Friday, June 10, 2011

TUNAHITAJI WABUNGE WALO NA UCHUNGU NA NCHI YAO KAMA ZITO KABWE, HAKIKA ZITO NI MWAKILISHI WA WATU MASKINI

Zitto ajitoa kupokea posho za Bunge  Send to a friend
Thursday, 09 June 2011 23:25
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
Exuper Kachenje
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi.Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.
Katika barua hiyo, ambayo gazeti hili limefanikiwa kuiona, Zitto alisema anaamini kuwa watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.
Zitto alisema kuwa posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao.

"Kwa mujibu wa Sheria ya Utawala wa Bunge (National Assembly Act of 2008) na kwa mujibu wa Masharti ya Kazi za Mbunge niliyokabidhiwa, ninastahili kupata posho za vikao, (sitting allowances) kila ninapohudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake,"alisema Zitto na kuongeza:
"Ni imani yangu kuwa posho ya kikao haistahili kulipwa kwa mbunge na mtumishi mwingine yeyote wa Serikali kwani kuhudhuria kikao ni sehemu ya kazi yangu,".

Kupitia barua hiyo, Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha, alieleza kwamba amekuwa akipendekeza posho za vikao hivyo ifutwe, jambo ambalo pia limo katika mapendekezo ya chama chake (Chadema) katika Bajeti ya 2011/2012.
"Nimekuwa nikipendekeza kuwa posho hii ifutwe. Chama changu cha Chadema pia kimependekeza jambo hili katika mapendekezo yake ya Bajeti 2011/2012," alisema Zitto na kuendelea:
"Mpaka hapo mfumo wa kulipana posho za vikao utakapofutwa, ninaelekeza kwamba stahili zangu zote za posho zielekezwe katika Taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).., utaratibu huu uanze kuanzia tarehe 8/6/2011."


Katibu wa Bunge agoma kuizungumzia
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa jana kama amepokea barua hiyo ya Zitto, alisema kuwa, yeye kama mtendaji wa mhimili huo wa Dola, anapokea barua nyingi, hivyo si rahisi kukumbuka kama barua hiyo imefika ofisini kwake.

Lakini akasema, hata kama barua hiyo itakuwa imemfikia ofisini, kanuni na taratibu haziruhusu Bunge kutangaza habari za mtu binafsi.Alisema ofisi yake hairuhusiwi kuandika masuala binafsi ya wabunge yanayofikishwa ofisini na kwamba hilo linawezekana ikiwa mhusika (Zitto), ameruhusu lifanyike kwa maandishi.
"...Haturuhusiwi kuandika habari  za mtu. Nikiwa Katibu wa Bunge, napokea barua nyingi 'personal' (binafsi), lakini kama yeye mwenyewe amewaambieni kuwa kaleta barua hiyo, basi mwambieni pia atuandikie barua kuturuhusu na sisi ili tulitangaze hilo," alisema Dk Kashililah.
Bajeti ya posho kulipa walimu laki moja
Uamuzi huo wa Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, umekuja huku taarifa za utafiti wa taasisi ya Policy Forum inayojihusisha na tafiti mbalimbali za sera zikionyesha kuwa, katika mwaka 2008/2009, Serikali katika bajeti yake ilitenga Sh506 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho.

Kwa mujibu wa utafiti huo, ambao taarifa yake ilitolewa mwaka uliopita, fedha hizo ni sawa na mishahara ya mwaka mzima kwa walimu 109,000 ambao ni robo tatu ya walimu wote nchini.
Kwa mujibu wa utafiti huo mwaka 2009/10 kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya posho za watumishi wa umma kilikuwa sawa na asilimia 59 ya malipo ya wafanyakazi wa ngazi ya chini .  

