Friday, April 1, 2011

BABU KAMA KAWA AENDELEA KUGAWA DOZI YA KIKOMBE

Mawaziri wengine wapata kikombe  Send to a friend
Sunday, 27 March 2011 05:59
0diggsdigg
Neville Meena  na Mussa Juma, Loliondo
Mchungaji akimimina dawa tayari kwa kuwanywesha wateja wake
NI kama mbio za kupokezana vijiti kwa mawaziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ambao wanaendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge, Loliondo kwa ajili ya kunywa dawa ya kutibu magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile.

Jana ilikuwa ni zamu ya mawaziri wawili ambao ni Ezekiel Maige wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Hovisya, ambao walifika Samunge na kila mmoja kupata kikombe cha babu.

Mawaziri hao walifika Loliondo asubuhi kwa ndege ya Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) kisha kwenda Samunge na jioni waliondoka kwenda mkoani Manyara.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Loliondo mara baada ya kurejea kutoka Samunge, Maige alisema: "Nimekunywa dawa mimi binafsi, si kwa niaba
ya Serikali wala kitu kingine chochote…".

Maige ambaye pamoja na Hovisa walionekana kuwa na haraka kutokana na kubanwa na sheria za uwanja wa ndege kutotumika zaidi ya saa 12.00 jioni, pia alizungumzia mazingira ya utoaji wa dawa hiyo akisema lazima zichukuliwe hatua za haraka kubadili mfumo wa sasa wa utoaji.

Alisema hivi sasa taratibu za utoaji wa dawa hiyo  si nzuri kwani zinawalazimisha baadhi ya wagonjwa kukaa kwenye foleni kwa siku saba wakisubiri zamu zao hali ambayo alisema ingeweza kuepukwa.

Kauli ya Maige imekuja wakati ambao Serikali inasubiriwa kutoa tamko rasmi kuhusu kuendelea ama kusitishwa kwa tiba hiyo baada ya kujadili hali ilivyo katika vikao vilivyokuwa vikiongozwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.

MTOTO WA MKULIMA HALI YA MAISHA YA WATANZANIA WENGI NI MBAYA HAKUNA HAJA YA UTAFITI

Kweli Waziri Mkuu hajui hali ngumu inasababishwa na nini!  Send to a friend
Thursday, 31 March 2011 21:21
0diggsdigg
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
JUZI Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda,  aliitaka Taasisi ya Kuondoa Umaskini  nchini (Repoa) kufanya utafiti wa kina kujua ni kwa nini wananchi wa kawaida wanalalamikia hali ngumu ya maisha wakati kitaifa uchumi unakua. Kwa maana nyingine ni kwamba, Pinda kama Waziri Mkuu na msimamizi wa shughuli za Serikali hajui kwa nini Watanzania wanaendelea kuwa maskini wakati mazingira ya kiuchumi yanatoa fursa ya watu kuondokana na tatizo hilo, ambalo kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo linavyozidi kukua.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 16 wa  Repoa, Pinda alieleza kuwa Serikali inatumia tafiti zinazofanywa na taasisi hiyo kupata ufumbuzi wa tatizo hilo na mengine yanayolikabili taifa.

Hii ni changamoto nzuri kwa Repoa ambayo imethaminiwa na kwamba inafanya kazi nzuri inayoweza kuisaidia Serikali kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoihangaisha nchi yetu katika nyanja za uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.

Kwa maana hiyo basi, Repoa inatakiwa kufanya kazi ya ziada kuvumbua tatizo la umaskini uliotopea unaoendelea kuongezeka miongoni mwa wananchi wa kawaida ili Serikali ichukue hatua, kwa kuwa mpaka sasa inaamini kuwa uchumi wa nchi unakua hata kama bei za bidhaa zinaendelea kupaa kila wakati.

Hata hivyo, tunadhani jukumu kubwa liko mikononi mwa Serikali kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa taarifa na ripoti za tafiti zilizofanyika kitaalamu na kuwasilishwa kwake.

Tunasema hivyo kwa sababu, kama hakuna dhamira ya dhati katika kutekeleza na kusimamia hakuna kitakachobadilika, hata kama Repoa watafanya kazi nzuri na kuandaa ripoti inayotoa mwongozo na njia ya kukabiliana na umaskini  hakuna kitakachofanyika.

Tuna kila sababu ya kusema hivyo, kwa vile hatuamini kama kweli Serikali yenye vyanzo vingi vya kupata taarifa, ikiwamo kukua na kuanguka kwa uchumi haijui kwa nini wananchi wanalalamikia hali ngumu ya maisha.

