Tuesday, June 7, 2011

Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi

RAIS Jakaya Kikwete amewasilisha taarifa ya Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania kwa umma.

Wakati akiwasilisha taarifa hiyo alisema, Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.


Rais Kikwete alisema kwa hali ya uchumi, kwa maana ya viashiria vya uchumi jumla, Tanzania iko mahali pazuri licha ya nchi kukumbwa na athari za msukosuko wa uchumi duniani katika mwaka wa 2008/2009, ukuaji wa uchumi ni mzuri.


“Kwa wastani wa asilimia saba tangu mwaka 2001 hadi 2010, Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi.


Katika kipindi hicho, pia mfumuko wa bei umekuwa wastani wa chini wa kiwango cha asilimia 10 licha ya kuyumba mwaka 2009 kutokana na matatizo ya bei za mafuta na chakula duniani kwa ujumla,” alisema Rais Kikwete.


Rais Kikwete aliwasilisha taarifa ya mpango huo wa miaka mitano wa kuanzia 2011/2012 – 2015/2016, wakati akizungumza na Taifa kutoka kwenye Ukumbi wa St Gaspar mjini hapa, akishuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa, wabunge, mabalozi na wananchi kupitia televisheni.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi; Waziri Mkuu Mizengo Pinda; Spika wa Bunge, Anne Makinda, wakuu wa vyombo vya Dola, wabunge, mabalozi kadhaa, ni miongoni mwa walioshiriki katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Mipango katika Ofisi ya Rais.


Rais Kikwete alisema makusanyo ya mapato ya ndani yameongezeka sana kwa wastani wa Sh bilioni 84.7 kwa mwezi kwa mwaka 2001/2002 hadi Sh bilioni 430 kwa mwezi katika kipindi cha Julai mwaka 2010 hadi Aprili mwaka huu.


“Makusanyo mazuri ya mapato ya ndani yametuwezesha kuongeza uwezo wa bajeti ya Serikali kutoka Sh 1.76 trilioni mwaka 2001/2002 hadi Sh trilioni 11.6 mwaka 2010/2011.


Mauzo yetu ya nje yamefikia dola za Marekani milioni 5,876.5 mwaka 2010 na akiba yetu ya fedha za kigeni ni dola za Kimarekani milioni 3.948.0 sawa na mahitaji ya kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi sita mwaka 2010,” alieleza Rais Kikwete na kushangiliwa na waliohudhuria hafla hiyo.


Rais Kikwete alisema makusudio makuu ya Serikali katika mpango huo ni kuona kwamba, kwanza; vikwazo vya ukuaji wa uchumi vilivyopo vinatanzuliwa; pili; kujenga uwezo wa nchi wa kukuza uchumi wake na kuondoa umasikini haraka; tatu; kujizatiti katika kutumia kwa ufanisi na kimkakati fursa mbalimbali zilizoibuka nchini na katika mahusiano ya kiuchumi kikanda na kimataifa.


Pia alisema kusudio la nne, ajira ziongezeke kwa wingi zaidi ili kupunguza tatizo kubwa la ajira linalowakabili vijana na kuongeza kuwa dhana kubwa iliyobebwa na Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa ni “Kufungulia Fursa Tulizonazo za Kukuza Uchumi wa Taifa.”


Alisema Mpango huo umejengeka juu ya nguzo kuu nne za kimkakati ambazo ni kuendeleza uchumi wa jumla na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana hadi sasa na kutumia rasilimali zetu kama fursa ya kukuza uchumi; huku kipaumbele maalumu kitawekwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi na uendelezaji wa viwanda kwa kutumia malighafi na rasilimali zetu.


Aidha, Rais Kikwete aliyataja maeneo ya vipaumbele vya mpango kuwa ni kilimo, miundombinu, viwanda, utalii, rasilimaliwatu na kuendeleza matumizi ya Sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.


Alisema Mpango huo una malengo kwa kila kipengele, ikiwamo uchumi wa Taifa unatakiwa kukua kwa asilimia 8 hadi 10 kwa mwaka; mfumuko wa bei udhibitiwe chini ya kiwango cha asilimia 5; thamani ya mauzo ya nje ikue kufikia asilimia 23 ya Pato la Taifa; ukusanyaji wa mapato ya ndani ufikie asilimia 19 ya Pato la Taifa na kipato cha mwananchi kiongezeke hadi kufikia wastani wa dola za Marekani 650.


Kuhusu gharama za utekelezaji wa mpango huo, Rais Kikwete alisema utagharimu jumla ya Sh trilioni 42.5 kwa kipindi cha miaka mitano ikiwa ni wastani wa Sh trilioni 8.5 kwa kila mwaka
.

BAJETI YA TANZANIA NI LEO: WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA

Tuesday, 07 June 2011 21:09

Waandishi Wetu, Dar na Dodoma
MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta.

Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha.

Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo.

Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, bajeti ya serikali imekuwa ikisomwa siku za Alhamisi ya wiki ya kwanza ya Juni, lakini mwaka huu imebadilika ikielezwa kwamba hiyo ni kutokana na siku hiyo kuangukia siku ya Uhuru wa Uganda.

Akizungumza bungeni jana asubuhi, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema bajeti hiyo itatanguliwa na hotuba ya hali ya uchumi itakayosomwa pia na Waziri Mkulo.Alisema hotuba hiyo itasomwa asubuhi, wakati ile ya bajeti itasomwa jioni.

Baadhi ya mawaziri akiwamo Mkulo wameifagilia bajeti hiyo huku Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) likitoa mapendekezo na matumaini yake.

CTI: Tunataka bajeti ya uchumi wa viwanda

Shirikisho hilo limesema kuwa linaisubiri kwa hamu bajeti hiyo likitaka iwe ya kukuza uchumi na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.Kauli ya CTI huku likilalamikia kupanda kwa gharama za uzalishaji zilizotokana na mgawo wa umeme wa Tanesco.

Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Christine Kilindu alisema jana kwamba serikali inapaswa kutoa bajeti ambayo pia itaondoa kodi zinazoumiza uzalishaji mkubwa.Alisema kodi kubwa zisizo za msingi zinachangia kupanda kwa gharama za uzalishaji ambao mwishowe husababisha kupanda kwa gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida. 

"Tunataka bajeti ambayo itaondoa kodi zinazokwamisha uzalishaji mkubwa na ukuaji uchumi, tunataka bajeti itakayopunguza makali ya maisha kwa mwananchi kwa kumwezesha kupata bidhaa kwa urahisi," alisema Kilindu.

Alisema bajeti hiyo inapaswa pia kuweka mazingira mazuri na yanavyovutia kibiashara ili kuifanya Tanzania kuwa kituo muhimu cha uwekezaji.Alisema kwamba anategemea kuona umeme ukiwekewa mazingira ya kukuza uchumi na uwekezaji nchini, akisema bila kufanya hivyo hakuna kitu kitakachofanyika.

"Bila umeme hakuna kitu chochote, serikali inapaswa kuongeza nguvu na msukumo kuona umeme siyo tu unamulika maisha ya watu kwa kutoa mwanga, bali iwe ni nguvu ya kusukuma ukuaji wa uchumi wa nchi."

Mawaziri wapigia debe bajeti

Katika kujiwekea mazingira mazuri na kuzuia kubanwa na wabunge, baadhi ya mawaziri wamepigia debe bajeti za wizara zao huku Mkulo, akiahidi kuwa malimbikizo ya vyombo vya usalama yatalipwa mwezi huu.

Mara kwa mara baadhi ya wabunge wamekuwa wakitishia kukwamisha baadhi ya bajeti za wizara, kutokana na kukosa majibu ya msingi kwa mambo mbalimbali ya msingi.Jana asubuhi baadhi ya mawaziri walipokuwa wakijibu maswali bungeni walisisitiza kuwa mambo mengi waliyokuwa wakiulizwa yamezingatiwa katika bajeti.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Hamis Kagasheki, akijibu swali kuhusu malipo ya malimbikizo ya posho za polisi ikiwamo za wakati wa uhamisho, alisema wizara yake imeandaa mwongozo wa kisera wa namna ya kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.Alisema katika mwongozo huo ambao tayari ulikubaliwa na Wizara ya Fedha na Uchumi, wizara yake imejipangia utaratibu wa kutatua kero hiyo kuanzia kwenye bajeti ya mwaka huu.

Balozi Kagasheki alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Mohammed Sanya, ambaye alitaka kujua mkakati huo ukoje kutokana na tatizo hilo kuwa ni la muda mrefu. Baada ya majibu hayo, Waziri Mkulo alisimama na kukuongeza kuwa siyo malimbikizo ya polisi pekee, bali ya vyombo vyote vya usalama na kwamba serikali imejipanga kuhakikisha yanalipwa kabla ya mwezi huu kumalizika.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe naye alipigia debe bajeti ya wizara yake ambayo tayari ilisifiwa na Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kutokana na kugusa kila eneo huku ikitajwa kuandaliwa kwa weledi wa hali ya juu.

Akijibu maswali likiwamo lililohusu ujenzi wa Barabara ya Babati, Dareda hadi Minjingu na kuhusu kero za barabara katika Jimbo la Ludewa linaloongozwa na Profesa Raphael Mwalyosi, Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa wizara yake ni sikivu na mambo mengi yatazingatiwa ndani ya bajeti.

Alisema wizara iko makini na Bajeti ya Ujenzi imezingatia mambo mengi ya msingi huku akitupa kete ya kuomba uungwaji mkono kwa wabunge ili waipitishe.

Imeandaliwa na Ally Mkoreha, Dodoma; Ramadhan Semtawa na Patricia Kimelemeta, Dar es salaam

JE UNAJUA LINAH WA THT AMBAYE SASA AMEWAFUNIKA WAIMBAJI NGULI WA KIKE NCHINI TANZANIA, AMETOKEA WAPI?

Linah Sanga 'Linah'
Thursday, 12 May 2011 04:41
*Clouds Radio kupitia 'Nyuki live' ndiyo iliyomtoa
*Ataka kuwa wa kimataifa kama AY, Alikiba


Na Laurent Samatta

KAMA ni msikilizaji wa kituo cha radio cha 'Clouds', basi utakumbuka mwaka 2009, waliwahi kutangaza nafasi za bure kwa kijana yeyote mwenye uwezo wa kuimba, apige simu kwa namba walizotaja ili uweze kuimba na wao walikuwa wanarekodi ulichokiimba.

Programu hiyo ilipewa jina la 'Nyuki live', ambayo ilikuwa na lengo la kutafuta vijana wenye uwezo wa kuimba, hivyo vijana wengi walipiga simu na waliimba lakini mwisho wa siku walikuja kupatikana vijana watatu ambao walionekana kufanya vizuri.

Vijana hao hivi sasa wanafanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya kitu ambacho hata wale wengine ambao hawakupata nafasi ya kutoka wanatamani programu hiyo irudi tena ili waweze kujaribu.

"Siku hiyo nilikuwa nasikiliza muziki kupitia kituo cha radio 'Clouds', hapo nilikiwa mkoani Mbeya nikasikia tangazo likisema kuwa kijana yeyote ambae anajiona anaweza kuimba vizuri na akakubalika basi apige namba hiyo ili aweze kutuimbia na akionekana amefanya vizuri atapigiwa simu.

"Mimi kweli sikusita kupiga simu lakini kwa mara ya kwanza ilikuwa ngumu lakini nikajaribu kama mara tatu hapo ndipo nilipoonekana nimefanya vizuri, basi pale nikasubili majibu na mwisho wa siku nikapigiwa simu kuwa ni mmoja kati ya washindi watatu wa 'Nyuki live'.

"Sikuamini kama nimeshinda maana Tanzania kuna vijana wengi lakini bahati ikaja kwangu, hivyo nilipofika katika ofisi za Clouds kuna vitu pia wao walitaka kuviona kwangu kama sauti hivyo wakanipeleka Nyumba ya Vipaji Tanzania 'THT', kwa ajili ya kufundishwa namna ya kuimba na mtiririko wa sauti.