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Comments 

 
0 #85 @y2k 2011-06-10 13:40
Quoting Japhary Lyimo:
That is political KIINI MACHO,HOW IS HE SURVIVING??????? Kwa hela zake binafsi? Hela za Chama? Or kunamfadhili anamlipa kichini chini ili siku akitoka aanze kulipa fadhila? Tumeona Dr. SLAA alivyoingia kwenye mkataba na CHADEMA ili ajitoe muhanga kuachia Jimbo na kugombea Urais aliojua hata pata, na leo CHADEMA wanalazimika kumlipa posho na malupulupu kama mbunge. The same to ZITTO, "WE CALL IT A POLITICAL MOVE"

we mzee naona bado akili yako ijakomaa hata kama umezeeka basi umezeeka vibaya kama wazee wenzio wa CCM kama huna cha kusema bora kukaa kimya m-s.n.g.e
Quote
 
 
0 #84 Godson Galasi 2011-06-10 13:37
kwa kweli ztto anatambua nini anakifanya na ni kwa nini yyeye yuko bungeni,zitto ametambua wajibu wake kwa uwepo wake bungeni,ametamb ua thamani ya wapiga kura wake pamoja na watanzania wote waanaoishi maisha magumu kwa sababu ya u-mimi/ubinafsi wa wachache na kutotambua wajibu wao kwa watu waliowapatia kazi.kimsingi malipo ya posho ni wizi mtupu kwa mtu anayetekeleza wajibu wake kama sehemu ya kazi yake,na mimi nashangaa waziri mkuu kuto yaanglia haya kwa u-makini mkubwa!!?halafu pia nafikiri kupitia bajeti hii,kama waziri mkuu anauchungu na maisha ya watanzania tulitarajia kusikia ununuzi wa magari ya kifahri kwa kila mtu sasa basi ili kuokoa fedha za watanzania kupotea na badala yake kufanya kazi nyingine za maendeleo kam alivyofanya zitto kwa maana ya yeye kuonyesha mfano kwa wengine
Quote
 
 
0 #83 zabronsimon 2011-06-10 13:33
Fara John, tatizo wewe huna hoja , usiangalie mtu ametokea chama gani au kabila gani angalia amesema nini, na alichosema kinamaslahi kwa taifa zima na sio kwa wachache? John vip rafiki yangu mbona ishu ya Zitto ipo wazi kabisa haihitaji kuumiza kichwa? badilikeni jaman,achana na uchadema, uccm, u-cuf, lamsingi tujenge nchi yetu.
Quote
 
 
0 #82 JOHN 2011-06-10 13:25
we zanbron iringa mnadanganyika tu wachAGA WAPO TANZANIA NZIMA NYIE MNAFUATA UPEPO TU KWANI HUJUI CUF cha wapemba UDP cha bariadi na DP pekee ndo cha watanganyika. ULIZA WALID KABURU WA kigma mjini ambaye ndo alikuaga mbunge pekee wa chadema yupo wapi baada yan kuingia anga za wachaga. we wa liniiii mbona kama mjanja lakini huelewi mambo
Quote
 
 
0 #81 maskini wa kipato. 2011-06-10 13:16
Kabwe hongera sana,heri yako ukumbukae wenye shida,jaman hebu fikiria mwalimu na kamshahara kake ni sawa na posho ya wabunge ya kikao ya siku moja na nusu,kabwe ameliona hilo.Aisee zitto anaona mbali,huyu ndie yupo kwa maslah ya wananchi,wengin e ni kwa maslahi yao.wananch tunataka vitendo kama zito s maneno tu majukwaani.
Quote
 
 
0 #80 zabronsimon 2011-06-10 13:13
Wewe John htofautiani na John Chiligati(CCM) mbona majina ya akina John wanaakili nyie vipi? Zitto amefanya uamuzi mzuri. Halafu hiyo tabia ya kusema chadema ni cha wachaga ife mbona sisi tupo Iringa sio wachaga? Toweni hoja za msingi msimuige JK maana ni yeye alianzisha kwamba cdm ni cha wachaga baada ya kuishiwa sela wakati wa uchaguz.
Quote
 
