatiwa na Dewji ambaye utajiri wake ni Dola 560 milioni (Sh896 bilioni). Wengine na kiasi cha mali na fedha wanazomiliki kwenye mabano ni Rostam (Sh672 bilioni- Dola 420 milioni) Mengi (Sh448bilioni- Dola 280 milioni) na Mufuruki (Sh176 bilioni - Dola 110 milioni).

Matajiri hao wamepatikana baada ya kuangalia nafasi zao kifedha, ufanisi wa kampuni zao katika soko la hisa, mfumo wa wanahisa katika soko la hisa na mtiririko mzima wa fedha katika akaunti zao kwenye benki mbalimbali.

Jarida hilo linalotoka mara moja kwa mwezi kutoka Afrika Magharibi, limesema matajiri hao wa Tanzania ni kati ya Waafrika wenye utajiri ambao ni mabilionea 4,800 kutoka mataifa 17.
Asilimia kubwa ya watu 1,523 ni mamilionea na wamo katika ripoti ya watu matajiri Afrika.
Jarida hilo linataja jinsi matajiri hao walivyokuwa wajasiriamali wadogo kabla ya kuibuka na kuwa mabilionea.

Said Salim Bakhresa
Jarida hilo limesema chanzo cha utajiri wa Bakhressa ni mapato yanayotokanana uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viwanda vyake.

Mfanyabiashara huyo aliacha shule akiwa na umri wa miaka 14 na kuanzisha biashara zake. Alianza kuuza urojo Zanzibar na baadaye alifungua mgahawa miaka ya 1970.

Mgahawa huo ulipanuka na alitumia faida yake kufungua mashine ya kusaga pamoja kiwanda za usindikaji vyakula, huku akiunda Kundi la Makampuni ya Bakhressa.
Aliendelea kusindika vyakula mbalimbali na kutengeneza unga wa mahindi na baadaye kuanzisha kiwanda cha kuoka mikate na baadaye kutengeneza chocolate, ice cream, vinywaji na makasha ya kufungashia bidhaa. Kutokana na shughuli hizo, kwa mwaka huingiza Sh800 milioni.
Kampuni zake kwa sasa zinafanya biashara mbalimbail katika nchi za Tanzania, Uganda, Malawi, Rwanda na Msumbiji na ameajiri zaidi ya wafanyakazi 2,000.

Gulam Dewji
Mfanyabiashara huyo ana utajiri unaokadiriwa kufikia Dola 560 milioni kutokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Ni mmoja wa mataikuni wa Tanzania tangu miaka ya 1970 na kazi yake kubwa ilikuwa kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje.

Alianza na kampuni ndogo aliyoiita Mohammed Enterprises Tanzania, ambayo kwa sasa ni kati ya kampuni kubwa Afrika Mashariki na Kati.
Miongoni mwa mali zake ni Kiwanda cha 21st Century Textiles, moja ya viwanda vikubwa vya nguo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kampuni yake ina viwanda vinne, Tanzania na Msumbiji huku ikizalisha Dola 100 milioni kwa mwaka. Pia kampuni hiyo husindika juisi kwa matunda ya Tanzania, mafuta ya kula, sabuni na tishu.

Kampuni hiyo pia inamiliki kampuni ya bima, makontena, kampuni za kuuza mafuta ya petroli na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania nzima.
Hata hivyo, Gulam alisema jana kwamba takwimu zilizotolewa zimekosewa. Alisema kwa sasa yuko nje ya Dar es Salaam na atatoa taarifa sahihi atakaporejea.
“Kuna baadhi ya tarakimu zimekosewa niko Morogoro kuangalia biashara zangu nikirudi Dar es Salaam nitazungumza,” alisema Dewji.

Rostam Aziz
Ameelezwa kuwa utajiri wake umetokana na kuendesha shughuli zake mbalimbali ikiwamo kampuni za mawasiliano ya simu, madini na biashara za usafiri wa meli.
Mwanasiasa huyo mwenye asili ya Asia, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa Igunga mwaka 1993 na alishinda kwa vipindi viwili.

Aliachana na ulingo wa siasa mwaka 2011. Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya Vodacom ambayo ina wateja zaidi ya milioni nane.

Ameelezwa pia kuwa anamiliki Kampuni ya Ujenzi ya Caspian na sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya Hutchison Whampoa ya Hong Kong.
Akizungumzia utafiti huo, alisema: “Umefanyika kwa umakini isipokuwa tu kwa upande wangu wanasemas ninamiliki asilimia 19 ya Kampuni ya Vodacom kitu ambacho si sawa kwani ninamiliki asilimia 35.”

Reginald Mengi
Mengi anakimiliki kampuni mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, viwanda vinavyozalisha vinywaji baridi vya Coca-Cola na ana mgodi wa dhahabu.

Mfanyabiashara huyo baada ya kufanya kazi ya uhasibu ambayo ndiyo taaluma yake, alifanya biashara ya kutengeneza kalamu za wino zilizopata soko kubwa Afrika Mashariki.
Leo hii, IPP Group ambayo Mengi ni mwenyekiti wake, inamiliki magazeti mbalimbali ikiwemo Financial Times, ThisDay na The Guardian, televisheni mbili kubwa Afrika Mashariki na Kati EATV na ITV na vituo vya redio. Anamiliki Kampuni za IPP Gold na Handeni Gold.

Ali Mufuruki
Utajiri wake unatokana na biashara mbalimbali za rejareja na za ushirika.
Ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Tanzania Infotech Investment Group.
Kampuni hiyo inajumuisha Watanzania na Waganda kwa ajili ya kuuza bidhaa za Afrika Kusini za Woolworth.

Infotech hufanya kazi ya uendelezaji makazi na ukodishaji, matangazo na shughuli za mawasiliano.

Thursday, November 15, 2012

POLISI WASIINGILIWE NA CHAMA DOLA KATIKA UTENDAJI KAZI ZAO


RAIS Jakaya Kikwete juzi aliwaonya wanachama wa CCM akiwataka waache kubweteka kwa kuwategemea askari polisi katika masuala ya kisiasa, kwani kufanya hivyo watakuwa wanajidanganya.

