Friday, May 13, 2011

VIONGOZI WETU SI VYEMA KUINGILIA MAJUKUMU YA MAAFISA HABARI,HESHIMUNI WEREDI WA WANAHABARI

Ndimbo ajiuzuru Simba  Send to a friend
Thursday, 12 May 2011 21:05
Clara Alphonce
ALIYEKUWA Afisa Habari wa Simba, Clifford Ndimbo jana alitangaza kujiuzuru wadhifa wake kwa madai kuwa hashirikishwi kwa chochote na viongozi wake waliopo madarakani.

Ndimbo alijiriwa kuwa msemaji wa Simba ikiwa ni kigezo kimoja wapo cha kanuni za TFF na FIFA cha kuzitaka klabu zote za Ligi Kuu kuwa na vitengo vya Afisa Habari.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabri Ndimbo alisema ameamua kujiuzuru mwenyewe na wala hajashawishiwa na mtu yoyote ila ameamua hivyo kwa sababu viongozi wa Simba wamekuwa hawamthamini kwa kazi yake ya Afisa Habari wa klabu.

Alisema uongozi wa Simba hivi sasa chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage umekuwa ukimbagua kwa kutokumshirikisha kwa kitu chochote ikiwemo safari za timu na kufanya mikutano bila kumshirikisha na mambo mengine mengi tofauti na mkataba wake unavyoeleza.

Alisema ameamua kukatisha mkataba wake wa miaka miwili alioingia na klabu hiyo toka wakina Rage waingie madarakani  japo kipindi cha miezi tisa amekuwa akifanya kazi kwa hali ngumu, lakini alipokuwa akiwahoji viongozi wake walikuwa wakimuahidi watamtekelezea.

Alisema barua hiyo aliyoiwakilisha jana kwa uongozi Simba itakuwa ni barua ya pili baada ya ile ya awali aliyoandika Aprili 5, 2011 kutokubaliwa baada ya kikao na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji na Katibu Mkuu wa klabu na kushauriana mambo kadhaa ambayo yalimrudisha kuendelea na kazi.

Alisema ameamua kujiuzuru baada ya kuona kuwa hakuna utekelezaji wowote wa yale waliyokubaliana katika kikao chao walichokaa Jumatatu Machi 28, 2011 na kamati ya utendaji na kamati ya fedha makao makuu ya klabu Simba kuanzia saa 7 mchana.

Alisema hata hivyo anashukuru kwa ushirikiano aliopewa na wanachama wa Simba, wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Simba kwa kipindi chote kwani amepata uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania na klabu mbali mbali kupitia Simba ambalo kwa upande wake anaamini ni somo kubwa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #6 Kifaru 2011-05-13 15:04
Niliota hili lingetokea na limetokea.
Quote
 
 
0 #5 LUGEYE 2011-05-13 13:02
Mh Rage kweli umezidi maana kila kwenye taarifa za habari za michezo we ndo msemaji hv uoni aibu sasa nini kazi afisa wa habari?mlimwajiri kwa kaz ipi?Samata kauzwa we ndo umetoa habari sijui nan mwingine kauzwa we ndo msemaji!hv hujui mipaka ya kaz yako mh?hv hamuwaoni wenzenu wa ulaya jaman?Abromovich wa chelsea mmiliki wa timu tangu mwaka uanze umemuona au kumsikia mara ngapi kwenye tv au press conference?yeye ni mtu wa kutoa order tu wako watendaji aliowaajiri sio kila kitu yeye hata kama ni boss,usilete siasa na mpira plz!jifunze kwa Berluscon wa Italia.
Quote
 