Lakini, je ni kweli Serikali haijui sababu ya watu wa kawaida kukabiliwa na umaskini? Je, ni kweli Waziri Mkuu hajui kuwa kuna mfumuko wa bei kwa bidhaa zote? Kama anajua kuwa bei za vyakula na bidhaa nyingine muhimu ziko juu yakiwamo mafuta ya petroli, inakuwaje ashangae wananchi kulalamikia hali ngumu ya maisha pamoja na umaskini unaowaandama?

Inashangaza kusikia kwamba wakati wananchi wa kawaida ambao ndiyo wengi wanalalamika,  Serikali inasema uchumi wa nchi unakua na haijui kwa nini imekuwa hivyo! Katika hali  halisi, uchumi wa nchi unakuwaje na nguvu wakati wananchi wa kawaida ambao ndiyo wengi wana hali ngumu?

Hoja yetu inasimama katika msingi kwamba, pato la taifa la ndani linagawanywa na idadi ya watu.  Sasa kama watu wengi ni maskini, uchumi unakuaje?  Unakuwaje imara na bei zikiwa juu ambazo wananchi hawawezi kuzimudu?

Tunachojua ni kwamba kama kweli uchumi wa nchi unakua, kwa tafsiri ya uwiano wa mapato na wananchi wake maana yake hivi sasa utajiri uko mikononi mwa watu wachache wanaomiliki njia zote za uchumi.

Pia inamaanisha utajiri wa nchi hii unashikiliwa na watu wachache, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa jamii na taifa letu kwa ujumla.  Maana yake ni kwamba, ikiwa uchumi wa taifa uko mikononi mwa watu wachache ubepari umekomaa na ni hatari kwa taifa kwa sababu kwa kawaida bepari huangalia mazingira ya kibiashara kama yanaruhusu yeye kuendelea kuwepo, vinginevyo anaweza kuhamisha biashara zake  na kila kitu alichowekeza na kupata hapa nchini.

Mambo mengi yanayoweza kutokea katika hali hii ni kushamiri kwa rushwa na ufisadi, ukwepaji wa kodi ambalo pia limekuwa tatizo kubwa hapa nchini.  Haiwezekani uchumi wa taifa ukue wakati Mamlaka ya Mapato (TRA) inashindwa kuvuka malengo ya kukusanya kodi na wakati huohuo Serikali ikishindwa kutekeleza miradi ya maendeleo ya jamii  kwa kukosa fedha, mpaka zitoke kwa wafadhili.Tunamshauri Waziri Mkuu na Serikali kusema ukweli juu ya mambo yanayochangia hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi wake.

MMH NI ZAMU YA WAZIRI MAGUFURI KUNYA KIKOMBE CHA BABU WA LOLIONDO

Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo  Send to a friend
Thursday, 31 March 2011 21:56
0diggsdigg
Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, jana aliingia katika Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila na kupata kikombe cha dawa, kisha kutangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.

Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali itatumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia usafiri wanaokwenda kunywa dawa kwa Babu Masapila.

Barabara inayoingia katika kijiji hicho ambacho kimeshuhudia maelfu ya magari yakiingia kila siku tofauti na ilivyokuwa awali, ipo katika hali mbaya kiasi cha baadhi ya maneo kutoruhusu magari kupishana.

Kwa mujibu wa Magufuli, Serikali ilikwishatoa Sh500/-milioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu eneo la Kigongoni, Ngaresero, Samunge hadi kuungana na barabara ya kutoka mkoani Mara.

Dk Magufuli alisema jana ndio aliuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Makao Makuu kutuma Sh500 milioni ili kuharakisha ujenzi huo.

"Tayari fedha hizo zimeshatumwa Tanroads mkoani Arusha na Meneja wa Mkoa, Kakoko (Deodatus), niko naye hapa hivyo kazi itakwenda haraka ili watu wanaokuja kwa mchungaji kunywa dawa wasiendelee kuteseka," alisema Dk Magufuli huku akishangiliwa na mamia ya watu waliokuwa wakimsikiliza.

Waziri pia huyo alisema kwa mamlaka aliyonayo, atawasiliana na uongozi wa Mfuko wa Barabara ili utume fedha za dharura kiasi cha Sh50 milioni kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorogoro kwa ajili ya kufanya matenegenezo mengine ya barabara, wilayani humo.