Kikwete alitoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM uliofanyika kwa siku tatu mfululizo katika Ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.

Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema kitendo cha wanaCCM kuishi katika siasa kwa kutegemea Jeshi la Polisi hakipaswi kukubaliwa kwani kimepitwa na wakati.

“Mnaishia kulalamika tu kila siku, eti wanatukana halafu mnaishia kusema ndiyo kawaida yao…au utasikia mtu anasema eti Serikali haipo! Kazi ya Serikali siyo hiyo, hiyo ni kazi ya kisiasa maana hao ndio wenzenu,”alisema Kikwete na kuongeza:

“Sasa mnataka wakisema Serikali ya CCM haijafanya kitu polisi wawafuate, au wakisema Kikwete nchi imemshinda, polisi wakawakamate? Kama wakisema hatujafanya kitu ni kazi yenu kusema kwamba tumefanya kitu, waonyesheni barabara, shule na mambo mengine.”

Licha ya kwamba hakuwataja moja kwa moja, kauli za Rais Kikwete zilikuwa zikielekezwa kwa uogozi wa Chadema ambao kimsingi kinaonekana kuwaumiza vichwa CCM.

Huku akirudia mara kadhaa maneno hayo alisema, “Nataka mfahamu ndugu zangu kuwa tukiishi kwa kutegemea Jeshi la Polisi kufanikisha mambo yetu, tutakwisha na tutakwisha kweli.”

Kikwete aliwatuhumu viongozi wa upinzani kwamba ni waongo na kwamba wakati mwingine wamekuwa wakizusha mambo ambayo hayapo, huku wakijifanya kuwa na ushahidi wa kimaandishi.

Alimtaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kwamba kuna wakati aliwahi kuzusha kwamba yeye (Kikwete), na makada kadhaa wa chama hicho wakiwamo Rostam Aziz walikuwa jijini Mwanza usiku, wakati si kweli kwani siku waliyodai alikuwa Nachingwea mkoani Lindi kwenye mikutano ya kampeni za urais.

Katika mazingira hayo, aliwataka wanaCCM kila mahali kujibu hoja za wapinzani kwa kauli na vitendo na wasikubali kuburutwa kwani uongo ukiachwa kwa muda mrefu unageuka kuwa ni ukweli.

Aliwaeleza kuwa ukimya wao katika kujibu hoja za wapinzani ni sumu kwao na kwamba wenzao wameanza kuaminika zaidi yao licha ya kuwa CCM ndio wenye majibu yote.

“Mkijibu kwa hoja wanatulia, sio Polisi. Nakumbuka Mwigulu aliwajibu pale bungeni kuhusu bajeti yao mbadala. Walipoitoa kijana wetu akasimama na kupiga msumari kweli wakachanganyikiwa sasa hizo ndio kazi zinazotakiwa jamani,” alisisitiza Kikwete.

Mbali na hilo aliwaonya kuacha malumbano ya mara kwa mara akieleza kuwa hali hiyo inakibomoa chama.

Alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa wakitumia muda mwingi kukosoana wao kwa wao, huku wakitoa nafasi kwa adui zao.

Mwenyekiti huyo alisema hakuna mtu kutoka nje ya chama anayeweza kukidhoofisha CCM kwa hoja isipokuwa chama hicho kinaumizwa na wanachama wake ambao wamekuwa wakilumbana bila sababu.

Akizungumzia suala la wagombea urais aliwataka wanachama wenye nia kufuata taratibu zote za chama pamoja na kuvumiliana ili ifikapo Mei 2015, mkutano utafanya uamuzi wa nani anasimama kupeperusha bendera ya chama hicho.

“Kwa wale mnaotaka kugombea, andikeni hiyo tarehe tutakuja hapa kuteua, lakini msituvuruge lazima mfuate utaratibu. Utaratibu huo utatangazwa, maana mkianza kupita huko na huko ndiko tunakopata matatizo,” alisema Kikwete.

Kikwete juzi alichaguliwa kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa CCM baada ya kupata asilimia 99.92 ya kura zilizopigwa, huku kura mbili zikimkataa. Kadhalika mkutano huo uliwachagua Dk Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania – Zanzibar) na Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti (Tanzania Bara).

VURUGU ZA KIKUNDI CHA UAMSHO Z'BAR, KARUME ATUSHWA ZIGO


RAIS Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Aman Karume juzi usiku alizomewa na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku wakimwita kwamba ni mmoja wa wanakundi la Uamsho.

Uamsho ni kundi ambalo katika siku za hivi karibuni limekuwa likihusishwa na vurugu ambazo zimekuwa zikitokea Tanzania Visiwani, ambazo zimesababisha watu kadhaa kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Karume alikutana na zahama hiyo wakati akitoa hotuba ya kuwaaga wanaCCM baada ya kumaliza ngwe yake ya utumishi ndani ya chama hicho akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Dalili za Rais Karume kuzomewa zilianza baada ya baadhi ya wajumbe kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi kuanza kutaja neno ‘Uamsho’ kila alipokuwa akizungumzia matatizo yaliyopo Zanzibar.

Hali ilikuwa mbaya zaidi pale alipokuwa akizungumzia vurugu za kidini ambazo ziliikumba Zanzibar hivi karibuni zikiongozwa na kikundi cha Uamsho.

Karume alisema kuwa kikundi cha Uamsho kina haki ya kutoa maoni yake kuhusu muungano, lakini hakipaswi kufanya vurugu kama ambavyo kimekuwa kikifanya.

Wakati akiendelea kuzungumzia suala hilo, kelele nyingi zilienea katoka kwa wajumbe wa mikoa ya Zanzibar ambao walikuwa wakipaza sauti, “ Uamsho huyo….Uamsho huyo… Uamsho huyo….”

Hali hiyo ilimfanya wakati mwingine kukatiza hotuba yake na kulazimisha kuwatuliza watu hao kwa kusema “CCM oyeee….CCM…..oyeee…Mapinduziii….”
Hata hivyo, baada ya kelele hizo kuendelea Karume alionekana kuhamaki na kuwaambia wajumbe hao kwamba amechoka kusikia akiitwa jina hilo la Uamsho.

