Tuesday, June 7, 2011

JE UNAJUA LINAH WA THT AMBAYE SASA AMEWAFUNIKA WAIMBAJI NGULI WA KIKE NCHINI TANZANIA, AMETOKEA WAPI?

Linah Sanga 'Linah'
Thursday, 12 May 2011 04:41
*Clouds Radio kupitia 'Nyuki live' ndiyo iliyomtoa
*Ataka kuwa wa kimataifa kama AY, Alikiba


Na Laurent Samatta

KAMA ni msikilizaji wa kituo cha radio cha 'Clouds', basi utakumbuka mwaka 2009, waliwahi kutangaza nafasi za bure kwa kijana yeyote mwenye uwezo wa kuimba, apige simu kwa namba walizotaja ili uweze kuimba na wao walikuwa wanarekodi ulichokiimba.

Programu hiyo ilipewa jina la 'Nyuki live', ambayo ilikuwa na lengo la kutafuta vijana wenye uwezo wa kuimba, hivyo vijana wengi walipiga simu na waliimba lakini mwisho wa siku walikuja kupatikana vijana watatu ambao walionekana kufanya vizuri.

Vijana hao hivi sasa wanafanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya kitu ambacho hata wale wengine ambao hawakupata nafasi ya kutoka wanatamani programu hiyo irudi tena ili waweze kujaribu.

"Siku hiyo nilikuwa nasikiliza muziki kupitia kituo cha radio 'Clouds', hapo nilikiwa mkoani Mbeya nikasikia tangazo likisema kuwa kijana yeyote ambae anajiona anaweza kuimba vizuri na akakubalika basi apige namba hiyo ili aweze kutuimbia na akionekana amefanya vizuri atapigiwa simu.

"Mimi kweli sikusita kupiga simu lakini kwa mara ya kwanza ilikuwa ngumu lakini nikajaribu kama mara tatu hapo ndipo nilipoonekana nimefanya vizuri, basi pale nikasubili majibu na mwisho wa siku nikapigiwa simu kuwa ni mmoja kati ya washindi watatu wa 'Nyuki live'.

"Sikuamini kama nimeshinda maana Tanzania kuna vijana wengi lakini bahati ikaja kwangu, hivyo nilipofika katika ofisi za Clouds kuna vitu pia wao walitaka kuviona kwangu kama sauti hivyo wakanipeleka Nyumba ya Vipaji Tanzania 'THT', kwa ajili ya kufundishwa namna ya kuimba na mtiririko wa sauti.

Lakini namshukuru mungu pale sikukaa sana kwa sababu nilikuwa na juhudi katika kuimba na uwezo wangu ukawa mkubwa hivyo nilikaa darasani miezi miwili baada ya hapo nikaingizwa moja kwa moja kwenye bendi ya THT, inayojulikana kama 'Odama Band'.

Lakini mwaka huo huo wa 2009, kwa bahati nikachanguliwa katika Fiesta nikiwa kama msanii chipukizi lakini nilichokuwa nakifanya nilikuwa naimba kama msanii wa kusindikiza wale wengine ambao tayari walikuwa na nyimbo zao," anasema Linah.

Jina kamali la nyota huyo hatari ni Linah Sanga lakini wapenzi wengi wa muziki wa kizazi kipya wanamfahamu kama 'Linah', kwa sababau ndilo jina analotumia katika kazi zake za sanaa.

Nyota huyo ni mmoja kati ya wasanii wachache ambao muziki wao unafanya vizuri hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, kutokana na ubora wa kazi zake pamoja na sauti njinsi anavyoibana na kuifanya iwe ya kuvutia zaidi.

Akifanya mahojiano na maalumu na mwandishi wa makala haya hivi karibuni Linah, anasema kwa upande wake imekuwa tofauti na nyota wengine ambao wamekuwa wakifanya muziki kwa sababu ya kaka anaimba au baba anafanya muziki.

Anasema muziki kwake upo kwenye damu na tayari alishakuwa muimbaji wa kwanya katika kanisa ambalo walikuwa wanasali yeye na wazazi wake ambalo ni 'Ufufuo wa Uzima', huku akiwa katika Kwanya ya 'Grolia kwanya'.

Anasema baada ya kuitumikia kwanya hiyo kwa muda mrefu mwaka 2006, akapewa nafasi ya kuwa  mwalimu wa 'Grolia kwanya' ambapo alikuwa akifundisha namna ya kuimba na mtiririko wa sauti.

Anasema viongozi wa Kwanya hiyo walikubali uwezo wake hivyo wakaamua kumtumia katika Band yao inayoitwa 'Grolia Band', ambayo ilikuwa inatoa nyimbo zake kwenye vituo vya radio hapa nchini.

Linah anasema kipaji chake kilizidi kung'ara hasa pale alipochukuliwa na marehemu Docta Remmy Ongala na kumweka katika bendi yake iliyojulikana kwa jina la 'Remmy Ongala Band', ambayo ilikuwa inaimba nyimbo za kumfifu mungu kipindi hicho.

marehemu huyo wa kibao cha 'Kifo hakina huruma' kabla ya kuingia katika nyimbo hizo alikuwa akiimba nyimbo za kidunia lakini baada hapo aliamua kuokoka na kufanya kazi katika kanisa hilo ambalo nyota huyo alikuwa akisali.