Alisema fedha zilizotengwa kwa ajilii ya barabara za nchi nzima kupitia mfuko huo zinafikia Sh286 bilioni katika bajeti ya mwaka 2010/11, na kwamba upo uwezekano mkubwa wa fedha za dharura kupatikana kwa ajili ya matenegenezo ya barabara ya Samunge.

Matengenezo
Kwa mujibu wa Magufuli, matengenezo ya barabara hiyo ni muhimu sana kwani awali barabara hiyo kuanzia Mto wa Mbu ilikuwa ikipitisha magari kati ya 20 na 25 kwa siku lakini, sasa yameongezeka hadi 3,500 kwa siku.

"Nasema barabara hii ni muhimu sana hivyo nakuagiza Meneja wa Tanroads mkoa wa Arusha kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza barabara hii anafanya kazi usiku na mchana ili ikamilike, akizembea fukuza," alisema Magufuli na kuongeza:

"Sheria namba 17 ya mwaka 1997 na vifungu vyake inatoa mamlaka ya kuondolewa kwa mkadarasi anayezembea. Pia sheria inaelekeza kufikishwa mahakamani kwa wakandarasi wa aina hiyo, na
akitiwa hatiani na anaweza kufungwa miaka mitano. Hivyo basi sheria ipo na pale tutakapolazimika tutaitumia".

Magufuli aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Ngorogoro kuwasilisha maombi ya dharura ya fedha za matengenezo ya barabara katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ili kuwezesha matengenezo ya barabara nyingine kufanyika.

"Tukiacha barabara ya kuja huku, nimetembelea barabara zenu katika wilaya ya Ngorongoro, kwa kweli ni mbaya sana hivyo zinahitaji matengenezo,"alisisitiza.

Juzi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Eliasi Ngorisa, aliliambia Mwananchi kwamba halmashauri yake ilikuwa imeomba kiasi cha Sh400 milioni kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kuifanyia matengenezo ya dharura barabara zinazoingia kijijini Samunge.

Dk Magufuli pia alimwelekeza Meneja wa Tanroads mkoani Arusha kuandaa mpango wa matengenezo ya barabara za Ngorongoro na kuwasilisha mapendelezo yake serikalini kwa ajili ya utekelezaji wake.

"Kaandike mpango huo sasa na ulete ili tuone jinsi ya kufanya, kama hujui kuandika tafuta watu wakusaidie," alisema Magufuli na kusababisha umati wa watu
kuagua kicheko.

Waomba msaada
Tofauti na viongozi wengine waliowahi kufika kwa mchungaji Mwasapila, Waziri Magufuli aliruhusu maswali kutoka kwa wananchi waliokuwa wakimsikiliza.

Wengi wao walilalamikia hali mbaya ya mazingira. "...pamoja na kwamba wewe si Waziri wa Afya, lakini tunajua unatoka Serikalini, tunaomba utusadie maana afya zetu zipo hatarini. Huwezi kuamini kwani huko barabarani unakuta mtu anajisaidia haja kubwa hapo,na mtu mwingine anakula chakula, kwa kweli hali ni mbaya tunaomba msaada,"alisema Nicholas Mwangoka.

Akijibu hoja hiyo, Waziri Magufuli alisema atawasilisha taarifa yake kwa Waziri Mkuu ambaye yupo mkoani Arusha na kwamba anaamini kupitia njia hiyo waziri wa sekta ya afya atafikishiwa ujumbe ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

Mapema mchungaji Mwasapila kupitia kwa msaidizi wake, aliomba Serikali ijenge daraja katika mto wa Samunge ambao umekuwa kikwazo cha magari kuingia kijijini hapo kwani hufurika kila mvua zinaponyesha.

Pia mchungaji huyo alimshukuru Waziri huyo kwa ahadi aliyoitoa akisema kuwa hatua hiyo inamtia moyo kuendelea kutoa tiba kwa wagonjwa wanaofika nyumbani kwake.

"Nakushukuru sana kwa ujio wako na yale uliyoyasema, unatupa matumaini,unatupa moyo, asante tunashukuru sana," alisema Masapila.

Foleni yapungua Samunge
Katika hatua nyingine, foleni ya magari ambayo ilikuwa zaidi ya kilometa 30 kutoka eneo analotolea tiba mchungaji Masapila sasa imepungua.

Kupungua kwa foleni hiyo kumetokana na utaratibu mpya wa kuingiza magari katika kijiji cha Samunge ambao unatarajiwa kuanza leo, pia kutokana na kasi ya mchungaji huyo katika kugawa dawa.
  