“Nimechoka kusikia naitwa jina hilo ati,” alisema Karume na kuongeza:
“Hivi wengine wana vichwa vya samaki kwa nini mnapiga kelele wakati mimi ninapozungumza, si mniache nizungumze mambo ambayo ni muhimu zaidi kwa masilahi ya chama chetu.”

Hata hivyo, licha ya kutafuta namna ya kuwatuliza wanachama hao kwa maneno mengi na historia ya maisha yake tangu alipojiunga na Chama cha ASP mwaka 1970, bado hakukuwa na utulivu na safari hii kelele zilianza kwa pande zote za wajumbe.

Kwa upande wa wajumbe wa Bara, baadhi yao walikuwa wakipiga kelele za kumtaka kumaliza hotuba yake ambayo walisema ilishachukua muda mrefu huku wakisema hakuna cha ajabu alichokuwa akizungumza.

Mara baada ya kumaliza hotuba yake, Karume alihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Redio Deutche Welle ya Ujerumani, na alisisitiza kuwa Uamsho wana haki ya kutoa maoni yao kuhusu muungano, lakini hawaruhusiwi kuvunja sheria.

Aliwataka wanachama wa kikundi hicho kujenga hoja, kwani alisema wengine wana hoja za msingi, lakini wasitumie vitisho.

Karume alistaafu uongozi wa CCM katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Tanzania Visiwani) na nafasi yake ilichukuliwa na Rais wa sasa wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein.

Tofauti na utamaduni ambao CCM kimeujenga kwa viongozi wake wakuu, Karume aliendelea kuwa makamu mwenyekiti hata baada ya kustaafu urais wa Zanzibar, hivyo kumlazimisha Dk Shein kusubiri hadi juzi kuchukua nafasi hiyo.

Kwa kawaida, viongozi wa ngazi ya Rais wa Muungano na Zanzibar, baada ya kuondoka katika nafasi zao za uongozi wa nchi, pia huachia madaraka ndani ya chama na kumwachia Rais mpya.

Saturday, November 10, 2012

Serikali kitanzini hoja binafsi ya Zitto, watanzania wafuatia kwa jicho la tatu


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (kushoto) akimwonyesha Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo baadhi ya ushaidi aliokuwa nao wa hoja yake binafsi inayoitaka serikali kuchukua hatua dhidi ya watanzania walioficha fedha haramu nje ya nchi, mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi 

 NGUVU za Serikali za kutaka kuifuta hoja binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto ya kuitaka Serikali kuchukua hatua dhidi ya Watanzania walioficha fedha haramu nje ya nchi, jana zilishindwa baada ya wabunge kadhaa kumgomea Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema kufanya hivyo.
Dalili za Serikali kutaka kuzima hoja hiyo zilianza baada ya Jaji Werema kusimama na kutoa mapendekezo ya kufuta vipengele muhimu.
Hatua hiyo ilizusha mvutano mkali, huku baadhi ya wabunge wakisema Serikali inataka kuifuta hoja hiyo muhimu kwa mustakabali wa taifa.

Mapendekezo ya Werema
Katika mapendekezo yake, Jaji Werema alipendekeza kufanyika kwa marekebisho kwenye kipengele katika hoja hiyo ya Zitto ambacho kiliitaka Serikali iwasiliane na Benki ya Dunia ili kupitia Kitengo cha Assets Recovery Unit irejeshe nchini mabilioni ya fedha yanayomilikiwa na Watanzania katika benki za Uswisi na maeneo mengine yote ambayo hufichwa fedha ili kukwepa kodi.
Jaji Werema alitaka pendekezo hilo liondolewe kwa maelezo kuwa mamlaka za uchunguzi ikiwamo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa zinalifanyia kazi suala hilo.
Eneo jingine katika hoja ya Zitto ambalo Jaji Werema alipendekeza lifanyiwe marekebisho ni kuwapiga marufuku viongozi wa Serikali na watoto wao pamoja na Watanzania wengine kufungua akaunti nje akisema suala hilo litashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ya fedha za kigeni.
Pia alitaka pendekezo lililomo katika hoja ya Zitto cha kutaja akaunti za watu wenye fedha benki za nje na kuzichapisha katika vyombo vya habari lifanyiwe marekebisho kwa kuondolewa.
Alisema suala hilo ni gumu na linakwenda kinyume na sheria za benki zinazotaka kutunza siri za wateja wao.
Kuhusu pendekezo la kuitaka Serikali katika Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/13 kuanzisha kodi maalumu ‘Financial Transaction Tax’ ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction’ ili kuweza kuwa na rekodi za uhakika fedha za ndani na zinazotoka nje ya nchi, Werema alitaka lifutwe akisema hiyo inahitaji utafiti wa kutosha.
Alisema ofisi yake imechukua siku nyingi kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ikiwemo kwenda Uswisi na kwingineko na kwamba itashirikiana na vyombo binafsi vya uchunguzi kufanya kazi hiyo.
Pendekezo jingine lililopingwa na Jaji Werema lilikuwa ni kuitaka Serikali kuwabana Watanzania wenye fedha nje ya nchi waeleze walikozipata akisema kazi hiyo inaweza kufanywa na Takukuru.