"Remmy alikuwa akisali kanisa moja na sisi na baada ya kuniona naimba vizuri katika Kwanya yetu aliamua kunichukua na kunipeleka katika bendi yake, kwa kweri aliniamini kwa sababu sauti yangu ilikuwa ni nzuri ingawa kipindi hicho haikuwa nzuri kama ilivyo sasa," anasema.

Anasema baada ya miaka hiyo kupita alikuwa hajui kama anaweza kuja kuimba nyimbo za kidunia kwa sababu tayari alikuwa akiimba nyimbo za dini ambazo hadi anakuja kuchukuliwa na 'Nyuki live' kutoka 'Clouds' tayari maisha yake yalikuwa yamezoea kuimba nyimbo hizo.

Anasema tangu mwaka huo 2009 alikuwa tayari amesha achana na nyimbo za dini kwa sababu tayari aliingia katika ukurasa mpya wa kuimba nyimbo za kidunia, ambapo mwaka 2010 ndipo alipoamua kutoa wimbo wake wa kwanza ulikwenda kwa jina 'Atatamani'.

'Wimbo huo ndiyo ulikuwa wa kwanza kutoa tangu nilipochukuliwa na 'Clouds' na kuingia 'THT' lakini niliutoa nikiwa chini ya THT, na ndiyo maana watu wengi ambao hawanijui wanasema nimekulia hapo 'THT'," anasema.

Anasema wimbo huo uliweza kufanya vizuri na kumtambulisha katika muziki wa kizazi kipya, na kuanza kufanya shoo mbalimbali katika matamasha, ambapo wimbo wake wa pili 'Bora nikimbie' nao umeweza kufanya vizuri na kuzidi kumtagaza Afrika mashariki akiwa kama msanii chupukizi.

"Nashukuru mungu kwa sababu baada ya nyimbo hizo mbili nimeweza kufanya kazi nyingine za kushirikishwa na wasanii wengi kama Mrisho Mpoto wimbo wake 'Adela', Barnaba wimbo 'Wrong number', Sajna wimbo 'Sitaki kuumizwa' na wengine wengi.

Anasema baada ya nyimbo hizo mbili kufanya vizuri hivi sasa anatamba na albamu yake ya kwanza yeye nyimbo 10, ambayo imebeba jina la 'Atatamani' ikiwa na nyimbo kama Atatamani, Bora nikimbie, Chozi langu na nyingine nyingi zenye ubora wa kimataifa.

Linah anasema kwa upande wake hana fani ya kutunga nyimbo hivyo nyimbo zote alizotoa ametungiwa na rafiki yake ambae pia ni msanii 'Amini' pamoja na 'Barnaba Boy', ambao wamekuwa wakifanya kazi zao pamoja.

Kwa upande wa malengo Linah anasema amejiwekea mikakati ya kufanya kazi ambazo zitamtagaza kimataifa, ili aweza kuwa kama Ambwene Yessaya 'AY' au Ally Kiba 'Alikiba', ambao hivi sasa wanafanya muziki wao kimataifa.

Anasema hata hivyo katika suala la mafanikio, katika kipindi cha mwaka mmoja alichodumu katika muziki wake tayari amesha fanya mambo kama, kununua viwanja viwili kwa ajili nyumba pamoja na kuangiza gari nje aina ya Toyata VX, ikiwa pamoja na kuishi kwa kujitengemea.

Anasema kwa upande wa wazazi wake ambao wapo katika dini hawakuweza kumruhusu kwa mara ya kwanza kwa sababu walitaka aendelee na dini kwa vile waliamini muziki huo unaimbwa na watu ambao wamemtupa mungu kutokana na baadhi ya wasanii njinsi wanavyojiweka mbele ya jamii.

"Wazazi wangu ni watu wanaoamini dini hata mimi pia, lakini kwa mara ya kwanza ilikuwa ngumu sana kunikubalia lakini nikawaeleza sitakuwa na tabia kama baadhi ya wasanii wanavyofanya na kweri wakanipa ruhsa," anasema.

Anasema wazazi wake hadi sasa wanamuelewa kwa sababu hana tabia ambayo inaweza kuwakera kitu ambacho kila siku anaomba mungu asije akabadilika na kuwa na tabia kama baadhi ya wasanii.

Linah anasema hana elimu kubwa zaidi ya kidato cha nne, lakini anaamini atarudi shule ili aweze kumaliza elimu ya juu ambayo inawe kumsaidia hapo baadae ikiwa pomoja na kuchukua masomo ya sanaa katika chuo kikuu chochote Duniani.

Linah anatoa ushauri kwa wasanii pamoja chipukizi ambao wanaingia katika fani hiyo kuacha tabia ambayo inawapelekea wazazi kuhisi sanaa ni fani ambayo inavuja maadali hasa mbele za mungu

No comments:

Post a Comment