Tacaids yawaasa wagonjwa
Ellen Manyangu anaripoti kutoka Dar es Salaam kuwa, Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), imewataka wagonjwa waliokunywa dawa ya Mchungaji Masapila kutoacha kuendelea na dozi walizopewa hospitalini kwa kuwa dawa hiyo haijathibitika kutibu Ukimwi.

Mratibu wa  tume hiyo Dk Bwijo Bwijo alisema jana kuwa utafiti bado unaendelea kujua endapo kikombe hicho cha babu, kinaweza kutibu magoonjwa yanayoelezwa.

Alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mjadala ulioandaliwa na Kituo cha Radio Clouds FM na kufanyika katika hoteli ya Kempisky jijini Dar es Salaam jana asubuhi.

Akizungumza katika mjadala huo, Dk Bwijo alisema dawa ya Mchungaji Masapila bado inafanyiwa utafiti ili kuthibitisha kama inatibu, hivyo wananchi hawapaswi kuacha kutumia dawa za kitabibu ghafla.

Kwa mujibu wa Bwijo, jitihada za kuthibitisha ubora wa dawa hiyo bado zinaendelea kwa ufadhili wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Ukimwi (UNAIDS).

“Wagojwa wote walioko kwenye matibabu ya dawa za kitaalamu na wamekunywa kikombe cha dawa ya babu wasiache kutumia dawa zao mpaka itakapothibitishwa kuwa dawa hiyo ni halali na inatibu,” alisema Dk Bwijo.

 Mwenyekiti Mstaafu wa Mtandao wa Wanaoishi na Ukimwi Afrika (TANEPHA), Alex Margery, alisema suala la Loliondo limejaa sura ya Ukimwi na kutahadharisha kuwa watu wasiache kutumia dawa za kitaalamu kwa kuwa dawa ya babu bado haijathibitishwa.

Alisema walishajitokeza watu mbalimbali katika nchi za Kenya na Afrika Kusini na kutoa dawa zilizoaminika kuwa zinatibu maradhi sugu ikiwemo ukimwi, lakini baadaye zilisababisha watu wengi kufa kutokana na kuacha kutumia dawa za kitaalamu kwa imani kuwa wamepona.

“Hili ni jambo la hatari sana hasa kwa jamii yetu kwani wagonjwa wanaacha kutumia dawa za kisayansi zilizothibitishwa kutibu, au kupunguza makali ya maradhi waliyonayo kwa imani kikombe cha dawa wanachopewa Loliondo  kinawaponyesha…, "alitahadharisha Margery.

Aliongeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ARV zilikuwa katika dozi kubwa ya vidonge 14 kwa siku moja, lakini kadri siku zinavyoongezeka dozi hiyo inapungua na hivi sasa ni kidonge kimoja kwa siku.
Mtaalam wa Afya ya Jamii na Ukimwi, Dk Bennect Fimbo, alisema awali ugonjwa wa Ukimwi ulikuwa tishio kwa jamii kwa vile hawakuwa na uhakika wa mtu kuishi nao muda mrefu lakini, hivi sasa mtu anaweza kuishi nao kwa muda wa miaka 20.

Aliongeza kuwa mti wa Mugariga unaotumiwa na babu kama dawa umefanyiwa utafiti kwa muda mrefu, hivyo inapaswa uchunguzi wa ziada ufanyike ili kubaini mti huo unatibu magonjwa yapi na dozi yake.

Kandoro aweka udhibiti
Kutoka Mwanza Frederick Katulanda na Sheila Sezy wanaripoti kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, amewaagiza wasafirishaji wa watu wanaokwenda kutibiwa kwa Mchungaji Masapila kuwaorodhesha watu wote ili kuweka kumbukumbu.

Akizungumza jana katika kikao chake na wamiliki a mabasi, Kandoro alisema Serikali imepanga utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi kwa lengo la kupunguza msongamano na kuwezesha wagonjwa kumfikia babu haraka zaidi.

Alisema Serikali imetambua kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaoenda Loliondo kwa ajili ya matibabu hayo hivyo utaratibu huo mpya utasaidia kupunguza msongamano.

Alifahamisha kuwa kuanzia sasa magari yote yanayotoka Mwanza na Kagera na wageni kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi kwenda Loliondo, wanapaswa kujiandikisha jijini Mwanza na kuacha majini yao katika kizuizi cha Magu.

Magari yatakayoruhusiwa kuondoka na kupita katika vizuizi ni yale yenye nguvu maalumu (four wheel drive) na mbasi. Malori ya aina yote hayaruhusiwi kwenda huko, alisema.

