Saturday, April 30, 2011

ADHABU DHIDI YA VIGOGO AMBAO HAWAKUSAIDIA CAMPAIGN ZA CHAMA ZAANZA,


Tido Mhando afungua ukurasa wa adhabu hizo:
Ninampango wa kurudi kijijini kwangu Tanzania,na kushirikiana na wanakijiji wenzangu katika shughuri za maendeleo” hiyo ilikuwa ni kauri yake Tido baada ya kuulizwa na mtangazaji wa shirika la utangazaji la uingereza(BBC) anatarajia kufanya nini baada ya kustaafu kazi yake ya utangazaji (BBC). Binafsi namuona Tido kama muungwana aliyekuwa tayari kushirikiana na watanzania wenzake katika kuleta maendeleo na ndio maana pamoja na pesa nyingi alizopata mara baada ya kustaafu BBC lakini alikubari kutoa mchango wake wa uzoefu katika nchi yake, nasema Tido ni muungwana na mzalendo kwa kuwa hakutaka kubaki ughaibuni ambapo angepata kazi za mkataba na kupata mapesa mengi lakini akakubali kurudi Tanzania.
Mchango wa Tido unaonekana katika kulibadirisha television ya taifa(TVT) na kuwa Shirika la utangazaji la tanzania(TBC) ambayo imejiongezea watazamaji wengi si Tanzania tu bali hata nje ya nchi, TBC imeweza  kuondoa mtazamo wa watanzania wengi ambo awali walikiona chombo hicho kama cha chama kinachoongoza dola, TBC chini ya uongozi wake Tido hakika imekuwa kama chombo cha umma na si chombo cha ccm,hii imechangiwa na msimamo thabiti wa mkurugenzi wake ndugu Tido ambaye aliruhusu habari kurushwa pasipo upendeleo wa chama chochote cha siasa, dini, kabila na mahali.
Enzi za TVT mchakato majimboni uliosusiwa na wanaccm na ambao umekigharimu sana chama hicho na kupoteza viti vingi vya ubunge, usingeweza kuoneshwa  kama ulivyooneshwa na TBC, huo ni mfano tosha kwamba ndugu Tido alikuwa jasiri ambaye hakumugwaya hata bosi wake aliyempa ukurugenzi.
Leo kumekuwa ni mijadara mbalimbali mara baada kuona kichwa cha habari katika gazeti moja la kila siku likinadi kuwa Tido mhando ametimuliwa, mtangazaji wa leo wa  jambo Tanzania Raheli MHANDO wa  TBC hakuweza kusoma habari hiyo pamoja na mesaji nying tulizo mtumia kumtaka atufafanulie kuhusu habari hiyo! Wengi tunajiuliza je, mchango wa Tido katika TBC ulikuwa unapingwa hata na wafanyakazi wenzake wa TBC? Je mwajiri wa Tido ameona Tido hajafanya lolote katika kukiendeleza chombo hicho cha umma? Je Tido amekamatwa mchawi kwa CCM kupoteza viti vya ubunge na udiwani? Je Tido ni kigogo wa kwanza aliyefungua ukurasa wa adhabu dhidi ya waliochangia ccm kupoteza viti vya ubunge kwa kuruhusu mchakato majimboni? Maswali hayo tumekosa majibu yake kabisa kwa kuwa Tido kwetu sisi watazamaji wa TBC na wapenda habari zisizoegemea upande wowote, amekuwa ni shujaa wa kipekee ambaye hana hudi kupongezwa kwa kukuza democrasia hapa Tanzania na nchi za jilani kupitia TBC!
Hivi mcango wa Tido hauonekani mpaka kufikia hatua ya kufukuzwa kama mbwa ambaye hana uwezo wa kubweka au ubwa mla kuku wa kufugwa? Ugumu ulikuwa wapi kumuongezea muda wa miaka miwili ndugu Tido mhando ili kukamilisha mipango yake aliyokuwa nayo katika kukiendeleza chombo hicho cha umma wakati huu ambapo chombo hicho kinafanya mabadiriko ya kitechnolojia? Ndugu yangu Tido, je ulikuwa huelewani hata na wafanyakazi waliokuwa chini yako, mbona wanakwepa kuhabarisha umma habari zozote zinazokuhusu ili kuweka udharimu huo uliofanyiwa hadharani?udharimu huo uliofanyiwa ndugu yangu Tido, naufanisha na ule aliofanyiwa mhadhili wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof. Baregu ambaye naye alifukuzwa kama mbwa baada ya mkataba wake kuisha,  walau yeye alipedwa na jumuia nzima ya chuo kikuu ambao walifikia hata hatua ya kugoma ili kushinikiza Proffesa huyo masuala ya siasa arudishwe chuoni hapo.
Tukifuata ule usemi unaosema ukiona mwenzako anyoa wewe tia zako maji, basi vigogo wote ambao hawakuchangia katika kufanikisha kampeni za chama dola wajiandae kwa adhabu za kufukuzwa kama mbwa pasipo kujali mchango wenu katika taifa letu! Vigogo wa TANESCO ambao umeme ulikatika wakati wenye dola wakifanya kampeni, wakuu wa wilaya na mikoa ampapo wenye dola walizomewa na kusodolewa wakati wakifanya kampeni, na viongozi wa chama ambao hawakufanya maandalizi mazuri kuwapokea wenye dola wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kukodi piki piki na tex, nyote mjiandae kwa kuwa kigogo mwenzenu Tido wa TBC tayari amefungua ukurasa wa adhabu zichukuliwazo.
naitwa Leonard, nipo Rukwa.    