Wabunge wamshukia
Baada ya kutoa mapendekezo hayo, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alisema anamshangaa Mwanasheria Mkuu kwa kufanya marekebisho ambayo yanaizima hoja ya Zitto.
Huku akinukuu vifungu vya Kanuni za Bunge, alisema Mwanasheria Mkuu anataka kuua hoja hiyo na kwamba mapendekezo yake yanakwenda kinyume na kanuni ambazo zinataka kila badiliko katika hoja liwiane na jambo linalojadiliwa.
“Hoja ya mabadiliko ya Mwanasheria Mkuu kuondoa mapendekezo hayo, kwa maoni yangu yanakinzana na Kifungu 53 (3) (4) cha Kanuni za Bunge, kinachopendekeza kuwapo kwa mabadiliko na siyo kufuta hoja.
Alisema hatua ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupendekeza mabadiliko hayo ni kufuta hoja jambo ambalo alisema ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, mtu ambaye anaweza kuiondoa hoja ni mtoa hoja na si mtu mwingine yeyote.
Alimtaka Spika kutumia busara yake kumzuia Mwanasheria Mkuu kufuta hoja hiyo muhimu kwa mustakabali wa nchi.
Baada ya maelezo hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisimama na kuunga mkono mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu, huku akielekeza ‘makombora’ kwa Lissu kuwa anachokisema kinapingana na mtoa hoja Zitto, ambaye anakubaliana na Mwanasheria Mkuu.
Hata hivyo, Zitto alisimama na kutoa ufafanuzi kuwa hakubaliani na mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu yanazima hoja yake.
Baadaye Lukuvi alisema anaunga mkono pendekezo moja katika hoja ya Zitto la Serikali kuwasilisha bungeni ripoti ya uchunguzi katika Bunge la 11 na kwamba ili kasi hiyo iende vizuri yashirikishwe pia kampuni binafsi ya uchunguzi.
Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alipinga pendekezo la kuiondoa hoja hiyo na kuunga mkono azimio kwamba Bunge liiagize Serikali kufanya uchunguzi huo na ripoti yake iwasilishwe katika Bunge la 11 na ikishindwa, Bunge liunde kamati ndogo ya kufanya kazi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), Hawa Ghasia, aliuanga mkono mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akisema vyombo vya uchunguzi viachiwe kuchunguza mabilioni ya fedha yaliyopo nje ya nchi.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), alipinga akisema mapendekezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yalikuwa na lengo la kuua hoja hiyo akisema wabunge watafanya dhambi kubwa kuiondoa hoja hiyo ya msingi.
Sendeka alitaka hoja hiyo iboreshwe kwa kumtaka Zitto awataje hadharani watu ambao wameficha fedha nje ya nchi ili Watanzania wawafahamu... “Ukiwataja hawa hoja yako itakuwa na mashiko, tusaidiane na wala siyo fedheha kuwataja.”
Alitaka kamati iundwe kuchunguza jambo hilo ili ukweli ujulikane.
Baada ya kubanwa na wabunge, ndipo Jaji Werema alisimama na kulegeza msimamo wake kwa kurejesha pendekezo la Serikali kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi vya nje pamoja na wachunguzi binafsi kufanya kazi hiyo.
Alikubali pia pendekezo la kuitaka Serikali kuja na mkakati wa kueleza nini imekifanya katika Bunge la 11.
Aliwataka wabunge wote wenye majina ya watu walioficha fedha nje ya nchi kuyapeleka Takukuru au wamkabidhi yeye.
Baada ya hapo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisimama na kusema hoja ya Zitto haikuwa mbaya na kusema Mwanasheria Mkuu pia alikuwa na nia njema.
Alisema Serikali haiwezi kumficha mhalifu akisema kama mtu ameiba atachukuliwa hatua bila ya kumwonea haya. Aliungana na Mwanasheria Mkuu kutaka Serikali iachiwe jambo hilo ilifanyie kazi.
Akihitimisha mjadala huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema hoja ya Zitto haijatupwa bali, inaingia kwenye utaratibu wa Serikali wa kuyatekeleza maazimio hayo.
Alisema Serikali itapaswa kutoa taarifa ya utekelezaji wa hoja ya Zitto katika Bunge la 11 la Aprili) mwakani na kama ikishindwa, Bunge litaunda kamati kufanyia uchunguzi maazimio hayo.

Msimamo wa Zitto
Akizungumza baada ya uamuzi huo wa Bunge, Zitto alisema ameridhishwa na hatua hiyo akiamini kwamba itafanyiwa kazi.
Alisema amefurahi pia kwa kuwa hiyo ni mara yake ya kwanza kwa hoja yake kufanyiwa kazi na Bunge.

Sunday, October 28, 2012

TAFAKARI KISHA MWAMBIE ACHUKUE HATUA

JE TANZANIA INAHITAJI VIONGOZI WA NAMNA HII KATIKA ULIMWENGU HUU WA SAYANSI NA TECHNOLOJIA?

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Augustino Mulugo wakati akitoa hotuba yake katika mkutano wa wataalam wa elimu huko Afrika Kusini. (Picha na Youtube)
Na Walusanga Ndaki
JANA mtandao huu uliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari ‘MAKOSA’ YA WAZIRI MULUGO NI YA BAHATI MBAYA AU UFAHAMU MDOGO?…
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Augustino Mulugo wakati akitoa hotuba yake katika mkutano wa wataalam wa elimu huko Afrika Kusini. (Picha na Youtube)
Na Walusanga Ndaki
JANA mtandao huu uliandika makala iliyokuwa na kichwa cha habari ‘MAKOSA’ YA WAZIRI MULUGO NI YA BAHATI MBAYA AU UFAHAMU MDOGO?
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo akiendelea kuwasilisha hotuba yake. (Picha na Youtube)
Katika makaka hiyo tulionyesha makosa yaliyokuwa ndani ya hotuba ya naibu waziri huyo wa elimu aliyoitoa katika mkutano wa wataalam wa elimu huko Afrika Kusini mwanzoni mwa mwezi huu.
Baada ya wimbi kubwa la malalamiko ya umma kuhusu hotuba yake hiyo iliyokuwa imejaa dosari nyingi, waziri huyo leo alizungumza na kituo cha Clouds FM akikiri dosari hizo japokuwa kwa kujitetea kijanja.
Katika kuonyesha kwamba umakini kwa watumishi wa umma nchini ni mdogo sana,  ni jinsi waziri huyo alivyokuwa akiisoma hotuba hiyo bila hata kushitukia chochote.
Kwanza kabisa, kwa ufahamisho, ni kwamba mfumo wa sasa wa hotuba duniani ni kwamba msemaji anaposoma hotuba yake wakati huohuo huonyeshwa na kompyuta katika kiwambo ambapo washiriki wengine wanaweza kuifuatilia pia kwa kuisoma.
Mtandao huu umeandika yote yafuatayo kwa kufuatilia matamko ya hotuba ya Mulugo ambayo yalikwenda sambamba na hotuba yake ambayo ilionekana kwa ajili ya kusomwa.
Mfano wa kosa la kizembe la Mulugo ni pale aliposema kwamba Tanzania inapakana na nchi nane.  Miongoni mwa nchi hizo nane alizozitaja ajabu ni kwamba nchi ya Burundi haikuandikwa katika hotuba yake japokuwa aliitaja toka kichwani!
Jambo jingine, ni kwamba miongoni mwa nchi hizo zinazopakana na Tanzania aliitaja nchi moja kwa jina la “Congo DRC”, hii ni kwa mujibu wa alivyotamka katika hotuba yake na jinsi ilivyokuwa imeandikwa katika hotuba hiyohiyo.
Kiuhalisia, hakuna nchi kama hiyo inayopakana na Tanzania.
Nchi inayopakana na Tanzania miongoni mwa nchi nane alizozitaja ni Congo DR au Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.  Si “Congo DRC” aliyoitaja waziri Mulugo.
Kama Mulugo hakuliona kosa lake na alikuwa bado hajaliona hadi leo wakati anaongea na Clouds FM ni kwamba kirefu cha “Congo DRC” (kama kweli nchi hiyo ipo) ni “Congo Democratic Republic of Congo”!
Waziri Mulugo alisema kwamba neno Zanzibar alilitaja kimakosa kama Zimbabwe wakati wa hotuba yake akielezea nchi zilizounda muungano wa Tanzania, kwa vile msemaji aliyekuwa amemaliza kusema kabla yake alikuwa ametoka Zimbabwe.
Hata hivyo, katika kuisoma hotuba yake iliyokuwa imeandikwa “…islands of Pemba and Zanzibar…” aliisoma kama “…islands of Zimbabwe and Pemba…”.
Angalau kama kweli ni kwa kukosea angeisoma kama “…islands of Pemba and Zimbabwe…”, lakini  kwa vile hakuwa makini, jicho na akili zake vilikimbilia neno ‘Zimbabwe’ kwanza kabla ya kuitaja Pemba ambayo ndiyo ilikuwa ianze, kama hotuba yake ilivyokuwa imeandikwa!
Hebu ona hili lifuatalo!
Katika hotuba ileile, kuna aya iliyokuwa imeandikwa ifuatavyo: “The United Republic of Tanzania is located on the east cost of Africa.”
Hapa kuna makosa mawili yaliyokuwemo katika hotuba hiyo aliyoisoma.   Kosa kubwa la kwanza hapa ni neno “cost” ambalo ni la Kiingereza, maana yake ni “gharama” (likiwa ni nomino) au “kugharimu” (kitenzi).
Hivyo, hilo ni kosa la waziwazi na la kuchekesha na kuchefua lililokuwa katika hotuba ya Mheshimiwa Mulugo!
Neno sahihi lilibidi liwe “coast” yaani “pwani”.  Kwa mujibu wa hotuba hiyo ya Mulugo ambayo huenda aliiandika yeye mwenyewe au kuandikiwa, sentensi hiyo ya “The United Republic of Tanzania is located on the east cost of Africa” ingemaanisha nini?
Ingemaanisha kwamba “Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iko mashariki mwa “gharama” (au “gharimu”) mwa Afrika!
Unaona kichekesho hicho?!  Hiyo ni hotuba ya waziri wa Tanzania aliyoiweka kwenye mkoba, akapanda ndege, akafikia hoteli ya kisasa, akala na kulala ambapo kesho yake akaenda mbele ya wasomi wenzake na kupeleka hotuba hiyo ya kusikitisha!
Siyo hivyo tu, Mulugo aliingiza maneno mengine kutoka kichwani ambayo hayakuwemo kwenye hotuba yake hiyo.  Mfano, aliingiza neno “geographically” katika sentensi hiyo kabla ya neno “located”, kitu ambacho kilionyesha wazi hakuwa anaiamini au aliipuuza hotuba yake hiyo iliyokuwa imeandikwa!
Makosa ni mengi ajabu.  La pili ni  kwamba sentensi hiyohiyo aliisoma hivi: “The United Republic of Tanzania is geographically located in east Africa.”
Kwa aliyeisoma vizuri sentensi hii atangundua kwamba ilikuwa na kasoro mbili.  Ya kwanza ni kwamba Mulugo aliongeza neno “geographically” ambalo halikuwa limeandikwa katika hotuba hiyo.  Pili, ukiisoma vizuri sentensi hiyo kuna maneno ambayo aliyaacha katika hotuba hiyo ambayo yalikuwa yameandikwa.
Makosa ni mengi, na yote ni mfano mzuri wa uzembe na kazi za kulipua zinazofanywa na watumishi wa umma karibu katika kila kona.
Cha kusikitisha zaidi ni kwamba uzembe huu wa kisomi umefanywa na mtu ambaye akiwa anazungumza na Clouds FM alijisifu kuwa ni msomi na mtu ambaye aliwahi kuwa mwalimu, lakini uhalisia umeonyesha mapungufu yake makubwa!
Waziri Mulugo ni mmoja tu ya mifano ya kusikitisha na kuudhi inayokwenda kwa jina la viongozi, watu ambao wengi wao wamekuwa ni kichocheo cha kuwakatisha tamaa wananchi wenzao kwa kuwaongezea majonzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kutokana na kukosa umakini katika kazi zao.
Pia tukio hilo la Mulugo linachochea madai lukuki kwamba uongozi wa nchi hii ni jambo la “kupeana” kirafiki na si lenye kutokana na utaalam au utendaji bora!
Kwa Mulugo, njia ya kujitoa katika aibu hii na kupunguza hasira za Watanzania ni KUACHIA NGAZI MARA MOJA!

WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA 2012 WATEMBELEA TBL

Wednesday, September 5, 2012

Dr. Dre Aongoza kwa utajili katika mziki wa Hip Hop 2012

Dr. Dre (photo: Johnny Nunez, WireImage)Six years ago Dr. Dre was walking along the beach with Interscope Records chief Jimmy Iovine, pondering whether or not he should launch his own shoe line. "[Forget] sneakers," said Iovine. "Let's sell speakers!"
It might have been the best piece of advice the rapper-producer ever received. In 2008 he teamed with Iovine and a handful of other partners to launch Beats By Dr. Dre, which now sells more than half of the country's premium headphones ($100 and up). That's music to the ears of Dr. Dre, who collected $100 million pretax when handset maker HTC paid $300 million for a 51% stake in the company last year.

With $110 million in pretax earnings, Dr. Dre is this year's Hip-Hop Cash King—despite the fact that his long-awaited album, Detox, remains on the shelf. He's not the only one on the list who banks the bulk of his bucks outside the recording studio. Diddy ranks No. 2 with $45 million, thanks mostly to a share of profits from Diageo's Ciroc vodka; Jay-Z ranks third with $38 million, pulling in more than half his annual earnings from ventures including ownership stakes in cosmetics company Carol's Daughter, the Brookyln Nets and a joint venture with battery maker Duracell. Last year, Jay-Z topped the list with $37 million.
Jay-Z and New Jersey Nets owner Lewis Katz (photo: Johnny Nunez, WireImage)"The reality of it is, you want to do something that you own," says frequent Jay-Z collaborator Timbaland, who ranks No. 20 on the list with $6 million. "You want to own what you put your heart into. That's how you make money."
Kanye West ranks fourth on the list with $35 million, fueled by his Watch the Throne album with Jay-Z and the ensuing tour, followed by Lil Wayne at $27 million. The diminutive rhymester's latest album, Tha Carter IV, sold a million copies in its first week; he also launched clothing line Trukfit and a partnership with Pepsi's Mountain Dew, the first major product endorsement in the veteran rapper's career.
Lil Wayne is joined on the Cash Kings list by labelmates Drake (No. 6) and Nicki Minaj (No. 8), who banked $20.5 million and $15.5 million, respectively, thanks to new albums, tours and product endorsements with companies like Kodak and Pepsi. Their boss, Cash Money co-founder Bryan "Birdman" Williams, ranks seventh with $20 million. Even lower down on the list, artists are getting paid considerable sums to shill products.
"We've received a lot of income based around endorsements," says former Def Jam President Kevin Liles, who now manages a host of artists including No. 18 Young Jeezy. "A lot of brands are saying, 'Hey, there's a value proposition, instead of this freewheeling spending … I have some guaranteed curators and travel agents that can help me reach the consumer in a better way.'"
Yet for a few artists, music alone is a viable path to earning millions. No. 9 Eminem sold more albums last decade than any artist in the world, and continues to cash in from his extensive back catalog and occasional tour dates, pulling in $15 million.
Ludacris rounds out the top ten with earnings of $12 million. The multihyphenate mogul's non-musical ventures include Conjure cognac, headphone line Soul, voiceovers for RadioShack and roles in movies such as Fast Five and New Year's Eve.
"We work so hard that we never get a real chance to stop and reflect on what we've done sometimes," says Ludacris. "So the FORBES list is a great representation of, 'You know what, wow, we are out here working as hard as hell!'"

To compile the Cash Kings list, which charts pretax earnings for all living artists whose work is primarily classified as hip-hop or rap, we looked at income from touring, record sales, publishing, films, merchandise sales, endorsements and other ventures. Management, agent and attorney fees are not deducted; earnings are tabulated from May 2011 to May 2012 and based on data from Pollstar, the Recording Industry Association of America and Nielsen SoundScan, and from interviews with numerous managers, lawyers, record executives and some of the artists themselves.
All in all, hip-hop's top 20 earners pulled in $415 million last year, the most since 2008's $515 million. The more recent total got a heavy boost from Dr. Dre's impressive haul, but it doesn't mean he's resting on his financial laurels. Earlier this summer, he and his partners bought back half of the 51% stake in Beats that they sold to HTC nearly a year ago—meaning that fans waiting for his new album might have to hold out a little longer.
"I understand why Dre didn't finish Detox," says Liles, with a laugh. "It's called Beats."

Sunday, July 1, 2012

FEDHA ZA MATIBABU ZAPATIKANA,MADAKTARI WAKATAA MSAADA WA SERIKALI

Ulimboka apelekwa nje kutibiwa  Send to a friend
Sunday, 01 July 2012 08:12
0digg
Wananchi wakiwa wamelizunguka gari la wagonjwa lililompeleka Dk Steven Ulimboka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nje kwa matibabu.Picha na Silvan Kiwale

Geofrey Nyang’oro
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka amesafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.Kusafirishwa kwake kunafuatia hatua ya jopo la madaktari waliokuwa wakimhudumia, kueleza mabadiliko ya hali ya afya yake, yaliyosababisha figo kushindwa kufanya kazi, hali iliyolazimu pamoja na matibabu mengine, kwenda   kusafishwa damu.

Ingawa madaktari hao wamekataa kuweka wazi nchi anayopelekwa, kuna taarifa kwamba huenda amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini.

Katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) jana makundi mbalimbali ya watu yalifurika wakiwamo wanaharakati na ndugu wa Dk Ulimboka,  waliofika kwa lengo la kumsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Watu hao waliofika hospitalini hapo kuanzia asubuhi, waliendelea kubaki  eneo hilo hadi saa 6:45 mchana msafara ulipoanza.

Dk Ulimboka alisafirishwa kwa gari la kubebea wagonjwa la kampuni ya AAR. Alipofika uwanjani, alisafirishwa kwa  ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini, akisindikizwa na watu watatu.

Usiri safari ya Dk Ulimboka

Mapema jana asubuhi, taarifa za kusafirishwa kwake zilizagaa, lakini hapakuwa na mtu wa kuthibitisha safari hiyo na namna atakavyosafiri.

Katika safari hiyo, Dk Ulimboka amesindikizwa na  Dk Pascal Lugajo, kaka yake, Dk Hobakile Ulimboka na mke wake,  Dk Judith Mzovela.

