Tuesday, May 10, 2011

MAISHA NI MAGUMU MNO,

JK: Pato litaongezeka muhula huu  Send to a friend
Monday, 09 May 2011 21:44
0diggsdigg
Habel Chidawali,Dodoma
Rais Jakaya Kikwete, amesema kasi ya kukua kwa pato la Mtanzania ni ndogo na kwamba  juhudi za makusudi lazima zifanyike ili kuongeza pato hilo.Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma, alipokuwa akifungua semina elekezi kwa viongozi na watendaji wakuu kwa serikali.

Hata hivyo alitamba kuwa pato la Mtanzania litaongezeka katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa na kwamba hiyo inatokana na baadhi ya nchi wahisani, kuahidi kuongeza misaada kwa Tanzania.

Alisema katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, umasikini umepungua kwa asilimia mbili tu, lakini alisisitiza kuwa hiyo itabadilika kwa kiwango kikubwa katika muhula wa pili na mwisho wa uongozi wake.

Alisema mkakati uliopo  sasa serikalini ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025, Tanzania inakuwa nchi yenye uchumi wa kati na pato la Mtanzania wa kawaida linatarajia kufikia kati ya Dola 2,500 na 3,000 za Marekani, ikilinganishwa na Dola 600 za sasa.

Kuhusu kipindi cha miaka mitatu alisema kama mipango ya wahisani na Benki ya Dunia, itakuwa mizuri na kukubali kuisaidia Tanzania Dola 2.8 milioni za Marekani, taifa litakuwa katika nafasi mzuri ya kutengeneza ajira na kupambana na umaskini.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo wa nchi alisema hali ya nchi ni salama na itaendelea kuwa salama kama Watanzania, watashikamana na kuwa wamoja.Semina hiyo ilihudhuriwa na Waziri mkuu, Jaji mkuu, Mwanasheria mkuu mawaziri, manaibu mawaziri,makatibu na manaibu makatibu wakuu na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa na Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya.Mada zinazotarajia kutolewa katika semina hiyo itakayodumu kwa ipindi cha siku nne ni pamoja na masuala ya uongozi itakayowasilishwa na Msekwa.

Mada nyingi ni ushirikiano wa viongozi wa serikali na vyama vya siasa itakayowasilishwa Msuya, Masuala ya Uchumi (Mwakilishi wa Benki ya Dunia),Ulinzi (Wakuu wa vyombo vya Ulinzi)  na masuala ya Muungano ambayo yatazungumzwa na viongozi wahusika.

Katika semina hiyo serikali inapanga mipango ya muda mfupi na muda wa kati itakayoitekeleza katika kipindi cha miaka mitano.

Semina hiyo imefadhiliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Benki ya NMB.

No comments:

Post a Comment