MUUNGANO NIUTAKAO MIMI MWANANCHI WA KAWAIDA

Kumekuwa na hoja nyingi kuhusu muungano viswa vya Zanzibar na Tanganyika,ambavyo vyot kwa pamoja viliiunda Tanzania,waasisi wa muungano huo marehemu mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Shehe Abeid Karume walilenga kukuza na kudumisha undungu baina ya watanganyika na wazanzibara. Muungano ambao juzi umetimiza miaka 47 umepoteza malengo ya awali ya kujenga na kudumisha undugu,nionavyo mimi ubinafsi wa viongozi wa kisiasa walioshika dola baada ya waasisi Nyerere na karume ndio chanzo cha chokochoko za muungano.Nionavyo mimi waasisi wa muungano walifikia hatua ya kwanza ambayo ilizaa serikari ndogo ya Zanzibar na Serikari ya muungano wa Tanzania, hivyo ingekuwa jukumu la viongozi wa sasa kuendelea kujenga na kudumisha undugu kwa kendeleza hatua ya pili kwa kufanya serikari mbili kuwa serikari moja ya Tanzania yenye raisi mmoja tu badala ya serikari tatu au mbili ambazo zimekuwa zikipigiwa upato. Sioni kwanini viongozi wa kisiasa wanaendeleza kuweka vitu ambavyo kwa namna moja au nyingine ndio vyanzo vya chokochoko za muungano wetu? kulikuwa na na haja ipi kwa zanzibar sehemu ya Tanzania kuwa na Bendera yake,wimbo wake wa taifa,majeshi yake na serikari yake? viongozi wa kisiasa tuache ubinafsi, sisi wananchi wa kawaida tungependa kuona muungano wa zanzibar na Tanganyika unazaa serikari moja chini ya raisi mmoja ili kuwa na nguvu za kuharakisha maendeleo ya Tanzania kwa ujumla wake! Kuna ugumu upi zanzibar ambayo wakazi wake ni takribani millioni moja sawa na idadi ya watu katika mikoa mingine tanzania,kuongozwa na wakuu wa mikoa kama ilivyo kwa mikoa mingine?hakika kero za muungano zitakoma pale ambapo tanzania itakuwa na serikari moja tu.