 
+1 #4 HAMAD SIMBA DAMU 2011-05-13 09:58
RAGE NI MWANASIASA, SAYANSI YAKE NDIYO HIYO YA KUMUONA KILA SIKU NA WAANDISHI WA HABARI WAKATI MSEMAJI WA KLABU YUPO NA ANALIPWA MSHAHARA HII NI AJABU,,,!!RAGE USITUHARIBIE KLABU YETU KAMA ULIVOVURUGA FAT, ENDELEA NA UBUNGE NA DHAMANA TULIYOKUPA SIYO YA KUMILIKI KILA KITU MWISHOWE TUTAAMBIWA HATA MINUTES ZA KIKAO UNATAKA UWE UNACHUKUA WEWE...SOKA LA SASA NI LA KISOMI HUENDESHWA KISOMI KWA KILA MMOJA KUSIMAMIA IDARA YAKE...
Quote
 
 
0 #3 Mosses 2011-05-13 08:25
Kaka Ndimbo ndio soka la bongo viongozi wetu wako kimaslahi zaidi.Nafikiri kungekuwa na chuo cha kuwapa mafunzo viongozi wote wanaotaka kuongoza vilabu,ama wangepata basi nafasi ya kwenda hata kwa chini hizi za bara la ulaya nakujifunza ni kwa namna gani watu wanafanya kazi kama team work
Quote
 
 
0 #2 Gulio 2011-05-13 08:22
Kwa kweli hiyo ni dalili mbaya wanasimba - tuliambiwa mambo yataendeshwa kisayansi - sayansi iko wapi hapa? - kwa nini mtumie waandishi wa habari badala ya kuyamaliza ndani kwa ndani? Acheni mambo ya siasa ndani ya klabu tutaambulia aibu badala ya mafanikio
Quote
 
 
0 #1 A 2011-05-13 05:50
Mbona hivo tena Simba au ndio mnataka kuwa maadui kicheko? Huu sio hata kidogo wakati wa malumbano bali ni wakati wakujipanga upya na kuirejesha Simba katika ahadi yake. Kwanini hamzitatui tafauti zenu kwa njia ya busara na ukimya na hivo nndivo wanavofanya waungwana. Simba inasifika kwa ustaarabu. Madhali kazi ipo na kila mmoja anataka kuona maendeleo, lazima kuwepo tafauti za maoni kwa lengo la kufikia mafanikio wala sio mtafaruki. Jamani jeepusheni na mambo ambayo yatayotupeleka kubaya. Chondeni hatutaki kusikia mijadala ya kubomowa tunataka mijadala ya kujenga. Tunapingia magazetini tunataka kufurahi na wala hatutaki kulia. Simba ina viongozi wenye ujuzi na waliosoma na msiwache mambo kufika hadi hiyo.
Quote
 
This little and beautiful girl was found 
uswahili,mburahati-dar es salaam

sometimes our reasoning and thinking
may be restricted by the environment
people we are enbraced as our friends

The failure of  previous set goal provides
an opportunities to plan for new goals

Net-working has power in recent world
only if u do it with a plan

Clean enviroment should be enhanced
for our health and proper thinking
because dirty environment results into
 unproper thinking

PENYE UKWELI,UONGO HUJITENGA! CCM KAMA HAINA JIPYA HIVI?

Marando, Nape ni jino kwa jino  Send to a friend
Thursday, 12 May 2011 22:06
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye
Ramadhan Semtawa na Elias Msuya
CCM na Chadema, vimeendeleza siasa za jino kwa jino kufuatia viongozi wake kuzidi kurushiana makombora yaliyobeba tuhuma ndani yake.Jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alimtaka Dk Willibrod Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema aliombe radhi Bunge, huku Chadema nayo ikimtaja Nape kwamba ni mtuhumiwa wa ufisadi wa EPA uliofanyika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo Sh133 bilioni zilikwapuliwa. 

