Wednesday, March 16, 2011

ELIMU KUHUSU KATIBA KWA WATANZANIA



Katiba iweke misingi ya usawa na fikra za utaifa  Send to a friend
Wednesday, 16 March 2011 00:00
0diggsdigg
Na Charles Kayoka
HIVI karibuni, hasa wakati na baada ya uchaguzi, gumzo juu ya udini katika siasa limeibuka na limekuwa moja ya mada katika mikutano ya CHADEMA. Niliona bango moja katika maandamano likisomeka, “Udini ni ghilba za Wanasiasa.” Nami nakubaliana na maelezo hayo ya kuwa wanasiasa wanapoona wanashindwa kupata uhalali wa kutawala wanakimbilia makundi yao ya kiimani kuomba msaada kwa kisingizio kuwa watu wa imani ingine- imani pinzani, hawamtaki kwa sababu ya kuwa wa imani tofauti.

Hili huweza kupata mashiko kama watu wa dini husika hawana uwezo wa kufanya upembuzi yakinifu. Ndio maana udini unaweza kuwa ni ghilba tu ya wanasiasa kuomba msaada wa kundi.

Lakini kwa Tanzania udini katika siasa hauwezi kuelezeka kwa kauli rahisi namna hii! Udini ni matokeo ya matumizi ya makusudi ya nguvu za kundi ili kujijengea uhalali wa kuendelea kuwepo madarakani na pia kutumika kama ajenti wa kuwasaida watu wa kundi lako kwa sababu wamekutuma ufanya hivyo, au unahisa una wajibu wa kufanya hivyo.

Kumekuwa na madai ya namna hiyo dhidi ya uongozi tangu wakati wa Nyerere. Na hakuna Rais Tanzania aliyekwepa tuhuma za kuwa anatumiwa na dini yake. Lakini wakati huu pia tuhuma hizi aidha zinasema uongozi uliopo unatumiwa kidini au unawatuhumu wapinzani kuwa wawakilishi wa dini.

Hizi ni dalili kuwa Tanzania kama nchi imekosa itikadi unganishi ambayo ingewatambulisha viongozi kwa itikadi hiyo na tungetambuana hivyo kama raia na uongozi ungepimwa kwa utekelezaji wa itikadi husika.

Nchi inapoendeshwa kwa msingi wa fedha na mashindano katika kupata fedha na mali, ni wazi umoja utajengwa kwa msingi wa fedha na mali. Lakini kwa sababu binadamu lazima tuishi katika makundi, dini na kabila huweza kuwa moja ya makimbilio ya kujengeana umoja na kujitambua.

Lakini ufisadi unapozidi na kuwa kupata ajira, kwa mfano,kunategemea unajuana na nani, ukoo, kabila au dini, ni lazima watu watadhani kuwa ili ufanikiwe ni lazima uwe na uhusiano wa kiitikadi na anayekusadia kufanikiwa.

Udini unaweza kutokana na kukosa fikra yakinifu ya vyanzo, na katika kutatua matatizo, hasa ya umasikini. Watu wanaweza kudhani wamekuwa masikini kwa sababu tu watu wa dini fulani wanatawala badala ya kuuchungunza mfumo mzima wa uchumi unavyowafanya watu wote masikini na wachache matajiri.

Kwa kawaida huwa ni rahisi hao matajiri wachache kuwaghilibu mlio wengi kwa lugha za kuwafanya msione ukweli wa jinsi wanavyowanyonya. Na mkadhani hata ni matajiri kwa kudra ya Mwenyezi Mungu.

Lakini kutokukubali kufanya mkutano wa katiba ambako ndiko kutakapo patikana majadiliano ya namna siasa itakavyoendeshwa kunaweza kuwa moja ya chachu ya udini.

Katiba ni chombo muhimu sana katika kujenga itikadi ya umoja wa kitaifa. Wanaohofu isitengenezwe kwa mkutano wa pamoja wanaogopa kuwa ile misingi wanayoitumia sasa ya udini na ukabila itaondolewa na watawajibika kwa misingi ya usawa na fikra za utaifa. Wananchi tusidanganyike.

mohamedmusta@gmail.com This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it , 0766959349

1 comment: