Thursday, May 12, 2011

SI HAKI KUFUNGA SHULE KWA UTOFAUTI WA ITIKADI ZA VYAMA

Wabunge Chadema wageuka mbogo  Send to a friend
Wednesday, 11 May 2011 21:27
0diggsdigg
Boniface Meena, Kwela
WABUNGE wawili wa Chadema jana walikuwa mbogo baada ya kufanya ziara katika Kijiji cha Lusaka, Jimbo la Kwela, mkoani Rukwa na kubaini  Shule ya Sekondari Lusaka imefungwa bila maelezo.Mbali na hilo wabunge hao waliwaeleza wananchi kwamba wamebaini mbolea ya ruzuku inayotolewa na serikali ni ufisadi mtupu kwa sababu wananchi wanatozwa fedha nyingi kununua mbolea ya ruzuku.

Wananchi wa Kijiji cha Lusaka walilalamika mbele ya wabunge hao kwamba Serikali imekuwa ikiwanyanyasa na kibaya zaidi imefunga Shule ya Sekondari ya Kijiji hicho baada ya wananchi wa eneo hilo kumchagua Diwani wa Chadema.

Mbali na hilo wananchi hao walilalamika mbele ya wabunge hao kwamba shule hiyo iko moja tu katika eneo hilo na ilifungwa ghafla miezi mitatu iliyopita na viongozi wa Seriklali wa Manispaa ya Sumbawanga Vijijini bila kutoa maelezo yoyote.

Baada ya kusikia malalamiko ya  wananchi wa eneo hilo, Mbunge wa Viti Maalumu kutoka mkoani Arusha, Joyce Mukya na Raya Ibrahimu kutoka Zanzibar walikwenda katika shule hiyo na kuwaona madiwani wakiendelea na kikao na kushindwa kupata maelezo kutoka kwa madiwani na mbunge wa jimbo hilo.

Mukya aliwaambia wananchi hao kwamba atapambana na viongozi wa halimashauri hiyo ili ajue ni kwa nini shule hiyo imefungwa bila maelezo na kusababisha wanafunzi kutokwenda shuleni.

"Yani ni aibu, nitakufa nao kwa kuwa wamefunga shule halafu wanafanyia vikao vya madiwani kwenye majengo ya shule bila kujali haki za wanafunzi kusoma, hawa watu sijui ni wa aina gani,"alisema Mukya.

Alisema hilo ni moja ya maswali atakayowasilisha bungeni kwenye maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu ili aelezwe ni kwa nini shule hiyo imefungwa."Kata ina vijiji vitano, tunataka tujue ni kwa nini shule imefungwa, tutaliwasilisha bungeni kutaka kujua hilo. Inashangaza sana kwa nini mbunge wenu ananyamaza kuhusu shule kufungwa na anafanya mikutano huko ndani bila hata kujali,"alisema.

Raya Ibrahimu alionekana kuchukizwa na kitendo hicho na kuishambulia serikali kwa kushindwa kuwajali wananchi wake hasa wanachanga fedha zao kujenga shule, lakini zimekuwa zikifungwa bila wananchi kuelezwa sababu za kufanya hivyo.

"Unajua hawa watu wanatia aibu, mimi sijui ni wa aina gani watu wazima wanafunga shule bila kufikiria madhara gani wanafunzi wanapata, halafu wakikimbilia mijini wanalalamika," alisema.

Alisema kitendo kilichofanywa na Serikali kinatia aibu kwa kuwa kinasababisha vijana kukimbilia mijini kwa ajili ya kuuza pipi na biskuti.

Raya alisema suala la huduma za jamii limekuwa ni vituko kijijini ambako kuna barabara mbovu na aliwashauri wananchi kuipunzisha CCM ili wajifunze kuwajali wananchi wao.

Kuhusu mbolea alisema ni bora serikali ikaondoa ruzuku kwenye mbolea ili ishuke bei na wananchi wanunue kwa bei ya chini."Serikali iondoe vocha za ruzuku kwa kuwa zinafaidisha watu wachache na kuwaumiza wananchi wengi ambao ni masikini,"alisema Mukya.

Alisema nchi inanuka rushwa kwa sababu wananchi wamekwua wakilalamika kutopata mbolea kwa kuwa kila mtu ni mla rushwa."Viongozi wa CCM wanachukua zile vocha wanajigawia. mwananchi maskini akitaka vocha mpaka utoe rushwa, mbolea ni kwa ajili yenu ninyi watu maskini ili mjikomboe kwa vijana kufanya shughuli za kilimo, lakini inashindikana kutokana na ufisadi unaofanyika kwenye vocha hizo,"alisema Mukya.

No comments:

Post a Comment