Tuhuma hizo kutoka kila upande, ambazo sawa na siasa za jino kwa jino, zimekuja baada ya Nape kutaja alichokiita unafiki wa Dk Slaa kwa kushinikiza kulipwa mshahara wa Sh7.5 milioni na Chadema, wakati alikataa mshahara wa Sh7 milioni alipokuwa mbunge akidai ni mkubwa na uliwanyonya Watanzania.Vyama hivyo jana kwa nyakati tofauti, kila kimoja kiliongeza mashambulizi dhidi ya kingine, ambapo Nape alikwenda mbali zaidi akimtaka Dk Slaa aliombe radhi Bunge na wabunge kwa alichoeleza kuwa Dk Slaa alipokuwa Mbunge wa Karatu, alichochea chuki kwa wananchi dhidi ya taasisi hiyo.

"Najua Chadema watakuwa wanajibu, lakini nasema msimamo wangu uko mbele zaidi kwamba Dk Slaa aliombe radhi Bunge na wabunge, kwani alichochea chuki kwa wananchi dhidi ya Bunge, halafu yeye anakuja kuchukua mshahara zaidi ya ule aliojidai kuukataa. Huu ni unafiki," alisisitiza Nape.Nape alisema Dk Slaa ni Padre hivyo pia alipaswa kuungama kwa Mungu kwa kutokuwa mkweli ndani ya dhamira yake."Bahati nzuri Dk Slaa ni Padre, namshauri pia amuombe radhi Mungu, kwani amekuwa akipita mitaani kupandikiza chuki miongoni mwa Watanzania kumbe naye hana maadili yoyote," aliongeza Nape.

Alifafanua kwamba mshahara anaolipwa Dk Slaa ni kodi ya wananchi inayotokana na ruzuku, hivyo ni matumizi mabaya kumpa mshahara mkubwa kama huo wakati aliukataa akiwa mbunge.Kama alivyofanya katika mkutano wa kwanza aliofanya Kata ya Ulugu jimboni Iramba, Nape alisema ataendeleza mashambulizi dhidi ya Dk Slaa katika mikutano yake yote itakayofanyika mkoani Singida ili kuweka wazi maovu ya kiongozi huyo kwa kile alichokiita uchonganishi.

"Hapa naelekea Iramba Mashariki, lakini ninachosema ni kwamba, nitaendelea kuwaeleza Watanzania unafiki wa Dk Slaa. Hatutaki viongozi wanaoeneza chuki wakati wao wenyewe hawana maadili yoyote,"aliongeza.
Alisema ndani ya Chadema wapo baadhi ya watu wanalipwa kiasi cha fedha ambacho ni kidogo na wanaishi kwa shida kubwa hivyo, kama Dk Slaa ni mwadilifu awaangalie hao.

MJumbe wa kamati kuu ya Chadema Mabere Marando akionyesha ripoti ya fedha ya chama hicho kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
Chadema waja juu
Lakini mkutano na waandishi wa habari jana, licha ya kufafanua kuhusu mshahara wa Katibu Mkuu wake, Dk Slaa na ununuzi wa magari, Chadema jana  ilimuita Nape kuwa ni 'Vuvuzela' na kwamba hana sifa ya kuinyooshea kidole Chadema. “Tuna ushahidi wa kutosha kuwa mmoja wa watu walionufaika na fedha za EPA kupitia kwa Jeetu Patel ambaye ameeleza vizuri jambo hili katika maelezo yake mbele ya kamati ya Rais,” alisema Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Anthony Komu.
Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Mabere Marando alidai kuwa Nape aliwahi kuomba kugombea ubunge kupitia Chadema baada ya kushindwa kupata nafasi hiyo kupitia CCM, lakini wakamtosa kwa kuwa hakuwa na sifa.

“Nilikuwapo kwenye kikao cha kumjadili Nape, tukaona kuwa hana sifa kumzidi John Mnyika ambaye sasa ni mbunge” alisema Marando. Lakini akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Nape aliwataka Chadema kutoa ushahidi unaoonyesha kuwa alihusika na ufisadi wa EPA.

