Thursday, March 17, 2011

KILIO CHA WASANII WOTE NCHINI TANZANIA NIA HAKI ZA KAZI YA MIKONO YAO,

KILIO CHA WASANII WOTE NCHINI TANZANIA NIA HAKI ZA KAZI YA MIKONO YAO,  Send to a friend
Thursday, 17 March 2011 08:56
0diggsdigg
Kituo cha wasanii wachoraji Mwenge jijini Dar es Salaam
Na Charles Kayoka
Jicho la Msafiri kwa leo liko Dar-es-Salaam, Mwenge, kijiji cha wachongaji. Lengo mahsusi ni kuzua mjadala juu ya namna ya kulinda au kuanzisha haki miliki kwa wabunifu wa sanaa za uchongaji. Ninaamini kuwa mfumo wa kibiashara wa sasa hauwapatii faida kubwa wabunifu, na hata taifa kwa ujumla.

Nilivutiwa kwenda Mwenge baada ya kufika duka moja hapa jijini na kukuta bidhaa za uchongaji zikiuzwa kwa bei ya juu, kama mara tatu ya ile inayouzwa pale Mwenge kijijini. Nikajiuliza kama tofauti hii kubwa ya bei kama inampatia msanii faida au kuwa msanii akishaiuza bidhaa yake anakosa udhibiti kabisa wa biashara ya bidhaa hiyo na hivyo hawezi kupata faida inayoweza kumuinua kimaisha.

Majadiliano na wafanyabiashara na wasanii yamenionyesha kuwa kuna changamoto kadhaa zinazofaa kufanyiwa kazi. Changamoto ya kwanza ni kukosekana kwa wanunuzi wengi wa Kitanzania ambao wangewezesha biashara hii kuneemeka. Nikaambiwa wengi wa Watanzania huja pale kununua bidhaa za mavazi- T-shirts, vikoi na vitambaa vya magauni na kwa kiwngo kidogo hereni  na bangili.

Watanzania hawana utamaduni wa kununua vinyago kwa ajili ya kupamba majumbani mwao. Sababu hasa nini? Ili kuwafanya watanzania kupenda kupamba kazi za sanaa katika nyumba zao kunahitajika msukumo wa kibiashara na mtazamo mpya utakaojenga hamasa ya kupenda vitu vyetu hasa kazi za sanaa.

Hapo awali niliwahi kupata malalamiko kuwa bidhaa zinapobuniwa Tanzania na kwenda nchi za jirani huko huweza kutolewa nakala nyingi na kuuzwa nje ya Afrika Mashariki kwa bei ya juu. “Sio hivyo tu ndugu mwandishi, sisi tunatambua kuwa bidhaa zetu za usanii zikinunuliwa na wageni kutoka nchi jirani zikifika huko zinagongwa mihuri kuwa zimetengenezwa huko na sio kuwa zimetoka Tanzania kama chanzo asilia,” aliniambia msanii mmoja.

Licha ya kuwa hakuna juhudi wanazofanya kuweka mfumo wa kudhibiti haki miliki na kuweka haki za ubunifu- intellectual property rights, wasanii hawa hawajui soko la bidhaa zao na wengi hutegemea walanguzi wa kati kununua na hao ndio wanaowatafuta wanunuzi nje ya nchi. Kwa kukosa maarifa ya kibiashara wasanii wabunifu hawawezi kujua kama wananyonywa  na kuwa wana haki ya kulinda rasilimali zao na pia kufaidika kutokana  na ubunifu wao.

Lakini wao wenyewe nilipoongea nao walisema kuwa hawaoni shida. Tangu mababu ubunifu umekuwa ni mali ya umma. Ukibuni sanaa ni sawa mwenzio akikuiga na kuuza na kufaidika kutokana na ubunifu wako. Wenzetu ulaya wanaweza kuzuia kuigiza kwa sababu wameanza vizuri kwa kulinda haki za wabunifu. Sisi hatukuanza hivyo, kwa maelezo yao, basi tuendelee kwa mtindo huuhuu.

Aidha wafanyabiashara wanaonunua bidhaa toka kwa wasanii wanasema msanii hana haki ya kudai kuwa usanii wake unaigizwa au kurudufiwa kwa sababu akishauza kazi haki ya kumiliki ubunifu wake anaiuza pia.  Sijui watu wa COSOTA na wizara ya viwanda na wanasheria wanaojihusisha na haki hizi za ubunifu wanaweza kusema nini kuhusu hili.

Sidhani kama Ulaya unaweza kufanyia mzaha kiasi hiki haki za ubunifu wa msanii. Kuwa unabuni sanaa yako kwa mtindo wako wa pekee, inavutia wanunuzi, halafu wanunuzi wanaamua kuirudufu kwa kadri wanavyoweza na msanii (mbunifu) asilia akabaki tu akiona upujufu huu ukitendeka na akanyamaza.