 
-1 #79 JOHN 2011-06-10 13:02
CHADEMA WWOTE KUTOKA UCHAGANI LAZIMA WAITISHE KIKAO KUKUJADILI, WE HAYA SHAURI YAKO YALIYOKUKUTA MARA BAADA YA UCHAGUZI BADO HUJAKOMA. NAKUONEA HURUMA SANA NDUGU. HAO WACHAGA HAWATAKUSAMWE KWA HILI UNAACHA PESAA MEKU AISE
Quote
 
 
+2 #78 Lucas Haule 2011-06-10 12:54
Zitto Kabwe, natamani kuzaa mtoto nimwite, Zitto Kabwe. Hizi ndiyo akili, huu ndiyo ufahamu, haya ndiyo majukumu ya kiongozi. watawla hawawezi kufanya hivyo. BABA MUNGU, NAAMINI UNANISIKIA, MWONGOZE KIJANA HUYU ILI AFIKIE KILE AMBACHO WENYE FIKRA HABA HAWATAKI AFIKE, MWEKE AWE KIONGOZI WETU KWA AJILI YA UTUKUFU WA JINA LAKO, AMINAA!
Quote
 
 
+2 #77 Hellen Gupta 2011-06-10 12:54
Hakika Zitto una upendo wa dhati kwa nchi yetu na wananchi wetu. Wachache wako tayari kuachia pesa zao binafsi ili wengine wanufaike. Hongera sana. Tunakuombea Mungu akulinde, uzidi kufanya maajabu kama haya. Naye atakubariki sana.
Ciao.
Quote
 
 
+1 #76 zabronsimon 2011-06-10 12:53
hongera!!!!!!!! !!!!!!!!!!!!!!! ! Zitto. John chiligati (CCM)ziiiiiiiii iiiiiiii umeleta kichefuchefu.
Quote
 
 
+2 #75 Rasvin 2011-06-10 12:44
Mh Zitto Safi sana uliona mifano ya bunge la Germany. Sasa kama kweli wabunge wetu wanataka maendeleo basi huo ni mfano tosha wa kukubalina na mahamuzi aliyofanya Zitto. Sio kupenda posho tu, kwani masaa ya kazi ni wajibu wako kufanya kazi si unalipwa mshaara wako wa kila mwezi. Ndio wenzetu uku wanavyo fanya, na shangaa Nnchi kama Tanzania ina malipo mengi sana ya posho za vikao sio Bunge tu, ata kwenye ofisi za serikali. Bless Up Zitto kwa uamuzi wako.
Ras Vin. Medical Instute Heidelberg.
Quote
 
 
+1 #74 macso 2011-06-10 12:33
Zitto anakubalika. Initiative kama hizi ndio tunataka Tanzania. Hongera Zitto. Hata kwenye tathmini watu wengi wanamkubali sana. Ukurasa wake umejaa sifa tofauti na za mafisadi tathmini.com/.../...
Quote
 
 
+2 #73 pechi 2011-06-10 12:32
kweli zito umenenea
Quote
 
 
+2 #72 zabronsimon 2011-06-10 12:26
hayo ni mawazo yako hafifu, haiwezekani mtu upo ofisini kwako eti ulipwe posho, Hongera Zitto, okoeni hizo bilion 280 za posho.
Quote
 
 
+2 #71 zabronsimon 2011-06-10 12:19
BIG UP!!!!!!!!!!!!! !!!!!!! ZITTO, JOHN CHILIGATI(CCM), NI FISADI, MNYONYAJI, HANA HURUMA, ETI POSHO WAANZE KUTOLIPWA UPINZANI, HALAFU CCM WATAANZA KUTOLIPWA MIAKA IJAYO, HUYO KIONGOZI NI FARA
Quote
 

No comments:

Post a Comment