Madaktari watoa tamko

Baada ya Ulimboka kusafirishwa, madaktari walilaani kitendo cha kutekwa na kupigwa mwenzao na kuitaka Serikali itoe tamko juu ya usalama wao.

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Edwan Chitage aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo na vitisho vya kufukuzwa kazi wanataaluma hao kunakofanywa na Serikali, kumezua  hofu kwa  madaktari wote nchini.

“Tunaamini Serikali inawajibika kwa watu wake, kwa hali ilivyo sasa madaktari wapo kwenye hofu kubwa, tunataka itoe tamko juu ya usalama wa madaktari,” alisema Dk Chitage.

Akizungumzia hali ya Dk Ulimboka, alisema imekuwa ikibadilika mara kwa mara hali ambayo imesababisha kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi .

Chitage alisema kama Serikali ingekuwa na nia ya kuboresha huduma hospitalini hapo ingeweza kununua mashine ya CT Scan ambayo alisema bei yake ni sawa na Toyota ‘Shangingi’ moja.

Kwa upande wao wanaharakati wa haki za binadamu, jana walifika Uwanja wa Ndege wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti wakilaani kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka.

Dk Chitega alisema hadi kufikia jana, walikuwa wamepata fedha zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya matibabu yake. Juzi madaktari hao walisema wanahitaji Dola za Marekani 40,000 (Sh63.2 milioni) ili kumtibu mwenzao nje ya nchi.


Serikali na tiba ya Ulimboka


Wakati mgomo wa madaktari ukiingia siku ya nane leo, Serikali imesema ilikuwa tayari kugharimia matibabu ya Dk Ulimboka.

Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja jana alisema Serikali ilikuwa tayari kugharimia matibabu ya daktari huyo.

Mwamaja aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa ni haki ya mgonjwa anayepewa rufani ya kutibiwa nje, kugharimiwa na Serikali, lakini
msaada huo wa Serikali ulikataliwa na madaktari hao na kuitaka ikae mbali na matibabu ya kiongozi wao.

“Sisi tulishaanza maandalizi ya kugharimia matibabu yake, lakini madaktari wenyewe walikataa msaada wa Serikali,” alisema Mwamwaja.

Hali yazidi kuwa tete

Kutokana na mgomo huo, uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi, umewatimua zaidi ya madaktari 80 walioko kwenye mafunzo kwa vitendo.

Hadi kufikia juzi, madaktari 146 walikuwa wamefukuzwa kutokana na mgomo huo katika hospitali za Bugando na Sekou Toure mkoani Mwanza na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na ile ya Mkoa wa Dodoma.

Mbeya

Habari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya zinadai kwamba, baada ya uongozi wa hospitali hiyo kulazimika kuomba madaktari wengine kutoka hospitali za jijini Mbeya ili kuongeza nguvu, madaktari hao nao wameonekana kutoridhishwa na ombi hilo.

Habari hizo zinasema kwamba, licha ya madaktari hao kupatikana na kwenda hospitalini hapo, walisikika wakilalamika kwamba wao hawapo tayari kufanya kazi sehemu yenye mgogoro na kwamba wao hawawezi kufanywa kama chambo kwa kuhofia usalama wao.

Akizungumza kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo,  Dk Eliuter Samky alikiri kuzidiwa na kusuasua kwa utoaji huduma kwa wagonjwa ambapo alisema kuwa hadi sasa huduma zinazotolewa ni zile za dharura pekee na zile za kawaida wagonjwa wanaambiwa waende Hospitali ya Mkoa.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Dk Seif Mhina, alisema kwa sasa hali inaendelea vizuri kutokana na kujipanga vyema kukabiliana nayo, licha ya kuwa bado kuna tatizo la upungufu wa vitanda hivyo kusababisha wagonjwa kulala chini.

Tanga

Baadhi ya wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya  Bombo, wameitaka Serikali kukaa pamoja na madaktari ili kumaliza tatizo hilo.

Wamesema hali iliyofikia sasa ni mbaya hivyo ni busara pande hizo mbili kukaa meza moja kutatua mgogoro huo bila kujali nani kati yao amesababisha.

Sakina Abdallah ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi ya Gallanis, alisema amesikitishwa na baadhi ya wanasiasa wanaoshabikia kutekwa Dk  Ulimboka.

“Binafsi hali inayoendelea ya mgomo wa madaktari inanihuzunisha sana kwani tunaoumia ni sisi wananchi tunaotibiwa katika hospitali hizi,” alisema Sakina.


Godfrey Jambia ambaye ni majeruhi aliyelazwa katika hospitali hiyo, alisema Serikali inatakiwa kutatua madai ya madaktari hao ili kuwanusuru raia wasio na hatia.

                   
NCCR yaivaa Serikali

Chama cha NCCR-Mageuzi kimesema Serikali ina maswali ya kujibu kutokana na kushindwa kutatua mgomo wa madaktari nchi nzima.

Chama hicho kimesema Serikali haitakiwi kutumia nguvu ya dola kumaliza mgomo na kuitaka ifute kesi iliyofunguliwa mahakamani ili kukaa meza ya majadiliano na madaktari hao kwa kuwa raia wasio na hatia, wanapoteza maisha kwa kukosa matibabu.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu (Nec) ya chama hicho Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa chama, James Mbatia, alisema hata kama suala hilo limefika mahakamani, bado linazungumzika kwa kuwa afya za Watanzania zinawahusu wote.

“Hivi Serikali inashindwa kuliondoa jambo hilo mahakamani na kukaa meza moja na madaktari kumaliza tatizo hili..., katika hili lazima tuseme, yaani watu wanakufa tukae kimya, haiwezekani hata kidogo,” alisema Mbatia na kuongeza:

“Ubabe hauwezi kuingizwa katika uhai wa Watanzania, kama majadiliano ya awali hayakufanikiwa basi wawekwe watu makini watakaosimamia majadiliano haya, hata wabunge wanaweza kusimamia suala hili, mgomo huu hauna itikadi za vyama unawahusu wananchi wote.”