Lakini namshukuru mungu pale sikukaa sana kwa sababu nilikuwa na juhudi katika kuimba na uwezo wangu ukawa mkubwa hivyo nilikaa darasani miezi miwili baada ya hapo nikaingizwa moja kwa moja kwenye bendi ya THT, inayojulikana kama 'Odama Band'.

Lakini mwaka huo huo wa 2009, kwa bahati nikachanguliwa katika Fiesta nikiwa kama msanii chipukizi lakini nilichokuwa nakifanya nilikuwa naimba kama msanii wa kusindikiza wale wengine ambao tayari walikuwa na nyimbo zao," anasema Linah.

Jina kamali la nyota huyo hatari ni Linah Sanga lakini wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya wanamfahamu kama 'Linah', kwa sababau ndilo jina analotumia katika kazi zake za sanaa.

Nyota huyo ni mmoja kati ya wasanii wachache ambao muziki wao unafanya vizuri hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, kutokana na ubora wa kazi zake pamoja na sauti njinsi anavyoibana na kuifanya iwe ya kuvutia zaidi.

Akifanya mahojiano na maalumu na mwandishi wa makala haya hivi karibuni Linah, anasema kwa upande wake imekuwa tofauti na nyota wengine ambao wamekuwa wakifanya muziki kwa sababu ya kaka anaimba au baba anafanya muziki.

Anasema muziki kwake upo kwenye damu na tayari alishakuwa muimbaji wa kwanya katika kanisa ambalo walikuwa wanasali yeye na wazazi wake ambalo ni 'Ufufuo wa Uzima', huku akiwa katika Kwanya ya 'Grolia kwanya'.

Anasema baada ya kuitumikia kwanya hiyo kwa muda mrefu mwaka 2006, akapewa nafasi ya kuwa  mwalimu wa 'Grolia kwanya' ambapo alikuwa akifundisha namna ya kuimba na mtiririko wa sauti.

Anasema viongozi wa Kwanya hiyo walikubali uwezo wake hivyo wakaamua kumtumia katika Band yao inayoitwa 'Grolia Band', ambayo ilikuwa inatoa nyimbo zake kwenye vituo vya radio hapa nchini.

Linah anasema kipaji chake kilizidi kung'ara hasa pale alipochukuliwa na marehemu Docta Remmy Ongala na kumweka katika bendi yake iliyojulikana kwa jina la 'Remmy Ongala Band', ambayo ilikuwa inaimba nyimbo za kumfifu mungu kipindi hicho.

marehemu huyo wa kibao cha 'Kifo hakina huruma' kabla ya kuingia katika nyimbo hizo alikuwa akiimba nyimbo za kidunia lakini baada hapo aliamua kuokoka na kufanya kazi katika kanisa hilo ambalo nyota huyo alikuwa akisali.

"Remmy alikuwa akisali kanisa moja na sisi na baada ya kuniona naimba vizuri katika Kwanya yetu aliamua kunichukua na kunipeleka katika bendi yake, kwa kweri aliniamini kwa sababu sauti yangu ilikuwa ni nzuri ingawa kipindi hicho haikuwa nzuri kama ilivyo sasa," anasema.

Anasema baada ya miaka hiyo kupita alikuwa hajui kama anaweza kuja kuimba nyimbo za kidunia kwa sababu tayari alikuwa akiimba nyimbo za dini ambazo hadi anakuja kuchukuliwa na 'Nyuki live' kutoka 'Clouds' tayari maisha yake yalikuwa yamezoea kuimba nyimbo hizo.

Anasema tangu mwaka huo 2009 alikuwa tayari amesha achana na nyimbo za dini kwa sababu tayari aliingia katika ukurasa mpya wa kuimba nyimbo za kidunia, ambapo mwaka 2010 ndipo alipoamua kutoa wimbo wake wa kwanza ulikwenda kwa jina 'Atatamani'.

'Wimbo huo ndiyo ulikuwa wa kwanza kutoa tangu nilipochukuliwa na 'Clouds' na kuingia 'THT' lakini niliutoa nikiwa chini ya THT, na ndiyo maana watu wengi ambao hawanijui wanasema nimekulia hapo 'THT'," anasema.

Anasema wimbo huo uliweza kufanya vizuri na kumtambulisha katika muziki wa kizazi kipya, na kuanza kufanya shoo mbalimbali katika matamasha, ambapo wimbo wake wa pili 'Bora nikimbie' nao umeweza kufanya vizuri na kuzidi kumtagaza Afrika mashariki akiwa kama msanii chupukizi.

"Nashukuru mungu kwa sababu baada ya nyimbo hizo mbili nimeweza kufanya kazi nyingine za kushirikishwa na wasanii wengi kama Mrisho Mpoto wimbo wake 'Adela', Barnaba wimbo 'Wrong number', Sajna wimbo 'Sitaki kuumizwa' na wengine wengi.

Anasema baada ya nyimbo hizo mbili kufanya vizuri hivi sasa anatamba na albamu yake ya kwanza yeye nyimbo 10, ambayo imebeba jina la 'Atatamani' ikiwa na nyimbo kama Atatamani, Bora nikimbie, Chozi langu na nyingine nyingi zenye ubora wa kimataifa.

Linah anasema kwa upande wake hana fani ya kutunga nyimbo hivyo nyimbo zote alizotoa ametungiwa na rafiki yake ambae pia ni msanii 'Amini' pamoja na 'Barnaba Boy', ambao wamekuwa wakifanya kazi zao pamoja.

Kwa upande wa malengo Linah anasema amejiwekea mikakati ya kufanya kazi ambazo zitamtagaza kimataifa, ili aweza kuwa kama Ambwene Yessaya 'AY' au Ally Kiba 'Alikiba', ambao hivi sasa wanafanya muziki wao kimataifa.

