Monday, May 16, 2011

JE KUNA UHUSIANO KATI YA UFAULU WA WANAFUNZI NA UPATIKANAJI WA CHAKULA MASHULENI?

Weekend imeenda pouwa sana mtu mzima kwizera! kuhusu mada inayohusanisha chakula na ufaulu wa wanafunzi mashuleni,ni kweli kuna uhusiano mkubwa kati ya ufaulu wa wanafunzi na chakula,vijijini mara nyingi vyakula huwepo kwa wingi wakati wa mavuno lakini msimu wa mavuno ukishapita wanakijiji wengi hukubwa na tatizo la chakula kwa kuwa hawana elimu ya uhifadhi wa chakula,lakini pia mafuno wanakijiji wanayopata hayawawezeshi kufikia msimu mwingine wa mavuno. Hivyo,sehemu nyingi za vijijini wanafunzi wanafunzi hukubwa na njaa,mwanafunzi mwenye njaa hukosa hamasa ya kujifunza kwa bidii kwa kuwa muda mwingi watakuwa wanfikiria namna ya kukabili njaa inayowakumba badala ya kufuatilia yale wanayofundishwa na walimu mashuleni.Ndugu yangu Kwizera mimi mwenyewe ni mhanga wa kutokufaulu vizuri mitihani yangu ya primary school kwa tatizo la njaa,nakumbuka mimi na wenzangu tulikuwa tunakabiri njaa zetu kwa kwenda kuwasidia wafanya biashara kusukuma baiskeli zao zilizobeba mizigo kupanda mlima RUSUNWE wilayani KASULU kuelekea Burundi,na kisha kupatiwa fedha kiduchu ambazo tuliweza kunnua chakula, hali hiyo ilituathiri sana kitaaluma kwa kuwa kazi za kusukuma baiskeli kupanda mlima RUSUNWE tulikuwa tunaifanya wakati wa masomo. Hali hiyo ingeweza kuzuwilika kama tungekuwa tunapewa chakula mashuleni maana tungeelekeza mawazo yetu na fikira zetu katika masomo badala ya kuelekeza mawazo yetu na fikra zetu katika kusukuma baiskeli kupandisha mlima RUSUNWE ili kupata fedha za kununulia chakula.
Hivyo kama kutakuwapo mpango unaotekelezeka wa kuwapatia wanafunzi wa shule zetu za msingi chakula walau cha mchana,licha ya kuongeza ufaulu wa wanafunzi lakini pia mpango wa chakula mashuleni utaweza kuongeza mahudhurio ya wanafunzi mashuleni,kupunguza utoro reja reja wa wanafunzi mashuleni na kuongeza molari za wanafunzi kujifunza na kufuatilia kile wanachofundishwa madarasani.
Mimi ni LEONARD KILAMHAMA

No comments:

Post a Comment