Wasanii wetu, nilipowauliza kama wanasajili kazi zao za ubunifu, wakasema kuwa hawajui kama wanaweza kufanya hivyo na kuwa wameona waishi kadri walivyozoea kwani hata wao huletewa kazi za ubunfi kutoka nje na kuzirudufu na kujipatia fedha kwa njia hiyo. Waakala wa usajili wa kampuni, hataza na alama za biashara – BRELA inapaswa kufanya kazi zaidi ili kulinda haki za kundi hili.

Mmoja wa wachuuzi wa sanaa mwanamama alisema kuwa tatizo liko pia upande wa serikali. Anaamini kuwa Mashirika kama HANDICO kama ilivyokuwa zamani yangeweza kuratibu ulinzi wa haki za wabunifu wa sanaa; aidha aliamini kuwa Shirika linalohusiana na Utalii, SIDO, au wizara ya viwanda wanatambua kabisa kuwa usanii unaweza kuleta pato kwa Watanzania na taifa, lakini wanaona kinachotendeka wao wananyamaza.

“Kama leo hii watu wa nchi jirani wanauuza Mlima Kilimanjaro kama wao na sisi tunashindwa kuzuia hilo iweje tuweze kudhibiti uharamia wa bidhaa za sanaa unaofanywa na wageni?” Aliuliza mfanyabiashara huyo. Hivi ukifika Afrika Kusini ukaona kazi ya Kimasai imewekwa mhuri kuwa imetengenezwa Zambia hapana shaka utashituka hasa kama nchi itakuwa na utaratibu wa kusajili bidhaa zake. Mara moja utajua kuwa kuna uharamia na wasanii wan chi yako wananyonywa na unaweza kuchukua hatua.

Mfanyabiashara mwingine alisema kuwa yeye anatambua kuwa biashara ya sanaa ina fursa kubwa ya kuajiri watu wengi na kama ikiimarishwa ingeweza kuwa sekta madhubuti ya kutoa ajira kwa Watanzania wengi kuanzia huko kunakokatwa miti, wachongaji na  wauzaji wa ndani. Alisema kumekuwa na tabia ya kutojali kazi za kijadi wakati inaonekana wazi kuwa wageni wanakuja kwa makundi kununua bidhaa na kwenda nazo  nje.

Kama mpingo unapatika Tanzania kwa wingi zaidi kuliko sehemu nyingine Afrika, inakuwaje serikali haioni kuwa hii ni hazina ya taifa na inayoweza kulipatia taifa kipato.  Nadhani hii ndio changamoto kubwa ya wafanyabiashara wa kazi za ubunifu.

Wakati wasanii wa nyimbo, vitabu na picha wanaweza kulinda haki zao za ubunifu, hawa wa kazi za uchongazi hawaoni kuwa inawezekana, na kuwa hakuna baba mlezi wa kuwasaidia kutambua haki hizo. Mtu anaweza kutambua ugumu wa kuanzisha mchakato wa kulinda ubunifu katika kazi za sanaa, lakini kwa nia na makusudi, hakuna lisilowezekana kufanyika.
Kama serikali inatambua kuwa hili ni swala la uhai wa taifa na kuondolea umasikini wananchi, ni lazima ianzishe mchakato utakaowahusisha wataalamu na wadau mbalimbali kufikia mahali ambapo hatimaye sekta hii inatambulika na haki za wasanii zinalindwa.

Hizi sio changamoto rahisi kwa sekta hii, lakini zikifanyiwa kazi na tukafanikiwa

utaliiupdate@gmail.com This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it , 0766959349

1 comment:

  1. Kwenye usajili wenyewe walioko huko Hawajui umuhimu wa kusajili kazi za wasanii, kwa stahili hiyo hata wasanii wenyewe wanakosa influence ya hiyo kitu,
    Tatizo la hapa Tanzanina si wasanii pekeyao ni Watanzania Wote wavivu kujifunza na kuapply kile walicho jifunza, kwasababu kama tungekuwa na mioyo ya kujifunza sidhani kama mambo ya kipuuzi kama haya yangetukuta vile yanatukuta sasa hivi.
    Kuhusu haki za wasanii, wale COSOTA hawajui umuhimu wao Tanzania na kwenye copywright za wasanii, wote hawajui na hawajui wako pale kwa kazi gani, Mimi sija wahi kusikia hata siku moja wamefanya survey ya kushtukiza kuangalia Kazi za wasanii walio sajiliwa zikihujumiwa hiko mitaani.
    Sasa wanafanya nini Pale? au wanasubiri mwisho wa mwezi wapokee mishahara kisha wakatusue tu na vitoto vidogo vya kike na kiume?

    ReplyDelete