Anasema hata hivyo katika suala la mafanikio, katika kipindi cha mwaka mmoja alichodumu katika muziki wake tayari amesha fanya mambo kama, kununua viwanja viwili kwa ajili nyumba pamoja na kuangiza gari nje aina ya Toyata VX, ikiwa pamoja na kuishi kwa kujitengemea.

Anasema kwa upande wa wazazi wake ambao wapo katika dini hawakuweza kumruhusu kwa mara ya kwanza kwa sababu walitaka aendelee na dini kwa vile waliamini muziki huo unaimbwa na watu ambao wamemtupa mungu kutokana na baadhi ya wasanii njinsi wanavyojiweka mbele ya jamii.

"Wazazi wangu ni watu wanaoamini dini hata mimi pia, lakini kwa mara ya kwanza ilikuwa ngumu sana kunikubalia lakini nikawaeleza sitakuwa na tabia kama baadhi ya wasanii wanavyofanya na kweri wakanipa ruhsa," anasema.

Anasema wazazi wake hadi sasa wanamuelewa kwa sababu hana tabia ambayo inaweza kuwakera kitu ambacho kila siku anaomba mungu asije akabadilika na kuwa na tabia kama baadhi ya wasanii.

Linah anasema hana elimu kubwa zaidi ya kidato cha nne, lakini anaamini atarudi shule ili aweze kumaliza elimu ya juu ambayo inawe kumsaidia hapo baadae ikiwa pomoja na kuchukua masomo ya sanaa katika chuo kikuu chochote Duniani.

Linah anatoa ushauri kwa wasanii pamoja chipukizi ambao wanaingia katika fani hiyo kuacha tabia ambayo inawapelekea wazazi kuhisi sanaa ni fani ambayo inavuja maadali hasa mbele za mungu

WCHUNGAJI VIPI TENA MNABAKA KONDOO WENU?

Mchungaji KKKT jela kwa rushwa ya ngono

Na Eliasa Ally, Iringa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, imemhukumu kifugo cha miaka mitano Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Michael Ngilangwa, baada ya
kupatikana na hatia ya kuomba rushwa ya ngono kwa  mwanafunzi ili amsaidia masomo.

Mchungaji Ngilangwa alikuwa mwalimu wa sekondari ya Pomerini iliyopo wilaya ya Kilolo.

Akitoa hukumu hiyo mjini hapa jana, Hakimu wa Mkazi wa Mahakama Iringa, Bi, Martha Mpaze, alisema mshitakiwa wakati wote wa  kesi hakuwa na shahidi, ambapo alijitetea mwenyewe.

Upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi watano. Alisema mshitakiwa katika utetezi wake, alisema kesi hiyo ni ya kubambikizwa kosa hilo kutokana na wivu uliokuwepo kati yake na baadhi ya walimu wa sekondari ya Pomerini kumfanyia.

Alidai walimu hao walifanyia fitina baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Mkuu wa Shule Pomerini, hatua iliyomwongezea maadui ambao walikuwawakimfanyia fitina na kuandaa mazingira ya mtego ili ili akamatwe na mwanafunzi.

Alisema katika utetezi wake, Mchungaji Ngilangwa alidai baada ya kushika wadhifa huo  wazazi wengi walikuwa wakimpelekea matatizo ya watoto wao, akiwemo mzazi wa mwanafuzni aliyemshitaki kwa madai ya kumuomba  rushwa ya ngono.

Alisema siku ya tukio mshtakiwa aliyokamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) alipigiwa simu na mama wa mwanafunzi huyo kuwa wanatoka Dar es Salaam hivyo aliomba awatafutie vyumba katika nyumba za kulala wageni.

Katika utetezi wake alidai kwamba alikwenda nyumba ya  wageni na kuchukua vyumba viwili kimoja cha kulala watu wawili.

Alidai kwa kuwa ulikuwa ni usiku, alichukua chumba namba 4 kwa ajili yake.

Bi. Mpaze alisema mshtakiwa anaonekana kuwa na makosa kwa kuwa katika kitabu cha wageni alijaza kuwa anatoka Njombe kwenda Iringa wakati siyo kweli.

Alisema ukweli ni kuwa mshtakiwa alikuwa anatoka Pomerini kwenda Iringa mjini.

Alisema kuwa ushihidi mwingine ambao unamtia hatiani Mchungaji Ngilangwa ni ule wa TAKUKURU kumkuta na vidonge vya kuzuia mimba, ambavyo alimpatia mwanafunzi wake ameze kwa kuwa wangefanya ngono bila kutumia kondomu.

Hakimu huyo alisema ushahidi mwingine ni ule wa ujumbe ambao TAKUKURU ilinasa sauti walipokuwa wakiongea na mwanafunzi wake.

Hakimu huyo alikuwa akimwambia mwanafunzi huyo aende chumba namba nne ndiko wangelala.

"Mshtakiwa anatiwa hatiani kwa ushahidi mwingine ambapo TAKUKURU ilimkuta akiwa na mwanafunzi wake huyo saa 5:00 usiku wakati sheria ya nyumba hiyo ya kulala wageni walipokutwa inakataza watu wasio wanandoa kulala chumba kimoja.

Hakimu huyo alisema kama TAKUKURU wasingewahi mwanafunzi huyo angebakwa na azma yake ya kuomba rushwa ya ngono ingetimia.

Mshtakiwa huyo alipotakiwa kujitetea aliomba mahakama imfikirie kwa kuwa ana watoto wanne wanaomtegemea, wawili wanasoma sekondari na wengine shule ya msingi.

Mchungaji Ngilangwa aliongeza kuwa mzazi wake ni mzee wa miaka 82, hivyo hana mtu wa kumtunza.

Akitoa hukumu Hakimu Bi. Mpaze, alisema mahakama imezingatia kuwa mkosaji wa mara ya kwanza lakini akahukumiwa adhabu wa miaka mitano jela.

Katika kesi ya pili ya kuomba rushwa ya ngono mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya sh. 500,000 au endapo atashindwa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.

