MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
“Kama CCM wakitumia polisi sisi
tutapambana kwa njia nyingine ambayo sio vurugu wala kugombana na vyombo
vya dola” alisema Mbowe".
0
inShareMWENYEKITI wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema mwaka 2013
utakuwa mwaka wa chama hicho kutumia nguvu ya umma, itakayolenga
kuishinikiza Serikali kuyafanyia kazi mambo ya msingi ambayo yamekuwa
yakipigiwa kelele tangu mwaka 2010.
Amesema kutokana na hali hiyo kuanzia Januari
mwakani hakuna kulala wala mtu kupumua, kwamba chama hicho kitafanya
harakati za kisiasa za aina yake ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho
Operesheni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C).
Akisoma maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho
iliyokutaka kwa siku mbili Dar es Salaam jana, Mbowe alisema tangu 2010
wamekuwa wakiitaka Serikali kutekeleza masuala mbambali lakini imekuwa
haifanyi hivyo.
“Kama CCM wakitumia polisi sisi tutapambana
kwa njia nyingine ambayo sio vurugu wala kugombana na vyombo vya dola”
alisema Mbowe.
Alifafanua, “Septemba 9, mwaka huu tulifanya
kikao cha Kamati Kuu baada ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa
Televisheni ya Channel Ten, Daudi Mwangosi na kumwandikia barua Rais
Jakaya Kikwete tukimtaka aunde tume huru ya kimahakama ya uchunguzi wa
jambo hili, ila mpaka leo kimya.”
Mbowe ambaye alikuwa ameambatana na Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk Willbroad Slaa alisema, “Pia nimewahi kukutana
na Rais Kikwete na kumsisitiza suala hili, lakini mpaka leo hii umepita
zaidi ya mwezi mmoja hakuna jibu lolote.”
Alisema kwa muda wa miezi mitatu chama
hicho kilisitisha mikutano yake ya M4C iliyokuwa ikifanyika mikoa
mbalimbali nchini, ili kusubiri hatua zitakazochukuliwa na Rais Kikwete
baada ya kumwandikia barua hiyo, ambayo pamoja na mambo mengine ilitaka
kuchukuliwa hatua kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, maofisa wa juu
wa Jeshi la polisi pamoja na Makamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro na
Iringa.
Alisema katika kikao hicho mambo
yaliyojadiliwa na ambayo watakayowasilisha bungeni ni pamoja na
kutofanyika kwa chaguzi za marudio katika kata 13 nchini, licha ya kuwa
umeshapita zaidi ya mwaka mmoja.
“Katika hili inaonekana wazi kuwa CCM ina hofu
ya kushindwa, zipo kata 13 nchini ambazo zipo wazi kwa zaidi ya mwaka
sasa na uchaguzi haujafanyika, hii ni kinyume na sheria za uchaguzi
zinazoeleza kuwa uchaguzi unatakiwa kufanyika ndani ya siku 90 baada
jimbo au kata kutokuwa na mwakilishi” alisema Mbowe.
Alisema jambo jingine lililojadiliwa ni
kuboreshwa kwa daftari la kudumu la wapiga kura ili kila mwananchi
mwenye sifa za kupiga kura awe na haki ya kufanya hivyo.
“Jambo jingine ni Katiba, kamati kuu imetoa
mapendekezo yake kwamba wakati mchakato wa kupata Katiba Mpya
ukiendelea, tunataka ufanywe utaratibu wa kubadili sheria mbalimbali
ikiwemo ya uchaguzi ya mwaka 1985,” alisema Mbowe.
Alifafanua zaidi, “Sheria hii ikibadilishwa
italifanya taifa kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi isiyofungamana na upande
wowote pamoja na kuboresha daftari la kudumu la wapigakura.”
source facebook
Haya ndiyo tuliyoadhimia kama kamati kuu ya chama, kikao kilichodumu kwa siku mbili mfululizo hapa jijini Dar es salaam,
1.KIKAO cha kamati kuu kilikuwa cha
kawaida ,hakuna jambo la dharula
2.Mchakato wa katiba mpya usiathiri
mabadiliko ya sheria nyingine kama
mabadiliko ya sheria ya uchaguzi
3.Mwaka 2013,ni mwaka wa nguvu ya
umma,hakuna kubembelazana na
serikali rais kikwete hajajibu madai ya
yetu kwa hiyo tutamshinikiza.
4.sehemu ambazo CCM wanaogopa kuitisha
uchaguzi,tutawalazimishwa kuitisha
uchaguzi kata za arusha
mjini,sengerema,nk.ziko 15
5.Uongozi wa KARATU wa CHADEMA
Tumeusimamishwa kwa muda mpaka chama
kitakapokamilisha uchunguzi wake
huko wanasheria Marando na Prof Safari
watachunguza kashfa za mtu mmojammoja
huko karatu, kumekuwa na kashfa kwenye
miradi ya maji na ardhi.
6.Hatua za kisheria kufuatia matukio ya
uchaguzi wa ilemela mwanza,baada ya
madiwani 2 kufukuzwa uanachama
zitaendelee kuchukuliwa,pia hatua za kisiasa
zianzishwe kudai uwajibikaji wa
halmashauri ya jiji la mwanza ili haki
itendeke.
7.kamati kuu imetambua kutapatapa kwa
CCM juu ya sera zake za katiba mpya,elimu
bure na bei ndogo za vifaa vya ujenzi CCM
haiaminiki,kwa hiyo CHADEMA tutaendelee
kuunganisha umma ili CCM iondolewe 2014
na 2015
8 M4C itaendelee kwa kasi mapema mwaka
2013,sekretariati itatangaza ratiba januari.
9.juu ya hoja binafsi za wabunge wetu zito na mdee(kuhusu uporaji wa
ardhi na mabilioni ya Uswis),pamoja na
hoja ya Tundu Lisu juu ya uteuzi holela wa
rais wa majaji,kamati kuu imependekeza
maazimio ya bunge yafuatwe na baadaye
kidogo kama hairidhiki kamati kuu
itaelekeza nini kifanyike kwa hatua za ziada
10.Kamati kuu imesikitika kuwa rais
amepuuza barua ya yetu juu ya
kuunda tume ya kimahakama kuhusu
mauwaji mbalimbali nchini.hivyo M4C
itatumika mwaka 2013 kumshinikiza rais
kujibu barua hiyo na kutekeleza yale barua
inaelekeza yafanyike
Kamati kuu imesisitiza kuwa mwaka 2013
ni mwaka wa nguvu ya umma,na hakuna
tena kubembelezana na serikali.
Sisi kama chama tunatambua mchango wenu sana, kwa pamoja tutapata mabadiliko tuyatakayo
Kiongozi wenu
Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
No comments:
Post a Comment