“Atoe ushahidi hadharani, unajua hawa watu ni waongo, hata Watanzania watawashangaa,” alisema Nape.
Kuhusu suala la kuhamia katika chama hicho, Nape alisema: “Tena uandike kabisa, mimi ndiyo ninao ushahidi wa wao kunitaka nikagombee kupitia chama chao nikakataa, kwa sababu siwezi kuhamia kwenye chama cha Wachagga, kile ni chama cha ukoo,” alisema Nape.

Mishahara ya Makatibu Wakuu
Akifafanua mshahara wa Dk Slaa, Komu alisema kuwa Katibu wake hawajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi cha Sh 7.5 milioni kama inavyodaiwa bali analipwa Sh 1,725,000 milioni wakati mbunge analipwa Sh 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.
Alifafanua kuwa Dk Slaa pia hulipwa Sh900,000 za mafuta kwa ajili ya kwenda na kurudi ofisini. Vingine ni malipo ya nyumba, mawasiliano na uwajibikaji na hivyo kuufanya mshahara wake kufikia Sh7,174,000 kwa mwezi.

“Sekretarieti ya Kamati Kuu ilipeleka pendekezo hilo katika vikao vyake vya Kamati Kuu na Baraza Kuu na pendekezo hilo likapitishwa kwa njia ya uwazi na likaingizwa katika mpango kazi wa chama,”  alisema Komu.
Naye Mabere Marando alikituhumu CCM kuwa kinamlipa Katibu Mkuu wao Sh 11 milioni akisema:  “CCM wanapigia kelele mshahara wa Dk Slaa, mbona Mukama (Wilson) analipwa Sh11 milioni?. Mbona Rais Jakaya Kikwete analipwa posho nyingi tu? Ofisi yake iko Dodoma, lakini akienda huko analipwa posho, akirudi Dar es Salaam analipwa,” alisema Marando.

 Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai ya Marando, Mukama alikataa kutaja mshahara wake akisema kuwa ni siri yake.
 “Mimi leo ndiyo natimiza mwezi mmoja tangu niingine ofisini, hata mshahara wenyewe sijauona. Mshahara ni siri yangu mwenyewe, nimeingia hapa baada ya kustaafu kwa hiyo ndiyo hivyo, naomba msiniingize kwenye hizo ‘debate’ (malumbano)” alisema Mukama.

Lakini akijibu hoja hiyo, Nape alisema kuwa Mukama analipwa mshahara kulingana na daraja la viongozi na hurekebishwa kama watendaji wengine serikalini.
“Katibu Mkuu wetu analipwa Sh1.5 milioni na hukatwa kodi. Vilevile hulipwa posho isiyokatwa kodi ya Sh300,000. Hayo mengine ya usafiri ni mambo ya kawaida tu. Usafiri anao na hulipiwa umeme wa LUKU na nyumba. Siyo suala la kificho hilo,” alisema Nape.

Mafuso ya Chadema
Wakijibu hoja ya Nape kuwa Chadema kimenunua magari chakavu, walikanusha wakisema kuwa magari hayo licha ya kutokuwa chakavu, siyo magari ya kawaida bali ni mitambo maalumu ya uenezi.

“Katika magari hayo kuna vipaza sauti (Public addressing system 3 sets) zenye thamani ya dola za Marekani 148,000 (Sh 222 milioni), jenereta tatu kila moja Sh15.5 milioni sawa na Sh47,000,000,” alifafanua Komu.

Naye Marando alisema kuwa chama ndiyo kilimwomba Mwenyekiti Freeman Mbowe awauzie magari hayo ndipo akakubali. “Mimi mwenyewe nilihusika kumwomba Mbowe atupe magari yale, akakubali. Baada ya hapo Kamati Kuu iliunda kamati ya watu wanne chini ya makamu mwenyekiti Zanzibar Mohamed Issa kumwomba mwenyekiti akiachie chama magari hayo.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Abdallah Safari alisema kuwa CCM inatumia ujinga wa Watanzania kama mtaji wake na kuwataka Watanzania kutoyumbishwa na propaganda za CCM.