2 Maoni:

Anonymous said...
Mahakimu mara nyingi hawachunguzi sana kiini cha kosa (Natural causes) huwa hazipo kwenye makosa. Kwa mfano, mfadhaiko wa akili huchukuliwa kama something done deliberately. Hata mtu kubaka, huwa kuna mfadhaiko wake ambao hata wao mahakimu huwa nao na huenda kwa ajili ya kuwa Mheshimiwa yanafichwa lakini wanayo makosa makubwa (deep) na grave kwani wengine hulala na housemaids, ambayo ni kama kubaka, lakini kwa vile ni mheshimiwa, hai-surface. Rushwa ya pesa na ngono ni kitu kiko kwa hawa mnao waita waheshimiwa. Vile vile yabidi Mahakimu wasomee psychology kwa kina kikubwa. Kwa kesi hii husika, this was a trap, and nothing but a delibrate trap ambayo huyu mwalimu kwa kuishi kwake kijijini, hakujua kuwa anategewa. Kuna kitu kikubwa ndani ya hii kesi. Huyu mwalimu inaonekana anao maadaui wamemzingira, msichana alitumwa, wazazi walioomba kutafutiwa vyumba walikuwa na lengo baya na pana toka kwa walio watuma na si hao tu kuna pia wengine ambao wako involved. Lakini mlipaji ni Mungu. Adhabu yao itafuata. Acha mtu wa watu akatumikie kifungo lakini walio sababisha, upanga ni juu yao milele.Na huyu Hakimu hana uelewa mpana, akasome tena kwa kina.
Anonymous said...
Pambaf! Unasumbuliwa na siasa kali, nani alimtuma aende gesti usiku? nani alimwambia adanganye anakotoka na anakoenda kama alikuwa hana nia mbaya? Mwache akachunge kondoo midume jela! Mzinzi tu huyo hana cha uchungaji! Hivi kweli huyo unaweza kumpa binto yako amlee kiroho? Wee, utaambulia mjukuu!

MAASKOFU WAKERWA NA KUTUHUMIWA KWAMBA WAO NI DRUG DEALERS, WAJA JUU

Kauli ya Rais Kikwete yawakera maaskofu  Send to a friend
Monday, 06 June 2011 21:08
0diggsdigg
Boniface Meena
JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT), imempa Rais Jakaya Kikwete saa 48 ikimtaka awataje hadharani viongozi wa madhehebu ya dini aliosema wanahusika na biashara ya kuuza dawa za kulevya na kwamba asipofanya hivyo itakuwa ni aibu kiongozi huyo wa taifa.

Makamu Mwenyekiti wa CCT, Askofu Dk Valentino Mokiwa alisema hayo jana wakati jumuiya hiyo ilipokuwa ikitoa maazimio ya Mkutano wa 45 wa Halmashauri Kuu ya jumuiya hiyo.Askofu Mokiwa alisema kauli ya Rais Kikwete imewasikitisha kwa kuwa amewahusisha viongozi wote wa dini jambo ambalo si zuri mbele ya jamii.

" Rais ataje majina ni kina nani wanahusika na ndani ya saa 48 awe ameyataja la sivyo itakuwa ni aibu zaidi kwake na serikali," alisema Mokiwa.Alisema wanategemea Rais Kikwete atafanya hivyo na kinyume chake atakuwa hajawatendea haki wananchi.

Akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, juzi kwenye ibada maalumu ya kupewa daraja la Uaskofu na kusimikwa Mhashamu Askofu John Ndimbo wa jimbo hilo, Rais Kikwete aliwaonya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini akiwataka kuacha tabia ya kushiriki biashara ya kuuza dawa za kulevya, badala yake washirikiane na viongozi wa serikali katika kudhibiti biashara hiyo haramu.

Alisema kuwa baadhi ya viongozi hao wa dini wamekuwa wakishiriki kufanya biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafanyia mipango vijana kuwatafutia hati za kusafiria kwenda nchi za nje kwa ajili hiyo.

“Inasikitisha sana na kutisha. Biashara hii haramu sasa inawavutia hata watumishi wa Mungu, taifa letu litaharibika tusipokuwa makini katika hili, baadhi yenu tumewakamata,” alisema.

Msimamo juu ya Katiba Mpya

Akisoma tamko lao baada ya mkutano wa Halmashauri Kuu wa 45, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula alisema jumuiya hiyo imeitaka serikali kusimamia kwa umakini suala la Katiba Mpya hasa katika ukusanyaji wa maoni.

Alisema kuwa ukusanywaji huo wa maoni kwa wananchi na makundi yote ya kijamii ni muhimu ukafanywa na chombo huru.

"Kazi hii isiharakishwe na wala isicheleweshwe. Yafaa iwe imekamilika mapema ndani ya muda wa kadri kabla ya kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015," alisema.

Askofu Kitula alisema kuwa serikali inapaswa kuangalia ufa uliopo kati wananchi wa kawaida na wale wenye nacho kwani unazidi kupanuka na kuibua matabaka."Hali hii inasababisha malalamiko miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yetu. Malalamiko na ukweli huu umechukuliwa na wadau wa vyama vya siasa kufanya maandamano ambayo yamekuwa yakiwavutia wananchi wengi."

Alisema hali hiyo inachangia hali ya kisiasa kuwa tete hasa ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani ambako bei ya mafuta iko chini zaidi ya Tanzania na nchi hizo zinapitisha mafata hayo hapa."Serikali isahihishe jambo hili pasipo kuchelewa. Vyama vyote vya siasa vihamasishe wananchi kuleta maendeleo bila kujadi itikadi za vyama vyao."

Askofu Kitula alionya kuhusu siku za ibada na kutaka ziheshimiwe na watu wote na mamlaka zote. Alisema ni vyema serikali isipange matukio muhimu ya kitaifa kama  uchaguzi mkuu na uchaguzi wa serikali za mitaa siku za ibada.

"Kadhalika, wahadhiri na wakufunzi wa vyuo vikuu, vya elimu ya juu na taasisi zake wasiwapangie wanafunzi mitihani au mazoezi ya vitendo siku za ibada," alisema Askofu Kitula.