Habari Hii imeandaliwa na Fidelis Butahe, Claud Mshana, Dar, Burhani Yakub,Tanga na Godfrey Kahango, Mbeya

Sunday, June 10, 2012

NAPE ASHIDWA KUKANUSHA MADAI YA CHADEMA KTK VIWANJA VYA CHADEMA-SQUARE

Saturday, 09 June 2012 08:13
0digg
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye
Dotto Kahindi na Leon Bahati
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema chama chake hakina mpango wa kuutumia mkutano wake wa leo kwenye Viwanja vya Jangwani kujibizana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake, kitajikita zaidi katika kutoa somo kwa wajumbe wapya wa mashina na viongozi wa matawi Mkoa wa Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya Nape inatoa mtazamo tofauti na tetesi kwamba  CCM kitatumia mkutano huo kukijibu chama hicho kikuu cha upinzani ambacho nacho kilifanya mkutano kwenye viwanja hivyo hivi karibuni.
Katika mkutano huo ambao Chadema kilizindua Mpango wake wa Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) mwishoni mwa mwezi uliopita, kiliorodhesha shutuma nyingi dhidi ya Serikali ya CCM zikiwemo za kusababisha maisha magumu kwa Watanzania.

Nape alisema mkutano huo uliandaliwa na CCM Mkoa wa Dar es Salaam hata kabla ya huo wa Chadema na lengo lake ni kuwakutanisha viongozi wapya wa chama hicho tawala na viongozi wa juu wa chama na Serikali, wakiwemo mawaziri watakaofafanua shughuli zao za kiutendaji.
“Mkutano huu unalenga kuwafundisha wajumbe wa nyumba kumi na viongozi wa mashina waliochaguliwa hivi karibuni namna ya utendaji wa Serikali, kwa kuwa wao bado ni  wapya kiuongozi na wanahitaji kupewa somo,” alisema Nape.

Alipoulizwa kama mkutano huo ni moja ya hatua za kufuta nyayo za Chadema hasa baada ya kuzindua M4C, Nape alisema: “Mkutano huu tuliuandaa mapema kabla hata ya Chadema hawajafanya mkutano wao. Ila kilichochelewesha ni Mkutano wa Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM,” alisema Nape na kuongeza:

“Mkutano huu awali, ulikuwa ufanyike ndani ya ukumbi lakini kwa kuwa watu wengi walipenda kushiriki tumeamua kuufanyia Jangwani ambako wanachama na viongozi wa CCM watapata fursa ya kusikia sera za viongozi wa chama na watendaji wa Serikali.”

Aliwataja mawaziri ambao watakuwa katika mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ambaye atazungumzia masuala ya usafiri wa reli, bandari na anga na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ambaye atazungumzia masuala ya miundombinu na barabara.

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira ambaye atazungumzia hatima ya Watanzania katika masuala ya ajira na vijana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ambaye atazungumzia mipango ya wizara yake.

M4C
Mei 25 mwaka huu, Chadema kilizindua mkakati wake mpya wa ‘Movement For Change-M4C’ ukiwa na lengo la kukiandaa chama hicho kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwataka wanachama na wananchi kwa ujumla kukichangia fedha chama hicho ili kufanikisha kampeni aliyoielezea ni ya kukiondoa CCM madarakani mwaka 2015.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alisema maisha ya Watanzania si mazuri, vyakula vinaongezeka bei kutokana na Serikali ya CCM kutokuwa makini hivyo akawataka wabunge wa chama hicho kuibana kupitia Bunge lijalo la Bajeti.

Aliilaumu Serikali kwa kutotumia vizuri kodi za Watanzania kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa kuwalipa watumishi ambao nafasi zao hazina manufaa kwa wananchi.
Dk Slaa alilalamikia kitendo cha kuongeza kodi katika mafuta ya taa ili watu wasichakachue mafuta ya dizeli akisema ni mwiba kwa Watanzania.

R.I.P BOB MAKANI, TUTAUENZI MCHANGO WAKO KATIKA KUPIGANIA DEMOKRASIA NA MAENDELEO NCHINI TANZANIA


 Send to a friend
Sunday, 10 June 2012 09:38
0digg
Mzee Bob Makani
Na Mwandishi Wetu
MWASISI wa Chadema na Mwanasheria mkongwe nchini Bob Makani, amefariki dunia usiku katika hospitali ya Aga khan, jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Makani alizidiwa ghafla saa 3: 00 usiku wa kuamkia leo na kukimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako alifariki dunia saa 4.15 usiku.

“Amekuwa anaumwa muda mrefu, mara kadhaa akipelekwa hospitali na baada ya muda anaruhusiwa, lakini hii ya sasa alikua nyumbani akazidiwa ghafla wakampeleka hospitali na ilipofika saa 4.15 wakasema amefariki,” alisema Zitto.

Zitto alisema kuwa, suala la wapi utakapozikwa Makani ambaye ni Katibu Mkuu wa Kwanza na Mwenyekiti wa pili wa Chadema, litajulikana baada ya kujadiliana na familia ya marehemu.

“Suala la wapi atazikwa kama ni Shinyanga ama Dar es Salaam, litajulikana baada ya kuzungumza na familia yake, kwa sasa tunashughulika kwanza na kuhifadhi mwili wa mzee wetu,” alisema Zitto.
Zitto alisema msiba wa utakuwa nyumbani kwa marehemu eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kwa siku za hizi karibuni afya yake imekuwa ikizorota na kumfanya kuripotiwa kuanguka mara kwa mara alipokuwa akifanya shughuli zake.

Januari 17 mwaka huu katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema Regia Mtema, Makani alianguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu.

 Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake

Alikuwa Katibu Makuu wa kwanza wa Chadema kati ya mwaka 1993 hadi 1998, alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 na amegombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa mara tatu kati ya mwaka 1995 na 2000 na mwaka 2005.

Kazi ambazo amewahi kuzifanya serikalini; alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 1966 na elimu yake ana shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha Makarere nchini Uganda.

Ni mzaliwa wa Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga akitokea kwenye ukoo wa kichifu wa Makani.