Akizungumzia suala la nauli kuwa juu, Kandro alisema serikali haitaingilia utozaji wa nauli bali kuhakikisha inaboresha mazingira ya Loliondo na kwamba nauli zitashuka zenyewe.

MI9CHONGO YA KUSOMA HIYOOOO


Fri, April 1, 2011 9:35:48 AM
New Zealand Open Development Scholarships | 8 Fully Funded PhD Scholarships | Apply Today
...
From:
Scholarship-Positions.com <admin@scholarship-positions.com>
...
Add to Contacts
To:leonardkilamhama@yahoo.com

New Scholarships from Scholarship-Positions.com April 1, 2011
Home   Search in Universities   Post a Job Free   Subscribe  
Subscribe in Reader


Please forward this email to your friends if they are also interested in scholarships.

2011 New Zealand Open Development Scholarships for Applicants from Selected Developing Countries, New Zealand
New Zealand Open Development Scholarships for Students from Bolivia, Ecuador, Honduras, Kenya, Mongolia, Nepal, Nicaragua, South Africa, Tanzania, Zambia, China,.. [Read Full Scholarship Detail]


8 Fully Funded PhD Scholarships at the University of Salzburg, Austria
2011- Doctorate Programme in the field of Imaging the Mind Consciousness, Higher Mental and Social Processes at University of Salzburg.. [Read Full Scholarship Detail]

2011 China Postgraduate Scholarship by Tan Kah Kee Foundation 
Tan Kah Kee Foundation Announce Tan Kah Kee Postgraduate Scholarship 2011 Study Subject: Courses  offered by Tan Kah Kee Foundation.. [Read Full Scholarship Detail]


10 ESRC Doctoral Training Studentships at University of London, UK
Ten ESRC-funded studentships in the social sciences are available as part of the Goldsmiths and Queen Mary ESRC Doctoral Training.. [Read Full Scholarship Detail]


2011 Project Assistant and JRF Positions in CSIR-Central Mechanical Engineering Research Institute, India
CSIR-Central Mechanical Engineering Research Institute offers Project Assistant and JRF Positions 2011 Study Subject: Robotics & Mechatronics, Microsystem Technology, Rapid.. [Read Full Scholarship Detail]

Overseas Scholarships for Computer Science Postgraduate Programmes at Heriot Watt University, UK
Funding for Postgraduate  Scholarships in Computer Science for International Applicants 2011 - 2012, UK Study Subject: Computer Science or Information.. [Read Full Scholarship Detail]


Achievement Scholarship and Foundation Scholarship in Swiss German University, Indonesia
Scholarships in Undergraduate programme in the field of Information Technology, Accounting, Pharmaceutical Engineering and Biomedical Engineering at Swiss German University.. [Read Full Scholarship Detail]


2011 Emerging Leaders in the Americas Program, Canada
Undergraduate and Graduate Scholarships for the applicants of Caribbean,Central America,North America,South America by Government of Canada in Canada-2011 Study Subject:Study.. [Read Full Scholarship Detail]


2012 Canada-CARICOM Leadership Scholarships Program in Canada
Undergraduate and Graduate Scholarships Program in the field of Good Governance, Prosperity, Rule of Law, Democratic Development, Pure and applied.. [Read Full Scholarship Detail]


2011 Canadian Commonwealth Scholarship Program
Graduate Canadian Commonwealth Scholarship Program for the applicants of Asia-Pacific and Africa by Government of Canada-2011 Study Subject:Open to all.. [Read Full Scholarship Detail]


2011 ECBA Scholarships Positions in Law, Pennsylvania
The Erie County Bar Association Scholarships  Positions in Law2011, Pennsylvania Study Subject: Law Employer: The Erie County Bar Foundation Level:.. [Read Full Scholarship Detail]


Maria Pia Gratton International Award at University of Illinois, USA
2011 -International Award for female graduate at University of Illinois in USA Study Subject:Academic and cultural experience Employer: University of.. [Read Full Scholarship Detail]


Kurdish Studies PhD Studentship at University of Exeter, UK
2011-Doctorate studentship in the field of Kurdish Studies of at University of Exeter in UK Study Subject:study of the Kurds.. [Read Full Scholarship Detail]


2011 PhD Studentship: fMRI Decoding of Mental State at Radboud University, Netherlands
Doctorate studentship in the field of fMRI Decoding of Mental State at Radboud University,Nertherlands -2011 Study Subject:fMRI Decoding of Mental.. [Read Full Scholarship Detail]