CCT yazungumzia tiba asilia

Kuhusu tiba asilia, CCT imetoa wito kwa serikali kusaidia katika utafiti na matokeo yake yawekwe bayana ili kuwaondolea wananchi hofu ikiwa ni pamoja na huduma zitakazothibitishwa kupatikana mahali pengine nchini.

"Kadhalika, serikali isimamie utunzaji wa mazingira ili miti na mimea mingine yenye vyanzo vya tiba asili istawi na kupatikana muda wote," alisema Askofu Kitula.Aidha, CCT imesisitiza msimamo wake kutaka mambo ya kuendesha shughuli za dini yatenganishwe na mamlaka ya kuendesha nch

USHINDI WA PEOPLES POWER-Mbowe huru, polisi watumia ndege ya JWTZ

Mbowe huru, polisi watumia ndege ya JWTZ  Send to a friend
Monday, 06 June 2011 21:17
0diggsdigg
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kukubali dhamana ya kesi yake, muda mfupi baada ya kufikishwa Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi. Picha na Mussa Juma
Waandishi Wetu.MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe jana aliachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, baada ya kusomewa mashtaka ya kutotii amri halali ya kuhudhuria mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya mkusanyiko wa watu bila ya kibali na vitendo vya uchochezi.
Aidha, mahakama hiyo imemkataa mdhamini wake wa awali, Julius Margwe baada ya kuwa na shaka na mwenendo wake. Diwani wa Kata ya Elerai (Chadema), John Bayo alijitokeza na kuwa mdhamini mpya wa Mbowe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alisema mdhamini huyo amekataliwa kutokana na kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo pamoja na kukabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso hivyo, kuamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

 Juzi, Mbowe alisafirishwa chini ya ulinzi hadi Arusha akitokea Dar es Salaam baada ya kukamatwa na polisi. Akizungumzia safari hiyo, Mbowe alidai kuwa alipelekwa kwa ndege ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) usiku wa manane huku akisindikizwa kwa magari manne ya askari wa kutuliza ghasia, kuanzia Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi mahakamani hapo huku akilalamikia hali hiyo na kusema ni matumizi makubwa ya fedha na rasilimali za umma.

"Wamenisafirisha kuja Arusha kwa ndege ya JWTZ kama mtuhumiwa wa ujambazi. Haya ni matumizi makubwa ya fedha na rasilimali za umma. Ile ndege ina uwezo wa kubeba zaidi ya watu 100, wametuleta watu watatu, mimi kama mtuhumiwa, Kamishna mmoja wa polisi Wilaya ya Ilala na Kamishna wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)," alidai Mbowe.

Hata hivyo, JWTZ limekanusha likisema halikuwajibika na tukio hilo la kumsafirisha huku polisi nayo ikimtaka Mbowe asijitafutie umaarufu wa kisiasa kwa mgongo wa suala hilo.

Mbowe alifikishwa mahakamani mjini Arusha jana saa moja asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali. Alikuwa katika gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser VX, lililokuwa likisindikizwa na magari mengine manne ya FFU.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mbowe alisema hajutii kuwekwa mahabusu na kusafirishwa hadi Arusha.Pia alisema kukamatwa kwake na kuwekwa mahabusu kamwe hakutasitisha harakati za Chadema kudai haki na demokrasia ya kweli ndani na nje ya Bunge.Alisema alipokuwa katika mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, hakuteswa na polisi wala kupigwa lakini alikuwa chini ya ulinzi hadi alipofikishwa Arusha jana alfajiri.

Kukamatwa kwake mwishoni mwa wiki kulichafua hali ya hewa ya kisiasa baada ya juzi, mamia ya mashabiki wa Chadema kupiga kambi Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, wakishinikiza mwenyekiti wao aachiwe huru kabla ya kupelekwa mahakamani Arusha.
Baadaye, juzi saa 7:00 usiku vyanzo huru vilidokeza kwamba Mbowe alisafirishwa kwa ndege hiyo ya JWTZ akiwa na maofisa waandamizi wa polisi kutoka Dar es Salaam na wanajeshi watatu.

Kauli ya JWTZ
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema hadi jana mchana hakuwa na taarifa zozote kuhusu jeshi kuwajibika katika suala hilo.
Alisema hilo lilikuwa suala la polisi na mahakama huku akisisitiza kuwa hajaona nafasi ya JWTZ katika mchakato huo.

"Ndiyo kwanza unaniambia wewe (mwandishi) kuhusu JWTZ kutumia ndege yake kumsafifirisha huyo mtu. Ninachoweza kukwambia hakuna kitu kama hicho na jeshi halikuwajibika kwa lolote," alisisitiza Mgawe na kuongeza:
"Tukio hilo linawahusu polisi na mahakama wao ndiyo wanaojua na ndiyo waliopaswa kuwajibika siyo jeshi. Kwa hiyo kama una vyanzo vyako vingine sijui sisi tunasema hakuna kitu kama hicho.''

Mahakamani Arusha
Baada ya kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka na kisha kuchiwa kwa dhamana, wafuasi wake waliokuwa wamefurika mahakamani hapo, walishangilia na kumbeba juu kwa furaha.

Kabla ya kuachiwa kwa dhamana Hakimu Magesa alisema mdhamini wa awali wa Mbunge huyo wa Hai, Margwe amekataliwa kwa sababu mbali na kuieleza uongo mahakama kuwa alikuwa akifika mahakamani hapo, haina sababu ya kuendelea naye kwani tayari ana kesi ya jinai ambayo hatima yake haifahamiki.Kuhusu Mbowe hakimu huyo alikiri kwamba mahakama iliruhusu washtakiwa wabunge kuhudhuria kikao cha Bunge la Bajeti , lakini kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri kwamba akamatwe.

“Ila sasa mkaendelee na vikao vyenu vya Bunge kama tulivyosema awali, lakini wadhamini wenu lazima waje mahakamani kila kesi itakapotajwa na tunaondoa amri ya kukamatwa na sasa utaendelea na dhamana yako ya awali,” alisema Magesa.

Kabla ya hakimu huyo kutoa uamuzi huo, alimpa nafasi Margwe ya kueleza sababu za kutofika mahakamani.
Margwe alisema Mei 27, mwaka huu hakufika kwa sababu alikuwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso na Mei 30 alifika mahakamani lakini kwa sababu hakupewa nafasi ya kusema lolote, hakujitokeza.

Wakili upande wa utetezi, Method Kimomogoro aliiomba mahakama hiyo, kuondoa amri ya kukamatwa kwa mteja wake na kutaka apewe dhamana yake ya awali ili aweze kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti ambalo yeye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.

Alimtetea mdhamini huyo kwa kutofika mahakamani na kusema kuwa hiyo ipo kwa kila mtu hata kwa mawakili akisema huwa wanasahau tarehe za mahakama na ndiyo sababu huziandika, hivyo kwa mwananchi wa kawaida ni lazima atasahahu tarehe hizo.

Wakili wa Serikali, Juma Ramadhani aliiomba mahakama hiyo itoe onyo kali kwa mshtakiwa kwa kutofika mahakamani hapo mara anapohitajika na pia kumtaka yeye na wenzake wawe na mawasiliano ya karibu na wadhamini wao ili wasikose kufika mahakamani hapo.

“Mnajua hii ni kesi ya jinai, lazima muwepo mahakamani na mkikosa lazima wadhamini wawepo ili kuondoa utata, ila hofu tuliyo nayo ni pale tutakaposubiri kikao cha Bunge kiishe ndipo washtakiwa waje mahakamani ni muda mrefu sana, hivyo naomba wakili wa utetezi awasiliane na washtakiwa kupata siku ya nafasi ili kuanza kutoa maelezo ya awali,” alisema Juma.Alisema hana shaka juu ya dhamana ya Mbowe isipokuwa mdhamini wake akisema hajui anachokifanya na kusema hafai kuwa mdhamini. Aliiomba mahakama kutoa uamuzi juu ya mdhamini huyo.

Hata hivyo, Wakili Kimomogoro alipinga hoja ya kutaka mahakama impe onyo Mbowe kwa sababu kosa lililojitokeza halikuwa ka kwake na kwamba Mahakama ilimpa udhuru Aprili 29, mwaka huu kesi hiyo ilipotajwa na kutoa sababu kwamba watakuwa katika vikao vya Bunge la Bajeti hivyo kuiomba mahakama imrejeshee dhamana yake ya awali.

Baadaye Hakimu Magesa alitoa uamuzi wa kumwachia Mbowe kwa dhamana ili aendelee na vikao vya Bunge la Bajeti hadi hapo Juni 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena. Hata hivyo, Mbowe na wabunge wenzake wanaohusika na kesi hiyo, hawatakuwapo mahakamani katika tarehe hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari na wafuasi waliofurika mahakamani hapo mara baada ya kuachiwa, Mbowe alisema hakuwa na kosa la kukamatwa na ndiyo sababu mahakama haikumhoji hata swali moja.

“Ila mimi naheshimu mahakama, lakini sitakosa kusema pale wanapokosea kama vile baadhi ya watumishi wa mahakama wanakubali kupewa amri na viongozi wa serikalini ili mradi tu kutimiza matakwa yao,” alisema Mbowe.
Alisema hakukuwa na sababu za msingi za kutumia rasilimali za Serikali ambayo ni mali za umma na kumsindikiza kama mhalifu ilihali hakuwa hata na silaha moja.Alisema anashukuru kwamba polisi hawakumfanyia vitendo vyovyote vibaya isipokuwa walimnyima haki yake ya msingi ya kuwa na uhuru wa kuwasiliana na watu.


Wafuasi Chadema wasitisha shughuli za mahakama
Mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika katika Viwanja vya Mahakama hiyo walisababisha kusitishwa kwa muda kesi nyingine kutokana na eneo hilo kutawaliwa na kelele. Kesi nyingine ziliendelea kusikilizwa saa 5:00.

Wafuasi hao wa Chadema bila kujali eneo hilo la mahakama, walikuwa wakipiga kelele za 'peoples power' na baada ya Mbowe kuachiwa walianza kuimba: “Wamebana wameachia, wamebana wameachia,” huku wakimbeba kiongozi huyo juu juu.

Mamia ya watu walizuiwa kuingia ndani ya Mahakama hiyo huku polisi wakiwa wametanda kudhibiti uvunjifu wa amani.Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema mara kadhaa alikuwa akitoka nje ya Ukumbi wa Mahakama kuwaeleza wafuasi wa chama hicho kilichokuwa kikiendelea ndani huku akiwahimiza kutokatishwa tamaa katika kudai haki yao.

Lema alisema kukamatwa kwa Mbowe ni ishara ya ushindi wa chama hicho kuchukua dola miaka ijayo.
"Msihofu hata kina Mandela waliteseka hivi hivi, lakini baadaye walikamata dola na chama. Tutaongoza nchi hii miaka michache ijayo, hawa polisi watakuwa wakitulinda sisi badala ya kutukamata kamata," alisema Lema.

Maoni ya wananchi
Baadhi ya wakazi wa Arusha wameelezea kushangazwa kwao na matumizi makubwa ya fedha za umma katika kumkamata Mbowe na kumfikisha Arusha kisha kuachiwa kwa dhamana.
Mmoja wa wakazi hao, George Kavishe alisema kitendo cha kujisalimisha Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwa ndege ya jeshi na kusindikizwa kwa magari ya Serikali ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

"Sasa kama walijua akifika hapa atapewa dhamana tu kwa nini wasingemalizia Dar es Salaam suala hili? Ni jambo la ajabu," alisema Kavishe ambaye ni mfanyabiashara. Mkazi mwingine Lucas Kaaya, alisema hatua ya polisi kumfikisha Mbowe mahakamani akiwa chini ya ulinzi imedhihirisha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

"Ingekuwa sisi watu wa chini, leo hapa dhamana isingetoka tena tungepewa siku 14 za kukaa magereza sasa hili ni funzo tuheshimu vyombo vya sheria kwani hakuna amani bila haki," alisema Kaaya.