SCIBE PhD Position at Oslo School of Architecture and Design, Norway
Doctorate Positions in the field of Scarcity and Creativity in the Built Environment in Oslo School of Architecture and Design.. [Read Full Scholarship Detail]


2011-PhD Position in Philosophy of Law, Radboud University, Netherlands
Doctorate positions in the field of Philosophy of Law at Radboud University in Netherlands-2011 Study Subject:Philosophy of Law Employer:Radboud University.. [Read Full Scholarship Detail]


Adam Smith Fellowship and College Lectureship in Political Economy, UK
Pembroke College Announce Adam Smith Fellowship and College Lectureship in Political Economy, UK Study Subject: Political  Economy Employer: Pembroke College.. [Read Full Scholarship Detail]


Dean’s Award for Outstanding Scholarship Nomination at Michigan Tech, USA
Michigan Tech – Houghton, MI Announce Dean’s Award for Outstanding Scholarship, USA Study Subject: Courses offered by Michigan Tech –.. [Read Full Scholarship Detail]


Last Minute Deadline: World Bank Scholarship Program 2011-March 31 2011
Are you a national of a World Bank member country? Then you might be eligible for Japan/World Bank Graduate Scholarship.. [Read Full Scholarship Detail]


India Study Abroad Fellowships by Inlaks Foundation 2011
2011 Inlaks Shivdasani Foundation Announce Ravi Sankaran Fellowships,  India Study Subject: Sport Employer: Inlaks Shivdasani Foundation Level: Master Scholarship Description:.. [Read Full Scholarship Detail]


Fellowships for International Students in USA- 2011

This section includes the fellowships of 2011 for those students who want to study in USA. These fellowships are open for those also who want to work with their studies in USA. So these scholarships provide them a great opportunity to buildup a bright future. The eligibility criterion may vary accordingly. Let’s have a look [...]


[Read More..]

Media Education: An Emerging Field

With the stupendous growth of the media industry, Media education has witnessed a dramatic change over the last decade. Due to this phenomenal growth demand for well trained, professional journalists is very much on the higher side. Face of Media Education has entirely changed today. Big Media Houses have opened up private journalism colleges which [...]


[Read More..]

Scholarships for International Students in UK-2011

This section of the scholarships bolg includes the Scholarship for those students who want to study in UK. These scholarships provide them a great opportunity to buildup a bright future. The eligibility criterion may vary accordingly. Let’s have a look on these scholarships. 2011 International Postgraduate Scholarship at University of Strathclyde, UK Organization: University of [...]


[Read More..]

Clinical Research: A Viable Option for Science Graduates

Clinical research a viable and a lucrative option for science graduates. With the discovery and introduction of biotechnological drugs, the pharmaceutical and biotechnology industry is booming and expanding. Companies like Amgen, Genentech, UCB etc have given new and prominent dimensions to this field. Companies like Pfizer, Johnson and Johnson, Novartis are some well known Pharmaceutical [...]


[Read More..]


Applying for GRE? Join LearnWordlist.com for Free!


Scholarship-Positions.com Question Answer Forum
http://scholarship-positions.com/forum/
Scholarship-Positions.com on Twitter
http://twitter.com/newscholarships
Help Others
Forward this Newsletter.
 
 
 
Scholarship tags
2008 2009 Assistant Assistantship Australia Available Biology College Denmark DOCTORAL Fellow Fellowship Foundation France Germany Graduate IndiaInstituteInternational Molecular National Norway PhD PhD Position Position Postdoc Positions Postdoctoral Postgraduate Program ProgrammeResearch Scholarship ScholarshipsSchool Science Student Students Studentship Switzerland Technology UK University USA
 
Links
Home
Scholarship Forum
Search in Worldwide Universities
Post a Job Free
IndiaJobs.co.in
Scholarship-Positions.com
Scholarship Positions: Scholarships Financial Aid Fellowships, PhD, Postdoctoral, Graduate College Scholarships Find College University Scholarships and Financial Aid Positions Free
Scholarship-Positions.com
International Scholarships and Financial Aid Information Services
Office: 106 Civil Lines, Church Road, Bareilly, India, 243005
Forward This Email: Do you know some one who would benefit from this email, please forward it to them.


To unsubscribe or change subscriber options visit:
http://www.aweber.com/z/r/?7AzMDCxMtCwcHOysbMwctEa0nCwcTGxsLA==