Polisi wadhibiti maandamano kwa amani
Polisi jana, walifanikiwa kuzima maandamano ya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamejiandaa kufanya hivyo wakiwa wamebeba majani wakiashiria amani. Viongozi wa jeshi hilo walifanya mazungumzo na Mbowe na viongozi wa Chadema mkoani Arusha na kuwasihi waondoke mahakamani kwa magari yao, ili kuzuia maandamano yasiyo na kibali.

Baada ya kukubaliana, Lema aliamua kuondoka mahakamani hapo kwa pikipiki aina ya Toyo na wafuasi wachache, hasa vijana walianza kumfuata nyuma lakini walipofika makutano ya Barabara ya Nyerere walitawanywa na polisi.

Polisi:Mbowe hakuonewa

Akizungumzia kitendo cha Jeshi hilo kumkamata Mbowe, Kamishna wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja   alisema kuwa kiongozi huyo alikamatwa kama ilivyo kwa watu wengine na hakuonewa inavyodhaniwa na baadhi ya watu.
Aliwataka Watanzania kutokubali kutumiwa na wanasiasa wanaotaka umaarufu kwa nguvu kwa kulazimisha kufanya maandamano kinyume na sheria.

Chagonja aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, kiongozi anayetaka kuingia madarakani kwa mtindo wa kushawishi wananchi kufanya maandamano si mzuri.

“Wapo viongozi wa kisiasa wanaotumia wananchi kujipatia umaarufu. Nawaonya wananchi wakumbuke kwamba yatakayowapata ni hasara kwa familia zao, kwa nini ukubali kushinikizwa na mtu mwenye lengo la umaarufu na wewe unakubali?”

“Alikamatwa baada ya kushindwa kutii amri ya mahakama ni utovu wake wa nidhamu na  sheria iko wazi kwamba kama mtu hajafika mahakamani bila sababu za msingi hati ya kukamatwa inatolewa. Kama kuna ugomvi, Chadema ingeilalamikia mahakama si Jeshi la Polisi.”

“Nchi hii ni ya amani, mtu yeyote atakayeleta uchokozi hatutamuonea aibu, hatuwezi kukubali kumnyamazia mtu wa namna hii, kama anachimba shimo basi atumbukie mwenyewe,” alisema Changonja na kuongeza:“Mbunge akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge atapigwa pingu tu, maneno yanayosemwa kuwa mbunge ana kinga ni ya kutapatapa tu.”

Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Peter Kivuyo alisema katika mafunzo ya jeshi hilo kuna aina moja tu ya kumkamata raia: “Ili kumkamata Rais wa nchi kuna taratibu zake, lakini watu wengine wanakamatwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.”

Katika hatua nyingine, Jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia  watu watatu wakiwamo wanafunzi wawili  wa vyuo kwa tuhuma za kufanya fujo na maandamao, huku wakiwa na mabango yenye ujumbe unaochochea nchi kuingia katika machafuko ya umwagaji wa damu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi mmoja wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambaye ni mkazi wa Kijitonyama na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) anayeishi katika Hosteli za Mabibo pamoja na mkazi mwingine wa Tegeta.
Kova alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na vurugu zilizojitokeza baada ya Mbowe kukamatwa na jeshi hilo kwa kukaidi agizo la mahakama.
Kova alisema kumejitokeza tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwachochea vijana kuingia mitaani kufanya fujo kwa madai ya kuwa wanadai haki yao kikatiba.

“Jeshi la polisi haliko tayari kuvumilia tabia hii na tutatoa adhabu kali kwa yeyote atakayehusika kuwahamasisha au kuwachochea vijana kuleta machafuko. Kama fujo za jana (juzi) zilizochochewa na viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa kuhamasisha vijana kuingia mitani wakiwa wamevaa fulana pamoja na kubeba mabango yenye ujumbe unaochochea nchini kuingia katika machafuko ya umwagaji damu,” alisema.
Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma na Moses Mashalla, (Arusha); Ramadhan Semtawa, Fidelis Butahe, Hadija Jumanne na Aziza Masoud (Dar)

SAKATA LA JAJI MKUU WA KENYA KUTUHUMIWA KULA KIBOGA LINAENDELEA

Willy
Dk Willy Mutunga
Jaji mkuu mteule nchini Kenya Dk Willy Mutuga amekanusha kama anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
Mutunga aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na kamati maalum ya bunge.
Kamati hiyo ya bunge ilifanya vikao vyake vya siku mbili kusikia shutuma zilizotolewa dhidi ya walioteuliwa kuchukua nyadhifa za jaji mkuu,naibu jaji mkuu na mwendesha mashtaka mkuu.

Anashiriki

Hatua hii ilichukuliwa baada ya baadhi ya watu na hasa makanisa yakidai walioteuliwa si watu wanaozingatia maadili ya kifamilia kukiwemo na shutuma kuvaa hereni kwenye sikio la kushoto kwa Dk Mutunga ni ishara kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
"Sishiriki mapenzi na wanaume,ila siwezi kuwabagua wanaume au wanawake wanaoshiriki mapenzi hayo,mimi mwenyewe mpwa wangu ni wa jamii hio",alisema Dk Mutunga.

Mchakato

Naibu jaji mkuu mteule Nancy Baraza pia alikuwa na muda wake wa kujitetea,alipoulizwa kwa nini alikita utafiti wake wa shahada ya uzamifu katika suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.
Baraza alisema anafanya hivyo kwa kuwa alitaka kuwa mbunifu na kufanya utafiti wa kipekee ambao haujawahi kufanywa nchini Kenya.
Baada ya vikao hivyo kwa uma ambavyo vimetumika kuwatathmini tena wateule,majina hayo yatawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura,ikiwa wataidhinishwa basi watachukuwa nyadhifa na iwapo watakataliwa bai mchakato wa usaili